Maarifa Ndani Ya Masomo Ya Biblia.

Maarifa Ndani Ya Masomo Ya Biblia.

Share

Samwel Kibiriti Ni Mwalimu Mwalimu wa Neno la Mungu lililobeba Maarifa makubwa Sana ya rohoni, unapokuwa katika hii page utapokea haya Maarifa.

02/11/2024

MADHABAHU YA IBADA YA SIKU MPYA, KIZAZI CHA KUSUDI LA MUNGU DUNIANI ( 98 ).

Bwana Yesu Kristo asifiwe mwana wa Mungu karibu katika IBADA ya SIKU MPYA ya Leo ambapo Mungu Baba atatuhudumia Kwa Mkono na nguvu zake.

TAFAKARI YA NENO LA MUNGU KATIKA KITABU CHA MATHAYO 18:1-4 SIKU YA LEO JUMAMOS NOVEMBER 02.

Kitabu Cha Mathayo 18:1-4 Biblia inasema hivi kwenye Tafsiri ya Neno Biblia kwamba

"Wakati huo, wanafunzi wakamjia Yesu na kumuuliza, Je, nani aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa Mbinguni?
Yesu akamwita mtoto mdogo na kumsimamisha katikati yao. Naye akasema: Amin, nawaambia, msipookoka na kuwa k**a watoto wadogo, kamwe hamtaingia katika Ufalme wa Mbinguni. Kwa hiyo mtu yeyote anyenyekeaye k**a huyu mtoto, ndiye aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa Mbinguni".

🔶 Hili ni swali la muhimu sana ambalo wanafunzi wa Bwana Yesu walimuuliza kuhusu kuwa mkuu kwenye ufalme wa Mbinguni na Yesu Kristo aliwajibu majibu mazuri sana

Aliwaambia ili mtu aweze kuwa mkuu kwenye ufalme wa mbinguni ni lazima kwanza aweze KUOKOKA maana yake awe amemwamini na kumkiri Yesu Kristo k**a Bwana na Mwokozi wa maisha yake Kisha aishi maisha ya unyenyekevu kwenye Wokovu wake mbele za Mungu huyo atakuwa mkuu katika ufalme wa mbinguni.

Kwahiyo hapa tunajifunza kwamba ni LAZIMA UWEZE KUOKOKA k**a Bado hujaokoka Kwa KUMWAMINI NA KUMKIRI YESU KRISTO K**A BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO wewe hutaweza kuingia kwenye ufalme wa mbinguni haijalishi dini yako na dhehebu lako na mahali unaposali ni lazima Leo ukubali KUOKOKA

Kisha baada ya KUOKOKA ni lazima kila siku ya maisha yako hapa duniani UISHI MAISHA YA UNYENYEKEVU mbele za Mungu kwa kuishi kwa KUONGOZWA NA NENO LA MUNGU hivyo hakikisha Neno la Mungu umelipa nafasi ya kwanza ndani ya moyo wako na kuliruhusu likuongoze nawe unalifuatilia kwa Kulitii na kufanya maagizo na maelekezo yake Mungu maishani mwako.

➡️ Mungu anavyotutafsiri ni tofauti na taratibu za dini zetu zinavyotutafsiri hivyo hakikisha unaishi kwa KUONGOZWA NA NENO LA MUNGU kila siku na kila jambo unalofanya msingi wake uwe katika Neno la Mungu pake yake.

🔶 K**a Bado hujaokoka na Leo unasema Mwalimu Kibiriti Mimi nataka NIOKOKE NA KUONGOZWA NA MCHUNGAJI YESU KRISTO nataka nikukaribishe kwa wewe kufanya SALA HII YA TOBA toka ndani ya moyo wako na Mungu atakusamehe na kukufanya Mtoto wake.

SALA YA KUOKOKA IOMBE KWA IMANI MBELE ZA MUNGU:

Ee Mungu wewe ni Muumbaji wangu na ulimtoa mwanao wa pekee Yesu Kristo afe pale Msalabani kwaajili ya dhambi zangu nimekuwa mbali na uso wako Mungu lakini siku ya Leo ninakubali kurudi kwako Mungu Mimi...... Ninakubali kumwamini Yesu Kristo na kumkiri kuwa ni Bwana na Mwokozi wa maisha yangu

Nakuomba Bwana Yesu lifute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na kuliandika upya jina langu kwenye kitabu cha Uzima na Leo Mimi nimeokoka na Yesu Kristo wewe ni Bwana na Mwokozi na Mchungaji wa maisha yangu asante Mungu Baba kwa Neema hii ya Wokovu katika jina la Yesu Kristo Roho wako Mtakatifu awe kiongozi na mwalimu wangu katika maisha haya ya Wokovu Kila siku Amen".

➡️ Kwa kufanya SALA hii nataka kukutangazia kuwa tayari umeokoka karibu kwenye Ufalme wa Mungu na hakikisha Sasa unaishi kwa kuongozwa na Neno la Mungu karibu sana tumzalie Mungu Baba matunda kwenye maisha yetu ya kila siku hapa duniani, usisite kuwasiliana nami na kunieleza ushuhuda huu mkubwa wa Wokovu ili nizidi kukuombea mbele za Mungu.

🔶 Leo ni siku mpya ambayo Mungu Baba ametupa kuishi ya tarehe 02 November hivyo tuweze kuiombea mbele za Mungu.

KIRI MAOMBI HAYA KWAAJILI YA SIKU MPYA YA LEO:

Mungu Baba nakushukuru kwaajili ya maisha yangu hapa duniani asante kwa siku mpya ya Leo...... Ambayo umenipatia nafasi hii ya Mimi kuishi asante kwa Uzima na Uhai wako nami naitakasa siku ya Leo kwa Damu ya Yesu Kristo na kuifungua kwa Jina la Yesu Kristo na kuibariki kwa Jina la Yesu Kristo natangaza nitaishi katika siku iliyotakasika na kubarikiwa kwa Jina la Yesu Kristo

Ninaziombea mbingu zangu za Maisha ziweze kufunguka na kuwa wazi kwa Jina la Yesu Kristo nami nayaombea malango yangu ya maisha yafunguke na kuwa wazi daima mchana na usiku hayatafungwa kwa Jina la Yesu Kristo

Mungu Baba ninaomba Baraka zako juu ya maisha yangu ya siku ya Leo ya...... ulinzi wako uwe nami na Mkono wako unitendee mema na kunihifadhi kwa Jina la Yesu Kristo asante kwaajili ya maisha ya kila mtu wa familia na uzao na nyumbani mwangu ninawaombea mbele zako Mungu ukutane na maisha yao na kuwalinda na kuwatunza na kuwaongoza katika maisha yao ya kila siku hapa duniani kwa Jina la Yesu Kristo ninaomba na kuamini Amen.

