09/02/2026
Bustani Ya Maswahaba
Yatakiwa tuishi kama wao.
09/02/2026
19/06/2025
239
BIN SHIHABU.
Swahaba wa mtume s.a.w Ambae, amepokea takribani hadithi 84 kutoka kwa mtume s.a.w, na alishiriki vita katika Ukhalifa wa Abubakar na Omar takriban Radhi za Allah ziwe juu yake.
Nasaba yake ni:
Twariq bin Shihabu bin Abdushams bin Salama Al Ahmasiyy
Ni katika maswahaba ambao wamepokea hadithi na kadhaa kupitia kwa Abubakar, Omar, Othman, Ally,Bilal pamoja na maswahaba wengine.
Pia ni katika maswahaba ambao wameidiriki Jahilia na baada ya kusilimu alishiriki vita takriban 33 na katika mji alioishi ni mji wa Kufa, ambapo imenukuliwa alikuwa akisema katika Jahilia,: "Bora ya dini ni dini ya Al zarkaly"
Katika Kufa kwake mwanachuoni wameandika ya kuwa amekufa mwaka wa 83 ingawa baadhi ya riwaya zinasema amekufa mwaka 82
Rejea:
Twabaqatul Kubra
17/06/2025
238
BIN DHIHAK
Swahaba wa mtume s.a.w Ambae anamambo mengi mazuri aliyoyaacha k**a alama katika uislaamu.
Nasaba yake:
Thabit bin Dhihak bin Khalifa bin Tha'alaba bin Adiy bin Ka'ab bin Abdil Ash-hal Al ansaary
Mama yake ni: Asmaa bint Murshida bin Jabru kutokea Ausi.
Amesema Imam Abdul Barry kuwa Thabit amezaliwa mwaka wa 3 Baada ya Hijra, na Ibn Hajar Al asqalany anasema "amezaliwa mwaka wa 3 baada ya utume, kwa sababu mtu aliezaliwa mwaka wa 3 baada ya hijra hawezi kushiriki Hudaibia Wala kushiriki baii kwa sababu mpaka kufika wakati huo atakuwa na miaka 3" Ibn Hajar
Vilevile wanachuoni wametofautiana juu ya mwaka wake wa Kufa baadhi wanasema 45H na wengine k**a Abuu Jafary Altwabary na Abuu Ahmad Alhakim wanasema amekufa katika kipindi Cha fitna wakati wa Ibn Al Zubair mwaka 65H.
Radhi za Allah ziwe juu yake.
04/06/2025
237.
Swahabat wa mtume s.a.w Ambae aliozeshwa siku aliyozaliwa.
Nasaba yake ni:
Sahlah bint Aswim bin Adiy bin Aljadd bin Ajlan bin Haritha bin Dhabia bin Harami bin Ja'al bin Amru Al-Ajlaaniyyah Albalwiyyah Al-Ansaariyyah.
Amezaliwa siku ya vita ya Khaybara ambapo mtume s.a.w alimwita Sahlah ikitokana na Dua "Sahhallahu Amrakum"
Ameeleza: "Nimezaliwa siku ya Khaibarah mtume akaniita Sahlah Kisha akasema: "Sahhallahu Amrakum": Kisha akanipiga na mshale na akaniozesha kwa Abdurahman bin Awf siku niliozaliwa".
04/06/2025
236.
.
Swahabat wa mtume ambe amechangia mama na Khalifa Othman bin Afan, na alisilimu kabla ya hijra ambapo Ibn Sa'ad amemtaja k**a Mwanamke wa Kwanza wa kiswahaba kuhama kuelekea Madina na miongoni mwa wanawake walimbaii mtume s.a.w
Nasaba yake
Umu kulthum bint Uqbah bin Abi muait bin Abii Amru bin Umayya bin Abdishamsi Alquraishy AlUmawiyy.
Mama yake ni: Arwaa bint Kareez.
