WADUKUZI 10 HATARI ZAIDI WA KOMPYUTA DUNIANI
Wadukuzi wanatumia maarifa yao ya kipekee kufikia au kupata taarifa nyeti kwa njia isiyo halali. Kutumia maarifa siyo kitu kibaya au kisicho halali, bali tatizo linaanza pale ambapo maarifa hayo yanatumika kuvunja sheria.
Wadukuzi hutafuta madhaifu kwenye mifumo mbalimbali ya kompyuta na kisha kuyatumia kuiba taarifa au kufanya uhalifu mwingine.
Kutokana na kukua kwa ulimwengu wa teknolojia ya intaneti, idadi ya wadukuzi imeongezeka sana. Wadukuzi mbalimbali wamekuwa wakiishangaza dunia kwa jinsi wanavyotumia maarifa yao ya kipekee kufanya matendo ambayo ni tishio.
Naamini ungependa kufahamu baadhi ya wadukuzi waliotisha zaidi duniani. Fuatilia makala hii nikujuze wadukuzi 10 hatari zaidi wa kompyuta.
1. GARY MCKINNON
GaryMnammo mwaka 2001, McKinnon mzaliwa wa Scotland alitumia maarifa yake ya msimamizi wa mfumo (system administration) wa kompyuta kuingilia mfumo wa kompyuta wa jeshi la Marekani. Alipoingilia mfumo huu alifuta mafaili muhimu na kupelekea hasara ya maelfu ya dola. Mdukuzi huyu alituhumiwa kwa kutekeleza udukuzi mkubwa kwa jeshi ambao haujawahi kutokea.
2. MICHAEL BEVAN na RICHARD PRYCE
BevanWadukuzi hawa kwa pamoja waliingilia kompyuta za jeshi la anga la Marekani, NASA, na NATO mnamo mwaka 1996 na kuhamisha na kufuta mafaili kadhaa. Tukio hili lilikaribia kusababisha vita kati ya Marekani na Korea kaskazini kutokana na kuvuja kwa taarifa za siri juu ya mpango wa nyuklia kwenye jeshi la anga la Marekani (USAF).
3. KEVIN MITNICK
Mitnick anafahamika kwa kuingilia mifumo ya simu na makampuni ya kompyuta pamoja na kubadili taarifa muhimu kwenye seva husika za kompyuta. Alikuwa akijihusika pia kuiba nywila (password) ili kuingia kwenye barua pepe kadha wa kadha. Mitnick alik**atwa mwaka 1995 na kush*takiwa kwenda jela miaka mitano. Jambo la kushangaza sasa Mitnick anaendesha kampuni ya kuwasaidia watu kujilinda na wadukuzi kwenye mtandao.
4. VLADIMIR LEVIN
Kwa kutumia maarifa yake ya udukuzi, Levin ambaye ni raia wa Urusi aliingia kwenye seva za benki ya Citibank na kuiba dola milioni 10 kutoka kwenye akaunti mbalimbali. Baadaye alik**atwa huko Uingereza, lakini Citibank waliweza kupata dola 400,000 tu kati ya milioni 10 zilizoibiwa.
5. MICHAEL CALCE
Calce alifahamika kwa jina la MafiaBoy. Akiwa mwanafunzi wa sekondari huko Quebec Canada, Calce alitekeleza aina ya udukuzi unaojulikana k**a DDoS attack kwenye tovuti maarufu k**a vile Yahoo, FIFA, Dell, Amazon, eBay na CNN. DDoS attack ni udukuzi ambao wadukuzi huzalisha maelfu au hata mamilioni ya watumiaji bandia wanaotoka kufikia tovuti fulani kwa wakati mmoja; kwa kufanya hivi tovuti husika huzidiwa kwa kushindwa kuwamudu na kuisababisha isipatikane.
Waathiriwa wa udukuzi huu wa Calce walishangaa jinsi udukuzi ulivyokuwa mkubwa, inakadiriwa kuwa udukuzi huu ulisababisha hasara zaidi ya dola bilioni moja duniani kote.
6. JEANSON JAMES ANCHETA
Ancheta aliweza kutengeneza mashine 500,000 za kutengenezea botnets; Botnets ni marobot ambayo hutumiwa kufanya DDoS attack. Hata hivyo vyombo vya dola ikiwemo FBI vilimk**ata na kumsh*taki k**a injinia mdukuzi anayetisha.
7. ADRIAN LAMO
Adrian Lamo alikuwa mdukuzi tofauti na wengine kwani yeye hakuwa na makazi maalumu. Alitumia maeneo ya uma yenye mtandao k**a vile intaneti cafe, migahawa n.k ili kufanya udukuzi wake. Kwa njia hii ilikuwa ni vigumu kumk**ata. Lamo pia alikuwa maarufu kwa kuwaonyesha wadukuzi wengine madhaifu mbalimbali kwenye mifumo ya kompyuta. Hata hivyo baadaye Lamo alik**atwa kutokana na kuhusishwa na Wikileaks.
8. OWEN WALKER
Walker alitumia jina la bandia la AKILL kutekeleza uvamizi kwenye tovuti na mifumo kadha wa kadha ya kompyuta. Mdukuzi huyu anafahamika sana kutokana na kirusi chake cha Akbot, ambacho kiliingia kwenye mifumo mbalimbali ya kompyuta na kusababisha uvamizi usioisha. Inakadiriwa kuwa Akbot imesababisha hasara ya zaidi ya dola milioni 26.
9. ALBERT GONZALEZ
Huyu ni mdukuzi wa Cuba anaedaiwa kuwa na uwezo wa kutisha sana wa kuiba kwenye kadi za kibenki na mifumo ya mashine za kutolea pesa (ATM) kwenye miaka ya 2000. Albert alitumia taarifa za wateja kwa njia isiyo halali kufanya miamala yenye thamani ya dola milioni 200 za kimarekani.