➡️ Nakutakia Siku njema ya Baraka na Neema ya Mungu na Mungu akufanikishe katika kila jambo na Mkono wake uzidi kutenda katika Familia na uzao wako kila siku. Tukutane tena katika LANGO LA IBADA YA SIKU MPYA kesho majira ya saa 10 ALFAJIRI.

Mimi ni rafiki yako katika Kristo Yesu

Mwalimu Samwel Kibiriti.

November 02, 2024

Dar es salaam Tanzania.

KWA USHAURI WA KIROHO NA MAOMBEZI WASILIANA NAMI KWA NUMBER HII YA UTUMISHI PIA TUMIA NUMBER HII KUWA CHOMBO CHAKO CHA SADAKA MBELE ZA MUNGU +255 765 867574 NA MUNGU AYABARIKI NA KUYAFUNGUA MAISHA YAKO.

Tuungane tena siku ya Kesho ambapo tutakaa kwenye Maombi kwa pamoja mbele za Mungu kushughulia chanzo kingine kilichokwamisha maisha yetu.

Washirikishe wengine IBADA hii nao wapate Maarifa na kufunguliwa na Mungu ili waishi maisha ya uhuru.

Photos from Maarifa Ndani Ya Masomo Ya Biblia.'s post 29/10/2024

MADHABAHU YA IBADA YA SIKU MPYA, KIZAZI CHA KUSUDI LA MUNGU DUNIANI ( 94).

Bwana Yesu Kristo asifiwe mwana wa Mungu karibu katika IBADA ya SIKU MPYA ya Leo ambapo Mungu Baba atatuhudumia Kwa Mkono na nguvu zake.

SIKU 10 ZA KUOMBA MBELE ZA MUNGU KUSHUGHULIA VYANZO VILIVYOKWAMISHA MAISHA YAKO ROHONI.

Haya ni maombi ya kushughulikia vyanzo ambavyo vimetufanya tusiishi katika maisha yetu ya Kusudi hapa duniani hivyo Kwa maombi haya mbele za Mungu atatufungua na kutuweka huru.

( Day 8 mbele za Mungu ):

➡️ MAOMBI YA LEO NI KUSHUGHULIKIA CHANZO CHA NYUMBA ULIZOWAHI KUISHI NA ZIKAKWAMISHA MAISHA YAKO.

🔶 Wapo watu wengi ambao wanashindwa kuishi kwenye Kusudi la Mungu na kuyaishi maisha yao halisi ya uumbaji kwasababu kwenye ulimwengu wa roho wamekwamishwa na chanzo cha nyumba walizowahi kuishi au wanazoziishi Leo hii, hivyo k**a unataka kuishi kwenye Kusudi la Mungu ni lazima uingie kwenye Maombi na kujifungua kwenye vifungo vyote vya rohoni ulivyofungwa na maadui kupitia nyumba ulizowahi kuishi na kulala.

ZABURI 127:1

🔶 Ukisoma huu mstari uko wazi kwamba jambo la nyumba nila kiroho zaidi tofauti na unavyodhania kimwili hivyo kuna mahusiano makubwa ya kiroho kati ya maisha yako na nyumba unayoishi au kulala. Ni lazima uitazame nyumba kwa jicho la kiroho zaidi nawe utagundua mambo mengi ya kiroho kwenye nyumba na mifumo yako ya maisha.

YOSHUA 24:15

🔶 Ukisoma hapa Yoshua anasema yeye na nyumba yake watamtumikia Mungu maana yake aliingiza nyumba yake na Kila kilichomo kwenye nyumba katika utumishi wa Mungu wake. Hii ina maanisha kwamba nyumba unayoishi kiroho inaweza kuwa kwenye Utumishi wa Mungu au miungu na nyumba za watu wengi ziko kwenye utumishi wa miungu migeni ndio maana maisha yao yamefungwa na kukwamishwa kiroho sababu ya nyumba walizolala zilikuwa tayari kwenye utumishi wa miungu migeni hivyo ni lazima uingie kwenye Maombi na kujifungua kwenye huo utumishi wa miungu uliofungwa kupitia hiyo nyumba.

AMOSI 3:11

🔶 Biblia inasema nyumba inaweza kutekwa nyara kwahiyo k**a uliwahi kuishi au kulala kwenye nyumba ambayo ilishikiliwa na miungu baada ya kuiteka unaona tayari kuna kitu cha kiroho Cha upande wa giza kilifanyika maishani mwako na kujikuta husongi mbele za kimaisha sababu kuna namna rohoni umek**atwa kupitia kwenye mlango wa nyumba.

ISAYA 13:21-22

🔶 Biblia inasema na majini watacheza kwenye nyumba hapa unatakiwa kuona kuwa kuna viumbe wa giza wanaweza kuingia na kuishi kwenye nyumba za wanadamu na k**a uliwahi kuishi kwenye nyumba yenye hali k**a hii maana yake maisha yako yamefungwa na hao viumbe wa giza waliokuwa na uhalali kwenye hiyo nyumba Sasa ni lazima uingie kwenye Maombi na kujifungua ili uweze kuwa huru.

Saa nyingine unaona kwenye hiyo nyumba unayoishi usiku kuna vitu vinatembea na kuwasumbua na kuwapigia kelele hiyo ni ishara kwamba kuna viumbe wa giza wameingia na mnaishi nao kwenye hiyo nyumba nao watahakikisha wanayadhibiti maisha yenu na hata saa nyingine kujikuta kwenye hiyo nyumba mnateseka kwa magonjwa na kuota ndoto za ajabu ajabu au kuandamwa na matukio yasiyoelezeka kimaisha.

