Twariqatul Qadiria Arrazakiya Al Jailaniya

Twariqatul Qadiria Arrazakiya Al Jailaniya

Share

Deen/Education/Teachings/Hadith/Reminders

22/12/2022

Deep

20/10/2022

Wisdom ❀️

14/10/2022

Just pray everything will be fine

25/09/2022

Imekuwa tabia yetu kuamini kila kinachotokea katika maisha yetu ya kila siku ni mipango ya Mungu, kuna wakati jitihada zako binafsi zinaweza kuwa na nafasi kubwa katika kubadili mfumo mzima wa maisha yako… Mungu husubiri kuona mabadiliko ndani yako kisha baraka zake hushuka na kuwa sehemu ya maisha yako

Zingatia na amini wewe ni moja ya sehemu kubwa sana ya maisha yako

23/09/2022

Read again and again

20/09/2022

Ukiamua kuipa nafasi dunia ikuonyeshe upande sahihi na ukayaruhusu maisha yako kuishi kulingana na nyakati, kaa ukitambua ipo siku utafurahia maamuzi yako na kuona ubora kwa kila hatua katika maisha yako

18/08/2022

Hakuna mwanadamu aliemkamilifu basi ni wajibu wa kila mmoja wetu kuomba msamaha kwa yale yasiyomkamilisha kwa namna yeyote ile,

Hii ni moja ya namna ya kuweza msamaha kwa mola wetu katika yale mapungufu yetu ya kibinadamu

15/08/2022

Kawaida ya mwanadamu kutafuta mtu wa kumlaumu kwa nafasi fulani hii ni sababu ya namna ambavyo tumeumbwa mara chache sana na watu wachache sana wenye uwezo wa kutambua uchangiaji wao katika jambo fulani…
Ni wazi na kila mmoja wetu a napaswa kutambua ya kuwa haijalishi katika nini ila mara nyingi maamuzi huwa ni yako na matokeo mara zote husababishwa na kile ambacho umekiamua mwenyewe kuliko kile ambacho kimesababishwa na mtu mwingine ndani ya maamuzi yako!!

Wewe ndio sababu ya kila kinachotokea ndani ya maisha yako! Kuwa na maamuzi sahihi hakuna kitu kirahisi katika hii dunia!

Everything has a price you have to pay

17/07/2022

Watch this

Angalia hii

14/07/2022

NINE GOLDEN RULES EXTRACTED IN QUR'AN FROM SURATUL (HUJURAT).

*1. "Fa Tabayyanu":*
Investigate: when you receive an information,
lest you harm people out of ignorance.

*2. "Fa Aslihu"*
Make settlement: between your brothers as believers are brothers.

*3. "Wa Aqsitu":*
Act justly: whenever there is a dispute try for settlement and act justly among both parties as Allah loves those who act justly.

*4. "La Yaskhar":*
Don't ridicule people, perhaps they may be better than you to Allah.

*5. "Wa La Talamizu":*
Do not insult one another.

*6. "Wa La Tanabazu":*
Do not call each other with offensive nicknames.

*7. "Ijtanibu Kaseeran minaz-Zan":*
Avoid negative assumptions, indeed some of the assumptions are sins.

*8. "Wa La Tajassasu"* :
Do not spy on each other.

*9. "Wa La Yagtab":*
Do not backbite each other. Its a major sin equivalent to eating your dead brother's flesh.
WHAT A FOOD FOR THOUGHT MY BROTHER'S & SISTER'S.
May Allah guide us, protect us and make it easy for us and our love ones . Aaaamin.,

12/07/2022

πŸ”–πŸ”–πŸ”–πŸ”–πŸ”–πŸ”–πŸ”–πŸ”–πŸ”–

*Laiti mtoa sadaka angejua kwa yakini kwamba sadaka yake inapokelewa kwa Mwenyezi Mungu kabla ya kuingia mkononi mwa masikini,ingekuwa ladha ya mtoaji....ni kubwa kuliko ladha ya mpokeaji..*

*-Ibn alqayyim*

Je unajua faida ya kutoa sadaka?
Sikilizeni enyi watoa sadaka, nyinyi na ambao wanasaidia kufikisha sadaka..

1- *Sadaka ni mlango miongoni mwa milango ya pepo*

2-Sadaka ni bora ya matendo mema, na sadaka bora ni kulisha chakula

3- *Sadaka inamfunika kivuli mtoaji na inamuondosha kwenye moto*

4-Sadaka inazima ghadhabu za Mola na joto la kaburi

5- *Sadaka ni jambo bora la kumzawadia maiti na inamfaa zaidi, na Mola anaitunza*

6-Sadaka ni usafisho, na utakaso wa nafsi na huongeza mema

7- *Sadaka ni sababu ya furaha kwa mtoa, na ni sababu ya kung'ara uso wake siku ya kiama*

8- Sadaka inaleta amani kutokana na hofu siku ya fazaa kubwa, na humfanya mtoa sadaka asipatwe na huzuni

9- *Sadaka ni sababu ya kughufiriwa dhambi na kusamehewa makosa*

10- Sadaka ni miongoni mwa bishara za mwisho mwema na sababu ya dua ya Malaika

11- *Mtoa sadaka ni mbora wa watu, na sadaka thawabu zake ni kwa kila aliyeshiriki*

12- Mwenye kutoa sadaka ameahidiwa kheri nyingi na ujira mkubwa

13- *Kutoa ni miongoni mwa sifa za wacha Mungu, na sadaka ni sababu ya mapenzi ya waja wa Mola kwa mtoa sadaka*

14- Sadaka ni ishara miongoni mwa ishara za ukarimu na alama miongoni mwa alama za ukarimu na wema

15- *Sadaka ni sababu ya kukubaliwa dua na kuondoshewa matatizo*

16- Sadaka inaondoa balaa na inaziba milango sabini ya mabaya ya dunia

17- *Sadaka inazidisha umri na mali, na ni sababu ya riziki na nusra*

18- Sadaka ni ponya, dawa, na shifaa

19- *Sadaka inazuia moto, gharika, wizi, na inazuia kifo kibaya*

20- Sadaka ujira wake ni ule ule japo ukitoa kwa wanyama au ndege..

*🌴Na sadaka bora ni ile unayoifanya sasa.. ni kueneza maneno haya kwa nia ya sadaka kwani kila anayetekeleza maneno haya na akawafundisha wanaokuja, basi ujira wake uko kwa Mola wake kwa idhini yake*🌴

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Website

Address


Magomeni
Dar Es Salaam