27/03/2026
Idara ya special mwaka Jana mlifanya vizuri Kiasi Cha idara yenu kupewa mtaji na shirika la OSNET, kwa ajili ya kilimo cha mbogamboga pamoja na utengenezaji wa sabuni ambazo shule na wadau wengine wananunua kwa matumizi mbalimbali.
Tunashukuru sana Shirika la OSNET kwa mchango wao katika shule yetu
20/03/2026
Wanafunzi wetu wakiendelea kujisomea kwenye maabara ya Computer with full internet
27/02/2026
Matokeo ya mchezo wetu dhidi ya Kaloleni Secondary.
Tumeshika nafasi ya pili kati ya timu Nne za KANDA C. Hivyo tumeshindwa kusonga mbele hatua inayofuata.
Tutajipanga upya kwa ajili ya mashindano mengine.
23/02/2026
Timu yetu ilikua dimbani leo dhidi ya Felix Mrema Sec. Tumeibuka washindi.
KITUO KINACHOFUATA
π Arusha Secondary
π
Jumatano 25 Feb 2026
ποΈ Uwanja wa Arusha Sec.
β²οΈ Saa 9 Alasiri
17/01/2026
Matokeo ya Upimaji Kidato cha II β 2025 πβ¨
Juhudi, nidhamu na mshikamano vinaendelea kuzaa matunda Themi Sekondari. Hongera wanafunzi na walimu wetu ππ
17/01/2026
ππ» THEMI SEKONDARI | DIGITAL TECHNOLOGY SUPPORT
Shule ya Themi Sekondari imepokea msaada muhimu kutoka kwa FINNISH SPECIAL EDUCATION IN AFRICA () katika awamu mbili:
πΉ Awamu ya Kwanza:
β
Computer 14 za wanafunzi
β
Computer 5 za walimu
β
Mafunzo ya walimu
β
Mtambo 1 wa Solar
β
Printer 1
β
Meza na Viti
β
Movable Whiteboard ndogo 1
β
Projector 2
β
Internet Connection
πΉ Awamu ya Pili:
β
Computer 15 za wanafunzi
β
Mouse 29
β
Movable Whiteboard kubwa 2
β
Projector 1
β
Tablet 6
π Tunashukuru sana kwa mchango huu unaoimarisha elimu ya TEHAMA na ujumuishi shuleni kwetu.
07/06/2025
Siku ya Ijumaa, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, ilitangaza majina ya wanafunzi wa kidato cha Nne 2024 waliochaguliwa kuendelea na masomo ya Kidato cha tano na Elimu ya vyuo vya kati na Ufundi kwa mwaka 2025.
Wanafunzi 123 kutoka shule ya Sekondari Themi ni miongoni mwa waliochaguliwa kuendelea na masomo: ambapo wanafunzi 94 watajiunga Kidato cha Tano, huku 29 wao wamechaguliwa kujiunga na Elimu ya vyuo.
Uongozi wa shule ya Sekondari Themi unawatakia mafanikio tele katika masomo yao.
Kuona majina bonyeza π link kwenye bio yetu.
09/03/2025
Tarehe 7 March siku ya Ijumaa wafanyakazi wa Tanesco Mkoa wa Arusha waliazimisha siku ya wanawake Kwa kuja kupanda miti ya matunda Shule ya Sekondari Themi, waliambatana na Mh Meya wa Jiji la Arusha na kiongozi wao Engineer Zawadi, aidha walisaidia gharama za chakula Kwa wanafunzi takribani 35, tunawashukuru Sana
23/01/2025
Matokeo ya Kidato cha Nne 2024.
25/12/2024
Tunawatakia heri ya sikukuu ya Christmas ππ