Pugu Boys Secondary and High School

Pugu Boys Secondary and High School

Share

P. O. Box 9090,
Dar Es Salaam. School Motto: Aim At Excellence. Docebit Vos Omnia.

03/06/2026



Form Six PCB, Class of 2020.

02/06/2026

Family ✊❤️


30/05/2026

REPOST FROM PUGU ALUMNI

Tumepokea kwa masikitiko makubwa na huzuni nyingi taarifa ya kifo cha Elisha Lucas, mwanafunzi wa Kidato cha Nne Pugu Boys Secondary and High School

Kwa hakika, tumepoteza mwanafamilia, ndugu na rafiki yetu mpendwa. Kuondoka kwake kumeacha pengo kubwa na majonzi makubwa katika mioyo yetu.

Tunatoa salamu za pole kwa Mkuu wa Shule, walimu, wanafunzi, familia, ndugu, jamaa, marafiki, na wote walioguswa na msiba huu mzito. Katika kipindi hiki kigumu, tunaungana kwa moyo mmoja kuomboleza msiba huu na kushiriki maumivu ya waliobaki.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, Amina!

Pumzika kwa amani, Elisha Lucas. Utaendelea kukumbukwa daima 🕊️🙏

29/05/2026

TANZIA

Kwa huzuni na majonzi makubwa, familia ya Shule ya Sekondari Pugu tunaomboleza kifo cha mwanafunzi wetu mpendwa wa Kidato cha Nne, Elisha Lucas, kilichotokea usiku wa kuamkia leo.

Leo familia ya Pugu imepoteza mmoja wa watoto wake. Wanafunzi wamepoteza rafiki, walimu wamepoteza mwanafunzi wao, na dunia imepoteza kijana mwenye ndoto na maisha yaliyokuwa bado yanaendelea kujengwa.

Katika kipindi hiki kigumu na chenye maumivu, tunaungana kwa moyo mmoja kutoa pole za dhati kwa wazazi, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu mzito. Tunamuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na awape nguvu wote wanaopitia maumivu ya kuondokewa naye.

Pumzika kwa amani, Elisha Lucas. Jina lako na kumbukumbu zako vitaendelea kuishi ndani ya familia ya Pugu milele.

Photos from Pugu Boys Secondary and High School's post 29/05/2026

STANDARD CHARTERED TANZANIA YAWAFIKIA WANAFUNZI PUGU SEKONDARI

Siku ya Jumamosi, tarehe 23 Mei, Standard Chartered Tanzania ilitembelea Pugu Boys Secondary and High School kwa ajili ya kikao cha kujitolea kilicholenga kutoa ushauri na kuwajengea uwezo wanafunzi wetu.

Kikao hicho kiliongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Standard Chartered Tanzania, Bw. Herman Kasekende, pamoja na wafanyakazi wengine wa taasisi hiyo, ambapo wanafunzi walipata elimu kuhusu uchaguzi wa taaluma, elimu ya fedha, namna ya kukabiliana na ushawishi wa marafiki pamoja na kufanya maamuzi sahihi katika maisha.

Tunajivunia ushirikiano huu unaoendelea kuwekeza katika kizazi kijacho na kuwasaidia vijana kufikia ndoto na uwezo wao kamili.

Photos from Pugu Boys Secondary and High School's post 29/05/2026

Pata Ujuzi Gawia Umma.

Photos from Pugu Boys Secondary and High School's post 28/05/2026

REPOST FROM PUGU ALUMNI

Usikose Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Pugu Alumni, Jumapili hii!

Jiunge kupitia Google Meeting:
https://calendar.app.google/aKDBH5SiBDSVrDgBA

Pia jiunge na WhatsApp Group la Alumni kupitia link iliyopo kwenye bio.

28/05/2026



Form Six EGM, Class of 2008.


28/05/2026

2001 ✨

Meet our Form One students back in 2001 — from left: Abdul Salehe, Arphaxad Mukama, and Andrew Hayuma.


Photos from Pugu Boys Secondary and High School's post 27/05/2026

The boys wish you a Happy Eid al-Adha.

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Address


P. O. Box 9090
Dar Es Salaam
12112

Opening Hours

Monday 07:15 - 14:25
Tuesday 07:15 - 14:25
Wednesday 07:15 - 14:25
Thursday 07:15 - 14:25
Friday 07:15 - 11:15