Mwongozo Tv Tanzania

Mwongozo Tv Tanzania

Share

﴿وَذَكِّرْ فَإِنَّ الذِّكْرَىٰ تَنْفَعُ الْمُؤْمِنِينَ۝٥٥
《mawaidha,Qur-an na hadith》
💡NURU YA MAARIFA
https://www.youtube.com/@MWONGOZOTV-tp8hy

06/06/2026

"Hakika kwa kumkumbuka Allah nyoyo hutulia."
— Qur'an, Qur’an (Surat Ar-Ra'd 13:28)

06/06/2026

ulio mkubwa zaidi #

عن عبد الله بن عمر رضي الله عنهما قال: قال رسول الله ﷺ: *«إِنَّ أَبَرَّ الْبِرِّ صِلَةُ الْوَلَدِ أَهْلَ وُدِّ أَبِيهِ»*

( Muslim, Na. 2552)

⏩"Hakika miongoni mwa ukamilifu mkubwa wa wema ni mtoto kuwatendea wema watu ambao baba yake alikuwa akiwapenda na kuwa nao karibu."

⏩Mtume ﷺ anabainisha kuwa baada ya mzazi kufariki au hata akiwa hai, si katika wema tu kumtendea yeye vizuri, bali pia ni katika ukamilifu wa kumheshimu mzazi kuwaheshimu na kuwatendea mema marafiki zake, ndugu zake na watu aliokuwa akiwapenda.

⏩Neno "أبر البر" linamaanisha kiwango cha juu sana cha wema na utiifu kwa wazazi. Hivyo mtu anayewatembelea marafiki wa baba yake, kuwasaidia, kuwaulizia hali zao na kuwaheshimu, anakuwa ameonyesha sehemu ya ucha-Mungu na wema wake kwa baba yake.

⏩Watu wengi hudhani kuwa kumfanyia mzazi wema huisha baada ya kufariki kwake. Lakini Uislamu umefundisha kuwa kuna milango ya wema ambayo huendelea hata baada ya kifo cha mzazi, miongoni mwake ni:

1️⃣Kumwombea dua.
Kutekeleza wasia wake wa halali.

2️⃣Kuwaunganisha ndugu zake.

3️⃣Kuwaheshimu marafiki zake.

4️⃣Kuendeleza mema aliyokuwa akiyapenda.

⏩Ndiyo maana Mtume ﷺ hakusema "kuwafanyia wema wazazi" tu, bali akataja hata watu waliokuwa na uhusiano wa mapenzi na urafiki na baba.

⏩Mfano wa Kivitendo
Ikiwa baba yako alikuwa na rafiki aliyekuwa akitembeleana naye mara kwa mara, kisha baba akafariki, ukawa unaendelea kumtembelea huyo rafiki, kumjulia hali, kumsaidia anapohitaji na kumheshimu kwa sababu ya baba yako, basi umeingia katika hadithi hii.

⏩Vilevile kwa upande wa mama, marafiki zake, dada zake, ndugu zake na watu aliokuwa akiwapenda wanastahiki kupewa heshima kutokana na nafasi ya mama.

Faida
Uislamu unahimiza kutunza mahusiano ya kijamii.
Wema kwa wazazi haukatiki kwa kifo chao.
Kuwaheshimu marafiki wa wazazi ni alama ya uadilifu na shukrani.

⏩Mtoto mwema hutunza urithi wa mahusiano mema aliyoyaacha mzazi wake.
Miongoni mwa sababu za kupata radhi za Allah ni kuendeleza mema yaliyokuwa yakifanywa na wazazi.

⏩Funzo
Muislamu wa kweli hapimi wema wake kwa wazazi kwa kuwapa chakula au mali tu, bali pia kwa kuhifadhi heshima yao hata baada ya kufariki kwao. Anawaheshimu waliowaheshimu, anawaunganisha waliokuwa karibu nao, na anawaombea rehema.

⏩ Allaah Amesema:
*"Na sema: Mola wangu! Warehemu wawili hao k**a walivyonilea nikiwa mdogo."*
(Surat Al-Israa: 24)

⏩Hivyo, kumwombea mzazi, kuwatembelea marafiki zake, kuendeleza mahusiano yake mema, na kuwafanyia ihsani watu aliokuwa akiwapenda ni katika milango mikubwa ya birrul-walidayn (wema kwa wazazi).

Wabillah Tawfiiq

05/06/2026

Watoto wa mtume صلى الله عليه وسلم

05/06/2026

Je wafahamu

05/06/2026

ALLAHUMMA AMIIN 🤲

04/06/2026

صلى الله عليه وسلم

04/06/2026

Cha halali ndio bora zaidi na kina furaha

04/06/2026

ALLAHUMMA AMIIN 🤲

03/06/2026

Usihuzunike

02/06/2026

Amiin

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address

Chamazi
Dar Es Salaam