KUMBUKUMBU LA TORATI 20:5

🔶 Biblia inasema nyumba zinawekwa wakfu hivyo nyumba inaweza kuwekwa wakfu kwa Mungu au kwenye miungu k**a uliwahi kulala na kuishi kwenye nyumba iliyowekwa wakfu kwenye miungu hapo maisha yako lazima yamefungwa na hizo roho za miungu ni lazima uingie kwenye Maombi na kujifungua kwa Damu ya Yesu na Jina la Yesu Kristo ili uwe huru na kuishi maisha ya Kusudi la Mungu hapa duniani.

LUKA 11:21-22

🔶 Ukisoma Biblia inasema kwamba nyumba huwaga zinalindwa kiroho na malaika wa Mungu au mapepo/majini wa kuzimu hivyo k**a uliwahi kulala au kuishi kwenye nyumba iliyokuwa inalindwa na mapepo maana yake roho hizo za mapepo zilifunga maisha yako k**a hujaweza kudhibiti hali ya kiroho ya hiyo nyumba kipindi kile ulipoingia kuishi au kulala na Leo mambo yako yameharibika na maisha yako yamekuwa magumu sana kumbe ulik**atwa na maadui kwenye nyumba uliyowahi kulala na kuishi.

Katika ZABURI 34:7 Biblia inasema malaika wa Mungu wanafanya kituo na eneo mojawapo ambalo malaika hufanya vituo ni kwenye nyumba wanazoishi wateule wa Mungu hivyo hivyo ukilala kwenye nyumba iliyochini ya utawala wa kuzimu maana yake kuna mapepo na majini wamefanya vituo vyao vya makazi kwenye hiyo nyumba Sasa k**a uliingia na ukalala tu na kuishi bila kuharibu na kudhibiti hiyo ya kiroho ya hiyo nyumba tayari maisha yako yalik**atiwa pale na Leo mateso hayaondiki kwako ingia kwenye Maombi na jifungue kwenye Kila nyumba uliyowahi kulala na kuishi na ukaitumiwa kukufunga kiroho nawe utakuwa huru.

KUMBUKUMBU LA TORATI 5:6, 7:8

🔶 Mungu aliwatoa wana wa Israeli katika nyumba ya utumwa hii ina maanisha kwamba nyumba inaweza kubeba mazingira ya utumwa na mwanadamu akiishi ndani yake hufungwa na huo utumwa ili asiweze kuwa huru. Ndio maana unajikuta unaotaga ndoto uko kwenye nyumba fulani uliyowahi kulala au kuishi hiyo ni ishara kuwa nafsi yake ilifungwa kwenye hiyo nyumba na ili uwe huru na kusonga mbele lazima uingie kwenye Maombi na kuikomboa na kuifungua nafsi yako iliyofungwa kwenye nyumba hiyo.

Kuna mambo mengi ambayo kiroho yanaweza kufanyika kwenye maisha ya mwanadamu kupitia nyumba na Mimi kwenye utumishi huu nilioubeba wa Mungu nimekutana na watu wengi waliofungwa kiroho kupitia nyumba walizowahi kulala na kuishi na hata wengine kwenye nyumba wanazoishi shetani na maadui wamezitumia kiroho kuwafunga na kuwatesa kimaisha pasipo wao kujua

Ndio maana niliandika kitabu kiitwacho PATA MAARIFA YA KIROHO KUHUSU NYUMBA UNAYOISHI lengo kubwa la kitabu hiki ni kuelezea uhusiano wa maisha ya mwanadamu na nyumba anayoishi na kulala, kwenye kitabu nilifundisha sababu za Shetani kuteka nyumba pia nilifundisha aina ya Nguvu ambazo shetani amewaibia wanadamu na kuwadhibiti wasizitumie maisha mwao lakini pia nimefundisha aina mbalimbali za maombi ya kujifungua kwenye nyumba ili kuwa huru na pia nimefundisha namna ya kuiombea nyumba hivyo hakikisha unapata NAKALA ya kitabu hiki kitakujenga na kukusaidia sana kiroho na utapata uelewa mkubwa kuhusiana na jambo la nyumba.

KIRI MAOMBI HAYA KWA IMANI:

Mungu Baba kwa Jina la Yesu Kristo ninakushukuru kwa Neema yako na upendo wako juu ya maisha yangu asante kwaajili ya Uhai na Uzima ambao umenipa Mimi na kuwapa watu wa familia na uzao na nyumbani mwangu asante kwa siku mpya ya Leo...... Ninaibariki kwa Jina la Yesu Kristo na kuitakasa kwa Damu ya Yesu Kristo na kuifungua nami natangaza nitaishi katika siku iliyobarikiwa na kutakasika kwa Jina la Yesu Kristo

Mungu ninafuta kwa Damu ya Yesu Kristo maishani mwangu uhalali wowote wa shetani na kuzimu na roho zote za giza walionao maishani mwangu kupitia nyumba nilizowahi kulala na kuishi natangaza huo uhalali wao uondoke kwenye maisha yangu kwa Jina la Yesu Kristo

Leo Mimi...... Ninayafungua maisha yangu kwa Jina la Yesu Kristo yaliyofungwa rohoni kupitia nyumba nilizowahi kulala na kuishi na nafsi yangu iliyofungwa kwenye hizo nyumba Leo ninaikomboa na kuifungua kwa Jina la Yesu Kristo kila mtu wa familia yangu na uzao wangu na nyumbani mwangu ambaye maisha yake yamefungwa kupitia nyumba walizowahi kulala na kuishi Leo nayafungua maisha yao kwa Jina la Yesu Kristo

Ninaomba Mungu kwa Mkono wako unifungue katika vifungo vyote vya kiroho ambavyo shetani na kuzimu na maadui walinifunga kupitia nyumba nilizowahi kulala na kuishi Leo naomba hivyo vifungo viharibike maishani mwangu na kuvunjika na maisha yangu yapate kuwa huru kabisa kwa Jina la Yesu Kristo

