ANZA Kufanikiwa Kibiashara

ANZA Kufanikiwa Kibiashara

Share

THIS IS OFFICIAL PAGE FOR JOSEPH MAYAGILA, THE DIRECTOR OF STUDIES AND TRAINING AT FANIKIWA JOURNALISM SCHOOL ARUSHA, www.fjs.ac.tz

Naitwa JOSEPH MAYAGILA ni mwandishi wa vitabu na mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha (A.J.T.C), Unaweza kupata nakala ya vitabu hivi ambavyo tayari viko sokoni (KUBUNI BIASHARAIKUPASAYO,FANIKIWA KIBIASHARA NAJINSI YAKUWA TAJIRI) Call: 0764969063

12/09/2025

Biashara ina hatua 5 katika kukua. Hatua ya kwanza ni hatua ya "kabla ya kuzaliwa"
(Au kujitungisha Mimba kichwani). Hatua hii ndiyo inazaa Wazo la Biashara (Business Idea).

Wazo (la biashara) ndiyo kiini au uhai wa kiuchumi. Ukipoteza huu uhai, unakuwa umekufa kiakili.(Akili jangwa au ugumba)

Wazo la biashara ni nini? Ni taarifa kuhusu Jambo au kitu cha thamani ambacho watu wanakihitaji, na wako tayari kukigharamia au kukinunua kutoka kwako katika muundo fulani. Hata ukiamua kuwapa bure kitu hicho, watakutamkia maneno ya baraka kwasababu kitu hicho ni kitu cha thamani.

Zingatia neno "kitu cha thamani" na Zingatia neno kukiweka katika "Muundo" fulani

Je unajua jinsi ya kujitungisha mimba kichwani ili uzae wazo la kibiashara, hasa wazo kinara la kukupa upenyo wa kiuchumi au la kufanya watu wakutamkie maneno ya baraka?
Na je unaweza kutengeneza muundo unaofaa kwa wazo hilo?

Kiwanda chako cha kichwani cha kuzalisha mawazo ya kibiashara kina hali gani, na unakula taarifa gani hasa ili kiwanda kiwe na tija?

Kwanini Mungu kabla ya kuumba Dunia, alisema, "Iwe Nuru?"

Yesu alikuja duniani bila Yohana Mbatizaji kumtangulia kwanza? Uchumi mkuu unaweza kuja kwako kabla ya hekima, maarifa na ufahamu kutangulia kwanza akilini mwako? (Mithali 3:13-16)

Mungu akubariki!🙏🏿
Joseph Mayagila
Idara ya Miradi na Maendeleo TAG - Jimbo la Arusha Mashariki

1. Tunaendelea kuuza hisa za kiwanda cha maji ya kunywa cha TAG, Jimbo la Arusha Mashariki. 0715769615
2. Kuna kongamano kubwa la Wanaume wote wa TAG (CMF) tarehe 23 hadi 25 hapa TAG Betheli Christian Centre Kijenge nyuma ya Polisi (0754298 850)
3. Hakuna mtu anayeenda juu kimaisha(kiuchumi) bila kupigia magoti kitu fulani.

22/08/2024

*********************
*********************
UNAPATA PESA LAKINI HUJUI UFANYE BIASHARA AU MRADI GANI?

AU UNA MAWAZO MAZURI LAKINI MTAJI WA KUFUNGUA HIYO BIASHARA HUNA?

AU VYOTE VIWILI HUNA? MTAJI HUNA NA MAWAZO HUNA? AU BIASHARA UNAYO TAYARI, LAKINI NI PASUA KICHWA?

Jiunge na mafunzo ya Biashara na Ujjasiriamali BURE kwa siku 14, yaani wiki mbili ili ujipime k**a una maarifa ya kutosha ya kuendesha biashara uliyonayo au unayopanga kufanya kupitia kozi maalum ya awali ya biashara na ujasiriamali. Kozi hii inakuandaa kufungua biashara inayoweza kuajiri angalau wafanyakazi wawili.
Baada ya mafunzo haya ya wiki mbili, utakuwa umejipima na kuona k**a unahitaji mafunzo zaidi au la. Mafunzo haya ya kujipima uwezo ni kwa watu wote wanaotaka kujifanyia tathmini binfsi kuhusu uwezo wao wa kubuni na kuendesha biashara kwa ufanisi.

Mafunzo haya yataanza rasmi tarehe15/9/2024 na kuisha tarehe 30/9/2024
Mafunzo haya ni bure, na ili uweze kushiriki, unajisajiri kwa kutuma neno MAFUNZO kwenda namba 0715769615. Jambo la pili, unatakiwa kuwa na simu yenye Whatsap kwa kuwa mafunzo yote yatatolewa kwa njia ya whatsap kwa siku hizi 14 mfululizo.
Mafunzo haya yanatolewa na Idara ya Miradi na Maendeleo ya Jimbo la Arusha Mashariki la kanisa la TAG, kwa ushirikiano na Chuo cha Uandishi wa Habari na utangazaji cha Fanikiwa Journalism School( Arusha)

Nafasi hii ni kwa watu 100 tu watakaojisajiri kabla ya tarehe 15/9/2024
*****************
*****************

