بحوث الاقتصاد الإسلامي Islamic Economics Researches

بحوث الاقتصاد الإسلامي Islamic Economics Researches

Share

Uchumi na Biashara kwa Mtazamo wa Qur'an na Sunna Sihihi kwa Ufahamu wa Salaf

21/06/2026

ADABU 30 ZA BIASHARA

•Miongoni mwa mambo ya msingi kuyazingatia katika Biashara kwa mujibu wa Qur na na Sunna ni :-

1.Nia njema katika kuanzisha Biashara
2.Kujifunza Fiqh ya Biashara na Miamala.
3.Ukweli
4.Uwaminifu
5.Maneno mazuri kwa wateja
6.Kufanya Biashara ya Halali
7.Biashara isizue kufanya Ibaada(Swala)
8.Kutoa Zaka na Sadaka
9.Kuinamisha Macho
10.Kuandika Madeni

11.Kuheshimu Mikataba
12.Kujiepusha Miamala ya Haramu Mfano Riba na Kamari
13.Kuacha Kupunguza Mizani na Vipimo
14.Kuacha kulalia watu katika Bidhaa zao.
15.Kuacha kufanya Biashara Barabarani.
16.Kujiepusha na Mikopo bila sababu za msingi.
17.Kuwahi kutoka sokoni mapema baada tu ya kumaliza Biashara.
18.Maridhiano katika Biashara
19.Kuweka bayana Dosari za Bidhaa
20.Kujiepusha na Viapo

21.Kuharakisha Kulipa Deni kwa wakati
22.Kumtegemea Allah katika Biashara
23.Kujiepusha na Ushirikina
25.Kuuza Bidhaa ambayo haipo .
26.Kumvumilia mwenye deni.
27.Kukubali Kumrudishia Mteja Pesa zake na rudisha Bidhaa ikiwa anasababu ya msingi.
28.Usafi katika Sehemu ya Biashara
29.Kuacha Tabia ya Kuficha Bidhaa ili kupandishi bei ya Bidhaa.
30.Kujihadhari Ghishi.

Allah aturuzuku Chumo la Halal.Aamen.

وصلى الله وسلم وبارك على نبينا محمد وعلى آله وصحبه أجمعين.

Muandishi :-
Ally Yahya Al-Qusheiry
Dar es Salaam-Tanzania
☎️+255 652082775

03/06/2026

MIRATHI YA KIISLAMU

Hii ni Makala fupi inayo elezea Elimu ya Mirathi kwa mujibu wa Sharia ya Kiislamu.

1.MAANA YA ELIMU YA MIRATHI

•Elimu ya Mirathi ni Elimu inayo elezea namna ya kugawa mali alizo acha Marehemu kwa mujibu wa Qur an n Sunna.

2.MALI ZA MAREHEMU

•Mali za marehemu(التركة‏)ni kitu chochote ambacho amekiacha Marehemu katika mali,ambazo zipo katika kuu tatu:-

(i)Vitu vinavyo shikika(الأعيان‏)mfano pesa,magari,nyumba ,mashamba n.k
(ii)Haki(الحقوق‏) alizo kuwa anastahiki Marehemu mfano Haki Ufumbuzi kitu fulani.
(iii)Manufaa‏(المنافع‏).

3.HAKI ZINAZO HUSU MALI YA MAREHEMU

•Kabla ya Kuanza kugawa mali aliacha marehemu ni lazima kuzingatia haki zifuatazo:-

(i)Kutoa Pesa za Ghalama za Mazishi ya Marehmu Mfano Sanda,Kaburi,muoshaji.
(ii)Kulipwa Madeni ya Bondi
(iii)Kulipwa madeni anayo daiwa marehemu,yawe ni Madeni ya Allah au Madeni ya Wanadamu.
(iv)Kutolewe Wasia ambao amecha marehemu k**a upo ,amabayo ni theluthi ya Mali (⅓)au chini hapo anapewa mtu ambae si mrithi k**a wasia warahemu utakavyo eleza.
(v)Ugawaji wa Mirathi kwa wanaostahiki kisharia.

4.NGUZO ZA MIRATHI

•Mirathi ya Kiislamu imejengwa juu nguzo tatu:-

(i)Anae rithiwa(Marehemu)
(ii)Mrithi
(iii)Mali inayo rithiwa.