Kila hatua zangu za Maisha zilizok**atwa kupitia nyumba walizowahi kulala na kuishi Leo nazikomboa kwa Damu ya Yesu Kristo hatua zangu za Maisha na kuzifungua kwa Jina la Yesu Kristo

Natangaza Kusudi la maisha yangu ya uumbaji lililofungwa kiroho kupitia nyumba nilizowahi kulala na kuishi Leo Damu ya Yesu Kristo na Jina la Yesu Kristo linafungua Kusudi la Mungu maishani mwangu nami nitaishi na kulitumikia kusudi la Mungu Kila siku maishani mwangu hapa duniani na watu wa familia na uzao wangu ambao wamefungwa na vifungo mbalimbali kiroho kupitia nyumba walizowahi kulala na kuishi leo natangaza kufunguliwa kwao kwa Jina la Yesu Kristo

Asante Mungu Baba kuyafungua maisha yangu na Mimi nitayaishi maisha yangu halisi ya uumbaji hapa duniani kila siku kwa Jina la Yesu Kristo na watu wa familia na uzao na nyumbani mwangu wataishi maisha yao halisi ya uumbaji hapa duniani kwa Jina la Yesu Kristo

Ninaiombea siku hii mpya nikiomba Baraka zako zizidi kuonekana maishani mwangu na Neema yako Mungu isimame nami na Mkono wako uzidi kunitendea mema Mimi na watu wa familia na uzao na nyumbani mwangu asante kwa ulinzi wako katika maisha yetu na hatua zetu za Maisha zinazongozwa na wewe Mungu Baba kila siku katika Jina la Yesu Kristo ninaomba na kuamini Amen.

➡️ Endelea kukaa kwenye haya maombi ya kujifungua kiroho kutoka kwenye nyumba ili uzidi kuwa huru.

Mimi ni rafiki yako katika Kristo Yesu

Mwalimu Samwel Kibiriti.

October 29, 2024

Mang'ola Karatu, Arusha Tanzania.

KWA USHAURI WA KIROHO NA MAOMBEZI WASILIANA NAMI KWA NUMBER HII YA UTUMISHI PIA TUMIA NUMBER HII KUWA CHOMBO CHAKO CHA SADAKA MBELE ZA MUNGU +255 765 867574 NA MUNGU AYABARIKI NA KUYAFUNGUA MAISHA YAKO.

Tuungane tena siku ya Kesho ambapo tutakaa kwenye Maombi kwa pamoja mbele za Mungu kushughulia chanzo kingine kilichokwamisha maisha yetu.

Washirikishe wengine IBADA hii nao wapate Maarifa na kufunguliwa na Mungu ili waishi maisha ya uhuru.

26/10/2024

MADHABAHU YA IBADA YA SIKU MPYA, KIZAZI CHA KUSUDI LA MUNGU DUNIANI ( 91 ).

Bwana Yesu Kristo asifiwe mwana wa Mungu karibu katika IBADA ya SIKU MPYA ya Leo ambapo Mungu Baba atatuhudumia Kwa Mkono na nguvu zake.

SIKU 10 ZA KUOMBA MBELE ZA MUNGU KUSHUGHULIA VYANZO VILIVYOKWAMISHA MAISHA YAKO ROHONI.

Haya ni maombi ya kushughulikia vyanzo ambavyo vimetufanya tusiishi katika maisha yetu ya Kusudi hapa duniani hivyo Kwa maombi haya mbele za Mungu atatufungua na kutuweka huru.

( Day 5 mbele za Mungu ):

➡️ MAOMBI YA LEO NI KUSHUGHULIKIA CHANZO CHA ROHO YA UGANGA WA KIENYEJI NA USHIRIKINA ILIYOKWAMISHA MAISHA YAKO.

🔶 Chanzo kingine ambacho kimek**ata na kukwamisha maisha ya wanadamu hapa duniani ni uganga wa kienyeji na ushirikina nataka ufahamu kwamba uganga ni roho kamili kutoka kuzimu ambayo imebeba utendaji kazi wa kishetani na roho hii imehusika sana na inazidi kuhusika kukwamisha maisha ya wanadamu wasiishi kwenye Kusudi la Mungu na kuishi maisha yao original hapa duniani

Kwahiyo hakikisha unaingia kwenye Maombi mbele za Mungu na kuivunja na kuisambaratisha roho hii ya uganga wa kienyeji na ushirikina ambayo imevamia maisha yako na kukufungua usiyaishi maisha yako halisi ya uumbaji wa Mungu hapa duniani.

2Mambo ya Nyakati 33:4

🔶 Ukisoma Biblia inasema wazi kuwa akafanya uganga hivyo maisha yako yanaweza kufanyiwa mambo ya uganga wa kienyeji na ushirikina ili yafungwe na kujikuta unaishi maisha ya kuteseka na magonjwa na maisha magumu ambao sio mpango wa Mungu hivyo hakikisha unavunja kila uganga wa kienyeji na ushirikina uliofanyiwa kwa siri kwenye madhabahu za kishetani.

Hesabu 23:23

🔶 Katika mstari huu Biblia inaweka wazi kwamba uganga wa kienyeji unaweza kukaa juu ya maisha ya mtu hivyo hakikisha unasambaratisha roho ya uganga wa kienyeji iliyokaa juu ya maisha yako na juu ya maeneo mbalimbali yanayogusa maisha yako sababu ukiiacha hiyo roho ya uganga wa kienyeji izidi kukaa juu ya maisha yako itahakikisha hauishi maisha yako ya Kusudi hapa duniani pia itahakikisha unaishi maisha magumu naya kuteseka na kulia na huzuni kila siku hivyo tumia Mamlaka ya Jina la Yesu Kristo kuivunja na kuisambaratisha roho ya uganga wa kienyeji na ushirikina maishani mwako.

