*KINACHOSEMA _HASA_ NI MOYO, SIO MDOMO*
✍️Abdillah Kitota (MMEDSC)
Mpendwa msomaji, unaweza kushangaa kusikia kwamba *kinachosema _hasa_ ni moyo, siyo mdomo.* Ndiyo! Tena siyo hivyo tu, bali pia *kinachosikiliza _hasa_ ni moyo, siyo masikio, na kinachoona _hasa_ ni moyo, siyo macho.* Hii ni kutokana na Mola wetu Mlezi Mtukufu alivyobainisha kwenye Qur'an; na hata alivyotuonesha kupitia ishara za tiba ya nyurolojia.
Wakati Mola wetu Mlezi Mtukufu akithibitisha kile alichokisema Mtume Muhammad Swalla Llaahu 'alayhi wasallam kuhusu alipomchukua kwenye safari yake ya *_mi'iraj_* , alisema:
مَا كَذَبَ الْفُؤَادُ مَا رَأَىٰ
*Moyo [wake] haukusema uwongo uliyo yaona (Qur'an, 53:11).*
Kimsingi, pamoja na kwamba kwa picha ya nje kauli hiyo inaonekana kubainisha tu kuwa Mtume Swalla Llaahu 'alayhi wasallam hakusema uongo aliyoyaona huko kwenye hiyo safari yake, *lakini vilevile imekuja kwa umaalumu sana.*
Inaelezea jambo kubwa la safari ambayo Mtume Swalla Llaahu 'alayhi wasallam alioneshwa ishara nyingi mno kubwa kubwa, *na imetumia muundo wenye mazingatio makubwa sana kwa mwenye kuzingatia.*
Kwa kusema kwake moyo haukusema uongo uliyoyaona, ni dhahiri shahiri kwamba, tofauti na wengi katika watu wanavyoona _kikawaida_ kuwa mdomo ndiyo unasema na macho ndiyo yanaona, imekuja *_kimbinu_* [kiuumbaji] zaidi kwa kubainisha kwamba, *kinachosema _hasa_ ni moyo, na kinachoona _hasa_ ni moyo.*
Hivi ndivyo alivyotuonesha kupitia ishara za tiba ya nyurolojia. _Kiuhalisia_, masikio na macho ni k**a *media [kipokeo na kipitisho]*; kwayo taarifa kutoka nje *zinapokewa na kupitishwa* mpaka kwenye moyo na ubongo ambapo hufasiriwa [na kuhifadhiwa], kisha *mrejesho [taarifa iliyofasiriwa]* ndiyo unarudishwa kwenye masikio na macho, *kisha ndiyo unatenda, ikiwemo kusema n.k.*
Hata hivyo, kwenye kauli hiyo umetajwa moyo peke yake kwa sababu; kwa mujibu Mola wetu Mlezi Mtukufu alivyotuonesha kupitia ishara katika tiba ya nyurolojia, moyo huushinikiza ubongo ili utoe amri ya mwisho ya kutenda, *ikiwemo kusema.*
Kuhusu muujiza huu, utaona pia imekuja aya nyingine inayosema kwamba:
أَفَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَتَكُونَ لَهُمْ قُلُوبٌ يَعْقِلُونَ بِهَا أَوْ آذَانٌ يَسْمَعُونَ بِهَا ۖ فَإِنَّهَا لَا تَعْمَى الْأَبْصَارُ وَلَٰكِن تَعْمَى الْقُلُوبُ الَّتِي فِي الصُّدُورِ
*Je! Hawatembei katika ardhi ili wapate kuwa na nyoyo zao za kuzingatia, au masikio ya kusikilia? Kwani hakika si macho yanayo pofuka, lakini zinazo pofuka ni nyoyo ziliomo vifuani (Qur'an, 22:46).*
Hivyo, tunaposikiliza, tunapotazama na tunaposema tuzingatie kwamba kinachosikiliza, kinachotazama na kinachosema _*hasa*_ ni moyo. Tunakumbushana kuwa makini na tunachosikiliza, tunachotazama na tunachosema; kwa kuwa masikio, macho na mdomo vipo pale k**a *media* ya *kupokea na kupitisha* taarifa tunazosikiliza, tunazotazama na tunazosema kutoka nje na kuzituma kwenye moyo na kupokea amri kutoka kwenye moyo baada ya moyo kuzifasiri taarifa hizo.