5.MASHARTI YA MIRATHI

•Masharti ya Mirathi ya Kiislamu ni mambo tatu:-

(i)Kufa kwa anae rithiwa
(ii) Uhai wa anae rithi
(iii) Kujua sababu ya kurithi.

6.SABABU ZA KURITHI

•Sababu za kurithi kwa mujibu wa Sharia ni tatu:-

(i)Ndoa :-Ikiwa ndoa imefungwa kwa usahihi ,mume na mke warithiana ikiwa mmoja atafariki .
(ii)Nasabu:-Nasabu ndio sababu kuu ya Urithi katika Sharia Kiislamu.
(iii)Walaa: Hii ni haki ya kurithi anayo pewa mtu alie muachia mtumwa huru.

7.VIZUIZI VYA MIRATHI

•Mtu anaweza kuzuiwa kurithi na kukosa mirathi ikiwa ana moja ya moja ya mambo yafuatayo :-

(i)Kuua:Ikiwa mrithi atamua anae mrithi bila haki ya Kisharia ,muuaji atajinyimwa mirathi.
(ii)Utofauti wa Dini:-Ikiwa mrithi ni dini tofauti na mrithiwa hakuna kurithiana hapo ,mfano Mtoto ni muislamu ,baba ni Mkiristo,au Baba ni myahudi.
(iii)Mtumwa:-Mtu ambae ni mtumwa harithi wa harithiwi.

8.WARITHI

•Warithi ni watu wote ambao wanatokana na sababu za Kisharia za mirathi zilizo tajwa hapo juu ,na warithi wapo wa aina kuu mbili:-

WARITHI WA KIUME

•Warithi wa Kiume kwa ujumla ni watu wafuatao:-

(i)Baba wa Marehemu
(ii)Mtoto wa Kiume wa Marehemu
(iii)Mjuu wa Kiume wa Marehemu
(iv)Babu wa Marehemu
(v)Baba mdogo(Ami) wa Marehemu
(vi)Kaka wa Marehemu
(vii)Mume wa Marehemu
(viii)Alie achia mtumwa huru.

WARITHI WA K**E

•Warithi wa K**e kwa ujumla ni watu wafuatao:-

(i)Mama wa Marehemu
(ii)Bibi wa Marehemu
(iii)Binti wa Marehemu
(iv)Mjuu kuu wa K**e wa Marehemu
(v)Dada wa Marehemu
(vi)Mke wa Marehemu
(vii)Aliemucha mtumwa huru.

ZINGATIA:-

•Walio tajwa katika orodha ya warithi haimanishi kuwa wote wanarithi kwa pamoja bali kuna masharti kila mmoja ili pate hiyo mirathi.

9.AINA KURITHI

•Namna ya kurithi katika Sharia ya Kiislamu kupo kwa aina kuu mbili:-

(i)Kurithi kwa Mafungu maalumu yalio tajwa na Sharia.
(ii)Kurithi kwa kusubiri kinacho baki baada ya kuwapa wanao rithi mafungu yao.

9.MAFUNGU YA MIRATHI

•Mafungu ya Mirathi kwa mujibu wa Sharia yapo sita k**a ifuatavyo:-

(i)Nusu ya Mali (½)
(ii)Robo ya Mali(¼)
(iii)Thumuni ya Mali(⅛)
(iv)Theluthi mbili ya Mali (⅔)
(v)Theluthi ya Mali(⅓)
(vi)Sudus ya Mali (⅙).

ZINGATIA :-

•Kila fungu katika mafunga hayo lina warithi wake wa mujibu wa Sharia na masharti yake k**a tutavyo eleza huko mbele InshaAllah katika makala ziyazo.

•Ipo fungu lingine ambalo ni Theluthi ya Mali ilio baki ب⅓,hili tutalielezea katika mirathi ya mama wa marehemu InshaAllah.

Allah aturuzuku Elimu yenye manufaa.Ameen.

وصلى الله وسام وسلم وبارك على نبينا محمد وعلى آله وصحبه أجمعين.

Muandishi:-
Ally Yahya Al-Qusheiry
Dar es Salaam-Tanzania
📞255 652082775

30/05/2026

NI NINI ?

