Rayyaan International

Rayyaan International

Share

Elimu na habari

28/07/2025
Photos from Rayyaan International's post 04/06/2025

Kumakucha Bolisa... Kweerire wee...

Assalaamu aleykum wanabolisa' wanakondoa, wakazi wooote wa. wilaya Kondoa na Chemba na mkoa wa Dodoma......

Karibuni saaaaana Bolisa Kondoa tarehe 21.6.2025 siku ya Jumamosi kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa sita mchana .... kwenye hauli na dua ya kujiombea na kuwaombea wazee, taifa, viongozi na dunia kwa ujumla.....

Assalaamu aleykum viongozi wa BAKWATA wilaya wakiongozwa na Alhaj sheikh Nchalo na viongozi wa CCM na viongozi wa serikali wilaya wakiongozwa na DC Hajjat Fatma Almasi ......

Assalamu aleykum na tengi sana vijana, wazee, na akinamama wa Mondo, Soya, Makamaka, Dalai, Tandala, Magebuta, Sambwa, Busi, Kinyasi, Ikengwa, Kiteo Mauno, Bumbuta, Kisaki, mpaka Huruvi na Itaswi....

Karibuni sana wooote ndugu zangu wa Goima, Songambele, Jinjo, Churu, Jangalo , Hamai, Itolwa, Mwilanji na Mrijo mpaka njoro...

Karibuni sana Mnenia, Itundwi, Filimo, Cheke, Potea, Bambare, Masange, Kandaga, Itololo mpaka Sauna Kisese na Dachenche na Mitati...

Karibuni sana wenzangu wote wa Kidoka, Kambi ya Nyasa, Chemba, Paranga, Kelema Sori, Kingale, Isini, Serya, Unkuku, Gubali, Choka, Kolo, Kwadino, Isabe, Bukulu. Masawi, Bereko, Salanka, Salare, Kikilo, Ororimo. Thawi, na Sakami....

Karibu wazee wa Baura, Haubi na Mwisanga, Hebi, Ihari, Kwadelo, Mtakuja, Jenjeluse na Mwilanji...

Naaam!!
Sijawasahau wazee wa Mongoroma, Munguri, Bubu Changaa, Chololo, HondoMairo, Kwamafunchi na Mwembeni...

Karibuni sana wanangu wa B***a, Kilimani, Miningani, Kwapakacha, Mpalangwi, Ubembeni, Maji ya Shamba, Soweto, Tura. Nkangi, Itiso, Poisi, Tumbelo, Poisi na Hachwi...

Naaaam! Salamu hizi nakuomba wewe unaesoma zifikishe kwa wengine kupitia mitandao lakini kwa njia yoyote nyingine...

Naluomba Shere kwenye kurasa zako za Fb, Insta. Whats. Nk.

Karibuni maimamu wa misikiti yote wilaya ya Kondoa na Chemba .....

Karibuni masheikh na viongozi wa mikoa na wilaya kote nchini ...

Mimi ni mtayarishaji tu wa jambo lenu nyinyi ..
........

Dr. Harith Nkussa
Msemaji Maalum wa M***i
Jumatano 4.6.2025
Bolisa. Kondoa

Photos from Rayyaan International's post 16/03/2025

MSIMU WA DUA YA KITAIFA YA KIMKAKATI WAZINDULIWA BOLISA - KONDOA.
...

Msimu wa siku tisini wa Dua ya Kitaifa ya kimkakati wazinduliwa rasmi mtaa wa Bolisa wilayani Kondoa kwa dua maalum iliyoombwa na wazee maalum pamoja na Watoto wateule kwenye viwanja vya "Tripple S" Bolisa ambapo kwanza wamejiombea wao wenyewe, kuombea mtaa na nchi yao na vilivyomo na dunia kwa ujumla na kuwaombea marehemu wao wote na marehemu wanaostahiki kote duniani.

Kilele cha dua hiyo kitakuwa saa tatu asubuhi siku ya Jumatano tarehe 11.6.2025 ambapo zaidi ya watu elfu kumi wanatarajiwa kualikwa.

