Elimu Ya Utajiri

Elimu Ya Utajiri

Share

Mtu yeyote anaweza kuwa TAJIRI awe kaajiriwa au kajiajiri.

Photos 01/10/2019

Unakutana na watu unaanza kuongelea kile unachokipendelea na kukitaka wewe? Hapana bhana... hakuna anayetaka kujua wewe unataka nini. Sisi pia k**a wewe tunapendelea kuongelea na kufanya vile tunavyovitaka.
Unataka kumfanya mtu afanye unachokitaka?
K**a unataka mtu afanye unachokitaka wewe afanye.... basi usifikirie nini unachokitaka wewe bali fikiria anachokitaka yeye ndo ukitumie kumfanya afanye unachokitaka wewe. Njia pekee katika hii dunia ya kuwashawishi watu ni kuzungumzia kile wanachokitaka na kuwaonyesha namna gani wanaweza kukipata. Kumbuka hili leo ukitaka kumfanya mtu afanye kile unachotaka afanye.
Unataka kufanya biashara pamoja na mtu fulani? Au unataka mteja fulani anunue bidhaa zako? Basi jiulize utafanya nini kitakachomfanya yeye atake kufanya kile unachotaka wewe afanye?. Unataka mtu akupe kazi? Basi acha kusema nini unataka kutoka kwake… mwambie nini utamfanyia akikupa kazi, utaongeza nini kwa uwepo wako pale nk mfanye atake kukupa kazi. Unataka watu, kampuni, jamii, wafanyabiashara wengine watumie bidhaa zako? Waambie nini utawafanyia wakitumia bidhaa zako (faida gani watapata wakitumia bidhaa zako?) wala sio tu nini unataka kutoka kwao.
K**a kuna siri yoyote ya mafanikio basi ni kuweza kutambua nini ambacho mwingine anakifikiria kwa upande wake na kutambua nini unahitaji kwa upande wako wewe mwenyewe.
Somo kutoka kwa Bwana Dale Carnegie katika kitabu chake cha “How to win friends and influence people”

Photos 01/10/2019

ONYESHA UMUHIMU WA MTU PALE ANAPOFANYA JAMBO ZURI (Toa sifa zinazostahili kwa mtu anapofanya jambo jema)

Njia pekee ikayokuwezesha kumfanya mtu mwingine afanye chochote unachotaka afanye ni kumpa anachotaka. Ukiondoa vitu vingine ambavyo binadamu anahitaji k**a afya, chakula, pesa nk.... kila mtu anataka kuonekana muhimu kwa watu wengine.

Vipi hapo kazini kwako? Inakuwaje pale boss asipopenda jambo fulani ulilolifanya katika kazi yako?…mara nyingi huwa wanafoka sana... lakini k**a wakiipenda kazi yako uliyoifanya hawasemi chochote. Na vipi nyumbani mke au mume akikosea jambo mwenza wake atafoka hatari ila akifanya jema hakuna chochote kitakachozungumzwa.
Tumetekwa sana na kuwapambania watoto wetu maisha mazuri, kuishi vizuri na marafiki zetu, wafanyakazi wenzetu na wafanyakazi tuliowaajiri lakini TUMESAHAU KUWAPA MANENO MAZURI ambayo yatabaki kumbukumbu katika maisha yao yote.
Hakikisha sifa unazozitoa au umuhimu wa mtu unaouonyesha utoke kwa moyo mkunjufu na si vinginevyo. Hivi unafikiri anajisikiaje waziri, mhadhiri (lecturer) au muongeaji katika hadhara (public speaker) pale ambapo mpaka anamaliza kuongea hajapata hata kofi moja?

Kinachotokea kwa watu hawa kinatokea mara mbili kwa wafanyakazi maofisini, madukani, viwandani, familia zetu na kwa marafiki pia. Tunachotakiwa kufahamu ni kwamba wote ambao tunashirikiana nao katika mambo mbalimbali pia ni binadamu na wanahitaji waonyweshwe umuhimu wa uwepo wao karibu yetu. Anza kumfanya mtu ajione muhimu kwako leo.

