Risechamp Primary Schools

Risechamp Primary Schools

Share

This means the preparation for a useful life here on this earth and a preparation of pupils and workers for a life hereafter.

Guided by the philosophy of the Seventh-Day Adventist Church, we focus on spiritual growth, discipline, and character development from preschool through secondary school Risechamp Pre and Primary School has adapted Seventhday Adventist Philosophy of Education which holds holistic view of human being-that is restoration of the lost image of God in humankind through the harmonious development of the physical, mental, social and spiritual dimensions of life.

Photos from Risechamp Primary Schools's post 03/06/2026

πŸ˜„πŸŽ‰ Kwa kweli imependeza!

Kwa kuwa watoto wetu si wachoyo, wanawakaribisha nanyi muonje matunda ya furaha yao. πŸ˜‹πŸ½οΈ

Mambo ya Class Party hayo! Pilau tamu, nyama kwa wingi, vinywaji na burudani ya kutosha. Hatuwi wanyonge kabisa! πŸ˜‚πŸŽŠ

Karibuni wazazi wetu wapendwa muungane na watoto wetu katika kusherehekea mafanikio yao na kufurahia siku hii maalum pamoja.

🏫 Risechamp School – Mahali ambapo elimu, malezi na furaha hukutana.

02/06/2026

πŸ™βœ¨ Day 2 – Juma la Maombi Linaendelea βœ¨πŸ™

Tunajifunza kwa vitendo!

Leo wanafunzi wetu waliwasilisha igizo lenye mafunzo makubwa kuhusu mtu asiyeona, mlemavu asiye na mikono, na mlevi. Kulikuwa na makundi mawili ya watu; wale waliopita bila kutoa msaada wowote, na wale walioguswa mioyoni mwao na kutoa msaada kadiri walivyoweza.

Kupitia somo hili, watoto wamejifunza umuhimu wa huruma, upendo, kujali wengine na kuwa tayari kusaidia wenye mahitaji. Hata Yesu alitumia mifano na matendo kufundisha na kuelewesha wanafunzi wake walipokuwa wakimuuliza maswali.

Risechamp, tunaamini kuwa elimu bora inahusisha malezi ya mtoto kiakili, kimwili na kiroho, ili akue akimpendeza Mungu na wanadamu.

Tunaendelea kumkabidhi Mungu watoto wetu, tukiamini kwamba kwa kuwa tunamkimbilia Yeye, atawafanya kuwa vichwa na si mikia, viongozi na si wafuasi. Amen! πŸ™Œβ€οΈ

02/06/2026

Kesho, tarehe 3 Juni 2026, baada ya ratiba za maombi, wanafunzi wetu watakuwa na Class Parties maalum kwa ajili ya kuhitimisha Muhula wa Kwanza wa Mwaka wa Masomo 2026. πŸŽ‰πŸ“š

Ni wakati wa kusherehekea mafanikio, kujenga urafiki na kufurahia matunda ya juhudi zilizowekwa katika kipindi chote cha muhula. Tunawatakia wanafunzi wote siku njema yenye furaha, umoja na kumbukumbu nzuri.

Photos from Risechamp Primary Schools's post 01/06/2026

πŸ‘†βœ¨ Baadhi ya picha za watoto wetu wakiwa katika Siku ya Kwanza ya Wiki ya Maombi hapa Risechamp. πŸ™πŸ“–

Tunamshukuru Mungu kwa kuendelea kuwa pamoja nasi katika safari hii ya kiroho na kielimu. Mungu aendelee kuwabariki watoto wetu, wazazi na familia zote za Risechamp. πŸŒŸπŸ™

31/05/2026

May this beautiful Sunday bring peace, joy, love and countless blessings to you and your family. May God’s grace guide your steps and fill your heart with hope for the week ahead. 🌿✨

β€œThis is the day the Lord has made; let us rejoice and be glad in it.” β€” Psalm 118:24 πŸ“–πŸ’–

30/05/2026

πŸŽΆπŸ™ Watoto wanapomuimbia Mungu, mioyo yao hujazwa furaha, amani na upendo. Sifa na nyimbo za kumtukuza Mungu huwasaidia kukua kiroho, kujenga maadili mema na kumtegemea Mungu katika kila hatua ya maisha yao. ✨🌿

β€œMsifuni Bwana kwa nyimbo na vigelegele vya furaha.” πŸŽ΅πŸ’–

29/05/2026

πŸ™βœ¨ Wiki ya Maombi kwa Watoto Wetu – Risechamp

Kuanzia tarehe 1 Juni 2026 hadi 3 Juni 2026, tutakuwa na Wiki maalum ya maombi kwa watoto wetu hapa Risechamp, itakayoongozwa na Mtumishi wa Mungu, Mchungaji Yohana Sevuri. πŸŒΏπŸ“–

Tutatumia muda huu kumshukuru Mungu kwa neema yake kubwa ya kutuwezesha kuhitimisha salama muhula wa kwanza wa mwaka wa masomo 2026, pamoja na kuwaombea watoto wetu wapendwa katika safari yao ya elimu na maisha. πŸ™βœ¨

Tunawaalika wazazi, walezi na jamii yote kuungana nasi katika maombi haya muhimu. Mungu aendelee kuwabariki nyote kwa wingi. 🌟

πŸ“Œ Wazazi, tunawasihi hakikisheni hakuna mtoto anayekosa juma hili muhimu la maombi.

πŸ“– β€œWaacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie; kwa maana ufalme wa Mungu ni wa watu k**a hao.” β€” Marko 10:14

29/05/2026

πŸ™βœ¨ Happy Sabbath!

May this Sabbath bring peace, joy, rest, and countless blessings to you and your family. Let us rejoice and be glad in this beautiful day the Lord has made. πŸŒΏπŸ’–

Photos from Risechamp Primary Schools's post 29/05/2026

🌟 Hongereni sana dada mkuu na kaka mkuu wetu kwa kushika hatamu za uongozi! πŸ‘‘βœ¨

Tunawaombea hekima, ujasiri na moyo wa kuwatumikia wanafunzi wenzenu kwa upendo na uwajibikaji. Mungu awabariki sana na awaongoze katika safari yenu ya uongozi. πŸ™πŸ“š

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Address


Kwa Mzungu. Mpiji Magoe
Dar Es Salaam
100255

Opening Hours

Monday 08:00 - 04:00
Tuesday 08:00 - 04:00
Wednesday 08:00 - 04:00
Thursday 08:00 - 04:00
Friday 08:00 - 04:00