Adm ministries

Adm ministries

Share

Ancient of Day's Ministries
(Huduma za Mzee wa Siku)

Photos from Adm ministries's post 18/04/2026

WELCOME TO CHURCH TOMORROW 🙏🏽🔥
After 6 days of fasting and prayer…
it’s time for testimonies!

Come with your testimony, come with a grateful heart,
because God has done it—and He is still doing more.
đź“– Psalm 66:16
“Come and hear, all you who fear God; let me tell you what He has done for me.”

Tomorrow is not ordinary…
it’s a day to witness and declare what God has done in these 6 days.

👉 Don’t miss it. Come with someone. Come with your testimony.

———-
KANISANI KESHO 🙏🏽🔥

Baada ya siku 6 za kufunga na maombi…
sasa ni wakati wa shuhuda!

Njoo na ushuhuda wako, njoo na moyo wa shukrani,
kwa sababu Mungu ametenda na ataendelea kutenda.

đź“– Zaburi 66:16
“Njoni msikie, ninyi nyote mnaomcha Mungu, nami nitasimulia aliyoyatenda nafsi yangu.”

Kesho sio kawaida…
ni siku ya kuthibitisha yale Mungu amefanya kwa siku hizi 6.

👉 Usikose . Njoo na rafiki/ ndugu yako. Njoo na ushuhuda wako.

BwanaYukoPamojaNasi

18/04/2026

UMJUE SANA MUNGU, ILI UWE NA AMANI 🙏🏽

“Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia. Uyapokee, tafadhali, mafunzo yatokayo kinywani mwake, Na maneno yake yaweke moyoni mwako.”
Ayubu 22:21–22

Amani ya kweli haitokani na kelele za dunia wala mawazo mengi…
inazaliwa unapomjua Mungu kwa undani kupitia Neno lake na kuliruhusu likae moyoni.

👉 Ukimjua Mungu kwa kina:
hutayumbishwa na kila upepo wa mafundisho yasiyo na msingi wa Kristo,
hutapeperushwa na kila wimbi la mawazo,
utakuwa imara ndani ya kweli yake.

“Kwa hiyo tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu…”
Waefeso 4:14

📌 Kumjua Mungu = Amani ya ndani + Mema yanayokuja kwa wakati wake


18/04/2026

🔥 MJUMUISHO WA MAOMBI YOTE (DAY 1–5)
Tunakuja mbele za Bwana kwa siku ya maombi ya pamoja na kufunga, tukiunganisha maombi yote ya:
* Kanisa la ADM na ujenzi wake
* Viongozi na watumishi
* Familia, ndoa na watoto
* Vijana na mabinti
* Ulinzi, mafanikio na milango ya baraka

📖 Mathayo 18:19–20
“Wawili au watatu wakikubaliana duniani katika jambo lolote… litafanyika kwao na Baba yangu aliye mbinguni.”

🙌🏽 WITO WA MAOMBI
Tunakualika uje katika siku ya maombi, kufunga na kutafuta uso wa Mungu kwa pamoja.

⏰ MUDA
đź•— Kuanzia Saa 2:00 Asubuhi
📍 Ancient of Days Ministries – Tabata Kinyerezi, Mnadani

🔥 KUSUDI
* Kuunganisha maombi ya wiki nzima
* Kupokea majibu ya Mungu
* Kuimarishwa kiroho na kiimani
* Ukombozi na kufunguliwa kwa maisha ya watu wa ADM
* Kuona mkono wa Mungu katika kanisa na familia

🙏🏽 KARIBU TUOMBE PAMOJA



18/04/2026

🔥 DAY 6 NI MJUMUISHO WA MAOMBI YOTE (DAY 1–5)
Tunakuja mbele za Bwana kwa siku ya maombi ya pamoja na kufunga, tukiunganisha maombi yote ya:
- Kanisa la ADM na ujenzi wake
- Viongozi na watumishi
- Familia, ndoa na watoto
- Vijana na mabinti
- Ulinzi, mafanikio na milango ya baraka
- Ongezea maombi yako hapa…

📖 Mathayo 18:19–20
“Wawili au watatu wakikubaliana duniani katika jambo lolote… litafanyika kwao na Baba yangu aliye mbinguni.”

🙌🏽 WITO WA MAOMBI
Tunakualika uje katika siku ya maombi, kufunga na kutafuta uso wa Mungu kwa pamoja.

⏰ MUDA
đź•— Kuanzia Saa 8:00 Asubuhi
📍 Ancient of Days Ministries – Tabata Kinyerezi, Mnadani

🔥 KUSUDI
Kuunganisha maombi ya wiki nzima
Kupokea majibu ya Mungu
Kuimarishwa kiroho na kiimani
Ukombozi na kufunguliwa kwa maisha ya watu wa ADM
Kuona mkono wa Mungu katika kanisa na familia

🙏🏽 KARIBU TUOMBE PAMOJA




Photos from Adm ministries's post 17/04/2026

Day 5: KUOMBEA KANISA LETU 🙏🏽

Tunaomba kwa ajili ya viongozi wetu, watendakazi, na wana ADM wote, Mungu awalinde, awape neema, hekima na nguvu katika utumishi.

Tunaweka familia zote mikononi mwa Mungu, watoto, ndoa na hatima zao zilindwe.

Tunaomba mahitaji yote yakutane na mkono wa Mungu, kifedha, kiroho na kimwili.

Na juu ya yote, tunaombea ujenzi na maendeleo ya kanisa, umoja, ushindi dhidi ya wapinzani, na ufunguzi wa milango ya fedha mpaka kazi ikamilike kwa utukufu wa Mungu.