Photos 01/10/2019

1. USIKOSOE WENGINE WALA USILAUMU
Mara 99 kati ya mara 100 watu wanapokosea huwa hawajikosoi wenyewe kwa chochote kile ambacho watakuwa wamekifanya. Mara nyingi ukimkosoa mtu nae atajitahidi kutoa sababu za kujilinda kutokana na kile unachomkosoa. Kumkosoa mtu mara nyingi huweza kumfanya mtu kujitoa thamani, kujiona hana umuhimu na pia huweza kuleta chuki. Asilimia kubwa Kwa kukosoana huwa hatuleti mabadiliko chanya ya muda mrefu hata k**a yatatokea. Hujawahi sikia chuki ilivyoleta balaa baada ya ndugu kukosoana kwa jambo fulani? Wafanyakazi? Wanafamilia? Marafiki? na bado tatizo likaendelea kuwepo?

Mwizi, jambazi na fisadi ukiwakosoa kwa wanachokifanya lazima watafute sababu za kukitetea kile wanachokifanya na hiyo ndio kawaida ya binadamu. Huwa hatukubali kukosolewa. Jambo muhimu ninalotaka kulisema hapa ni kwamba mara nyingi kumkosoa mtu hakumfanyi kujiona ametenda kosa zaidi inamfanya mtu atafute sababu za kujitetea tu. Ni asili ya binadamu kuwalaumu wengine wote kasoro yeye.

Kwa hiyo kabla hatujamkosoa mtu leo basi tutambue kwamba huyo mtu ambae tunataka kumsahihisha ataishia kujitetea na mwisho wa siku kutulaumu sisi. Badala ya kuwalaumu wengine hebu tujaribu kuwaelewa kwanini wanafanya kile wanachokifanya?. Hii ni bora kwetu kuliko kukosoana, hii itatufanya tuwe na utu, tuvumiliane na kuoneana huruma. We unasemaje?

13/09/2019

Watu ambao hawapati mafanikio wana sifa moja kubwa maishani. Wanajua sababu sababu zote zilizowafanya wasifanikiwe lakini wana visingizio vingi vinavyojaribu kuelezea kutofanikiwa kwao. Tunachotakiwa kufahamu ni kwamba visingizio haviwezi tuingizia pesa... Tunachotakiwa ni kufanikiwa tu na si vinginevyo.

Tuangalie visingizio ambavyo wengi tunavitumia na TUVIEPUKE:
1. K**a nisingekuwa na mke na familia....
2. K**a ningepata msaada wa kutosha...
3. K**a ningesoma..
4. K**a ningepata kazi...
5. K**a ningekuwa na muda...
6. K**a nisingeogopa watu watakavyosema...
7. K**a ningepewa nafasi...
8. K**a hakitatokea kitu chochote cha kunizuia...
9. K**a ningezaliwa katika familia ya kitajiri...
10. K**a ningekutana na watu sahihi...
11. K**a ningekuwa na kipaji ambacho fulani anacho...
12. K**a ningetumia nafasi nilizozipata...
13. K**a ningesevu pesa zangu...
14. K**a boss wangu angenikubali....
15. K**a ningepata mtu wa kunisaidia...
16. K**a familia yangu ingenielewa...
17. K**a ningeishi katika mji ule....
18. K**a ningeweza kuanza tena...
19. K**a nisingekuwa na majukumu ya kulea watoto wangu...
20. K**a kipaji changu kingejulikana...
21. K**a nisingekuwa na madeni...
22. K**a ningepata mwanaume/ mwanamke sahihi...
23. K**a nisingepoteza pesa zangu...
24. K**a ningekuwa na biashara yangu mwenyewe...
25. K**a nisingefeli... Hivyo na visingizio vingine vingi si sababu ya kutofanikiwa. Tunachotaka kukisikia ni kwamba umefanikiwa hiko unachowaza kukifanya. Ukijenga tabia ya kutoa visingizio kila mara... hautauona kamwe UTAJIRI unaotaka kuwa nao.Hakikisha unaishinda nafsi yako kutokana na jambo hili. Hakikisha una shauku ya kutosha na mipango mikakati ya kufikia lengo... USITOE NAFASI kwa kisingizio chochote kwenye maisha yako.