Yaani, *garbage in, garbage out [ukiingiza taarifa chafu zinatoka taarifa chafu].*
Lakini vilevile jina la moyo lililotumika kwenye kauli hiyo *[fuad]* linabainisha hali ya kihisia ya moyo wa Mtume Swalla Llaahu 'alayhi wasallam wakati huo ametoka kwenye safari hiyo. *Moyo wake ulikuwa kwenye hali ya hisia kali sana za tafakuri na mazingatio kutokana na uliyoyaona.* Tafsiri hii ni kutokana na tafsiri ya neno *fuad* k**a ilivyobainishwa kwenye kamusi kongwe ya Ibn Manzur *[Lisan Al 'Arab].* Kwamba, limetokana na neno *fua'ad* lenye maana *joto kali [extreme heat].*
Yaani, kwa muhtasari, kutokana na kauli hiyo, kinachokusudiwa kubainishwa ni muujiza mkubwa, *na muundo wa kauli uliotumika ni ya kimuujiza pia.*
Kwa nyongeza, hayupo mwanadamu aliyeishi karne ya 7 wakati Qur'an inashuka angeliweza kusema kauli hiyo; *isipokuwa yule tu anayepokea wahyi [ufunuo] kutoka kwa aliyemuumba mwanadamu.*
Ishara za Kimaumbile katika Qur'an na Sunnah
Ishara za uwepo na utukufu wa mola wetu mlezi Allah s.w zama hizi za sayansi na technology
31/03/2025
*ENYI MLIO AMINI! MCHENI MWENYEZI MUNGU NA SEMENI MANENO YA SAWASAWA*
✍️Abdillah Kitota (MMedSc)
Mpenzi msomaji, tugeukie katika aya hizi ambazo ni maarufu sana; *hususan katika hotuba.* Mola wetu Mlezi Mtukufu anasema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا
*Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu na semeni maneno ya sawasawa (Qur'an, 33:70).*
يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَالَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَمَن يُطِعِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا
*Apate kukutengenezeeni vitendo vyenu na akusameheni madhambi yenu. Na anaye mt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, bila ya shaka amefanikiwa mafanikio makubwa (Qur'an, 33:71).*
Katika aya hizo, *_baseline_ [msingi]* imewekwa katika aya ya kwanza [ya 70]. Nayo ni *kumcha Mola wetu Mlezi Mtukufu na kusema maneno yaliyo sawasawa.* Na *matokeo* ya *_baseline_* hiyo yamewekwa katika aya ya pili [ya 71]. Nayo ni *kutengenezewa matendo yetu [tabia/maadili yetu kwa ujumla] na kusamehewa dhambi zetu.*
Hivyo, aya hizo zimeainisha kwamba, *_baseline_* ya kutengenezewa matendo yetu na kusamehewa dhambi zetu ni *kumcha Mola wetu Mlezi Mtukufu na kusema maneno yaliyo sawasawa.*
Neno la Kiarabu *ttaquu [mcheni]* lililotumika kwenye aya ya kwanza limetokana na neno *taqay* lenye maana ya *kuhofu [hususan kumhofu Mola wetu Mlezi Mtukufu];* tazama kamusi ya Hans Wehr. Aidha, *statement* ya pili kwenye hiyo aya ya pili [ya 71] imedhihirisha maana ya hofu hiyo. Nayo ni *kumtii Mola wetu Mlezi Mtukufu na Mtume wake [kwa kutekeleza aliyoyaamrisha na kuyaacha aliyoyakataza].*
Al Imam Ibn Kathir katika *Tafsir Al Qur'an Al 'Adhwim* anasema, kusema maneno ya sawasawa ni *kusema maneno ya kweli; ya moja kwa moja, bila kupotosha.* Yaani, muumini amepewa majukumu mawili makubwa: (1). *Amche Mola wake Mlezi Mtukufu.* (2). *Aseme maneno yaliyo sawasawa.* Yaani, asiishie tu kumcha Mola wake Mlezi Mtukufu; wakati kwenye *taasisi na jamii kwa ujumla* mambo yanaharibika. Vilevile, *_asimamie haki [ya Mola wake Mlezi Mtukufu na ya waja wake]_*; kwa kusema maneno yaliyo sawasawa. _Kusema maneno yaliyo sawasawa ndiyo kutengeneza *taasisi na jamii kwa ujumla.* Kinyume chake ni ufisadi; na inaweza kuathiri hata huo ucha-Mungu wake._
Vilevile, Al Imam Ibn Kathir anasema, kutengenezewa matendo yetu ni *_kutuongoza_ tutende matendo aliyoyaridhia katika njia yake.*
Hata hivyo, baadhi ya watu wanaweza kudhani kwamba, *ukimcha Mola wetu Mlezi Mtukufu na ukasema maneno ya sawasawa Mola wetu Mlezi Mtukufu anakutengenezea [anakuongoza] matendo yako yanakuwa mema katika njia yake* bila kuzingatia kwamba hili ni suala la qadar [makadirio] ya kimaumbile.
Kwa mujibu wa aya zingine nyingi zinazohusiana na matendo ya kicha-Mungu; mathalan Qur'an, 29:45 inayobainisha kwamba Swala inamzuia mtu kutenda matendo machafu na maovu katika njia ya Ibilisi, kutengenezewa [kuongozwa] huko kwa matendo yetu baada ya kumcha Mola wetu Mlezi Mtukufu na kusema maneno yaliyo sawasawa kumewekwa juu ya misingi ya kimaumbile. Kila kitu ni kwa mujibu wa qadar, na k**a tulivyosema, hii ni katika qadar za kimaumbile. *A well predetermined measure of submission.*
Hii inamaana kwamba, kumhofu Mola wetu Mlezi Mtukufu kwa kufuata aliyoyaamrisha [na kuacha aliyoyakataza] ni jambo ambalo ni *compatible [ni sambamba au ni kulingana]* na qadar ya kimaumbile ya miili yetu.
Ni kuufundisha mwili; *kupitia mifumo ya kimaumbile aliyoiinstall juu na ndani ya miili yetu,* kutenda matendo mema katika njia ya Mola wetu Mlezi Mtukufu. Moyo unafundishwa ili uushinikize mwili mzima; *kupitia ubongo,* utende matendo mema katika njia ya Mola wetu Mlezi Mtukufu.
Hivyo basi, kuongokewa matendo yetu katika njia ya Mola wetu Mlezi Mtukufu *siyo jambo kinalodondoka k**a baraka moja kwa moja kutoka mbinguni*; japokuwa Mola wetu Mlezi Mtukufu hashindwi kufanya hivyo.
Bali ni jambo linalotegemea *_baseline_* hiyo [makadirio hayo], na ndiyo inakuwa sababu ya Yeye kutusamehe dhambi zetu; *kisha tukifa katika hali hii ndiyo yanakuwa mafanikio halisi.*
Kwa msingi huu, ili kupata matokeo hayo ya kuongoka kwa matendo yetu [na kusamehewa dhambi zetu], kufuata yaliyoamrishwa na Mola wetu Mlezi Mtukufu na kuyaacha aliyoyakataza kunatakiwa kuwe kwa *JUHUDI NA UFANISI* wa kiwango cha juu sana; *ili kukidhi [au kufikia threshold ya] makadirio hayo ya kimaumbile na kutoa matokeo hayo.*
_*SIKU ROHO YANGU ITAKAPOKUWA INATOLEWA: TAFAKURI YANGU*_
✍️Abdillah Kitota (MMEDSC)
Ndugu msomaji, hakuna siku itapita bila kutafakari juu ya roho yangu. *NATAFAKARI:* roho yangu ni kitu gani? Sayansi yake ikoje? Ipo sehemu gani ndani ya mwili wangu? Imeenea mwili mzima au kuna sehemu fulani ya mwili imewekwa na inasambaza athari yake katika kila sehemu ya mwili k**a ilivyo kwa moyo? Inafananaje? Inashikika au haishikiki? Ni sehemu ya malighafi tuliyoumbiwa; k**a ilivyo kwa udongo na maji, au ni kitu kingine kabisa? Vipi itakavyokuwa ikitolewa mwilini mwangu? Nitahisi uchungu wa namna gani k**a inavyosemwa?
