19/06/2026
Siku ya 3.
Somo:UTUKUFU WA MUNGU.
HAGAI 2:9.
"Utukufu wa mwisho wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa kwanza, asema BWANA wa majeshi...".
*Ikiwa haujajifunza somo hili kwa siku 2 zilizopita ni vyema ukarudi kusoma toka mwanzo ili tuendelee kujifunza pamoja kwa mtiririko wa somo hili tulilofunuliwa na Roho Mtakatifu.
Leo tutajifunza kwa kuanza kuyaangalia...
MAMBO YANAYOMFANYA MUNGU ATUKUZWE KUPITIA MIMI NA MIMI NIPATE KUNUFAIKA KWA MUNGU KUTUKUZWA KUPITIA MIMI.
1.Uhusiano wangu mimi na Mungu.
uhusiano ni ushirika baina ya watu wawili au zaidi unaowaweka kuwa pamoja, huku ukiwa umebebwa na makubaliano fulani waliyopatania kuyafanya wakiwa pamoja.
kwa lunga nyingine ni kwamba hakuna uhusiano au ushirika unaowaweka watu kuwa pamoja ikiwa hakuna makubaliano waliyopatania kuyafanya wakiwa pamoja.
hivyo makubaliano na mapatano ndiyo yanayoleta uhusiano au ushirika kati ya mtu Mungu, mtu na mtu, watu na watu, nchi na nchi, kanisa na kanisa n.k.
*Shika:kwakuwa makubaliano na mapatano ndiyo yanayounganisha uhusiano au ushirika kati ya mtu na Mungu, mtu na mtu, watu na watu, nchi na nchi.
hayo makubaliano na mapatano yanapovunjika (kutokufanyika k**a walivyokubaliana na kupatana), uwe na uhakika huo uhusiano au ushirika wao utavunjika.
kwanini uvunjike?
Kwasababu kilichowaunganisha wakawa na uhusiano au ushirika wa pamoja ni makubaliano waliyokubaliana na mapatano waliyopatania kuyafanya wakiwa pamoja.
Amosi 3:3.
"Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?"
Kumbuka:kwakuwa Mungu ni Roho asiye na mwili, hivyo mtu anapokubaliana na kupatana kuwa na uhusiano na Mungu, Mungu huingia ndani yake na kutembea pamoja naye, akiambatana naye ili kumsaidia kuyatenda yale yote waliyokubaliana na kupatania.
Yohana 4:24, 1 Wakorintho 3:16.
Shika:"uwepo wa Mungu upo Kila mahali, lakini si kila kitu huubeba huo uwepo wa Mungu"
kwa maana nyingine ni kwamba Roho wa Mungu yupo Kila mahali, lakini Roho wa Mungu hakai ndani ya kila kitu"
Zaburi 139:7,8.
"Roho wa Mungu au uwepo wa Mungu hukaa ndani ya mtu mtakatifu pekee".
ni neema na raha iliyoje, katika vitu vyote alivyoviumba Mungu, Mungu anatafuta mtu atakayekuwa tayari kumkubalia ili akae ndani yake.
Isaya 66:1,2, 1 Wakorintho 3:16,17.
kumbuka:"Roho wa Mungu au uwepo wa Mungu unaweza kukaa juu ya kitu chochote, na hicho kitu kikatumika kwa kulitimiza kusudi la Mungu, na Mungu akatukuzwa kupitia hicho, lakini hicho kitu kisinufaike kwa chochote, kwa Mungu kutukuzwa kupitia chenyewe (hicho kitu kikatumika bure, pasipo kupata malipo yeyote kwa Mungu)".
hivyo ili mimi nipate kunufaika kwa Mungu kutukuzwa kupitia mimi, yanipasa kila nifanyapofanya jambo analolitaka Mungu nilifanye, nihakikishe ninalifanya huku uwepo wa Mungu ukiwa pamoja na mimi ndani yangu (Roho wa Mungu yupo ndani yangu), na siyo uwepo wa Mungu kunijia ukanikalia ili kumdhihirisha Mungu apate kutukuzwa katika jambo ninalolifanya na baadaye ukaondoka.
*uhusiano wa mtu na Mungu unapovunjika, Roho wa Mungu huondoka ndani ya huyo mtu.
Matendo 5:32.
-Mungu anachokitaka kwangu ni nimtii yeye kwa kuyafanya yale yote anayoyataka niyafanye k**a vile makubaliano na mapatano yetu yalivyokuwa mwanzo wa uhusiano wetu.
Roho wa Mungu anapokaa ndani ya mtu, huumbika ndani ya huyo mtu, kwa kuwekeza roho zake ndani yake (Isaya 11:2), ili apate kutenda kazi pamoja na huyo mtu katika yale anayoyataka ayafanye kwaajili ya utukufu wake (1 Wakorintho 3:9).
'huku ni kutengenezwa au kuandaliwa
kwa mtu kwaajili ya kufaa kuyafanya yale aliyomkusudia Mungu ayafanye'.
Mungu anapoumbika vya kutosha ndani ya mtu au anapojaa ndani ya mtu, haishii tu kujaa ndani yake, bali hutoka ndani yake na kufurika katika mwili na vilivyo katika mwili wake, ili apate kujitukuza kwa kutenda kazi kwa haraka na uwazi zaidi.
pia Mungu anapoumbika vya kutosha ndani ya mtu, ule ubinadamu wa mtu hufa, na Mungu kuishi ndani yake, na kutenda kazi ndani yake.
yaani Mungu mwenyewe ndiye anaishi na kutenda kazi ndani ya mtu.
*kumbuka: ili Mungu aumbike vya kutosha ndani ya mtu, na kujidhihirisha nje kwa uwazi zaidi, inategemea na kiwango cha uhusiano wa karibu kati ya mtu binafsi na Mungu (kiwango cha ushirika, kati ya mtu binafsi na Mungu).
Mfano:
1.Roho wa Mungu au uwepo wa Mungu katika vazi la Eliya.
2 Wafalme 2:9-14.
Elisha aliomba, mara dufu ya sehemu ya roho iliyokuwa ndani ya Eliya.
je! vazi la Eliya linahusiana vipi na roho iliyokuwa ndani ya Eliya? Kwasababu tunamuona Eliya anamjibu kuwa akimuona wakati akiondoka kwenda mbinguni, basi Elisha atapokea mara dufu sehemu ya roho yake .
Na ulipofika wakati wa Eliya kuondoka na kwenda mbinguni, Eliya alimuachia Elisha mavazi yake...na tunaona baadaye udhihirisho wa Mungu ukitembea na Elisha kwa mavazi ya Eliya.
2.Roho wa Mungu au uwepo wa Mungu katika vazi la Yesu.
Marko 5:25-34.
kutokana na Yohana 6:63 inasema 'Roho ndiyo itiayo uzima'.
je! Kuna uhusiano gani kati ya Roho kuachilia uzima kwa yule mwanamke aliyetokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili na vazi alilolivaa Yesu?
3.Roho wa Mungu au uwepo wa Mungu katika mifupa ya Elisha.
1 Wafalme 13:20,21.
Kuna uhusiano gani kwa mtu aliyekufa kufufuka baada ya mwili wake kugusana na mifupa ya marehemu Elisha?
Mungu akubariki kwa kuendelea kujifunza.
Tukutane tena wakati mwingine.
Roho Mtakatifu ni mwaminifu tunaamini atazidi kutufundisha zaidi na zaidi.
Kwa maswali, maoni, ushauri karibu sana.
18/06/2026
17/06/2026
26/05/2026
02/05/2026