10/09/2019

K**a bado hujapanga utaifanyia nini pesa yako ukiipata..... basi jua hakuna cha maana utakachoifanyia hata ukiipata. Panga leo

10/09/2019

Ipi nafasi ya mwenza katika maendeleo/ mafanikio ya mwenza wake...?? Je, mwanamke ana nafasi gani kwenye mafanikio ya mwanaume wake? na mwanaume ana nafasi gani kwenye mafanikio ya mwanamke wake? Nafasi ya mke kwa mume? Nafasi ya mume kwa mke?

Inasemekana wengi waliofanikiwa katika maisha yao basi nyuma ya pazia kuna mapenzi moto moto na ya dhati yanayompelekea akawa huru katika kufanikisha ndoto zake

Wengine wanasema maendeleo ya haraka yanaonekana kwa wengi baada ya kuingia kwenye ndoa... Kwa mtazamo wako unasemaje kuhusu hili? au utajiri hauhusiani kabisa na mahusiano ya mtu na mwenza wake?

04/09/2019

Kuna ule msemo wengi tunapenda kuutumia... "K**a unataka ufanye vizuri yakupasa kufanya mwenyewe". Wengi tunaamini ili kitu kiende sawa mf. biashara basi inabidi kufanya mwenyewe au kipindi inafanyika basi na wewe uwepo ili mambo yaende sawa.

Mara nyingi hii ni changamoto inayowakuta watu waliojiajiri au wenye biashara ndogo ndogo. K**a na ww inakukumba hii changamoto basi unachotakiwa ni kujifunza namna ya kuwaamini wengine kuwa wanaweza kufanya kazi nzuri k**a wewe au zaidi yako. Wengi tunaogopa huenda ukimwacha mtu kwenye biashara atafanya mambo sivyo ndivyo au kukuangusha kabisa mfano kwa kubana mapato nk.
Unachotakiwa kufahamu ni kuwa kwa lolote ambalo limekutokea au litakutokea ni lazima kujifunza kuwaamini wengine. Usipofanya hivyo basi biashara yako itaendelea kuwa ndogo miaka nenda rudi mana ni ngumu kukuza biashara au biashara yako kukua bila kuwaamini wengine.
JIFUNZE KUWAAMINI WENGINE k**a unataka kuwa TAJIRI

Photos from Elimu Ya Utajiri's post 04/09/2019

Una mtaji ila hujui biashara gani ya kufanya? Una biashara lakini unataka kuikuza zaidi na zaidi? una changamoto za biashara unahitaji ushauri?
Basi Kwa kushirikiana na kampuni ya tunakuletea huduma hizo na nyingine nyingi karibu yako na kwa ufanisi. Wasiliana nasi kupitia namba hizo kwenye picha hapo juu.

25/08/2019

Wengi wetu tunapata PESA huenda kwa kupitia kipato cha kawaida tu au wengine kupitia mshahara. Lakini tunashangaa sana kwa nini kila siku hatusongi mbele tunaishia tu kuwa pale pale tulipokuwa jana. Lengo la kutafuta kipato ni kuhakikisha siku moja tunaishi yale maisha ambayo ni ya ndoto zetu. Lengo ni hilo lakini wengi wetu hatufikii huko tunapotaka kufika nab ado tunashindwa kufahamu tatizo liko wapi.
Wengi tunaopata vipato vya kawaida ukiachana na wale wa mshahara tunaishia kutumia kila senti tuliyoipata katika matumizi ya kawaida. Hatuna vyanzo vinavyotuingizia pesa kwa maana hatuwekezi wala kukuza biashara zetu. Miaka nenda rudi tunakua pale pale wala hatusongi mbele.
Na sisi wengine ambao kipato chetu kinatokana na mshahara mara nyingi tunazidi kuwa na madeni kila pale ambapo mshahara unazidi kuongezeka. Mshahara mkubwa zaidi unamaanisha kuwa tunaweza kukopa pesa nyingi zaidi. Nini tunafanyia tukipata pesa hizo? Tutaenda kununua gari au kujenga nyumba nzuri. Ghafla bin vuu mshahara wa mwezi ujao unaingia… kinachotokea ni kwamba utatumika katika kufanya matumizi ya kawaida ambayo huwa yapo kila mwezi jumlisha na yale madeni ya mkopo tuliochukua bila kuisahau asilimia za bodi ya mkopo. Maisha ndio yanaenda ivo ivo miaka nenda miaka rudi. Halafu tunajaribu kuangalia tatizo lilipo hatulioni.