Maswali haya na mengine mithili ya haya yamekuwa yakinirejesha kwenye Qur'an na Hadithi/Sunnah kutazama kuwepo, ukubwa na utukufu wa Mola wangu Mlezi juu ya jambo hili.
Mara nikakutana na Hadithi iliyosimuliwa na sahaba Abdullah Ibn Mas'ud (Radhiya Llaahu 'anhu) na kuripotiwa katika rejea za Hadithi zinazotegemewa; zikiwemo sahihi mbili. Katika Hadithi hii, Abdullah Ibn Mas'ud (Radhiya Llaahu 'anhu) anasimulia:
Nilipokuwa natembea na Mtume Swalla Llaahu 'alayhi wasallam katika moja ya mashamba ya Madina huku amejiegemeza kwenye buwa la mtende, likapita kundi la Wayahudi huku wakisemeshana wao kwa wao: *muulizeni kuhusu roho,* wengine wakasema: msimuulize atawajibu majibu ambayo hayatawaridhisha. Baadhi yao wakasema: tutamuuliza. Hivyo, mmoja kati yao akasimama na kumuuliza: *O Abul Qasim roho ninini?*
Mtume Swalla Llaahu 'alayhi wasallam akakaa kimya kwa muda. Kisha akasoma: *Na wanakuuliza khabari za Roho. Sema: Roho ni katika mambo ya Mola wangu Mlezi. Nanyi hamkupewa katika ilimu ila kidogo tu (Qur'an, 17:85).*
Kwa majibu hayo kutoka kwa Mola wetu Mlezi Mtukufu, imenibainikia kwamba, *mwanadamu hakupewa elimu ya kufahamu roho ninini hasa [ni kitu gani na sayansi yake ikoje]?*
Niliposonga mbele kuisoma Qur'an zaidi na maelezo yaliyotolewa na baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu [ambayo huenda nayo yanarejea nyuma mpaka kwa Mtume Swalla Llaahu 'alayhi wasallam], ikanibainikia kwamba, hata hivyo, tumebainishiwa ishara chache sana zinazodokeza kuhusu roho, *lakini siyo zinazobainisha au kudokeza roho ninini hasa, na sayansi yake ikoje?*
Pia ikanibainikia kwamba, roho siyo kitu cha kiumbo k**a vilivyo vitu vingine vya kiumbo; *mathalan udongo na maji,* ambavyo Mola wetu Mlezi Mtukufu alivitumia k**a malighafi [sababu] ya kumuumba mwanadamu. Kwa maneno mengine, roho siyo *mwili wa kiumbo (physical body)* [uliojengwa kwa mwili na viungo vyake, na sehemu ya mwili isiyoshikika ambayo ni zao la moyo; yenye uwezo wa kuusukuma mwili kwenye halali au haram (tafsiri nyingine ya nafsi)], *bali ni mwili wa kiroho [spiritual body] usioweza kuonekana hata kwa mashine maalumu za kuuscreen mwili.* Kwa mujibu wa tafsiri nyingine ya nafsi [ya uwakilishi binafsi]; hasa nilipoisoma Qur'an, 32:9, imenibainikia kwamba, nafsi ya mwanadamu imejengwa kwa vitu vikuu viwili: *mwili wa kiumbo na mwili wa kiroho.*
Kwa kuwa roho ni *mwili wa kiroho,* huenda ndiyo sababu Mola wetu Mlezi Mtukufu anapodokeza kuhusu kitendo cha kumpulizia roho mwanadamu, anainasibisha roho na Yeye Mwenyewe moja kwa moja; *tofauti na anavyoeleza kwa uwazi kabisa kuhusu malighafi hayo aliyoyatumia kumuumba mwanadamu.* Mathalan, kuhusu udongo, imekuja katika Hadithi iliyosimuliwa na Abdullah Ibn Mas'ud (Radhiya Llaahu 'anhu) na maswahaba wengine kwamba, *ulichukuliwa kutoka sehemu mbalimbali za ardhi.* Suala la roho kuwa kitu cha kiroho ambacho Mola wetu Mlezi Mtukufu anainasibisha na Yeye Mwenyewe limenibainikia kwa uwazi kabisa kupitia aya zilizoainishwa hapa chini:
فَإِذَا سَوَّيْتُهُ وَنَفَخْتُ فِيهِ مِن رُّوحِي فَقَعُوا لَهُ سَاجِدِينَ
*Na nitakapo mkamilisha na KUMPULIZIA ROHO INAYO TOKANA NAMI, basi muangukieni kwa kumt'ii (Qur'an, 38:72).*
ثُمَّ سَوَّاهُ وَنَفَخَ فِيهِ مِن رُّوحِهِ ۖ وَجَعَلَ لَكُمُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَالْأَفْئِدَةَ ۚ قَلِيلًا مَّا تَشْكُرُونَ
*Kisha akamtengeneza, na AKAMPULIZIA ROHO YAKE, na akakujaalieni kusikia na kuona, na nyoyo za kufahamu. Ni uchache mnavyo shukuru (Qur'an, 32:9).*
فَإِذَا سَوَّيْتُهُ وَنَفَخْتُ فِيهِ مِن رُّوحِي فَقَعُوا لَهُ سَاجِدِينَ
*Basi nitakapo mkamilisha na NIKAMPULIZIA ROHO YANGU, basi mumwangukie kumsujudia (Qur'an, 15:29).*
Ishara nyingine iliyonibainikia inayodokezwa kwenye aya hizo ni kwamba, roho imetajwa k**a kitu cha mwisho *kuwekwa* ndani ya mwili wa mwanadamu *baada ya mwili wa mwanadamu kukamilika kuumbwa.*
Al Imam Ibn Kathir katika kitabu chake *Qiswasw Al Anbiya* ameeleza namna roho ya baba yetu Nabii Adam ('Alayhis salaam) ilivyowekwa. Kwamba, ilianza kuingia kichwani, akapiga chafya, kisha malaika wakamwambia sema alhmdulillah, akasema alhamdulillah, Mola wetu Mlezi Mtukufu akamwambia: Mola wako Mlezi Amekurehemu. Roho ilipofika machoni, akaangalia matunda ya peponi, ilipofika kwenye fumbatio [abdomen] akapata hamu ya kula, akaruka haraka kufuata chakula kabla roho haijafika miguuni, ili ale matunda ya peponi. Kisha Al Imam Ibn Kathir akanukuu Qur'an, 21:37 ambapo Mola wetu Mlezi Mtukufu amesema: *mwanadamu ameumbwa na haraka.*
Nikaendelea kubainikiwa zaidi nilipoirejea Hadithi ya Abdullah Ibn Mas'ud (Radhiya Llaahu 'anhu); ambayo nayo ni muttafaqun 'alayhi, inayobainisha hatua za makuzi na maendeleo ya mwanadamu ndani ya mfuko wa uzazi mpaka kwenye kuandikiwa yale *mambo manne [matendo, ajali, riziki, na mnyonge au mbarikiwa].* Katika Hadithi hii, kitu cha mwisho pia kutajwa ni kupuliziwa roho.
