Nyie ni watu wetu wa nguvu, tunajivunia uwepo wenu hapa!! Tunawapenda .
Ilboru Special Needs UNIT
Welcome to official page for Ilboru special needs unit. We promote and provide special educ
The Impossible Can Become POSSIBLE!
04/09/2020
TABIA ZA VIZIWI
Tabia ni matendo au mwenendo unaojirudia na kujenga mazoea ya kutendeka.
Tabia hupimwa au kuchunguzika kwa kutumia misingi ya kisayansi,kiimani au kijamii.
Tabia inaweza kuwa nzuri au mbaya kutegemeana na misingi hiyo.
Zifuatazo ni baadhi ya tabia za viziwi
1️⃣ Viziwi huongea kwa kukosa msawazo wa sauti. Anaweza kuongea kwa kutoa sauti kubwa sana au ndogo sana isioeleweka au kusikika vizuri.
2️⃣ Hukwazika haraka sana wasipotimiziwa mahitaji yao ndani ya wakati
3️⃣ Viziwi wengi hutembea kwa kuburuza au kusugua viatu chini. Kwa kuwa hawasikii sauti itokayo miguuni mwao, huona kawaida.
4️⃣ Hujiamulia mambo yao wenyewe. Mara nyingi huwa hawataki kuongozwa na mtu anayesikia katika mambo yanayowahusu.
5️⃣ Huwa na tabia ya kutomaliza maongezi wanapoyaanza,hivyo hufanya maongezi kuwa marefu.
6️⃣ Asilimia 90% ya viziwi ni wapole kitabia. Ukali na hasira wanazokuwa nazo ni matokeo ya kutotimiziwa mahitaji yao kwa sababu ya ugumu wa mawasiliano, kudharauliwa,kudhihakiwa, kunyanyapuliwa na kuchokozwa.
7️⃣ Viziwi wengi wana vipawa na ni watendaji wazuri wanaojali muda. Wakati wengine wanaosikia wanapozungumza wao hujikita kwenye shuguli zao.
8️⃣ Uziwi ukubwani huwaletea viziwi hali ya kutojiamini au kujitenga. Hii hutokana na wao kuogopa kudharauliwa au kudhihakiwa na wanaosikia.
9️⃣ Huchelewa kujitambua katika umri sahihi kutokana na ugumu wa mawasiliano wakati wa ukuaji, hususana viziwi wa kuzaliwa.
🔟 Baadhi ya viziwi hasa wa ukubwani hawapendi kutumia lugha ya alama badala yake hupendelea kutumia lugha ya mazungumzo kwa kusoma midomo.
Mwenye swali, boresho, nyongeza
Mbarikiwe sana
🙏🏿🙏🏿🙏🏿
14/07/2020
KIZIWI NI NANI?
..Kiziwi ni mtu yeyote ambaye uwezo wake wa kusikia sauti aidha umepungua au umeisha kabisa..
AINA YA VIZIWI
(1) Kiziwi kwa kuzaliwa ( congenitally deaf)
huyu ni mtu yeyote ambaye amezaliwa akiwa kiziwi na hajawahi kusikia sauti yoyote au lugha yoyote ya kusikia( spoken language)
(2) kiziwi kabla ya kupata lugha (Pre lingually deaf)
huyu ni mtu yeyote ambaye amezaliwa anasikia lakini amepoteza uwezo wake wa kusikia kabla hajapata (acquire) lugha ya kusikia,hivyo alipata kidogo lugha mama(mother tongue) na alijifunza kidogo lugha hiyo mama na ndugu wa familia
(3) kiziwi baada ya kupata lugha (post lingually deaf)
huyu ni mtu yeyote ambaye amezaliwa na uwezo wa kusikia lakini alipoteza uwezo wake wa kusikia baada ya kuwa ameshajifunza na kujua lugha ya kusikia na kuongea vizuri
NB; Ni vizuri kufahamu na kutofautisha makundi hayo tajwa ya viziwi hapo juu ili uelewe vizuri kwa nini wapo viziwi ambao wana uwezo mzuri wa kuongea na wapo wengine ambao uwezo wao wa kuongea ni mgumu, hawaongei maneno yanayoeleweka au sentensi zao hazipo sahihi wakati mwingine
PIA, kiziwi hutumia lugha ya alama k**a njia yao kubwa ya mawasiliano, wapo viziwi wenye uwezo mkubwa wa kusoma mdomo (lip reading/speech reading)
Kila mtu amlinde mwenzake, -19
Inclusive Society, tuchukue tahadhari Sana.
13/10/2019
Deaf Religion is Love, Happy Sunday.
13/10/2019
Church Time, Happy Sunday
23/03/2019
23/03/2019
Innocent faces, we love you.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Contact the school
Website
Address
Ilboru Special Needs Unit
Arusha
Opening Hours
| Monday | 07:00 - 15:30 |
| Tuesday | 07:00 - 15:30 |
| Wednesday | 07:00 - 15:30 |
| Thursday | 07:00 - 15:30 |
| Friday | 07:00 - 15:30 |