Kanisa likisimama, kizazi kinainuka.

16/04/2026

🙏🏽 POINTI ZA MAOMBI

1. Ee Bwana, kwa mamlaka ya jina la Yesu, ninaamuru kila kazi ya shetani kinyume cha uzao wa mwanamke iharibiwe kabisa, ifutwe mizizi yake na isisimame tena.
1 Yohana 3:8
“Kwa sababu hiyo Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.”

—

2. Ee Mungu wa mbinguni, walinde kwa nguvu zako watoto wote waliomo katika matumbo ya mama zao; usiruhusu mkono wa adui kuwagusa, na uwahifadhi salama mpaka kuzaliwa na hata baada ya kuzaliwa.
Zaburi 127:3
“Tazama, wana ndio urithi wa Bwana, uzao wa tumbo ni thawabu.”

—

3. Kwa jina la Yesu, ninainuka kinyume na kila roho ya utasa—iwe ya kiroho au ya mwili—na ninaitangaza kuwa imevunjwa; naachilia uzazi, uhai na matunda katika maisha ya wanawake wote.
Kutoka 23:26
“Hapatakuwa na mtu atakayeharibu mimba wala aliye tasa katika nchi yako.”

—

4. Ee Bwana, nalifunika uzao wa mwanamke kwa damu ya Yesu; ninaamuru kuwa adui hatakuwa na nafasi ya kuwaharibu watoto hawa wakiwa tumboni wala baada ya kuzaliwa.
Isaya 54:13
“Na watoto wako wote watafundishwa na Bwana, na amani ya watoto wako itakuwa nyingi.”

—

5. Ee Mungu, linda na simamisha kusudi la kuzaliwa kwa kila mtoto; kila alichokusudia tangu tumboni kisiingiliwe na adui, bali kitimie kikamilifu.
Wagalatia 1:15
“Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake…”

—

6. Ee Bwana, funua makusudi yako juu ya watoto wetu mapema; wafungue macho yao ya rohoni ili wajue wao ni nani ndani yako na waletwe katika hatima uliowaandalia.
Yeremia 1:5
“Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni nalikutakasa…”

—




15/04/2026

OMBA HIVI MWANA WA MUNGU 🧎🏽‍♀️🧎🏽‍♂️
1. Ee Bwana, ninaomba unifunue na unifute kila alama ya siri au ya wazi ambayo siyo yako katika maisha yangu, katika jina la Yesu.
Zaburi 139:23–24
“Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu; unijaribu, uyajue mawazo yangu…”

—

2. Kwa damu ya Yesu, ninavunja kila agano la ukoo, kifamilia au la kiroho lililoacha chapa isiyo ya Mungu juu yangu.
Wagalatia 3:13
“Kristo alitukomboa katika laana ya sheria, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu…”

—

3. Roho Mtakatifu, nifunike upya na unionyeshe k**a alama ya Mungu pekee iwe juu ya maisha yangu, mawazo yangu na mwili wangu.
Waefeso 1:13–14
“Mlikuwa mnatiliwa muhuri kwa Roho Mtakatifu wa ahadi…”

—

4. Ninafuta kila “antenna ya adui” iliyowekwa kunifuatilia au kunipangia mabaya katika ulimwengu wa roho.
Isaya 54:17
“Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa…”

—

5. Ee Bwana, nivae alama yako ya wokovu, ulinzi na mamlaka ili adui asiguse hatima yangu.
Ufunuo 7:3
“Msiidhuru dunia… hata tutakapowatia muhuri watumishi wa Mungu wetu…”


 
 


14/04/2026

🚶🏾‍♀️🚶🏾God never designed you to walk alone.

“And He gave some to be apostles, some prophets, some evangelists, some pastors and teachers, to equip the saints for the work of ministry, for the building up of the body of Christ.” (Ephesians 4:11–12)

It’s not just “me and God.”
There is wisdom in covering.
There is safety in guidance.
There is growth under spiritual authority.

As a person, you are not complete on your own.
You will always need the people God has placed over you.

Without guidance, you may lag behind.
You may repeat battles that wisdom could have helped you avoid.
But spiritual covering gives you speed.
It helps you grow faster, see clearer, and walk stronger.

Sometimes, God answers your prayers through a person He has appointed to lead you, correct you, and guide you through difficult seasons.

Honor the voices God has placed over your life. They are part of your becoming.

—

Mungu hakukusudia utembee peke yako.

Kuna hekima katika kuwa chini ya uangalizi wa kiroho.
Kuna usalama katika kuongozwa.
Kuna ukuaji chini ya mamlaka ya kiroho.

K**a mtu, hujakamilika peke yako.
Utawahitaji watu ambao Mungu ameweka juu yako.

Bila mwongozo unaweza kuchelewa.
Unaweza kurudia makosa ambayo ungeepuka kwa hekima.
Lakini uangalizi wa kiroho unakupa kasi.
Unakusaidia kukua haraka, kuona wazi, na kusimama imara.

Waheshimu wale Mungu ameweka juu yako. Wao ni sehemu ya mabadiliko yako.
📌Bonyeza linki ya YouTube kwenye bio kuangalia mafundisho yote:
SUNDAY SERVICE 12, April, 2026.


Photos from Adm ministries's post 14/04/2026

SUNDAY 12.04.2026 IN PHOTOS 🤍✨
Grateful for every moment, every smile, every quiet blessing this day brought.



Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Address


Kinyerezi Mnadani
Dar Es Salaam