Nira ni kifaa kinachotumiwa kumshurutisha mnyama atii kwa lazima. Vifaa vingine vinavyotumika kutiisha kwa lazima ni pamoja na kulabu, na hatamu.
Kulabu na hatamu hufungwa kwanye pua na shingo.
Bwana Yesu alitumia mfano wa vifaa hivyo kuonyesha vile mtu anavyotakiwa kusaidiwa kutii. Pia, mitume wa Bwana Yesu waliichukulia ile torati ya Musa k**a nira. Kwa sababu inaulazima. Ni lazima mtu aitii torati. Asiyeitii torati huadhibiwa.
Lakini Bwana Yesu alileta nira nyingine tofauti na hatamu na kulabu na nira ya Musa. Aliielezea nira hiyo kuwa ni laini, inayomsaidia mtu kutii, badala ya kumlazimisha. Nira ya Bwana Yesu inamfanya mtu apende kutii, moja kwa moja toka moyoni mwake.
Tuendelee kujifunza...
Stawi Ministries
Karibu katika ukurasa wa huduma ya Stawi. Huduma hii ni kwa ajili ya kufundisha Neno la Mungu
Kuishi moyoni
Mambo ya ROHONI
Dunia ina uhitaji mkubwa wa Mungu. Yaani, Mungu aonekane, akitenda kazi hapa duniani. Dunia ina uhitaji mkubwa wa kazi za Mungu. Watu wajue kuwa yupo Mungu anayemiliki, kutawala na kutiisha hapa duniani.
Sasa, ili hayo yatokee, itakuwa tu ni kwa kupitia watu waliofunuliwa na Mungu. Watu watakaotawala, kumiliki na kutiisha mazingira yao na mambo yao ndio watakaomdhihirisha Mungu hapa duniani. Hata sasa, kutawala, kumiliki na kutiisha ni nadra sana kwa watu.
Tuendelee kujifunza...
Pale unapopokea maarifa moja kwa moja toka kwa Mungu pasipo kupitia kujifunza kwa elimu ya kidunia. Unafahamu mambo, unaelewa, unapambanua kwa namna isiyotokana na elimu ya dunia. Hapo unakuwa umepokea ufunuo toka kwa Mungu
Mungu akijidhihirisha kwako utakuwa na ushuhuda wa kudumu
MUNGU AMEJIDHIHIRISHA KWA WATU KWA NAMNA NYINGI
Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njianyingi.......
Waebrania 1:1 (a)
Mungu hujitokeza kwenye maisha ya mtu binafsi. Kule kujitokeza kwenye maisha ya mtu binafsi kunaitwa Ufunuo wa Mungu.
Enzi hizo, Mungu alipojitokeza kwa watu binafsi, walifanya ukumbusho kwa kuweka alama au kutajia watoto wao majina yaliyoelezea kile alichokifanya Mungu kwenye maisha yao.
Mfano, "Hata sasa Mungu ni Ebenezer", ilitokana na mtu aliyetokewa na Mungu akaamua kufanya ukumbosho wa mahali alipotokewa na Mungu na kupatajia jina hilo la Ebenezer.
Tuendelee kujifunza zaidi......
Ujuzi mwingi, au maarifa huleta majivuno.
Mtume Paulo alizilinganisha credeintials zake zote na mavi. Pia, ameeleza kwenye 2 Wakorintho 8:1 kuwa, ujuzi, (maarifa) huleta kiburi. Mtu mwenye maarifa huwa anavimba kichwa. Huwa anayategemea yale maarifa. Huwa anajiona kuwa bora kuliko wengine kwa sababu ya maarifa aliyo nayo.
Lakini ndo trend ya siku hizi. Tuendelee kujifunza
Mtume Paulo Alifunuliwa Siri za Mungu
UFUNUO WA NENO LA KRISTO
Ufunuo ni haki ya kila mwana wa Mungu. Usipokuwa na ufunuo wa Neno la Kristo utaishi maisha ya kubahatisha sana. Na, ninafahamu kuwa wapo wapendwa wengi sana wanaoishi maisha ya kubahatisha kijumlajumla. Wanapapasapapasa k**a vipofu, na kupoteza muda mwingi sana wakihangaika huku, na kule, juu na chini, ili kupata kile ambacho Mungu alikwisha wapatia, au alikwishakiachilia bure.
Tuendelee kujifunza pamoja
WITO WA MTUME PAULO
Wito wa Kufundisha
Agizo kuu la Bwana Yesu ni kwenda ulimweni kwote kuwafanya mataifa wote kuwa wanafunzi wake.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Contact the school
Telephone
Website
Address
P. O Box 12345
Dar Es Salaam
0255
Opening Hours
| Monday | 09:00 - 17:00 |
| Tuesday | 09:00 - 17:00 |
| Wednesday | 09:00 - 17:00 |
| Thursday | 09:00 - 17:00 |
| Friday | 09:00 - 17:00 |
| Saturday | 09:00 - 17:00 |
| Sunday | 09:00 - 17:00 |