18/08/2025
NI BUUUURREE....!!! WAHI SASA!!
NI SHULE YA AWALI NA MSINGI INAYOPOKEA WANAFUNZI WENYE UMRI KUANZIA MIAKA MIWILI NA NUSU. MTAALA WA KUFUNDISHIA NI KIINGEREZA.
18/08/2025
NI BUUUURREE....!!! WAHI SASA!!
Wapendwa wazazi, walezi na wadau wa elimu,
kwa unyenyekevu mkubwa kabisa tunapenda kuwaalika katika Siku ya Wazazi itakayofanyika shuleni siku ya Jumamosi tarehe 26/11/2022 kuanzia saa tatu kamili asubuhi mpaka saa nane kamili mchana. Karibu ujionee wanachokipata watoto wakiwa shuleni. Karibu ujionee kazi yetu. Tutafurahi sana kuwa nawe.
Mkurugenzi
Wapendwa wazazi, walezi na wadau wa elimu,
Kwa unyenyekevu mkubwa kabisa tunapenda kuwaalika katika Siku ya Wazazi itakayofanyika shuleni siku ya Jumamosi tarehe 27/11/2021 kuanzia saa tatu kamili asubuhi mpaka saa sita kamili mchana. Karibu ujionee wanachokipata watoto wakiwa shuleni. Karibu ujionee kazi yetu. Tutafurahi sana kuwa nawe.
Mkurugenzi
27/10/2021
KARIBU UCHUKUE FOMU YA KUJIUNGA NA MASOMO MWAKA 2022 LEO.
Tunawatakia kila la heri wahitimu wote wa Darasa la Saba wanaoanza mitihani yao ya Taifa leo. Mwenyezi Mungu awatangulie na kuwaepusha na kila shari. Ameen
Mkurugenzi
07/04/2021
CHETI CHA USAJILI WA BALEWA DAYCARE
17/03/2021
TANZIA
Uongozi wa Balewa Daycare Centre umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Joseph Pombe Magufuli kilichotokea tarehe 17-3-2021. Tunatoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote. Tunaungana na Watanzania wenzetu katika maombolezo ya msiba huu mkubwa kwa taifa letu. Mwenyezi Mungu atujaalie subira na badala ya tulichopoteza.
Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.
Mkurugenzi
BALEWA NURSERY AND PRIMARY SCHOOL INAELEWA HALI NGUMU YA UCHUMI TUNAYOPITIA NA NDIO MAANA:
-ADA ZETU NI NAFUU SANA.
-ADA ZETU TUNATOZA KWA MWEZI.
-MZAZI HALIPII MIEZI AMBAYO MTOTO HAJASOMA.
SAMBAMBA NA HILO, TUNAZINGATIA UBORA WA HUDUMA ZOTE WAPATAZO WATOTO WANAPOKUWA SHULENI.
NAFASI ZINAPATIKANA KWA MADARASA YA AWALI NA DARASA LA I-III.
SHULE INAPATIKANA DAR ES SALAAM, KIBAMBA MONGONI. KM 2 NA NUSU KUTOKA KIBAMBA NJIAPANDA YA SHULE.
JIUNGE NASI LEO.
TUPIGIE: +255712964348
Balewa Daycare Centre Send a message to learn more
SHUKRANI
Kwa niaba ya uongozi wa Balewa Daycare Centre na Balewa Nursery and Primary School, napenda kutoa shukrani za dhati kabisa kwa wazazi, walezi na wadau wote wa elimu waliotuamini na kutuunga mkono. Hakika mmeonesha imani kubwa sana kwetu. Nasi jukumu letu ni kuhakikisha kuwa hatuwaangushi. Tunamwomba Mwenyezi Mungu tuwe sehemu ya ujenzi wa kizazi bora kabisa kitaaluma na kimaadili. Tunamwomba pia Mwenyezi Mungu atujaalie sote uwezo wa kutimiza majukumu yetu kikamilifu kwa ustawi wa watoto wetu. Kwa pamoja tunaweza.
Asanteni sana.
Mkurugenzi
04/01/2021
HUJACHELEWA BADO!!
Mkurugenzi wa Balewa Daycare Centre kwa heshima kubwa kabisa anapenda kutoa shukrani za dhati kwa wafanyakazi wote, wazazi, walezi, wanafunzi na wadau wote wa elimu kwa ushirikiano mkubwa mliouonesha mwaka huu 2020 katika kutimiza malengo ya taasisi yetu. Hakika mafanikio yote tuliyofikia ni kutokana na ushirikiano mliotupa. Mmekuwa chachu ya huduma bora na ya viwango. Tunawaomba muendeleze ushirikiano huu zaidi katika mwaka ujao wa 2021. Tunawatakia kila la heri katika mwaka 2021. Mwenyezi Mungu awabariki sana! Asanteni sana!
Mkurugenzi
| Monday | 08:00 - 15:00 |
| Tuesday | 08:00 - 15:00 |
| Wednesday | 08:00 - 15:00 |
| Thursday | 08:00 - 15:00 |
| Friday | 08:00 - 15:00 |