Aliolewa na wanaume wanne katika maisha yake ambao ni
1. Zaid bin Harith, Ambae alikufa siku ya Muutah Kisha.
2. Zubair bin Al-awam, Ambae alizaa nae mtoto mmoja Zainab baadae wakaachana Kisha,
3. Abdurahman bin Awf, Ambae alizaa nae watoto sita alipofariki ndipo akaolewa na
4. Amru bin Al-As. Alikaa nae mwezi mmoja umuu kulthum akafariki.
Ndugu zake wa karibu:
Othman bin Afan
Alwalid bin Uqbah
Amina bint Afan
Amarah bin Uqbah
Khalid bin Uqbah
Rejea:
Altwabaqatul Kubraa juzuu 10
Al-Iswaabah juzuu 8
03/06/2025
235.
.
Swahaba wa mtume s.a.w Ambae ndie alietengeneza Mimbar ya Mtume kipindi ambacho waislaam waliongezeka na wakawa wengi msikitini ndio mtume akashauriwa kutengeneza mimbari ya juu ili watu wa nyuma waweze kumuona wakati akikhutubu.
Imepokelewa na Nadhra kutoka kwa Jabir amesema: " Mtume alikuwa akikhutubu katika gogo la mtende akaambiwa wamekithiri watu na unakujia ugeni kutoka sehemu mbalimbali, Lau k**a ungemuamrisha kuwekewa kitu ukawa unapanda juu yake. Akamwita mtu akamuuliza: "unatengeneza Mimbar" akasema ndio akamuuliza:"jina lako": akasema Fulani akasema: "wewe sio mtu wake" Kisha akamuita mtu wa pili na watatu, akamuuliza: "Jina lako": akasema: " Ibrahimu" mtume akasema: "Simamia kutengeneza"
Baada ya utengenezwa mimbari mtume akaipanda ndipo gogo nikanyong'onyea mithili ya ngamia mpaka mtume akalituliza.
Radhi za Allah ziwe juu yake.
Rejea
Asadul Ghaabah
03/06/2025
234.
Swahaba wa mtume s.a.w Ambae ni miongoni mwa maswahaba waliosilimu mapema sana, lakini alikuwa akificha uislaamu wake kutokana na khofu iliyokuwepu juu ya makuraishi.
Historia inaonyesha alisilimu baada ya watu kumi kusilimu, yaani hata kabla ya kusilimu Omar bin Khatwab, wakati huo kabla ya hijra ya habashi na alikuja kushiriki hijra mwaka wa 6 baada ya utume wakati ambao mtume s.a.w alimkumbatia na kumbusu na siku moja alimwambia " watu wako ewe Nuaimu wamekuwa ni Bora Kuliko watu wangu" Nuaimu akasema: "Bali watu wako ni Bora zaidi ewe mtume wa Allah": Mtume akasema:"Watu wangu walinitoa ila watu wako walikukubali".
kufa kwake wanachuoni wametofautiana wakati gani amekufa kwani Ibn Hajar anasema: amekufa katika eneo la Ajnadeen wakati wa Ukhalifa wa Omar bin Khatwab, na wengine wanasema amekufa katika vita ya Muutah katika Uhai wa Mtume s.a.w.
Swahaba yupi ungependa kupata historia yake
26/04/2025
233.
BIN MIHSWAN
Swahaba wa mtume s.a.w Ambae ni mtoto wa shahaba "Wahbu" maarufu kwa jina lake Abuu Sinan bin Mihswan.
Amezaliwa mwaka wa 16 Kabla ya hijra na alifanikiwa kuwa katika maswahaba walioshiriki vita ya Badri,Uhdi na Khandaq.
Pia alishiriki sulhu ya hudaibia na alikuwa ni swahaba wa Kwanza kumbai'i (kumuunga mkono) mtume s a.w katika Baia ya Ridhiwan.
Nasaba yake ni:
Sinan bin Abi Sinan bin Mihswan bin Harthan bin Qais Al Asadiy, ndugu zake wa karibu ni Ami yake Ukasha bin Mihswan na Shangazi yake ni Ummu Qais bin Mihswan.
Sinan alikufa mwaka wa 32 Hijiria, rehma za Allah ziwe juu yake.
:
Twabaqatul Kubra Cha Ibn Saad.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Contact the school
Website
Address
Tandale
Dar Es Salaam