Maranatha Faith Assembly-Siloam Kawagware.

Maranatha Faith Assembly-Siloam Kawagware.

Share

A Christian based bibilical teaching in Kiswahili. A religious group of Marantha Faith Assembly Kawagware -Bungoma Region.

27/06/2025

Zaburi 30:4
Mwimbieni BWANA zaburi,
Enyi watauwa wake.
Na kufanya shukrani.
Kwa kumbukumbu la utakatifu wake.
Sing unto the LORD, O ye saints of his, and give thanks at the remembrance of his holiness.

Thank God for being alive, for all the good things you are experiencing,Let God's Will prevail.

For the Love of God 19/06/2025

Join our Whatsapp group for daily spiritual guidelines regardless if your church domain.

For the Love of God WhatsApp Group Invite

07/08/2024

Preachings by Pastor Morris Juma -Nairobi
BARAKA YA KUTOKA NA KUJIUNGA NA MFUMO WA KIMAONO (VISION CONNECTIN & NETWORK)
Mistari ya Neno
Luka 1:39-56
Yohana 1:29-34
• kila mabadiliko yanayotokea kwenye Maisha yako yana kusudi lake, yanakutoa Mahali fulani na kukupeleka mahali pengine.
• No matter what happens to you, Mungu anakuwazia mema.
• kuna baraka ya kutoka ambayo inakutengenezea Vision Connection and network.
• lli upate baraka ya kutoka kuna Mahali lazima utoke. Hata mtoto akiwa tumboni hawezi kuwa na hii Baraka mpaka atoke tumboni kwa mama yake.
Kutoka kitabu cha Yohana na Luka:
• Mariamu aliposhindwa kueleweka na familia, Mariamu aliamuakutoka akakutana na Elizabeth, Mariamu alipomsalimia Elizabeth akajazwa Roho Mtakatifu.
° Hiki kitendo cha Elizabeth kujazwa kilimuondolea Mariamu Self-doubting juu ya ule ujauzito aliokua ameubeba akaamini kweli mimba aliyobeba siyo ya kawaida, akaamini maneno aliyoambiwa na malaika kuwa Roho Mtakatifu atakujilia juu yako.
° Unaeeza ukawa na mashaka sana juu yako au maamuzi yako lakini unahitaji mtu mmoja tu wa kukuambia yuo are very right.
° k**a kwenye Maisha yako haujafikia Mahali ukawa na Self -doubting basi wewe bado haujawa na maono.
• Yesu na Yohana walikua Vision Connection tangu wakiwa tumboni. Hii Connection ndio ilimsababisha Yohana amtambulishe Yesu.
VISION & NETWORK
• Ndio kitu kinachohitajika zaidi kwenye Maisha yako
° Usitafute fedha, tafuta network na Connection. Hakuna kitu kinachoweza kuenda bila ya kuwa na Connection unahitaji Watu ili ukamilishe maono yako.
Mariamu na Elizabeth walitengeneza network kwa kusalimiana ni muhimu kusalimiana na watu na kuongea nao unapokutana nao. Ukishamaliza maombi ni lazima uhakikishe unatengeneza network.
Note: Network na Connections ulizonazo kwa watu zinalindwa kwa gharama ya adabu.
Vitu vya muhimu vya kufanya ili kutengeneza na kulinda Network na Connections na watu.
1. Usiombe pesa
2. Usitafute mahusiano ya kipuuzi. Na mtu mwenye Connection.

09/01/2023

Bwana Yesu asifiwe
Mwaka mpya
Week na next week upto 15the January
Ni kuombea walengo na matarajio yetu
Ya 2023
Kutakasa mwaka huu,siku kwa Siku,wiki kwa wiki na mwezi kwa mwezi kwa Damu ya Yesu Kristo
Jitamkie jambo njema
Omba kusudio ya Mungu lijidhihirishe mwaka huu
Blessed2023
May you HARVEST something great from the Kingdom of God.
Amen amen amen

12/12/2022

Bible verse of the week

Mathayo 15:13
[13]Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang’olewa.
But he answered and said, Every plant, which my heavenly Father hath not planted, shall be rooted up.