Hii ni Makala inayo elezea Iqaala ambayo ni moja katika Miamala ya Kiislamu katika Miamala ya Fedha:-

1.MAANA YA IQAALA(الإقالة ‏)

•Iqaala ni Makubaliano ya Kuvunja Mkataba wa Biashara baada ya kusihi baina ya muuzaji na mnunuzi.

Mfano:Bakari amenunua Simu kutoka kwa Hassan ,kisha Bakari akapata dharura ya Uhitaji wa Fedha au kujutia Biashara hiyo,akumuambia yule alie muuzia simu ,naomba tuvunje hii Biashara uchukue simu yako ,unirudishie pesa zangu,Hassan akikubali kurudisha pesa na kuchukua simu yake ,hapa kisharia kunakuwa kumefanyika muamala wa Al-Iqaala.Ni miongoni mwa miamala inayo onesha uungwana na ustarabu wa Uislamu.

2.HUKUMU YA IQAALA

•Iqaala ni Sunna na jambo lenye kupendeza ,mtu yeyote ambae anae mkubalia mtu kufanya muamala huu ,Allah amemuandalia ujira mkubwa siku ya Qiyaama.




25/05/2026

WASIA NINI ?

•Al-Wasia (الوصية‏)ni mali ambayo mtu anaitoa k**a zawadi baada ya kufa .


25/05/2026

HIBAH NI NI ?

•Al-Hibah(الهبة‏) ni Mali ambayo mtu anaitoa k**a zawadi katika hali ya Afya njema.


25/05/2026

ATWIYAH NI NI ?

•Al-Atwiyah(العطية‏) ni Mali ambayo mtu anaitoa k**a zawadi katika hali ya Maradhi ya kifo.


18/05/2026

NI NINI ?

Hii ni Makala fupi inayo elezea kuhusu moja ya Miamla ya Kifedha ambao ni Al-Hawala:-

1.MAANA YA HAWAALA

•Hawaala(حوالة‏) ni Muamala wa Kisharia ambao maana yake ni kubadilisha Deni kutoka kwa mtu mmoja au taasisi kwenda kwa mwingine.

2.HUKUMU YA HAWAALA

•Hawaala ni miongoni mwa Miamala ambayo inakubalika Kisharia ikiwa masharti na vigezo vimezingatiwa.

3.NGUZO ZA HAWAALA

•Muamala wa Hawaala umejengwa katika nguzo tano:-

(i)Anae hamisha Deni(المحيل‏)
(ii)Anae hamishwa/Mdai(المحال‏)
(iii)Anae hamishiwa deni(المحال عليه‏)
(iv)Deni (المحال به‏)
(v)Tamko la Muamala.

4.MASHARTI YA HAWAALA

•Miongoni mwa Masharti ya Muamala wa Hawaala ni :-

(i)Kulingana Madeni
(ii)Aina ya Deni ijulikane
(iii)Namna ya Deni ifahamike
(iv)Muda wa kulipa Deni uwe sawa.
(v)Deni limetulizana .

Mfano:-

•Bakari ana mdai Juma Elfu 50000/=,na Juma ana mdai Saidi 50000/=,Kisha Juma na mhamisha Bakari kutoka kumdai yeye ,bali amadai Saidi,ana muambia nimekuhamishia deni lako kwa Saidi ndie atakae kukupa.

➡Juma ndio Mdaiwa wa kwanza (المحيل‏).
➡Bakari ndio alie hamishwa(المحال‏)
➡Saidi anae hamishiwa Deni (المحال عليه‏)
➡Elfu 50000/= ndio Deni (المحال به‏).

ZINGATIA :-

•Baada ya Makubaliano ya Kuhamisha Deni ,mdaiwa alie hamisha deni ana kuwa si mdaiwa tena.
•Anae dai ana haki ya kukataa kuhamishwa ikiwa anako hamishiwa mtu huyo hawezi kulipa deni.

Muandishi :-
Ally Yahya Al-Qusheiry
Dar es Salaam-Tanzania
📞+255 652082775

16/05/2026

#الفرق بين بيع العينة وبيع التورق

14/05/2026

سلسلة قواعد وضوابط في المعاملات المالية

14-المعروف بين التجار كالمشروط بينهم

#قاعدة
#مالية
#تجارة

14/05/2026

سلسلة قواعد وضوابط في المعاملات المالية

13-يثبت تبعا ما لا يثبت استقلالا

#قاعدة
#مالية
#بيع

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address


Dar Es Salaam