22/07/2024
20/01/2024

Kwa mujibu wa "Bible" Watu wa Mungu wanaangamia kutokana na mambo mawili.(Zingatia neno watu wa Mungu):
Moja, wanaangamizwa kutokana na kukosa akili(Kukosa maarifa), Kukosa muda wa kutafuta akili, Yaani kudharau akili, au kutokutafuta akili au kutotumia akili. Yaani kuishi kijinga au kutumia maarifa kidogo au kutotumia bidii kutafuta maarifa, au kutogharamia maarifa k**a vile tunavyotumia bidii au gharama katika kutafuta fedha (Hosea 4:6)

Mbili ni kutokuona na kutokujiandaa kwa ajiri ya wakati ujao.( Kukosa maono). Kuishi tu hivi hivi bila kuwa na makusudi maalum ya siku za usoni na maisha ya baadaye ambayo yanaeleweka na kupangiliwa vizuri ili kukabiliana na hali mbalimbali. Yaani kutokuwa na picha ya "future". (Mithali 29:18)
Kwa hiyo ni agizo la kibiblia kwamba utengeneze maono yako kuanzia leo, na ni agizo la kibiblia kwamba utafute na kugharamia maarifa.
Joseph Mayagila, Biblical Economics
Bible Study, Fanikiwa Journalism School
0715769615

18/01/2024

Unaanza na Ulichonacho ili Upate Usichonacho. Ukianza na Usichonacho Unaweza Kupoteza Ulichonacho!

30/12/2023

Mawazo yako ni mbegu. Jenga tabia ya kujaribu Mawazo yako!

21/05/2020

FANYA MAMBO YASIYOWEZEKANA UTEGUE KITENDAWILI CHAKO DUNIANI
K**a siku zote unafanya mambo unayoyaweza tu, Akili zako zitakufa.
Ndege wanafanya mambo yanayowezekana, samaki wanafanya mambo yanayowezekana, na mifugo wanafanya yanayowezekana. Je umeamua kujiunga nao?

Ukithubutu kufanya mambo usiyoyaweza, akili yako itakua na utaingia ulimwengu mwingine wa kiakili. Akili zina ulimwengu. Kuna ulimwengu wa akili ya ngazi ya kwanza (Primitive mind), ulimwengu wa akili ya ngazi ya pili(common mind), na ulimwengu wa akili ya ngazi ya tatu (Renewed Mind ). Akili yako iko ulimwengu wa ngazi ipi? Kijana mmoja aliyeshinda mashindano ya uchoraji kwa ngazi ya dunia, alipoulizwa na waandishi wa habari, siri ya mafanikio yake alijibu “ Mimi siku zote huwa nafanya mambo nisiyo yaweza nikiamini ipo siku nitayaweza”

Haiwezekana kubadili historia yako au ya ukoo wenu au kuvunja “record”ya dunia, k**a utaendelea kufanya mambo hayo hayo tu unayoyaweza kila siku. Anza kufanya yasiyowezekana, magumu na yanayokuogopesha zaidi!

Maskini ya Mungu Mti, mti hauwezi kuhama mahali ulipoota na kwenda kuishi sehemu nyingine yenye rutuba zaidi! Mti Hauwezi kuomba msaada wakati wa matatizo ya upepo mkali au jua kali. Mti hauwezi kujifunza maarifa mapya ya jinsi ya kukabiliana na changamoto mpya! Mti hauwezi kufikiri au kutafuta taarifa mpya au kuomba ushauri kwa wataalam ili upate mafanikio zaidi. Kwanini? Kwasababu mti unafanya mambo yanayowezekana tu! Mti unaishi katika mazoea yake tu!

Je nifanyeje ili niwe na ujuzi wa kufanya mambo yasiyowezekana katika maisha yangu au katika biashara yangu?

K**a unapenda kujifunza zaidi kuhusu somo hili, Mimi Joseph Mayagila(Fanikiwa Journalism school Arusha), Nimeandika kitabu chenye kurasa 50, chenye kichwa KUBUNI BIASHARA IKUPASAYO. Nitakuuzia kitabu hiki kwa mkopo wa siku 30, kwa bei ya shilingi elfu tano(5000/=). Kitabu hicho nitakutumia kwa whatsap au kwa email yako katika mfumo laini(soft copy). K**a unahitaji kitabu hicho tuma neno “KITABU KWA MKOPO” kwa whatsap kwenda namba 0715 76 96 15, kisha utapata kitabu hicho baada ya dakika kumi tu ukisha kamilisha kujaza fomu maalum ya mkopo nitakayokutumia kwa whatsap.

Na k**a unataka kupata kitabu hiki kwa kulipa taslim(cash). Tuma neno KITABU KWA CASH kwa whatsap kwenda namba 0715 76 96 15. Kisha nitakutumia kitabu hicho baada ya dakika 10. Kisha baada ya kukipokea kitabu hicho, ndipo utafanya malipo.

ELIMU NI BAHARI, KARIBUNI!

Want your school to be the top-listed School/college in Aruscha?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Address

P. O. BOX 15689
Aruscha