Kwahiyo siku ya Leo Kaa kwenye haya maombi mbele za Mungu katika IBADA hii na kuishughulikia roho ya uganga wa kienyeji na ushirikina isikae tena na kutenda kazi tena maishani mwako nawe uwe huru kabisa, ivunje hii roho ya uganga wa kienyeji na ushirikina kwenye familia na uzao wako na kwenye hiyo nyumba mnayoishi, ivunje hii roho ya uganga wa kienyeji na ushirikina kwenye ndoa na kazi zako za mikono na kwenye Elimu ya watoto wako na kwenye uchumi wako na kwenye Afya yako na maeneo yote yanayogusa maisha yako.

KIRI MAOMBI HAYA KWA IMANI MBELE ZA MUNGU:

Mungu Baba katika Jina la Yesu Kristo ninakushukuru kwa upendo wako juu ya maisha yangu na upendo wako juu ya maisha ya watu wa familia na uzao na nyumbani mwangu asante kwa Uzima na Uhai ambao umetupatia na mema yote ambayo umezidi kututendea maishani mwetu na katika familia na uzao na katika nyumba zetu na miji yetu na nchi yetu

Ninaomba toba na rehema mbele zako Mungu kutokana na maisha yangu ninayoishi hapa duniani kila siku nimeziendea njia za uganga wa kienyeji na ushirikina na familia na uzao wangu tumeziendea njia za uganga wa kienyeji na ushirikina ninaomba uturehemu kwa Damu ya Yesu Kristo ili Leo Mungu utufungue kutoka kwenye vifungo vya roho hii ya uganga wa kienyeji na ushirikina na kila uhalali ambao Mimi na uzao wetu tumeipatia hii roho ya uganga wa kienyeji na ushirikina kutokana na njia zetu na matendo yetu huo uhalali ninaufuta kwa Damu ya Yesu Kristo na kuuondoa kwa Jina la Yesu Kristo hautakuwepo tena kuanzia sasa

Ninasimama mbele zako Mungu Baba kwa Mamlaka ya Jina la Yesu Kristo ninaivunja roho ya uganga wa kienyeji na ushirikina iliyokaa juu ya maisha yangu Mimi...... Na iliyokaa juu ya maeneo mbalimbali ya maisha yangu natangaza iweze kuvunjika na kusambaratika kwa Jina la Yesu Kristo na hii roho ya uganga wa kienyeji na ushirikina iliyokaa kwenye maisha ya watu wa familia na uzao na nyumbani mwangu ninaisambaratisha na kuivunja maishani mwao kwa Jina la Yesu Kristo

Ninayakomboa kwa Damu ya Yesu Kristo maisha yangu Mimi....... ambayo yametekwa na kuk**atwa na roho ya uganga wa kienyeji na ushirikina natangaza yaaachiliwe kwa Jina la Yesu Kristo na maisha ya watu wa familia yangu na uzao wangu na nyumbani mwangu yaliyotekwa na kuk**atwa na roho hii ya uganga wa kienyeji na ushirikina Leo ninayakomboa maisha yao kwa Damu ya Yesu Kristo

Mungu Baba ninatangaza kwa Jina la Yesu Kristo kuyafungua maisha yangu Mimi...... kutoka kwenye vifungo vyote vya roho ya uganga wa kienyeji na ushirikina ninaviharibu hivyo vifungo maishani mwangu kwa Jina la Yesu Kristo kila eneo la maisha yangu lililofungwa na roho ya uganga wa kienyeji na ushirikina ninayafungua maeneo yote hayo kwa Jina la Yesu Kristo na maisha ya kila mtu wa familia yangu na uzao wangu na nyumbani mwangu yaliyofungwa kwenye vifungo vya roho ya uganga wa kienyeji na ushirikina ninayafungua kwa Jina la Yesu Kristo

Ninaiharibu kabisa roho ya uganga wa kienyeji na ushirikina katika maisha yangu Mimi..... kwa Jina la Yesu Kristo haitatenda kazi tena naiteketeza kwa moto wa Yesu Kristo roho hii ya uganga wa kienyeji na ushirikina katika familia na uzao na kwenye hii nyumba tunayoishi na kwenye miji yetu na nchi yetu kwa Jina la Yesu Kristo

Asante Mungu Baba kwa Mkono wako na nguvu zako ambapo Leo umenifungua mimi..... na kuyafungua maisha yangu kutoka kwenye roho ya uganga wa kienyeji na ushirikina asante pia Mungu kuyafungua maisha ya watu wa familia na uzao na nyumbani mwangu kutoka kwenye roho hii ya uganga wa kienyeji na ushirikina katika Jina la Yesu Kristo

Ninakushukuru kwa siku mpya ya Leo ya..... ambapo ninaitakasa na kuibariki kwa Damu ya Yesu Kristo ninatangaza ninaishi katika siku iliyobarikiwa na kufunguliwa na kukombolewa na uwepo wako na ulinzi wako na Baraka zako na Neema yako Mungu Baba itakuwa pamoja nami siku ya Leo pia ulinzi wako Mungu na Neema yako na uwepo wako utakuwa pamoja na maisha ya kila mtu wa familia na uzao na nyumbani mwangu kwa Jina la Yesu Kristo

Asante kwa matendo yako makubwa unayozidi kunitendea Mimi na kuitendea familia na uzao wetu na nchi yetu ya...... kwa Jina la Yesu Kristo malaika wa ufalme wako Mungu wanihudumie maishani mwangu siku ya Leo katika Jina la Yesu Kristo ninaomba na kuamini Amen.

➡️ Endelea kukaa kwenye Maombi haya kadiri Roho Mtakatifu anavyokuongoza na Mimi nakutangazia Kwa Jina la Yesu Kristo Mungu amekufungua kutoka kwenye roho ya uganga wa kienyeji na ushirikina na uko huru kabisa kimaisha.

Mimi ni rafiki yako katika Kristo Yesu

Mwalimu Samwel Kibiriti.

October 26, 2024

Mang'ola Karatu, Arusha Tanzania.

KWA USHAURI WA KIROHO NA MAOMBEZI WASILIANA NAMI KWA NUMBER HII YA UTUMISHI PIA TUMIA NUMBER HII KUWA CHOMBO CHAKO CHA SADAKA MBELE ZA MUNGU +255 765 867574 NA MUNGU AYABARIKI NA KUYAFUNGUA MAISHA YAKO.

