Peas Care Academy

Peas Care Academy

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Peas Care Academy, College & University, Kivule kwa mzee wa simba, Dar es Salaam.

28/05/2022
25/05/2022
20/05/2022
20/05/2022

Michezo

20/05/2022
18/05/2022

Movie Kali sana

18/05/2022
18/05/2022

Afya ya akili

07/05/2022

Historian fupi ya mtoni kwa azizi ali

13/04/2022

NAMNA HISTORIA YAKO IMEATHIRI MAISHA YAKO
Ikiwa umepoteza matumaini ya kuwa na mahusiano mazuri na watu wengine,huna imani k**a utapata mtu wa kukupenda na kukujali au kukusikiliza tambua hali yako haijatokea kwa bahati mbaya kuna matukio yapo nyuma ya pazia

Kuna tabia ya kutaka kumfurahisha kila mtu au people pleaser hii husababishwa na makuzi ya mtu pia kuna madhara yake kisha watu hukata tamaa wakiona maisha yapo tofauti

Kuna watu walikuwa wema sana kwa wengine lakini hivi sasa sio wema tena badala yake wamekuwa hawana huruma hata kidogo

Jaribu kuangalia k**a unaamini yafuatayo
1.Natakiwa kufanya kazi zote ambazo watu wengine wanatarajia niwafanyie
2.Natakiwa kumjali sana kila mtu nyakati zote iwe wameomba msaada au hawajaomba

3.Natakiwa kumsikiliza kila mtu mwenye matatizo nyakati zote na kumtafutia ufumbuzi kwa nguvu zote

4.Natakiwa kuwa mwema sana na kuepuka kuumiza hisia za mtu yeyote
5.Natakiwa kuwafanya kipaumbele watu wengine kabla yangu

6.sitakiwi kusema hapana kwa mtu yeyote ambaye ataomba chochote kwangu
7.Natakiwa kuepuka kumvunja moyo mtu yeyote kwa njia zozote zile

8.Natakiwa kuwa na furaha na nisionyeshe uso wa hasira kwa mtu yeyote
9.Natakiwa kumfurahisha kila mtu na kuwapa furaha watu wote nyakati zote
10.Sitakiwi kumpa mtu yeyote mzigo wa kunipa msaada wa matatizo yangu au mahitaji yangu

Kisha unaweka matarajio yafuatayo ambayo sio sahihi
1.Watu wote wanatakiwa kunisifia, kunipenda, kunijali kwa sababu nimefanya yote hayo kwao

2.Kila mtu anatakiwa kuniunga mkono kwa sababu huwa nafanya kazi kubwa sana ya kuunga mkono kila mtu

3.Watu wote hawatakiwi kunikataa,kunikosoa,kwa sababu huwa natimiza matarajio yao yote siku zote

4.Watu wote wanatakiwa kunijali sana,kunipa msaada nikiwa na maumivu,kwa sababu huwa nasaidia sana watu wenye matatizo

5.Watu wote wanatakiwa kunisapoti,kuwa fair kwangu,kunifanyia wema kwa sababu huwa nafanya wema kwao nyakati zote

6.Watu wote hawatakiwi kuniacha mpweke,kunitenga,kunibagua, kunifikiria vibaya, kwa sababu siku zote najitoa kwao ili wawe wenye kunihitaji sana siku zote

7.Watu wote hawatakiwi kuwa na hasira dhidi yangu zote,wanatakiwa kutimiza ahadi,kupokea simu haraka sana na kujibu sms zangu haraka kwa sababu huwa nafanya hivyo kwao nyakati zote hata nikiwa na kazi nyingi

Baada ya kujiwekea hayo matarajio 7 ambayo sio halisi unapata matukio tofauti sana ambayo hukuachia maumivu makali sana

Matukio ambayo hujitokeza kwako ni
Watu wanakuja kwako wakiwa na matatizo na ukiwa na matatizo huwaoni,unakataliwa sana kuliko wengine,ahadi zinavunjwa sana,kila unaempenda haonyeshi hisia kwako,kila ukipanga jambo hakifanikiwi,unakuwa na hasira ndani kwa ndani na hujui chanzo

Kutokana na matukio ya kuumizwa sana mara kwa mara unajikuta umeanza kujenga tabia zifuatazo

Unajiona kuna kitu hakipo sawa na huwezi kukitambua,
Unajiona tofauti sana na wengine
Upo na hasira dhidi yako mwenyewe bila sababu

Umepoteza matumaini ya kuishi,huna malengo tena unakaa tu siku ziende

Unajilazimisha kufanya kazi lakini unaishia tu kupata hasira na kuishia njiani ,una ahirisha sana kazi zako

Unaficha maumivu yako ili watu wengine wasijue k**a unateseka ndani kwa ndani

Unajiona mnyonge sana ukiwa na wengine na huwezi kuchangamka ukiwa na watu

Upo na hasira za kila wakati na hujui zinatoka wapi,ukipata kikwazo tu unakata tamaa na kuvunjika moyo

Wengine hutumia nguvu kuziondoa hasira,wengjne pombe ,wengine kujitenga,wengine kuanza kulia kila siku

Unajichukia sana na kujiona hustahili kuishi,unajikosoa vibaya sana na kujilaumu kupita kiasi

Unajiona upo na dosari nyingi sana kuliko watu wote duniani
Huwezi kusimulia maumivu yako na matatizo yako hata kwa watu wako wa karibu

Unaamini utakataliwa sana hata ujitoe kiasi gani
Unaogopa kuanzisha mahusiano na mtu yeyote na kila anayetaka kujenga ukaribu na wewe unaanza kumkwepa au hujibu sms zake

Unaamini mtu yeyote akijua uhalisia wako hawezi kukupenda

NB(watu wenye matukio ya fedheha kubwa sana huwa wasiri sana kupita kiasi na ukitaka kumjua tu anavunja mahusiano au anakukwepa ,ukiuliza historia yake hajibu ,anakaa kimya au anabadili mada ,hataki ujue ndugu ,zake wala asili yake wala kazi zake au maisha yake binafsi ,mtaonana nje nje tu sio kujua anapoishi kwa sababu yupo na siri nzito zenye fedheha kubwa kupita kiasi hataki ujue chochote

Hujiona mvivu sana,hufanya kazi chini ya viwango,

Hawezi kufuata deadline zaidi huchelewa kumaliza kazi

Hutumia sana pesa bila mpangilio, huchanganyikiwa haraka sana kwa maelekezo makubwa

Chanzo cha yote hayo tazama historia yako.
Hukuwa karibu na wazazi,unaona upo na dosari kibao za muonekano,unajiona huna thamani kwa muda mrefu sana

Kupata kitabu cha
1.UTULIVU WA AKILI KIPINDI KIGUMU (Softcopy)
2.FIKRA ZAKO FURAHA YAKO (softcopy)
3TIBA YA MSONGO WA MAWAZO (hardcopy & softcopy)
4.BADILI FIKRA ZAKO BADILI MAISHA YAKO (hardcopy & Softcopy)
5.MALEZI YA UBONGO KISAYANSI( hardcopy & softcopy)
6.TABIA ZA WATU WALIOFANIKIWA (Hardcopy & softcopy)

7.MISINGI 10 YA FURAHA SIKU ZOTE (hardcopy &softcopy)

+255766862579
+255622414991

Imeandikwa na Psychologist
Said Kasege
Temeke,Dar es salaam

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address


Kivule Kwa Mzee Wa Simba
Dar Es Salaam
KARIBUNIPEASCAREACADEMY