WEWE NI NANI?

WEWE NI NANI?

Share

Open your mind

21/11/2023

UTAJIRI

Wengi wetu tunadhani utajiri ni mali,fedha au majumba au magari maviwanda nk huu ndio tunadhanj utajiri na wapo vikundi vya watu Vinapima utajiri wa mtu kupitia mali zake huu sio utajirI ni uongo utajirI ni kitu kingine kabisa

Leo kila mtu ukimuuliza atakwambia nataka kuwa tajiri ili iweje? Subiri majibu yake ndo utajua ni shida tu zinamfanya atake utajiri feki ambao hajui ni nini maana yake

Tunakubaliana kuna watu wana mali nyingi lakini walipo kufa mali zikapotea na watu wakasema mara ni freemason mara ana mali za ushirikina ni uongo sio kweli

Utajiri ni uwezo wa ndani alio nao binadam ambao anaweza kuumba uchumi mdogo na kuukuza mpaka kufikia uchumi mkubwa ambao watu Wanaona mali Zake, zile mali sasa sio utajiri bali ule uwezo alio nao ndani ndio utajiri ameweza kutumia uwezo wake na vitu vikatokea ndio maana baadhi ya famili wako matajiri ambao wakifa na mali zinapotea kwakua wao ndio watu pekee katika familia wenye uwezo wa kuumba huo uchumi mdogo kuwa mkubwa

Utajiri sio kila mtu anao huo uwezo sio wote wanao kila mtu anauwezo wake ndanI yake ndio maana wapo watu ukiwapa milioni mia miaka miwili ukirudi unakuta hana kitu na wapo watu Ukiwapa hiyo hiyo mia mwaka mmoja unakuta kawa na mali za thamani zaidi ya ile pesa uliyo mpa

Shule Ikilikuwa unakaririshwa kuwa kazi nzuri ni rubani daktari nk unalazimishwa usome lakini kuna waliojitafuta wakaacha kusoma wakawa wanaenda kwenye mpira wakirudi wanapigwa na wanaonywa wasiende,lakini walijisikiliza ndani yao kuna nini, matokeo yakitoka ni wa mwisho anapigwa anaambiwa anaendekeza michezo leo ndio wasakata kabumbu wakubwa si kwambii usisome sikiliza nini unaweza kuumba tokea ndani yako ufanye mambo yatokeee

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address

Kinondoni
Dar Es Salaam