JESUS Online TZ

JESUS Online TZ

Share

Jukwaa la Watumishi, Ndoa na Malezi &
How to Follow Jesus.

03/04/2023

Unafikiri unaweza kumbadilisha mtoto/ watoto wako?
Unafikiri unaweza kumbadilisha mke au mume wako? UKWELI HUWEZI.

Hakuna binadamu anayeweza kumbadilisha binadamu mwenzake. Tumepewa uwezo wa kufundisha na kuelekeza tu lakini sio kuwabadilisha.

Mpe Yesu nafasi, Muamini kuwa anaweza kumbadilisha. Acha kushindana naye, acha kumkalisha vikao na kumsemea kwa watu. Haitasaidia, Hali itazidi kuwa mbaya.

Onyesha Upendo wa dhati kwake na omba Yesu aingilie Kati, ambadilishe na Akubadilishe na wewe pia, (yawezekana na wewe unamakorokoro mengi), yaani omba wote mumjue Mungu na kumpenda.

Maombi ya jinsi hii yanajibiwa faster sana.

Usiangalie historia, usiangalie walichokifanya waliokutangulia.
Nasisitiza, wewe mtazame Yesu tu. Mtwike mzigo, yeye ndiye atashughulika na mtoto au mwenza wako, hata km kuna kikwazo kigumu sana Yesu anatosha.

30/03/2023

• Usikubali kuingizwa kwenye Mambo ya matambiko na kutoa kafara ya ukoo wao kisa ndoa

• Usikatwe viungo vyako ukaendelea kuishi naye kisa ndoa.

• Usimpe nyuma kisa unataka kulinda ndoa.

• Asikutishie kukuuwa ukaacha kuchukua
hatua eti unataka kulinda ndoa.
(Anaweza kukuuwa kweli ukaacha watoto wako na yeye akaishia gerezani).

Yaani usifanyiwe ukati ukaa kimya eti hii Ni ndoa.

Fahamu na Zingatia sana;
 UTU WAKO UNADHAMANI KULIKO NDOA YAKO.

Want your school to be the top-listed School/college in Arusha?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address

P. O. Box 1160
Arusha