Tuungane tena siku ya Kesho ambapo tutakaa kwenye Maombi kwa pamoja mbele za Mungu kushughulia chanzo kingine kilichokwamisha maisha yetu.

Washirikishe wengine IBADA hii nao wapate Maarifa na kufunguliwa na Mungu ili waishi maisha ya uhuru.

24/10/2024

MADHABAHU YA IBADA YA SIKU MPYA, KIZAZI CHA KUSUDI LA MUNGU DUNIANI ( 89 ).

Bwana Yesu Kristo asifiwe mwana wa Mungu karibu katika IBADA ya SIKU MPYA ya Leo ambapo Mungu Baba atatuhudumia Kwa Mkono na nguvu zake.

SIKU 10 ZA KUOMBA MBELE ZA MUNGU KUSHUGHULIA VYANZO VILIVYOKWAMISHA MAISHA YAKO ROHONI.

Haya ni maombi ya kushughulikia vyanzo ambavyo vimetufanya tusiishi katika maisha yetu ya Kusudi hapa duniani hivyo Kwa maombi haya mbele za Mungu atatufungua na kutuweka huru.

( Day 4 mbele za Mungu ):

➡️ MAOMBI YA LEO NI KUMUOMBA MUNGU AYAFUNGUE MAISHA YAKO ALIYOKUPANGIA KUYAISHI HAPA DUNIANI AMBAYO YAMEKWAMISHWA NA CHANZO CHA DAMU.

Wako watu wengi sana ambao wanashindwa kuishi maisha yao halisi ya uumbaji hapa duniani waliyopangiwa na Mungu kutokana na kukwamishwa na damu walizowahi kuzimwaga zisizokuwa na hatia na kujikuta nje ya maisha ya Kusudi la Mungu.

Fahamu kwamba damu inafanya kazi kwenye ulimwengu wa roho ila matokeo yake huonekana kwenye ulimwengu wa mwili hivyo unapoona husongi mbele kimaisha ni lazima rohoni Kuna chanzo kinachotumika kukukwamisha ambacho unahitajika kukifanyia kazi ili maisha yako yasonge mbele sawasawa na Mapenzi ya Mungu.

Mambo ya Walawi 17:11

🔶 Neno la Mungu linasema kwamba damu ni uhai hivyo unapomwaga damu unaondoa uhai wa kiumbe pia damu hufanya upatanisho hivyo unapomwaga damu kwenye mambo ya ushirikina au kwenye mambo ya uganga wa kienyeji au kwenye mambo ya miungu ujue wazi kwamba rohoni kupitia hiyo damu maisha yako yameunganishwa na madhabahu za kishetani ndio maana unajikuta maisha yako yanapigwa na maroho mbalimbali machafu kutoka kuzimu.

Mwanzo 4:8-16

🔶 Kaini alimwaga damu ya Habili isiyokuwa na hatia na kilichotokea damu ikatoa sauti na ardhi ikazuia mafanikio ya Kaini lakini pia ardhi ilimtengenezea Kaini aina ya maisha ya kutangatanga

Hii inatufundisha kwamba unapomwaga damu isiyokuwa na hatia iwe ya mwanadamu au damu ya mnyama au ndege hiyo damu itatoa sauti na kujikuta huwezi kuishi kwa utulivu kutokana na sauti hiyo ya damu lakini pia ukimwaga damu ardhi itasimama kinyume na maisha yako na itakuzuia usifanikiwe kwenye viwango vya utukufu wa Mungu na tena ardhi itageuza maisha yako badala ya kuishi maisha ya mafanikio na Baraka na ushindi na utulivu na Amani na furaha utajikuta unaishi maisha ya mateso na mahangaiko na magumu na kutokuwa na amani kabisa sababu rohoni Kuna damu uliyomwaga wewe au kumwagwa na uzao wenu hivyo ni lazima ukae kwenye Maombi mbele za Mungu kuomba Toba na Rehema.

Mwanzo 9:6

🔶 Mungu haruhusu kabisa mwanadamu kumwaga damu ya mwanadamu mwenzake hivyo ikiwa ni wewe au familia yenu na ukoo wenu walifanya matendo ya kumwaga damu unahitajika kuingia kwenye Maombi ya Rehema mbele za Mungu k**a unahitaji kuishi maisha ya Kusudi la Mungu hapa duniani na k**a unataka kuwa huru na usijaribu kabisa kumwaga damu iwe ya mwanadamu au ya wanyama au ya ndege kwenye mambo ya ushirikina na uganga wa kienyeji na kwenye ibada za miungu usijaribu kabisa tena.

Kutoka 12:13

🔶 Mungu aliwaambia Wana wa Israeli kwamba ile damu watakayoiweka kwenye miimo na milango ya nyumba zao itakuwa ni Ishara, hivyo kwenye ulimwengu wa roho damu inaweza kubeba Ishara ya aina fulani. Unaweza kujikuta unapitia mapigo mbalimbali maishani mwako Kuna damu ambayo imesimama kuwa ishara ya mapigo hayo ni lazima uingie kwenye ulimwengu wa roho na kuondoa Ishara zote za damu zilizoelekezwa maishani mwako ili usiendelee kupigwa kimaisha.

Ayubu 16:18

🔶 Ukisoma Biblia iko wazi kwamba Kuna kilio cha damu hivyo Kila damu inayomwagika iwe ya mwanadamu au mnyama au ndege huwaga inalia kutaka kulipizwa kisasi na kilio cha damu hakitakufanya ufurahie kabisa maisha yako ndio maana unaona wazi huna furaha ya maisha huna amani ya maisha huna utulivu wa maisha huna mafanikio n.k kwasababu rohoni kuna kilio cha zile damu ulizomwaga wewe au zilizomwagwa kwenye uzao wenu jambo la kufanya mbele za Mungu kuondoa kilio cha damu maishani mwako ni kuingia kwenye Maombi na Toba na rehema mbele za Mungu tu na kukubali kwamba ulimwaga damu isiyokuwa na hatia na Muombe Mungu akusamehe kwa damu ya Yesu Kristo Kisha Muombe Mungu ayafungue maisha yako kutoka kwenye vifungo vya damu ili uweze kuwa huru.