Kuna vitu vimepandwa ndani yetu,kwenye Familia,kwenye mahusiano ,kwenye ndoa,kwenye Ndoa,kwenye afya,pando ambalo asili yake si Mungu,LITANGOLEWA....
NGOA
pando.LA magonjwa
Pando LA usingizi Wa rohoni
Pando LA mateso
Pando LA mauti
Pando la uharibufu Wa akili,biashara,ndoa au huduma
Ingolewe ktk jina LA Yesu.
Tuwe huru Leo ktk jina LA Yesu...

Amen Amen Amen

12/12/2022

Yohana 9:1-7
[1]Hata alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa.
And as Jesus passed by, he saw a man which was blind from his birth.
[2]Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu?
And his disciples asked him, saying, Master, who did sin, this man, or his parents, that he was born blind?
[3]Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake.
Jesus answered, Neither hath this man sinned, nor his parents: but that the works of God should be made manifest in him.
[4]Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi.
I must work the works of him that sent me, while it is day: the night cometh, when no man can work.
[5]Muda nilipo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu.
As long as I am in the world, I am the light of the world.
[6]Alipokwisha kusema hayo, alitema mate chini, akafanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu tope za macho,
When he had thus spoken, he spat on the ground, and made clay of the spittle, and he anointed the eyes of the blind man with the clay,
[7]akamwambia, Nenda kanawe katika birika ya Siloamu, (maana yake, Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi anaona.
And said unto him, Go, wash in the pool of Siloam, (which is by interpretation, Sent.) He went his way therefore, and washed, and came seeing.

01/12/2022

Vita baada ya kumiliki
2 MAMBO YA NYAKATI 20
Vita dhidi ya Edomu
1Baada ya muda, majeshi ya Moabu na Amoni pamoja na baadhi ya Wameuni, waliivamia Yuda. 2Watu kadhaa walikuja wakamwambia mfalme Yehoshafati, “Jeshi kubwa limekuja kukushambulia kutoka Edomu, ngambo ya Bahari ya Chumvi. Tayari wamekwisha teka Hasason-tamari.”
YEhoshafati alichukuwa hatua ya kumwomba Mungu wakati jeshi kubwa la vita lilipokuwa limepanga maangamizi juu yao,alimkumbusha Mungu ukuu wake aliowafanyia babu zake na umiliki aliowapatia ktk nchi geni!
mchana wa leo na usiku wa leo, Omba Mungu akupiganie wewe na familia yako, na kanisa na nchi yetu, kuna wakuu wa giza wamekusanyika tayari kutuangamiza, wamejipanga kwa silaha mbalimbali,maarifa ya hali ya juu, na lengo lao ni kuleta uharibifu, kunyakuwa tulichomiliki, kutenganisha familia na kuweka mipaka kwa huduma, chukuwa nafasi mkumbushe mungu umbali alikutoa, tangu Jan hata sasa ni Dec, muujiza na baraka na zaidi ya yote uhai ulio nao, Mwambia nguvu sisi hatuna, wala mamalaka ya kupigana yeye mwenyewe atupiganie, Yehoshafati alieka tumaini kwa Bwana,nasi inatupasa kufanya hivo

12/11/2022

UWE salama katika Jina la Yesu.
Mwanzo 19:10-11
[10]Lakini wale watu wakanyosha mikono yao, wakamwingiza Lutu kwao nyumbani, wakaufunga mlango.
[11]Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakachoka kwa kuutafuta mlango.

Malaika Kwa Sura ya kibinadamu, wakaingia mji WA Soma,wakati Lutu alikuwa zamu,..( nawe baraka zimiminike wakati uko zamu..uko macho, yaani mambo mema yatokee ukiwa ktk Jina la Yesu) walipoingia kwake (Lutu) usiku wanamji WA Sodoma,wakazunguka nyumba yake na hata kutaka kuuvunja mlango ili wawatendee wale wageni (Malaika) uovu WA usinzi...lakini.....
Wakanyosha mkono..wakamwigiza Lutu Kwa nyumba na kufunga mlango...
Leo jioni hii Bwana atume Malaika akuweke salama, ndiyo wanapanga kushambulia huduma yako,au afya yako,au familia yako,labda KAZI ya mikono yako, ila Bwana atakuokoa Kwa mkono wake ..atakuweka mahali salama, na kufunga kila milango ya uharibifu,milango ya mateso,milango ya aibu, milango ya balaa,milango ya mahangaiko na uchungu, na milango ya utumwa ktk Jina la Yesu...
Kisha Malaika wale,walifanya wale waliozunguka nyumba ya Lutu vipofu,walione mlango tena...
Mlango ambayo Bwana atakuwekea WA usalama wako, Yule mateso hatauona tena, wawe vipofu Kwa Jina la Yesu, njia zao ziwe Giza na utelezi ktk Jina la Yesu..vikao walivyokaa vitaharibika mara Saba ktk Jina la Yesu, uharibu wao haitatokea kamwe ktk Jina la Yesu..matukio ya kichawi ya uovu,hasara,uchungu,na aibu tunayaweka upofu ktk Jina la Yesu...
Waliojiandaa wakuone ukilia, watangoja Sana maana,uwapo upande wetu,semeni,Nani awezaye kutushinda!?? Mungu ni ngome yetu tena msaada wetu ,na tumefanywa washindi Kwa Jina la Yesu..
UWE salama ,na familia yako na Mali yako ktk Jina la Yesu!!
Amen amen amen!🙏🏿🤍