Ikanibainikia pia kwamba, suala la roho ya baba yetu Nabii Adam ('Alayhis salaam) na roho zetu [watoto wake] *kuwekwa* mwishoni kabisa baada ya kukamilika kuumbwa, linadokeza ishara nyingine kwamba, roho ndiyo iliyokadiriwa kuwa sababu ya maisha halisi ya seli, makundi ya seli [tishu], viungo na mifumo yote ya mwili [ukiachana na reflex]. Kwa maana hii, huenda roho imeenea mwili mzima.
Ikanibainikia pia kwamba, ishara nyingine kuhusu roho inayodokezwa ndani ya Qur'an ni *kuhusu kutolewa kwake.* Qur'an inadokeza kwamba, roho inatolewa kwa muundo wa *kutokea chini kuja juu [bottom to the top]*; kinyume na roho ya baba yetu Nabii Adam ('Alayhis salaam) ilivyoingizwa *[juu kuja chini; top to the bottom].* Aya zifuatazo zinalibainisha hili:
كَلَّا إِذَا بَلَغَتِ التَّرَاقِيَ
*La, hasha! (Roho) itakapo fikia kwenye mafupa ya koo (Qur'an, 75:26).*
فَلَوْلَا إِذَا بَلَغَتِ الْحُلْقُومَ
*Yawaje basi itakapo fika roho kwenye koo (Qur'an, 56:83).*
Katika tafsiri ya Qur'an, 75:26, nikakuta kwamba, Al Imam Ibn Kathir anasema: *[wakati wa kifo] roho itavutwa nje ya mwili wako mpaka itafika kwenye mifupa ya koo [kabla ya kutolewa nje kabisa na kurudishwa kwa Mola wetu Mlezi Mtukufu].*
Nikabainikiwa pia kwamba, hapa kuna ishara zingine mbili zinazodokezwa kuhusu roho: ya kwanza, roho ni kitu kilichoenea mwili mzima [kwa sababu wakati wa kutolewa kwake inavutwa kutoka chini (miguuni) kuja juu; takriban sawa na kusema inavuliwa], na pili, kitendo hicho cha kuvutwa kwa roho kina ambatana na uchungu mkali sana wa kutolewa roho; na huenda kadiri inavyovutwa, sehemu ya chini ya mwili inakuwa ikipoa na kukoma maisha; kadiri mifumo ya mwili inavyozidi kucollapse *[the point of NO return].*
Haya ni miongoni mwa yaliyonibainikia. *Kwamba, siku roho yangu itakapokuwa inatolewa, itakuwa ikivutwa kwa muundo huo; huku uchungu ukiwa ni makali sana.*
Hata hivyo, *bado natafakari;* hasa kuhusu muundo huo wa kutolewa kwa roho [kuvutwa]. K**a kuvutwa huko kwa roho kutoka chini kuja juu kunauma sana, *huenda imebana sana, na huenda ikivutwa kwa nguvu uchungu unazidi kuwa mkali zaidi. Je! wakati roho yangu inatolewa [kifo], Mimi ni katika wanadamu watakaovutwa roho zao kwa nguvu. Au taratibu?*
*Kwa yakini, ni juu yangu MIMI na WEWE kutenda matendo yetu katika njia ya Mola wetu Mlezi Mtukufu k**a lilivyo lengo la kuumbwa kwetu; ili siku roho zetu zitakapokuwa zinatolewa zitolewe taratibu angalau kupunguza uchungu wa kutolewa roho. Japokuwa bado uchungu wake ni mchungu sana.*
Katika Sahih, imeripotiwa kwamba, wakati Mtume Swalla Llaahu 'alayhi wasallam akiwa kwenye uchungu wa kifo *[huku akijifuta jasho usoni],* alisema:
*Subhaanaka Llaah, inna lilmauti lasakarat [umetakasika Mwenyezi Mungu. Hakika mauti yana uchungu].*
Kwa hakika, suala la roho ni muujiza mkubwa sana. Unaotuonesha kwamba Mola wetu Mlezi Mtukufu Yupo, ni Mkubwa na ni Mtukufu. K**a Qur'an ilivyobainisha kuwa hatukupewa elimu kuhusu roho ninini hasa na sayansi yake ikoje, mpaka sasa hakuna mwanasayansi yeyote wa Biolojia au tiba ya sasa aliyejaribu japo kung'amua *asili ya roho [ni kitu gani hasa?], muda halisi wa kuwekwa kwake mwilini ndani ya mfuko wa uzazi na kwa utaratibu [mechanism] gani, na lini itatolewa na kwa utaratibu gani [lini mtu atakufa]?* Na hatatokea mwanasayansi atakayefahamu au hata kung'amua hakika hizi.