Tatizo kwa wote hawa kiujumla hatujui ni kwamba sio kutengeneza pesa…. TATIZO NI JINSI YA KUITUMIA ILE PESA TULIYOIPATA yaani ni nini cha kufanya baada ya kuipata, nini cha kufanya ili kuhakikisha bado inaendelea kuwa mikononi mwetu na sio tu kupeleka kwa wengine, kwa muda gani inakaa katika mikono yetu na kwa kiwango gani ile pesa tuliyoipata itatutumikia.

THUBUTU LEO KUUEPUKA au UMERIDHIKA HAPO ULIPO?

20/08/2019

MAONO: Hakikisha unaweza kuona pale ambapo wengine hawaoni. Ukiangalia kitu au sehemu fulani unaona kabisa pale fursa inapatikana japo wengi huenda wasione.

KUJIAMINI: Hakikisha una uwezo wa kujiamini kwa kile ambacho unakifanya au unapanga kukifanya. Watu huenda wakawa na mashaka au wewe mwenyewe ukawa na mashaka kwamba utafanikisha jambo lako au laa…. Lakini hakikisha unaJIAMINI muda wote na kusonga mbele.

UBUNIFU: Uwe na uwezo wa kubuni zaidi na zaidi...Huenda unataka kufanya au unafanya biashara ambayo wengine wanafanya hakikisha una uwezo wa kubuni namna ambayo itawafanya wateja kukuchagua wewe na sio yule. Pia uwezo wa kubuni hata kitu chako kipya na kuhakikisha kinakuwa bora na kupata watumiaji au wateja wengi na wengi zaidi.

UWEZO WA KUHIMILI KUKOSOLEWA: Utafiti unaonyesha hakuna mtu aliyefanikiwa ambae hajawahi kukosolewa. Vumilia kila jambo au usemi ambao unajaribu aj utajaribu kukukatisha tamaa na simamia msimamo wako kwamba jambo lako litafanikiwa.

UWEZO WA KUCHELEWA KURIDHIKA NA MAFANIKIO: Ni ngumu kidogo kwa wengi kufanya jambo hili, wengi tukishafanikiwa kidogo tunajisahau kabisa na kuendekeza mambo ambayo hayajengi. Hakikisha unajipa muda na kukusanya mafanikio zaidi na zaidi ya muda mrefu na si kupoteza dira na mafanikio kiduchu yaliyopatikana au yatakayopatikana

15/08/2019

Part 2... (13) UCHAGUZI MBAYA WA TAALUMA: Unataka kufanikiwa katika kipengele gani? dereva? askari? mfanyabiashara? mwandishi? mwalimu? msanii? nk... Ili ufike mbali chagua kitu ambacho utakifanya kwa moyo wako wote... hautachoka na mafanikio yatakuja
(14) KUTOELEZEKA NGUVU KUBWA KATIKA JAMBO HUSIKA: Kila sehemu upo... mara umeshika hili mara umeshika lile...hauko huku wala hauko kule.... Elekeza nguvu zako katika jambo ambalo unaamini litakupa mafanikio.
(15) MATUMIZI YA OVYO: Usiwe mtumiaji wa ovyo ovyo bila mpangilio... weka kiwango maalumu katika kipato chako ili uje ufanye mambo makubwa zaidi.
(16) KUZIDISHA BAADHI YA MAMBO: Kupenda kula sana, kunywa vilevi sana, kuendekeza ngono ni mambo ambayo yanafelisha wengi.
(17) KUTOKUWA NA UWEZO WA KUSHIRIKIANA NA WENGINE: Wewe Kufanya kazi na wenzako huwezi kabisa.... unapenda kivyako vyako. Chunga sana tabia hiyo...Ondokana nayo.
(18) KUTOKUWA NA UAMINIFU: Kuna wakati mtu anaweza asiwe mwaminifu kutokana na mazingira ambayo yanakuwa nje ya uwezo wae. Lakini mwingine ni kawaida yake kutokuwa mwaminifu. Hakuna matumaini kwa mtu ambae ameachagua kutokuwa mwaminifu. Tafadhali usiwe wewe.
(19) KUJISIKIA NA KUJIONA: Kamwe huwezi fanikiwa kwa hili
(20) UKOSEFU WA MTAJI: Hapa wengi wanaegemea na mara nyingi inawakumba ambao wanaanza biashara kwa mara ya kwanza....wanakosa mtaji ambao utawawezesha kuhimili makosa mbali mbali ambayo watayanya katika biashara zao kabla ya kukaa sawa. Anza popote ulipo sio lazima uanze na kiasi kikubwa. Pia unaweza hata kwa kuwa na wazo tu na kufikiria namna gani wazo lako linaweza kuwa pesa.
HIZI NI BAADHI TU...... KIPI KINAKUKWAMISHA HAPO katika part 1 na 2???

