22/05/2026
Habari za wakati huu tena ,nawasalimu kwa jina la Yesu,ni matumaini yangu sote ni wazima wa afya.
🖊Leo kwa neema ya Mungu nataka tujifunze kidogo kuhusu fedha,tuangalie kutokea hapa
✍️Mafundisho ya Yesu katika eneo la fedha alitufundisha hivi
Mathayo 6:21
[21]kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.
For where your treasure is, there will your heart be also.
✍️Ikiwa hazina(fedha) ilipo ndipo na moyo wa mtu ulipo ,ina maana fedha(hazina) ina nguvu ya kuuvuta moyo(nafsi),na ikiwa kwenye moyo kuna(akili,,hisia,maamuzi,dhamira nia n.k)
Ina maana fedha ya mtu ilipo ndipo ilipo nia,dhamira,maamuzi,hisia,akili na mambo mengine yanayohitaji nafsi,tukiunganisha na mstari huu
1 Timotheo 6:10
[10]Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.
✍️Kumbuka upendo ni hisia kwa hiyo k**a hazina ya mtu ilipo ndipo na moyo wake ulipo inamaana mtu huyo tayari upendo wake upo kwenye fedha(hazina)
Hivyo tunatazamia matokeo ya mtu huyo katika nyanja ya hisia,maamuzi,dhamira,akili na nia yatakuwa shina la mabaya
✍️Kwa ushahidi wa hili angalia viongozi,watu,watumishi wa Mungu mbalimbali ambao mioyo yao imevutwa na pesa jinsi ambavyo wamekuwa shina la mabaya na uharibifu
✍️Jambo lingine ni hili k**a hazina ya mtu ilipo ndipo na moyo wake ulipo ,ina maana fedha inauwezo wa kubeba moyo wa mtoa fedha
Ndio maana sehemu yeyote ambapo ilitangulizwa fedha ikapokelewa ni rahisi sana na ombi au dhamira,nia,maamuzi,matakwa n.k ya mtoa fedha kutekelezwa na yule aliyeipokea
Leo angalia fedha zinazotolewa k**a misaada mbalimbali katika nchi mbalimbali jinsi ambavyo zinakuja na roho za waliotoa fedha hizo
Lakini angalia kwenye familia maamuzi ya mtu mwenye fedha hata k**a yana madhara yatasikilizwa na kutekelezwa kwa sababu ya ile nguvu iliyomo kwenye fedha imebeba maamuzi yake na kuyapeleka kwenye mioyo ya wale ambao wananufaika na fedha anazokuwa anatoa.
Anagalia mabinti na vijana wangapi leo wamejikuta kwenye mahusiano yenye majuto kwa sababu tuu ilitangulia fedha ikateka mioyo yao ikaielekeza hazina/fedha ilipotoka
Daniel alilitambua hili tokea mwanzo ukisoma sura ya kwanza utaona laikini pia angalia hapa
Danieli 5:17
[17]Ndipo Danieli akajibu, akasema mbele ya mfalme; Zawadi zako zishike wewe mwenyewe; na thawabu zako mpe mtu mwingine; walakini nitamsomea mfalme maandiko haya, na kumjulisha tafsiri yake.
✍️🖊Mungu hakukusudia fedha kuwa na nguvu kuzidi moyo wa mtu ila dhambi ndio ilisababisha ndio maana Yesu akatueleza namna ya kufanya ili badala ya moyo kufuata hazina ,hazina ifuate moyo
Marko 3:27
[27]Hawezi mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu, na kuviteka vitu vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu; ndipo atakapoiteka nyumba yake.
✍️Fedha ina nguvu kuliko moyo wa mtu mpaka mtu amemruhusu Mungu kuingia ndani na kuulinda moyo ili awe na nguvu ya kuitawala fedha
Tahadhari:
1.Fedha ni nzuri na inatumika kuleta majibu ya mambo yote na ni ulinzi,hivyo tunapaswa kuitafuta ila tuwe na nguvu ya kuitawala kupitia Kristo,sijasema fedha ni jawabu nimesema inatumika kuleta jawabu
Mhubiri 7:12
[12]Kwa maana hekima ni ulinzi, k**a vile fedha ilivyo ulinzi; na ubora wa maarifa ni ya kwamba hekima humhifadhi yeye aliye nayo.
Mhubiri 10:19
[19]Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko,
Na divai huyafurahisha maisha; Na fedha huleta jawabu la mambo yote.
2.Husifurahie tuu kupokea fedha unayopewa jaribu kutafakari na kumuomba Mungu kwa msaada wa Roho Mtakatifu kujua fedha hiyo imebeba roho ipi?
Kuna wengi maisha yao yalibadilika kabisa baada ya kupokea fedha kutoka kwa watu mbalimbali
Mungu akubariki sana asantee kwa kujifunza na mimi ,ukiona vema na kupata neema mshirikishe na mwingine
07/05/2026
05/05/2026
04/05/2026
30/04/2026