Hii ni ishara nyingine inayotubainishia kwa uwazi kabisa kwamba, Qur'an ni maneno halisi ya Muumba wa mbingu na Ardhi; *ambaye ndiye Muumba wa mwanadamu.*
31/03/2025
*"KWANI SUNNAH NI HIYO HIYO TU YA KUOA ZAIDI YA MKE MMOJA"!?*
✍️Abdillah Kitota (MMedSc)
Ndugu msomaji, karibu tena kwenye uchambuzi wetu. Hilo ni swali linaloulizwa mara nyingi na wengi katika wanawake pale waume zao *wanapowaarifu juu ya dhamira yao ya kuongeza wake: wa pili, wa tatu au wa nne*
Kimsingi, ruhusa na sababu ya kuoa *wanawake tunaowapenda* zaidi ya mmoja [mpaka wanne] imetolewa katika Qur'an, 4:2-4 na 4:127. Ufafanuzi wake pia umetolewa kupitia Hadithi iliyosimuliwa na 'Urwa bin Zubair (Radhiya Llaahu 'anhu) kutoka kwa mama yetu 'Aaisha (Radhiya Llaahu 'anha) kwamba:
[Kipindi Qur'an inashuka] baadhi ya wanaume walikuwa wakiwalea mabinti mayatima na wakichanganya [katika matumizi] mali za hao mabinti mayatima walizorithi na za kwao. Sambamba na hilo, walikuwa *wakivutiwa nao kimapenzi [kuwa attracted] au wakitiwa majaribu [kuwa tempted]*; kiasi cha kuamua kuwaoa; lakini bila kuwalipa mahali zao walizostahiki ambazo wangeliweza kupewa na wanaume wengine ambao wangeliweza kuwaoa. Hata hivyo, kwa mujibu wa Hadithi zingine, kuna ambao walikuwa wakiwaoa kwa minajili ya mali zao walizorithi pekee, lakini hawajawapenda. Huku wengine wakikataa kuwaoa kwa sababu *hawana mali wala uzuri.*
Hivyo, kutajwa kwa *mvuto [attraction au fascination] au majaribu [temptation]* k**a sababu mojawapo iliyopelekea kuwaoa; lakini wakashindwa kuwalipa mahali waliyostahiki na kuwafanyia uadilifu katika mali zao walizorithi, *pamoja na kutolewa kwa ruhusa ya kuoa tunaowapenda,* kunabainisha kwamba *mwanaume yupo vulnerable [ni susceptible] zaidi na suala la kupenda [anapenda zaidi].* Na kunaingia pia kwenye ishara ambayo Mola wetu Mlezi Mtukufu ametuonesha leo hii kupitia tafiti za kibiolojia na kitiba.
Mathalan, ukiingia katika *PubMed*, utafiti wa kitiba *Sexual desire and s*xual activity of men and women across their lifespans: results from a representative German community survey*, uliochapishwa katika jarida la *BJU International*, na utafiti wa kitiba *Testosterone and s*xual desire in healthy women and men*, uliochapishwa katika jarida la *Archive Sexual Behavior*, ulionesha kwamba:
Baina ya wanaume na wanawake, wenye hamu zaidi ya tendo la ndoa [s*xual desire] na wenye shughuli zaidi ya tendo la ndoa; kwa maana ya kufanya mara kwa mara [s*xual activity], *ni wanaume.* Huo utafiti wa kwanza unasema: hamu ya tendo la ndoa inapungua kadiri umri unavyosonga; lakini wanawake ndiyo wanaoanza kupungukiwa na hamu ya tendo la ndoa ikilinganishwa na wanaume. Na kwa ujumla, wanaume wana hamu ya tendo la ndoa ya mara kwa mara na yenye nguvu ikilinganishwa na wanawake. Huo utafiti wa pili unaeleza kwamba, hamu ya tendo la ndoa ipo juu sana kwa wanaume ikilinganishwa na wanawake. Na inachangiwa kwa kiasi kikubwa na homoni ya *Testesterone.*
Aidha, tunafahamu kupitia ishara zingine za kimaumbile zinazotubainishia sheria zote zilivyowekwa juu ya misingi ya kimaumbile kwamba, Mola wetu Mlezi Mtukufu anapoweka sheria fulani ile sheria inakuwa inclusive [iliyokusanya kila kitu husika *kutokea* kwenye kuyazunguka maumbile yote husika kwa maana ya kuyalinda/kuyaongoza kiutendaji, kiafya n.k].
Kwa msingi huo, ruhusa hiyo inatubainishia kwamba, pamoja na kuweka msingi wa kusolve [kutatua] tatizo la uadilifu kwa upande huo, vilevile inabainisha kwamba, kwa wastani, *the very minimum threshold of s*xual satisfaction* kwa mwanaume [kiwango cha chini kabisa cha wanaume kutosheka katika hamu na shughuli ya tendo la ndoa], *ni mwanamke mmoja.* Halikadhalika, kwa umma huu wa mwisho ulivyoumbwa, *the maximum threshold of s*xual satisfaction* kwa mwanaume [kiwango cha juu zaidi kwa mwanaume kutosheka katika hamu na shughuli ya tendo la ndoa], *ni wanawake wanne; with exception to Nabii Muhammad Swalla Llaahu 'alayhi wasallam.* Na huu ndiyo wastani wa angalau kuukaribia uadilifu.
Msingi huo wa kimaumbile wa mwamaume ndiyo *unafit* kwenye asili halisi aliyoumbiwa mwanamke. Asili ambayo Mola wetu Mlezi Mtukufu alishatuonesha ishara zake katika Biolojia na tiba ya sasa.