Dua hiyo itaambatana na makongamano na mfululizo wa mihadhara na semina kuhusu Mazingira, Kujikwamua kiuchumi, Sayansi ya Ubunifu, tunu ya amani, tangamano baina ya wanadamu, sayansi ya maelezi na elimu ya familia.

Dua hiyo itatanguliwa na :-
1. Siku ya watoto
2. Siku ya wanawake
3. Siku ya Qur ani
4. Na Siku ya michezo

Kwenye kilele cha dua hiyo Tuzo kadhaa zitatolewa ikiwa ni pamoja na :-
1. Tuzo ya mwanamama msomaji wa Qur ani kwa Tajweed
2. Tuzo ya mwanafunzi wa k**e wa Shule ya sekondari msomaji mzuri wa Qurani kwa Tajweed
4. Tuzo ya mwanafunzi wa Sekondari wa kiume msomaji mzuri wa Qur ani kwa Tajweed
5. Tuzo ya Imamu bora.
6. Tuzo ya mzee msomaji mzuri wa Qur ani kwa Tajweed
7. Tuzo ya mtunzaji wa mazingira na mpandaji mzuri wa miti.

Misikiti na madrasa zote za halmashauri ya Kondoa zitaalikwa pamoja na viongozi wote wa BAKWATA na serikali kata zote za wilaya ya Kondoa wataalikwa kuhudhuria kilele cha dua hiyo.

Aidha viongozi wa BAKWATA na serikali wa mkoa wa Dodoma na wilaya zake zote wataalikwa pamoja na masheikh na viongozi wa BAKWATA na taasisi za kiislamu mikoani.

Kauli mbiu ya dua mwaka huu ni :-
"TUVUKE PAMOJA"

Wadau mbalimbali wanaombwa kushiriki kikamilifu kwenye dua hiyo pamoja na viambatanisho vyake
......

Dr. Harith Nkussa
Msemaji Maalum wa M***i
Jumapili 16.3.2025
Usongwi, Bolisa, Kondoa.

Photos from Rayyaan International's post 22/02/2025

USAJILI KIDATO CHA TANO ALGEBRA UMEANZA.

Taarifa maalum ya Mkuu wa Shule ya Sekondari Algebra ya Kigamboni mwalimu Walid Suleyman Gonja imesema Usajili wa wanafunzi wa kidato cha tano umeanza na kwamba nafasi za kuhamia kidato cha tano pia zipo.

Mwalimu Gonja amesema maadalizi yote kuwapokea wanafunzi wapya yamekamilika na kuwataka wazazi waendelee kuiamini shule hiyo na kuwaleta vijana wao ili wapate malezi mema na mazuri sana ya kidini na kujihakikishia ufaulu.

Amesema michepuo mbalimbali ya Lugha, Sanaa, biashara na sayansi inapatikana kwenye shule hiyo iliyoko Shangwe, Kigamboni.

Kwa maelezo zaidi piga sasa:

✳ 0715018089
✳ 0689627374
✳ 0786280141
✳ 0689489930
✳ 0769474602

21/02/2025

Hii hapa shule ya Algebra Secondari
Kigaboni

🔷 Algebra

Shule ya kiislamu Algebra, Chaguo bora kwa wazazi wanaojali

✳ 0715018089
✳ 0689627374
✳ 0786280141
✳ 0689489930
✳ 0769474602.

Naam mwanao anastahili ubora, ufaulu na malezi bora.

Kwa nafasi za masomo kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita UNAKARIBISHWA.

USAJILI WA KIDATO CHA TANO. UMEANZA RASMI

COMBINATIONS ZA SAYANSI, ARTS, LUGHA NA BIASHARA BILA KUSAHAU TAHASUSI MPYA ZA MASOMO YA DINI NA LUGHA YA KIARABU.

SHULE INAPOKEA WANAFUNZI WA KUTWA NA BWENI WAVULANA NA WASICHANA.

Photos from Rayyaan International's post 07/02/2025

Ukiwa Bolisa unapaswa kufanya mambo ya Bolisa na hasa ukuyaweza.

Usiku mwema.

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address

Dar Es Salaam
255