MZEE WA FACT

MZEE WA FACT

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from MZEE WA FACT, Education Website, Tanzanian, Dar es Salaam.

24/09/2025

You can fool some people sometimes,
But you can't fool all the people all the time.- "Bob Marley

Unaweza kuwadanganya baadhi ya watu kwa muda,
lakini huwezi kuwadanganya watu wote kila wakati.- "Bob Marley

20/09/2025

Madini ⬇️

Unaweza ukauvunja uaminifu wako ulioutengeneza kwa miaka 30 kwa ndani ya siku 1 tu, na bado ukahitaji zaidi ya miaka mitano kurekebisha ulipokosea ili uaminiwe tena na huenda isiwezekane kabisa 🫵

Uaminifu ni hazina kubwa sana kwenye ulimwengu huu wa sasa na hakuna chuo chochote kile duniani kinafundisha namna ya kuwa muaminifu.

K**a ni mfanyabiashara basi itumie hii k**a kanuni yako coz nowadays watu wana purchase bidhaa kwa sababu ya mtu fulani (brand)

My take; ⬇️

- Tuishi kwa kuzingatia msingi mkuu wa maisha,
- Punguza mikusanyiko na watu then jitahidi kuishi maisha yako 🫵
- K**a hautaweza kuwa daraja basi jitahidi usiwe ukuta 👐

All in all "We only live once", ukipata nafasi ya maisha usiache kuishi 🙏

18/09/2025

Katika miaka tuliyopo biashara hazishindani kwa bei pekee ila zinashindana katika kujenga mahusiano na wateja ⬇️

●Sikiliza wateja wako
●Wape huduma bora
●Jali matatizo yao hata baada ya mauzo
●Wape thamani zaidi ya bidhaa wanazonunua

Bila mahusiano, biashara zinadumaa 🫵

18/09/2025

Memories ⬇️

Miaka kadhaa iliyopita kumbukumbu zinanirudisha nipo darasani

Siku hiyo ilikuwa wazazi wamekuja shuleni kupokea ripoti za watoto wao na ilikuwa ni wito kutoka kwa walimu

Ripoti zilikuwa zinatolewa statistical yaani kuanzia wa kwanza mpaka wa mwisho tena mbele ya wazazi na anayepokea ni mzazi 🤔

Darasani tulikuwa wanafunzi 35 tu na mimi nilishika nafasi ya 30 kati ya hao 35, katika hao wa 5 niliowapita kuna wawili tulifanana marks (alama) kwa maana hiyo niliwapita wanafunzi 3 tu 😀

Ripoti ilipokelewa na mzazi na mara baada ya kupokea ripoti nilimuona akifurahi na akanipatia noti ya shilingi elfu 5, kwa wakati huo ni hela nyingi mno 🫵

Walimu walimshangaa sana kiasi cha kuleta kejeli na ndipo mzazi wangu aliwajibu "mimi siangalii wangapi wamempita/kuwapita ila ninachoangalia matokeo aliyopata muhula uliopita na huu uliopo amefanya nini" 🔨

My take; nilichojifunza ni kwamba unatakiwa kufocus na malengo yako pasipo kutazama mafanikio ya wenzio, 🫵
Katika game la maisha hutakiwi kushindana na mtu ila unatakiwa kutazama malengo yako tu, wapi unakwenda na si kutazama ya wenzio 💯

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address

Tanzanian
Dar Es Salaam