Moyo wa mwanamke ni *emotional centred [unahisia za haraka na kali] zaidi* ikilinganishwa na moyo wa mwanaume. Kiasi kwamba kitu kidogo sana; *ikiwemo kazi nyingi za nyumbani,* au neno dogo sana linaweza kumtoa kwenye ari siku nzima ya masaa 24; *kiasi cha kuharibu utaratibu wa kawaida wa taarifa zake za kineva na kihomoni; na kumharibia hamu na shughuli yake ya tendo la ndoa.* Yaani, mwanamke unavyomuona kitabia ni mzunguko wake mzima wa hedhi; *ambao unaweza kuharibiwa kirahisi kwa namna tofauti akawa vile unavyomuona kitabia.*
Wanawake wanapitia kwenye kipindi cha ujauzito ambacho; wengi katika wao huathiriwa na mabadiliko ya kineva na kihomoni wanayopitia kipindi hiki. Katika Qur'an, 46:15, mabadiliko haya yametajwa kwa jina la *kurhan* [neno la Kiarabu lenye maana ya *kulazimishwa* kifiziolojia wapitie kwenye hali ya *taabu*; kiasi cha kufanya mambo waliyokuwa hawayafanyi au kutofanya mambo waliyokuwa wanayafanya]. Kwa msingi huu, wengi katika wanawake wakiwa kwenye kipindi hiki, huwa ama *hawana hamu kabisa ya tendo la ndoa na shughuli yenyewe, au hawana hamu ya kutosha ya tendo la ndoa na shughuli yenyewe.*
Kitiba, baada ya mwanamke kujifungua anahitaji *takriban wiki 4-6 [mwezi mmoja na wiki mbili]* za kurecover via vyake vya uzazi; ikiwemo uke, mlango wa kizazi na mfuko wa uzazi [kwa maana ya muda wa kupona majeraha na kukatika kwa damu ya nifasi], ili arejee tena kwenye hali ya kuwa na hamu ya tendo la ndoa na shughuli yenyewe ya tendo la ndoa. Uislamu; kupitia Sunnah, umeweka *a fixed amount of time* kuwa ni siku 40. Hata hivyo, inaweza kuwa chini ya hapo k**a atarecover kabla ya kutimia siku 40.
Mwanamke huyu huyu anayesubiriwa kuressume hamu na shughuli ya tendo la ndoa yupo kwenye kipindi cha kunyonyesha alichokiaza mara baada ya kujifungua; *ambacho kitakwenda mpaka miaka 2 kwa wanaotimiza kunyonyesha.*
Akiwa kwenye kipindi hiki cha kunyonyesha, huingia kwenye mabadiliko mengine ya kifiziolojia. Homoni zilizokuwa zinausimamia ukuta wa mfuko wake wa uzazi *[estrogen na progesterone]* zinashuka, kisha zinakuja homoni zingine *[prolactin na oxytocin]* zinazohusika katika kuchakata na kutoka kwa maziwa na kuurejesha ukuta wa mfuko wa uzazi katika hali yake [mbinyo/msinyao wa mfuko wa uzazi] kwa kufuatana. *Kwa wanawake wengi sana,* homoni hizi nazo huleta mabadiliko makubwa kwenye hamu na shughuli ya tendo la ndoa, hasa homoni ya *prolactin.* Homoni hii humvutia mwanamke upande wa mtoto mpaka akawa ni mwenye kumpenda zaidi mtoto wake, na sehemu kubwa ya utulivu na mapenzi yake yakawa kwenye kumnyonyesha mtoto wake; na siyo mumewe.
Je! Mimi na wewe tujiulize, kwa mwanaume huyo tuliyemsoma kwenye makala hii; kupitia ishara za Mola wetu Mlezi Mtukufu katika Biolojia na tiba ya sasa, aliyeumbwa kwa *asili ya matamanio [hamu ya tendo la ndoa] ya mara kwa mara na yenye nguvu,* anaweza *kustahimili ipasavyo [bila kutamani wanawake]* akiwa na mwanamke mmoja? Tena mwanamke ambaye anavipindi vyote hivyo [vingi] vya kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa; kiasi cha kuathiri shughuli yenyewe ya tendo la ndoa?
Jibu ni kwamba, haiwezekani, isipokuwa kwa wanaume wachache sana ambao Mola wetu Mlezi Mtukufu hakuwaumba *exactly* hivyo: labda kawapa homoni pungufu ya *Testesterone* n.k.
Hivyo, tunawakumbusha wengi katika wanawake, wamche Mola wao Mlezi Mtukufu kwa kutowawekea *vigingi* waume zao kuongeza wake. Wajue na wazingatie kwamba, suala hili ni suala la kimaumbile; *ambalo wengi katika wanaume wameumbiwanalo.* Wanawake hawa wazingatie pia kwamba, kuwawekea *vigingi* waume zao kuongeza wake kunaweza kuwa ni katika njia ya Ibilisi inayopelekea *zinaa ya macho, zinaa ya masikio, zinaa ya miguu, zinaa ya mikono na zinaa yenyewe ya extramarital [nje ya ndoa].*
Allah Subhanahu wata'alah awafanyie wepesi nyoyo zao zifunguke wasiwawekee *vigingi* waume zao.