Zaburi 9:12

🔶 Biblia inasema Kuna mlipiza kisasi cha damu ambaye hufuatilia damu zote zilizomwagika zisizokuwa na hatia ziwe za mwanadamu au wanyama au ndege Kisha kuachilia mapigo Kwa hiyo aliyemwaga damu. Usijaribu kabisa kumwaga damu sababu utaadhibiwa kimaisha na kujikuta katika maisha ya mateso sana hapa duniani usishawishike kumwaga kabisa damu ya mwanadamu au kutoa mimba wala usishawishike kumwaga damu za wanyama au ndege kwenye mambo ya ushirikina au huko kwenye mambo ya waganga wa kienyeji au kwenye ibada za miungu sababu hizo damu zitafuatiliwa na mlipa kisasi cha damu nawe utapata adhabu itakayokutesa kimaisha na k**a ulimwaga damu ingia kwenye Maombi ya Toba na rehema mbele za Mungu naye atakusamehe na kukuondolea hizo adhabu.

Ezekieli 35:7

🔶 Katika ulimwengu wa roho damu inatabia ya kumfuatilia mwanadamu aliyeimwaga na kufuatilia uzao wake na hiyo damu haimfuatilii mwanadamu kukaa naye tu bali humfuatilia ili kumtesa hivyo hakikisha unaomba Toba na rehema mbele za Mungu ili maisha yako yasifuatiliwe na damu ulizowahi kuzimwaga wewe au zilizomwagwa kwenye uzao wenu

Na kumbuka Damu ya Yesu Kristo ndiyo peke yake inayotakiwa kufuatilia maisha yetu wala hazitakiwi damu za wanyama au ndege au wanadamu zitufuatilie kimaisha. Kumbuka ndani ya Damu ya Yesu Kristo Kuna sauti na utendaji kazi mbalimbali ndio maana Mungu anataka hii Damu ya Yesu Kristo peke yake katika safari yetu ya maisha hapa duniani ndio itufuatilie kwenye Kila eneo la maisha yetu ili tuishi kwa Kusudi lake.

Mathayo 27:25

🔶 Ukisoma hapa wale watu waliomtesa Bwana Yesu walipiga kelele kwamba damu iwe juu yao na juu ya watoto wao ninachotaka uone ni kwamba damu inaweza kukaa juu ya maisha ya mwanadamu au juu ya vitu vyake.

Nataka nikuulize swali hili kwenye ulimwengu wa roho juu ya maisha yako iko damu ya nani ya Yesu Kristo au zile ulizomwaga? Za wanyama na ndege na wanadamu?

➡️ Kwenye ulimwengu wa roho juu ya Ndoa yako iko damu ya nani ya Yesu Kristo au damu ulizomwaga za wanadamu na wanyama na ndege?.

➡️ Kwenye ulimwengu wa roho juu ya Kazi zako za mikono iko damu ya nani ya Yesu Kristo au zile ulizomwaga za wanadamu na wanyama au ndege?.

➡️ Kwenye ulimwengu wa roho juu ya maisha yako ya uchumi iko damu ya nani ya Yesu Kristo au zile ulizomwaga za wanadamu na wanyama na ndege?.

➡️ Kwenye ulimwengu wa roho juu ya maisha ya watoto wako iko damu ya nani ya Yesu Kristo au zile ulizomwaga za wanadamu na wanyama na ndege?.

➡️ Kwenye ulimwengu wa roho juu ya mifugo yako iko damu ya nani ya Yesu Kristo au zile ulizomwaga za wanadamu na wanyama na ndege?.

➡️ Kwenye ulimwengu wa roho juu ya familia na uzao na nyumba mnayoishi iko damu ya nani ya Yesu Kristo au zile ulizomwaga za wanadamu na wanyama na ndege?.

➡️ Kwenye ulimwengu wa roho juu ya Elimu ya watoto wako iko damu ya nani ya Yesu Kristo au zile ulizomwaga za wanadamu na wanyama na ndege?.

➡️ Kwenye ulimwengu wa roho juu Afya yako na mwili wako na majina yako iko damu ya nani ya Yesu Kristo au zile ulizomwaga za wanadamu na wanyama na ndege?.

🔶 Nataka niseme tena ni Damu ya Yesu Kristo peke yake ndiyo inayotakiwa kukaa juu ya maisha yako na Juu ya Kila kitu chako k**a unataka kuishi maisha ya Kusudi la Mungu hapa duniani lakini zikikaa damu za wanyama au ndege au wanadamu ujue kwamba maisha yako yatakuwa ya mateso na magumu sana hivyo unahitajika kuingia kwenye Maombi ya Toba na rehema mbele za Mungu kutokana na umwagaji wa damu uliofanya wewe au uliofanyika kwenye uzao wenu na nchi yenu na miji yenu na Mungu atasamehe na kurehemu kwasababu ya Damu ya Yesu Kristo kisha iruhusu Damu ya Yesu Kristo iwe juu ya maisha yako na Juu ya Kila kitu chako.

KIRI MAOMBI HAYA KWA IMANI MBELE ZA MUNGU:

Mungu Baba Kwa Jina la Yesu Kristo moyo wangu unakuazimisha na kukutukuza wewe asante kwaajili ya Uzima na Uhai ambao amekupa Mimi na kuwapa watu wa familia na uzao na nyumbani mwangu asante Kwa Mkono wako ambao unazidi kututendea mema na kutulinda na kututunza Kila siku ya maisha yetu hapa duniani kwaajili ya Kusudi lako la Uumbaji

Nimesimama mbele zako Mungu ninaomba Toba na rehema kutokana na umwagaji wa damu ambao Mimi..... Nimeufanya nakubali kukiri wazi mbele zako kwamba nimemwaga damu zisizokuwa na hatia pia ninaomba rehema zako Mungu kwaajili ya maisha ya Kila mtu wa familia na uzao na nyumbani mwangu kutokana na umwagaji wa damu walioufanya maishani mwao naomba Mungu tusamehe na kuturehemu kwasababu ulisema wazi kwenye Neno lako kwamba tusimwage damu za wanadamu au wanyama na ndege ila sisi tumeshindwa kutii Neno lako na ziko damu tumezimwaga tunaomba Rehema zako Mungu Kwa Damu ya Yesu Kristo

