KTO

KTO

Share

Karibu Tanzania Organization (KTO) works with Folk Development Colleges (FDCs) in Tanzania to supports non-formal education and training for young adults.

Photos from KTO's post 01/06/2024

Katibu Mkuu Wizara ya elimu na Mafunzo ya Amali (WEMA) Zanzibar, Mhe. Khamis A. Said akipata maelezo kuhusu Programu za KTO na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs) wakati alipotembelea banda la maonesho la KTO katika maadhimisho ya wiki ya Elimu, ujuzi na Ubunifu jijini Tanga.

Maadhimisho hayo yamefikia kilele May 31, 2024 ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amekuwa mgeni rasmi.


Photos from KTO's post 30/05/2024

Banda la Maonyesho la KTO na FDC, katika wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu jijini Tanga.

Photos from KTO's post 28/05/2024

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda, azindua maadhimisho ya wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika kwenye shule ya Sekondari ya Popatlal jijini Tanga.

KTO na vyuo vya Maendeleo ya wananchi vinashiriki maonesho haya ambapo bunifu mbalimbali zimewasilishwa.

Kauli mbiu ya maadhimisho haya ni: Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa uchumi shindani.

10/04/2024
Photos from KTO's post 08/03/2024

Siku ya Wananwake Duniani March 08, 2024: Wekeza kwa Wanawake kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii!

Katika kusherekea siku ya wanawake duniani tunawasherekea wanawake wote wanaofanya jitihada katika kulete maendeleo yao binafsi, jamii na taifa kwa ujumla.
KTO kwa kushirikiana na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs) wamewekeza kwa wanawake vijana kwa kuanzisha na kuendesha programu za Elimu Haina Mwisho ambayo ni maalumu kwa kuendeleza maarifa kwa wanawake vijana waliokatishwa masomo kutokana na sababu mbalimbali; na Mpira Fursa: programu ya kuendeleza soka la wananwake nchini, kwa kuwajengea uwezo wa kujiamini, kujithamini katika soka, kutambua fursa za kiuchumi, kufikia usawa wa kijinsia na maendeleo ya jamii.

Elimu na ujuzi wanaoupata kupitia programu hizi na nyinginezo ni kielelezo cha uwekezaji wenye lengo la kuwawezesha kujiendeleza kielimu na kiuchumi kwa kujipatia ajira, na kutambua fursa mbalimbali za kiuchumi, kutambua haki zao za msingi na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya jamii inayowazunguka.

Nafasi za masomo katika vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs) kanda ya kusini 05/02/2024

Mwaka mpya wa masomo umeanza!
Je unatamani kupata elimu ya Ufundi na haujapata chuo hadi sasa? Hujachelewa!
Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs) vilivyoenea nchini kote vinazo nafasi chache za kujiunga na masomo kwa kozi mbalimbali za Ufundi na elimu ya Sekondari (kupitia programu ya Elimu Haina Mwisho). Ni kwa wanawake vijana waliokatishwa masomo kutokana na sababu mbalimbali.
Kwa maelezo zaidi, wasiliana na chuo kilicho karibu nawe. Au tupigie simu 0789 615 782.


Nafasi za masomo katika vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs) kanda ya kusini

31/12/2023

Salaam za mwaka mpya

12/12/2023

Kigamboni FDC, Dar es Salaam

Photos from KTO's post 06/11/2023

Walimu Wakuu na walimu wa mchezo kutoka shule 18 za msingi za kanda ya kusini zinazotekeleza programu ya kuendeleza soka kwa wanawake na wasichana nchini - Mpira Fursa, wamekutana mjini Masasi kujadili utekelezaji wa programu hiyo pamoja na masuala ya ulinzi na usalama wa mtoto.
Mkutano huo wa siku moja uliofanyika Novemba 2, 2023 katika chuo cha Maendeleo ya Wananchi Masasi, umewakutanisha wakuu wa vyuo 9 vya Maendeleo ya Wananchi (FDC), Walimu wakuu, na walimu wa michezo wa shule hizo, ambapo kila chuo kinaratibu programu hiyo kwenye shule mbili za Msingi.
Programu ya Mpira Fursa inalenga kusaidia kukuza na kuendeleza soka la wanawake na wasichana nchini k**a njia ya kufikia usawa wa kijinsia na kuimarisha uchumi wa kijamii; Kukuza na kuimarisha hisia za kujitambua, kujiamini, kujithamini kwa wasichana, na kujua uelewa wao juu ya haki zao za msingi.
Malengo mengine ni kuwawezesha wasichana kuwa wacheza soka bora wenye ujuzi, wanaojiamini na kuzifahamu fursa za kiuchumi katika soka; Kuongeza ufahamu wa haki za mtoto, na umuhimu wa ulinzi wa mtoto katika jamii; na, Kupunguza idadi ya wasichana wanaokatishwa masomo katika shule za msingi.
Jumla ya shule 110 za Msingi zinashiriki katika programu ya Mpira Fursa ambapo kila shule imeanzisha timu ya Mpira wa miguu kwa wasichana. KTO inaziwezesha timu hizi kwa kuzipatia vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo mipira, jezi, filimbi n.k.


23/03/2023

05/02/2021

Karibu KTO

Welcome to KTO's official page!

Karibu Tanzania Organization (KTO) is a national level Non-Governmental Organization working as an umbrella organization for the Folk Development Colleges (FDCs) in Tanzania since 1990s. It was established as a result of cooperation between Tanzania and Sweden through Folk Development Colleges in Tanzania and Swedish Folk High Schools. The organization’s focus is to create well-informed social-economically empowered, active citizens in a just and sustainable society including initiatives that enable the response against sexual and gender-based violence support and promoting women’s rights, empowering women’s decision making, and enhance the FDC institutional capacity and of the public sector to address gender equality.

KTO has gained a long experience of non-formal education offering through community-based colleges, adult learning, pedagogical work, rural development, and training for young adults. Through FDCs, KTO provides training for young adults who have dropped out of the formal school system, including young mothers. The training offers an integrated vocational and secondary education program providing participants with life skills that prepares them for employment or pursuant of further education levels.

KTO’s function as an umbrella organization is to connect all 55 FDCs in the country and strengthen the FDCs as institutions in order for them to be able to fulfill their task in promoting adult education, folk education and community development. It plays an important role in working with local communities and local civil society organizations in promoting a better understanding, knowledge and respect for human rights, gender balance, and the connection between these rights and the serious problems facing people in their daily lives. Through FDCs, KTO has a nationwide network with the capacity to reach out to many people and communities, especially in rural areas where most of the FDCs are operating.

Our prongs programs – Elimu Haina Mwisho, skills development program, Mpira Fursa and Early Childhood development training endeavors to strengthen FDCs as platforms working for gender equality through lifelong learning and inclusive education. The objective is to strengthen young adults with a focus on young women’s rights and opportunities for active citizen engagement, and help them gain the skills to acquire formal-sector employment, self-employment and or continue their education even further.
For more information visit us at https://kaributanzania.or.tz/

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address


INFOSYS House Plot No. 17, Mwindu Lane, Kinondoni
Dar Es Salaam