10. ASTRA
ASTRA ni kundi la wadukuzi linalofanya kazi hadi hii leo na bado halijabainika. Mamlaka mbalimbali zimekuwa zikilifuatilia kundi hili lakini bado hawajaweza kubainisha hasa ni wapi liliko. Wengine wadai liko China huku mamlaka za Ugiriki zikidai kuwa si kundi bali ni mwanamahesabu mwenye miaka 58 kutoka Ugiriki.
Astra inakadiriwa kuwa imesababisha hasara za zaidi ya dola za kimarekani milioni 360. Udukuzi maarufu wa kundi hili ni pamoja na kuiba mipango mbalimbali ya jeshi la Ufaransa ya silaha na ndege na kuiuza kwa watu wengine.
ELIMU Darasa
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from ELIMU Darasa, Education, Dar es Salaam.
19/01/2018
ZIJUE NEMBO MAARUFU AMBAZO ZIMEBEBA UJUMBE ULIOJIFICHA.
1. FedEX
Nembo ya FedEx ni moja ya nembo yenye ubunifu wa hali ya juu!!! Ukiiangalia kwa mtazamo wa haraka utaona rangi mbili tofauti, lakini utakapoiangalia kwa umakini zaidi unaweza kuona Mshale ulioundwa katikati ya herufi E na X unaowakilisha uwepo wa njia kwa kampuni kufikiri na kusonga mbele zaidi katika mafanikio.
08/01/2018
🔎SeARCH TRICKS
2. TO CHECK WEATHER
(Kuangalia hali ya Hewa )
Kuangalia hali ya hewa ya eneo lolote, unachotakiwa kufanya ni kuchukua simu yako iliyounganishwa Internet na kwenda sehemu ya "Google search" na kuandika neno "weather" likifuatiwa na jina la eneo unalotaka kujua hali ya hewa. Mfano : "weather dar es Salaam" au "weather nairobi" Utapata kujua hali ya hewa mara moja katika sehemu husika.
05/01/2018
Binadamu wote tumepewa utashi wa kujitambua sisi wenyewe lakini pia na ujio wa kila mmoja wetu hapa duniani kwa kazi yake Maalumu. Je, wewe binafsi umepata kujijua ni mtu wa namna gani?
30/12/2017
🚫 PRECAUTIONS WHILE USING SOCIAL NETWORK
↪Tahadhari Unapotumia mitandao ya kijamii
#1. PERSONAL IS PERSONAL
Jambo la kuanza nalo ni kuchukua tahadhari wakati unapokuwa katika mitandao ya kijamii. Hakikisha taarifa zako binafsi zinabaki kuwa siri yako. Hii inamaanisha kwamba hupaswi kuweka taarifa zako zitakazokuthibitisha uhalisia wako. Mfano barua pepe (E-mail) pamoja na namba za simu kamwe usiziweke wazi zikaonekana na watumiaji wengine wa mitandao ya kijamii kwasababu wadukuzi (Hackers) wanaweza kutumia "wizi wa utambulisho (Identity theft) kudukua akaunti yako.
Namba za akaunti ya benki, vitambulisho ni lazima vihifadhiwe mbali na mitandao ya kijamii.
30/12/2017
🔎SeARCH TRICKS
1. KNOWING LOCAL TIME 🕑
(Kujua Muda/Wakati)
Je unataka kujua muda katika maeneo mbalimbali? Ni rahisi sana kujua muda wa mahali popote ulimwenguni, unachotakiwa kufanya ni kuchukua simu yako na kuandika neno "Time" na jina la jiji katika utafutaji wa Google.
Kwa mfano unataka kujua muda wa New York kwa wakati huo unaenda kwenye Google search unaandika "time New York" au muda wa London unaandika "time London" ama hapa kwetu Tanzania unaandika "time Dar es Salaam" Utapata kujua muda mara moja .
29/12/2017
🌎 INTERESTING QUESTIONS.
01. WHY IS SEA WATER SALTY? ↪Kwanini maji ya bahari ni ya chumvi?
⬇
Maji ya bahari ni ya chumvi kwasababu ya uwepo wa pamoja wa chumvi za madini, kemikali na mabaki ya wanyama wa baharini hivyo hufanya maji kuwa na chumvi. Wingi wa madini haya hutoka katika mito ambayo hupeleka maji yake baharini. Vilevile hali ya hewa ya mawe na miamba chini ya bahari.
Sababu nyingine ya bahari kuwa na chumvi ni uwepo wa maziwa ya chumvi k**a vile "Great salt" na "Dead sea" (bahari ya Mauti) yote haya yana chumvi mara 10 zaidi ya chumvi ya bahari.
Pia wakati wa uvukizi (evaporation) Maji Safi hutoka baharini kwa njia ya mvuke na kutengeneza mawingu ambayo huanguka tena k**a mvua na kulisha mito hivyo kufanya maji yaliyosalia baharini kuwa chumvi.
26/12/2017
HOW IS A RAINBOW FORMED?
A true marvel of nature, it is a wonderful arc of the spectrum of colors VIBGYOR. A rainbow is usually seen when sunlight passes through rain drops and is scattered
into a band of colors. The light is reflected once from the back of the rain drop and then from the front, thus we see a curved rainbow.
25/12/2017
XMAS MAKEUP LOOKS.
Glittery lips
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Contact the school
Telephone
Website
Address
Opening Hours
| Monday | 09:00 - 17:00 |
| Tuesday | 09:00 - 17:00 |
| Wednesday | 09:00 - 17:00 |
| Thursday | 09:00 - 17:00 |
| Friday | 09:00 - 17:00 |