31/03/2025
*KWA WANANDOA*
*TATIZO LA KUPUNGUA UWEZO WA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA KWA WANAWAKE*
✍️Abdillah Kitota (MMedSc)
Ndugu zangu, leo katika dawati letu la uchambuzi tuchambue kwa ufupi *tatizo la kupungua uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kwa wanawake [s*xual dysfunction in females]*; ambalo ni kinyume cha tatizo lililozoeleka la upungufu wa nguvu za kiume [kwa wanaume]. Wengi katika wanawake; na hata wengi katika wanaume, hudhani kwamba tatizo la kupungukiwa ufanisi katika tendo la ndoa linawahusu wanaume pekee; mara nyingi wanaume wakiwa ndiyo wenye kupewa lawama [kunyooshewa vidole]. Lakini kiuhalisia hata wanawake wanaweza kuwanalo tatizo hili. Tena kwa taarifa yako, kwa wanawake tatizo hili limeenea zaidi: *10-52% kwa wanaume na 25-63% kwa wanawake.*
Tofauti kidogo na ilivyo kwa wanaume, kwa wanawake, tatizo hili *hutokea kutokana na mwanamke kutokuwa na hamu au/na kushindwa kupata raha ya kutosha katika mzunguko mzima wa kujamiiana na mwitikio wake [s*xual-response cycle];* ambao umejengwa kwa hatua za:
1. *Hamasa/hamu/motisha [motivation].*
2. *Msisimko/mchecheto [arousal].*
3. *Kilele/mshindo [or**sm]*
4. *Kurudi kwenye level ya kawaida [resolution].*
*Tatizo la kupungua uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kwa wanawake* linaweza kuchukua sura tofauti; kutegemeana na sababu zake. Linaweza kutokea *kabla, wakati na baada ya tendo lenyewe la ndoa.*
Kwa ujumla, matatizo yanayohusiana na *kupungua uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kwa wanawake* yaliyoenea zaidi ni manne (4):
1. *Matatizo ya kilele/mshindo [or**smic disorders] k**a vile kushindwa kabisa kufika kilele [kitaalamu, anor**smia] n.k.*
2. *Maumivu wakati wa tendo la ndoa [kitaalamu, dyspareunia].*
3. *Hamu ndogo ya tendo la ndoa au kukosekana kabisa kwa hamu ya tendo la ndoa [hypoactive s*xual desire disorder]*
4. *Ugumu wa kushindwa kusisimuliwa/kuchechemuliwa [s*xual arousal disorder].*
Kati ya matatizo hayo, *kukosa hamu ya tendo la ndoa [lack of s*xual desire]* ndiyo tatizo lililoenea zaidi; *linalolalamikiwa zaidi.*
Kwa nyongeza, matatizo haya ya *kupungua uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kwa wanawake* yanaongezeka kadiri mwanamke anavyozidi kuwa mkubwa. Hata hivyo, yanaweza kumpata mwanamke mwenye umri wowote ule; *katika hatua yoyote ile ya maisha yake ya ndoa.* Na yanaweza kuwa ya muda mfupi *[temporary au transient]* au ya kudumu *[permanent].*
Ama kuhusu sababu zake, kuna sababu za *kiumbo* na *kisaikolojia.* Sababu za *kiumbo* zinajumuisha:
1. *Matatizo ya mwendo wa damu [blood flow disorder].* Matatizo haya yanajumuisha damu kushindwa kutiririka vizuri kwenye mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke k**a vile *uke, kisimi, na l***a [mashavu].* Viungo hivi vinahitaji damu ya kutosha wakati wa tendo la ndoa.
2. *Matumizi ya dawa na matibabu fulani.* Baadhi ya dawa na matibabu huathiri kazi za tendo la ndoa. Mathalan, matumizi ya *antidepressants [dawa za kutuliza/kutibu matatizo ya msongo, hofu, uraibu na maumivu ya muda mrefu]*; hususan *Selective serotonin reuptake inhibitors (SSRIs)*, yanaweza kupunguza msukumo wa tendo la ndoa. *Chemotherapy na matibabu mengine ya saratani* yanaweza kuathiri kiwango cha homoni na kusababisha matatizo haya.
3. *Hali za magonjwa ya wanawake [gynecological conditions].* Haya yanajumuisha *Endometriosis [tishu za ukuta wa mfuko wa uzazi zinakua na kutokeza], ovarian cysts [vifuko vigumu au vilivyojaa maji ndani au juu ya ovari], uterine fibroids [uvimbe usio wa saratani kwenye mfuko wa kizazi] na vaginitis [inflamesheni ukeni unaoweza kupelekea mwasho, ute na maumivu].* Matatizo yote haya yanaweza kupelekea maumivu wakati wa tendo la ndoa. Halikadhalika, *vaginismus* ni hali ya misuli ya uke kukaza au kusinyaa inayoweza kupelekea mwanamke kutokuwa thabiti kwenye tendo la ndoa.
4. *Mabadiliko ya kihomoni k**a vile homoni kutokuwa sawa [hormonal imbalance]* yanaweza pia kupelekea uke kuwa mkavu na hata kupungua ukubwa. Hali inayoweza kupelekea maumivu wakati wa tendo la ndoa. Kiwango kidogo cha homoni ya *estrogen* kinaweza pia kupelekea kupungua kwa hisia kwenye sehemu za siri za mwanamke. *Menopause, upasuaji na ujauzito* vilevile vinaweza kupelekea mabadiliko ya kihomoni.
5. *Hali fulani za kiafya.* Kuna matatizo mengi ya kiafya yanayoweza kupelekea *tatizo la kupungua uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kwa wanawake.* Matatizo haya yanajumuisha: kisukari, matatizo ya moyo, maumivu ya viungo, magonjwa ya mfumo wa kingamwili k**a vile multiple sclerosis n.k. Ulevi, uraibu vinaweza pia kuathiri ufanisi wa mwanamke kwenye tendo la ndoa.
Ama kuhusu *sababu za kisaikolojia* zinazosababisha *tatizo la kupungua uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kwa wanawake:*
1.*Mkazo* wa nyumbani au kazini vilevile unaweza kuathiri nguvu ya mwanamke katika tendo la ndoa. Kazi nyingi za nyumbani, kazi nyingi za kazini, mawasiliano mabaya baina ya mke na mume [lugha mbaya, lugha za ukali n.k], mwanamke kukosa matumaini na baadaye yake [kutooneshwa baadaye yake n.k], mwanaume kutokuwa na ujuzi wa kutosha wa kutatua migogoro ya kifamilia, mwanaume kutokuwa na ujuzi wa kutosha wa kubondi na mkewe; hususan wakati wa migogoro, mwanamke kutoridhishwa katika tendo la ndoa [kutochechemuliwa vya kutosha na kufikishwa kilele n.k], hali ngumu ya maisha; ikiwemo madeni ya vikoba, kutokuwa na maelewano na mume kwa muda mrefu au mara kwa mara; ni miongoni mwa vinavyosababisha mkazo kwa mwanamke; na k**a havitapatiwa majawabu vitapelekea msongo.
