24/01/2026
? Vioo vya kutengeneza vitu mbalimbali k**a vile bilauri, chupa za bia/soda, vioo vya nyumba n.k hutengenezwa kwa mchanga? Kivipi! Mchanga huchomwa kwa joto kali kiasi cha kufanya mchanga uyeyuke na kuwa kimiminika. Kimiminika hiki kikipoa ndipo huwa vioo/glass.
03/10/2025
mimea huzaa kabla ya wakati wake ikiwa imepata msongo? (stress). Kwa mfano, mboga zikikosa maji ya kutosha huchanua maua mapema na kutoa mbegu zikijua kuwa zinaweza kufa kabla hazijaacha uzao? Hivyo huzaa mapema ili ziache uzao wa kizazi kijacho.
Hivyo basi, k**a una bustani yako ya mboga mwagilia mboga zako maji ya kutosha ili zichelewe kutoa maua ili ufaidi mboga kwa muda mrefu.
Usisahau kutu_follow ili upate kujua mengine ambayo ulikuwa huyafahamu.
27/09/2025
?
Sehemu nyeusi ya jicho husaidia kusharabu mwanga uliotawanyika (absorption of dispersed light) ili kuhakikisha mwanga unapoingia kwenye retina hautawanyiki ili kusaidia kuona vitu kwa usahihi? .
13/09/2025
Je, wajua maji safi (pure water) hayapitishi umeme?
08/09/2025
:
Je wajua kuwa k**a ilivyo kwa kucha na nywele, ubongo pia hauna uwezo wa kuhisi maumivu? Kwa hio maumivu ya kichwa hayapo kabisa kwenye ubongo, maumivu hayo unayapata kwenye misuli inayozunguka fuvu la kichwa. K**a unajua, tupe sababu kwenye comment section.
16/09/2023
Karibu katika shule yako umlete mtoto, ndugu, jamaa au rafiki kwa ajili ya masomo. Kwa maelezo zaidi piga simu kwa namba zilizopo kwenye tangazo hili. Karibuni sana millard ayo
15/10/2022
Shule ya Sekondari Kimandolu iliyopo Jijini Arusha inatoa nafasi za kujiunga kidato cha kwanza kwa wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka huu na nafasi za kuhamia kwa kidato cha pili na tatu. Karibuni muwalete watoto wenu, wa ndugu, jamaa na marafiki kujiunga na shule yetu.
12/06/2022
Ndugu wana Kimandolu Secondary school, Salaam.
Kwa masikitiko makubwa nawajulisha kwamba mwalimu wa muda mrefu wa shule yetu, maarufu kwa jina la GG, ameunguliwa na nyumba yake siku ya Ijumaa tarehe 10/06/2022 saa 8 mchana. Moto umeunguza kila kitu kwa 99%. Hakuna kilichookolewa. Naomba tuungane kumpa Pole, na kumsaidia kwa hali na mali kadri tutakavyoguswa. Namba yake ya simu ni 0754093915 au 0683708383.
Tangazo hili limetolewa na uongozi wa shule tarehe 12/06/2022
16/01/2022
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kubariki kazi yetu. Naam, sasa tunaendelea kuona matunda yanayofanana na yale ya mwaka jana ππ