15/08/2019

Part 1--Jamii imejazwa na wengi waliofeli kuliko wachache waliofaulu. Nina imani wewe ni mmoja kati ya wachache waliofaulu k**a sio leo basi kesho....USIKATE TAMAA. Kuna sababu nyingi ambazo zinawafanya wengi wafeli, zifuatazo ni baadhi tu. Angalia ni zipi ambazo zinakukwamisha usifike pale ambapo unataka kuwa, halafu jirekebishe:
(1) KUTOKUWA NA LENGO KUU KATIKA MAISHA: Unataka ufike wapi kimaisha? Pambania kila siku kufika hapo
(2) KUTOKUWA NA SHAUKU YA KUSOGEA MBELE: Miaka nenda rudi wewe uko pale pale halafu hauoni tatizo lolote.... unahisi umeshafika... Ambae ana shauku ni yule ambae yuko tayari kupambana kwa kila hali kuhakikisha jana yake sio k**a kesho yake.
(3) KUTOELIMIKA: Kuelimika ni zaidi ya kwenda shule au kufika chuo kikuu... Aliyeelimika ni yule ambae amejifunza namna ya kupata chochote anachokihitaji kwenye maisha bila kuvunja haki za watu wengine na kisha akakiingiza katika matendo.
(4) KUTOKUWA NA NIDHAMU BINAFSI: Unaweza kujikataza mwenyewe kutofanya mambo mabaya ambayo yatakuletea matokeo hasi? Uwezo wa kujidhibiti mwenyewe
(5) AFYA DHAIFU: Bila afya bora hakuna cha maana kitakachofanyika...Hakikisha unakula vizuri, unafanya mazoezi, unalala sehemu safi na salama nk
(6) TABIA YA KUAHIRISHA MAMBO: Usisubiri muda sahihi..anza sasa...anza hapo hapo ulipo, Fanya kazi kwa vifaa vyovyote ulivyonavyo...vifaa bora vinakuja mbeleni.
(7) KUTOKUWA NA MSIMAMO: Wengi ni waanzilishi wazuri ila sio wamaliziaji wazuri...wengi tunaishia njiani. USICHOKE tafadhali
(8) TAMAA KUBWA YA KUPATA BILA KUFANYA CHOCHOTE: Tunataka kufanikiwa lakini kupambana hatutaki...ndio maana wengi tunaishia kwenye k**ari (betting)
(9) KUTOKUWA NA UWEZO WA KUFANYA MAAMUZI UTAKAYOYASIMAMIA: Wanaofanikiwa ni wale wanaofanya maamuzi kwa haraka na kuyabadilisha pole pole.. na wanaofeli ni ambao wanachelewa kufanya maamuzi na huyabadilisha mara kwa mara na kwa haraka sana.
(10) UCHAGUZI MBAYA WA MWENZA KATIKA NDOA: We mpenda maendeleo mwenzako hana habari... yeye starehe tu hawazi ya kesho nk Kuwa makini
(11) KUTOJARIBU: Jaribu bahati yako, chukua chance itakayokuja mbele yako. USIOGOPE
(12) UCHAGUZI MBAYA WA WASHIRIKA KATIKA BIASHARA: Tafuta watu ambao mna malengo sawa.. mtafanikiwa

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Address

Dar Es Salaam