06/11/2022

Kwa sababu umeonewa,Mungu ameamua kutoka hukumu ya haki Kwa ajili yako,Kwa sababu umenyanyazwa,Mungu hatanyamaza tena, alivyoona mateso ya Waisraeli kule Misri, na akawaokoa kutoka utumwani, basi ni wakati wako, uibuke mshindi ktk Jina la Yesu
Ni wakati wako ustawi kibiashara
Ni wakati wako kuinuliwa kihuduma,ni wakati wako ushuhudie utukufu WA Mungu,watakao teta nawe Mungu atateta NAO, wanapanga Vita juu yako, BWANA atapigana NAO,ktk Jina la Yesu!!

06/11/2022

Next week's verse
Zaburi 12:5
[5]Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge,
Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji,
Sasa nitasimama, asema BWANA,
Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.
Bwan Yesu asifiwe..
Ni wakati Mungu atashughulikia Hali yako
Umeonewa kwenye familia,au kazini na hata wengine kwenye huduma,au labda unaungua ,umepungukiwa Kwa namna Fulani,Mungu asema atakuweka SALAMA.
UWE salama ktk Hali ya mahusiano,au ndoa,UWE salama kazini, chochote unachopanga kufanya kiwe salama ktk Jina la Yesu.
Mungu akulinde uondokapo na urudipo ktk Jina la Yesu
Kuwa salama,ni kuwa na uhakika WA ulinzi WA Mungu, na aliye Chini ya mabawa ya Mungu,hata adui ainuke kulia au kushoto ataibuka mshindi...UWE mshindi wiki ijayo ktk Jina la Yesu.
Amen amen amen

05/11/2022

Verse of the day
Marko 16:19
Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.
Be blessed all

Kuna tukio hutokea baada ya kusema, Mungu akasema.....yakatokea...jihadhari na maneno yako,
Wakawatuma Kwa Yesu ili wamnase na maneno yake ,lakini hawakufaulu, kuwa majini Sana na maneno yako!!

Yesu alipeana mwelekeo Kwa wanafunzi,akawapa ahadi ya kuwa NAO,akapewa mbinguni, week kesho, Mungu atimize ahadi yake juu ya huduma yako, ahadi ya uponyaji,ahadi ya mafanikio,ahadi ya kuwa nawe, na uinuliwe juu ya vyote,sema Tu BWANA NIKO HAPA,USINIACHE.
amen amen amen

21/10/2022

Katikati ya Hali unayopitia Yesu atajitokeza wakati wake ukiwadia, wanafunzi walikumbwa na mawimbi,wakawa na hofu lakini Yesu akawajia akitembea juu ya maji,akatulia mawimbi,wakavuka ng'ambo salama...
Ondoa hofu na wasiwasi,wacha mawazo mengi mtumainie BWANA!
Akamwambia Yoshua,usiogope ,kuwa shujaa maana nitakuwa pamoja nawe ..na hakika Mungu WA Majeshi alikuwa naye siku zote
Yesu akawambia wanafunzi musiogope, wengi tunaogopa Sana kukataliwa,kushindwa,n.k lakini Neno la Mungu ni la kutumainia,ni la nguvu,laokoa,latetea,jifunze kumsikiza Mungu na kwenda sawasawa na kauli yake.
Ktk Jina la Yesu
Mwl pstr Wafula
AMEN amen amen

Want your school to be the top-listed School/college in Nairobi?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Website

Address


Kawagware
Nairobi