Ninakubali kukiri mbele zako Mungu kwamba katika familia yenu na katika ukoo wetu upande wa baba na mama na katika makabila yetu na katika miji yetu na katika Nchi yetu na taifa letu tumehusika kumwaga damu za wanadamu na tumehusika kumwaga damu za wanyama na ndege ninaomba Mungu tusamehe na kuturehemu kutokana na umwagaji wote wa damu tulioufanya kwenye mambo ya ushirikina na kwenye mambo ya uganga wa kienyeji na uchawi na kwenye ibada za miungu na kimila ninaomba rehema zako Mungu Kwa Damu ya Yesu Kristo

Ninaomba siku ya Leo Mungu Baba unifungue kwenye vifungo vyote vya damu vilivyofunga maisha yangu Mimi....... Na Kila kifungo cha damu kilichofunga maisha ya watu wa familia na uzao na nyumbani mwangu naomba Mungu wafungue na kuwaweka huru na Kila kifungo cha damu kilichoifunga familia na uzao na miji na nchi yetu tufungue Mungu Kwa Jina la Yesu Kristo

Ninaondoa Kila hatia ya damu iliyokaa juu ya maisha yangu Mimi....... Natangaza hizo hatia zote za damu ziondoke kwa Damu ya Yesu Kristo na Kila hatia za damu zilizokaa juu ya maisha ya watu wa familia na uzao na nyumbani mwangu ziondoke kwa Damu ya Yesu Kristo na kila hatia za damu zilizokaa juu ya familia na uzao na nyumba na miji na nchi ziondoke kwa Damu ya Yesu Kristo

Ninatangaza Damu ya Yesu Kristo iweze kunyamazisha damu zote za wanadamu na wanyama na ndege zinazosikika maishani mwangu na katika familia na uzao na nyumba na miji na nchi ili zinyamaze kimya katika Jina la Yesu Kristo

Mungu Baba ninaomba uniondolee Kila adhabu ambayo Mimi........ Nilikuwa naipitia maishani mwangu inayotokana na umwagaji wa damu hizo adhabu zisiwepo maishani mwangu tena Kwa Damu ya Yesu Kristo na Kila adhabu ambazo Mungu tulikuwa tunazipitia kwenye ndoa na kazi na Elimu na afya na uchumi na familia na uzao na kwenye miji yetu na nchi yetu Leo Mungu Kwa Rehema zako tuondolee hizo adhabu za umwagaji wa damu zisiwepo tena Kwa Damu ya Yesu Kristo

Ninaomba Damu ya Yesu Kristo iyakomboe maisha yangu na maisha ya watu wa familia na uzao na nyumbani mwangu na Damu ya Yesu Kristo iyafungue maisha yangu na maisha ya watu wa familia na uzao na nyumbani mwangu na miji yetu na nchi yetu ili tuweze kuwa huru na kuishi maisha ya Kusudi lako Mungu hapa duniani

Ninatangaza kwamba Kwa Damu ya Yesu Kristo maisha yangu yaliyokuwa yamekwamishwa na chanzo cha damu za wanadamu na wanyama na ndege leo kikwazo hicho cha damu kimeondolewa na Mungu wangu kwa Rehema zake katika Jina la Yesu Kristo na Mimi...... NINAISHI maisha yangu halisi ya uumbaji wa Mungu hapa duniani na kufanikiwa kwenye viwango vya utukufu wa Mungu kila siku kwa Jina la Yesu Kristo

Asante Mungu Baba kunifungua na kuniweka huru Mimi....... Na pia asante Mungu kuwafungua na kuwaweka huru watu wa familia na uzao na nyumbani mwangu kwa Jina la Yesu Kristo, asante kwa rehema zako ambazo zimetutoa kwenye mateso yote tuliyokuwa tunayapitia kutokana na umwagaji wa damu na Leo maisha yetu yamefunguliwa nasi tutaishi Kwa kulitumikia na kulikamilisha Kusudi lako la Uumbaji hapa duniani

Asante kwa Baraka zako Mungu na Neema yako Mungu na ulinzi wako Mungu katika maisha yetu na familia na uzao na nyumbani mwetu asante pia Kwa ulinzi wako Mungu katika miji yetu na nchi zetu asante pia kunifanikisha na kuniinua kwenye kazi zangu za mikono hazitakuwa za hasara Bali zitakuwa za Faida Kila siku katika Jina la Yesu Kristo ninaomba na kuamini Roho Mtakatifu niongoze yanipasayo Mimi........ Kuyafanya kila siku ya maisha yangu hapa duniani ili nizae Matunda kwaajili ya Ufalme wa Mungu katika Jina la Yesu Kristo Amen.

➡️ Endelea kukaa kwenye haya maombi mbele za Mungu kadiri Roho Mtakatifu anavyokuongoza. Naamini umebarikiwa na IBADA hii ya siku ya Leo na Mungu Baba ametuhudumia kwenye IBADA hii nakuomba nawe ufanyike Baraka Kwa Mungu kwa njia ya Sadaka zako kupitia Utumishi huu, tumia number ya Utumishi kutoa Sadaka zako Kwa Mungu.

Mimi ni rafiki yako katika Kristo Yesu

Mwalimu Samwel Kibiriti.

October 24, 2024

Mang'ola Karatu Arusha Tanzania.

KWA USHAURI WA KIROHO NA MAOMBEZI WASILIANA NAMI KWA NUMBER HII YA UTUMISHI PIA TUMIA NUMBER HII KUWA CHOMBO CHAKO CHA SADAKA MBELE ZA MUNGU +255 765 867574 NA MUNGU AYABARIKI NA KUYAFUNGUA MAISHA YAKO.

Tuungane tena siku ya Kesho ambapo tutakaa kwenye Maombi Kwa pamoja mbele za Mungu kushughulia chanzo kingine kilichokwamisha maisha yetu.

Want your school to be the top-listed School/college in Arusha?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Website

Address


Arusha