2. *Msongo.* Hii ni level ya juu zaidi ya *mkazo; ambayo wakati huu imekuwa tatizo la afya ya akili.* *Msongo* unaweza kupelekea kukosa hamasa ya kitu ulichokuwa na hamasa nacho kabla, ikiwa ni pamoja na tendo la ndoa.
Vyote *mkazo* na *msongo* vinasababisha kutolewa kwa homoni ya *cortisol* ambayo inashusha msukumo wa tendo la ndoa. Na vilevile vyote vinaathiri mwendo wa kawaida wa homoni zinazosimamia ufanisi wa tendo la ndoa.
*Kubwa zaidi hapa ni kwamba, moyo wa mwanamke; ambao kimsingi k**a ulivyo moyo wa mwanaume huzalisha homoni ya mapenzi [oxytocin], ni emotional centred zaidi kwenye msongo na mkazo kulikoni moyo wa mwanaume. Hivyo, unatakiwa kulindwa kwa juhudi zote.* Kuulinda moyo wa mwanamke ni kwa faida ya wote mwanaume na mwanamke mwenyewe. Mwanaume ukiulinda moyo wa mwanamke *inamaana unajiandalia mazingira mazuri ya kupewa mapenzi ya hali ya juu.*
3. *Manyanyaso ya kiumbo au kingono yaliyopita.* Ikiwa yalitokea katika wakati wa utoto inamaana yaliacha athari za kiumbo kwenye ubongo. Ikiwa yametokea ukubwani pia inamaana yameacha taarifa zisizorafiki moyoni na kwenye ubongo. Vyote hivi ni sumu kwenye tendo la ndoa.
4. *Masuala mbalimbali ya mahusiano.* Baadhi ya wanawake wanaweza kutokuwa na furaha na mwanaume kutokana na kutoridhikanaye kwa sababu mbalimbali za kiumbo [umbile lake] au kimaisha. Hapa kuna mambo mengi. Baadhi yake ni k**a kutokuwa na maelewano kwa muda mrefu au mara kwa mara, mwanaume kutokuwa na ujuzi wa kutosha wa kuliendea tendo la ndoa, lugha chafu ya mwanaume kwa mwanamke n.k. Maneno machafu yana asili ya kuua moyo; na kwa mwanamke inakuwa zaidi kutokana na asili hiyo ya moyo wake.
*Ama kuhusu matibabu,* yanategemea sana na aina ya ugonjwa wa *kupungua uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kwa wanawake* na sababu zake husika. Kuna ambayo yanahitaji kurekebisha tabia; ikiwemo kujifunza ujuzi mpya wa tendo la ndoa, kujifunza ujuzi mpya wa kubondi na mke; hususan wakati wa migogoro, kuna ambayo yanahitaji utulivu na furaha; ikiwemo kuepuka kutokuwa na maelewano, kuna ambayo yanahitaji kubadilisha mfumo wa maisha; ikiwemo ulaji na mtindo wa mahusiano, kuna ambayo yanahitaji matibabu ya kitaalamu k**a ushauri nasaha, intervention za kimatibabu ya kihospitali n.k.
*Kwa muhtasari:*
1. *Arousal techniques.* Ongea na mkeo juu ya mbinu mbalimbali za kumchechemua, kupandisha uhitaji wake wa tendo la ndoa. Soma vitabu vinavyoaminika pia; ikiwa ni pamoja na kuuliza kwa wajuzi wa mambo haya. Wanaume wengi wanatajwa kutokuwa na ujuzi katika kikiendelea tendo la ndoa, ikilinganishwa na wanawake. Hii inachangia sana kwenye *tatizo la kupungua uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kwa wanawake.*
2. *Ushauri na nasaha.* Unaweza kupata ushauri na nasaha kwa wataalamu wa ushauri na nasaha wa masuala ya kindoa au hata kwa wenye uzoefu wa kindoa; hususan k**a sababu za tatizo husika ni la kisaikolojia. Bila kusahau ushauri na nasaha za kitiba k**a tatizo linaangukia kwenye matibabu moja kwa moja; wakiwemo mental health professionals.
3. *Matibabu ya kihomoni [hormonal therapy].* Kutegemeana na dalili zako, daktari wako anaweza kukupa cream za kupaka juu [topical creams], dawa za kuingiza ukeni [vaginally administered medication], au homoni zinazokuwa administered orally.
4. *Matibabu.* *Flibanserin (Addyi®) na bremelanotide (Vyleesi™)* zinafaa zaidi kwa matibabu ya *tatizo la msukumo wa chini wa tendo la ndoa [hypoactive s*xual desire disorder (low s*x drive)]*; ambalo ndilo lililoenea zaidi. Hii ni kwa wanawake ambao hawajafikia umri wa kukoma uzazi (menopause).
5. *Usimamizi wa maumivu [pain management].* Kuna mbinu nyingi za kupunguza maumivu wakati wa tendo la ndoa. Unaweza kujaribu mitindo mbalimbali ya kuliendea [hili limebainishwa ndani ya Qur'an moja kwa moja], vilainishi vya uke, au mbinu za kutanua uke kabla ya tendo la ndoa. Daktari wako anaweza pia kushauri kuhusu vaginal dilators.
6. *Mazoezi.* Wanandoa wengi; hususan wanawake, hawana ada ya kufanya mazoezi. Weka ratiba maalumu kwa ajili ya mazoezi, kwani, mazoezi huimarisha na kuboresha umbo [linakuwa na mwonekano mzuri kwa mkeo/mumeo], huimarisha misuli ya nyonga *[pelvic-floor muscles]* na kutanua mishipa kwa ajili ya damu kujaa, huzalisha homoni za furaha na kuondoa mkazo n.k; *yote haya yanasimamia afya ya tendo la ndoa.*
Washukran!
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Address
Arusha