07/02/2024
Mshikamano VTC katika ushirikiano na chuo kikuu cha Maendeleo ya Jamii TICD ,Tumeungana na kufanya mdahalo wa kitaaluma juu ya mada mbalimbali katika kuibua changamoto zinazoikabili jamii na kuzitafutia ufumbuzi.
Mada zilizojadiliwa zilijikita katika changamoto za ukatili wa kijinsia na kujitambua kwa vijana hasa wanafunzi.
Mdahalo huu ulifanyika katika chuo cha MSHIKAMANO VTC 05/02/2024 na kuwahusisha wanafunzi, waalimu pamoja na maofisa kutoka kitengo cha utafiti na machapisho yanayohusu wanawake (NWRDC) Kilicho chini ya TICD .
05/12/2023
Tunamshukuru Mwenyenzi Mungu kwa Mahafali ya 26 ya Chuo Chetu Cha Mshikamano Vocational Training Center,yaliyofanyika tarehe 02/12/2023 na Mgeni Rasmi alikuwa Mhe.Baba Askofu Elias Kitoi Nasari wa KKKT.Dayosisi ya Meru.
23/11/2023
Tunamshukuru Mungu kwa chuo chetu cha Mshikamano VTC kutangaza bidhaa zetu za mbogamboga kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya World Vegetable Center mbele ya mgeni rasmi waziri mkuu mstaafu MIZENGO KAYANZA PETER PINDA .
25/09/2023
Tunashukuru sana kwa msaada wa majiko ya kisasa kutoka kwa rafiki wa Chuo chetu cha Mshikamano VTC kutoka United States of America, Wanafunzi wa Hotel management and food production watapata kujifunza zaidi kwa vitendo, kupata Uelewa mzuri wa Masomo yao na Kuongeza ufaulu.
17/03/2023
Wanafunzi wa HOTEL MANAGEMENT wakiwa kwenye mafunzo kwa vitendo 17/03/2023
17/03/2023
Ziara ya Mafunzo kwa wanafunzi wa waongoza watalii ( tour guide)