Vijana Na Fursa

Vijana Na Fursa

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Vijana Na Fursa, Personal coach, Dar es Salaam.

Nawasaidia Wanawake Na Wanaume Wa Kiafrika Kuwa Na Mfumo Wa Biashara Utakao Wawezesha Kutengeneza Kipato Cha Milioni 1 Nakuendelea Kwa Mwezi Kwa Mtaji Wa Tsh 125,400 tu.

24/12/2022

CAREER DEVELOPMENT

Kipi bora kujiajiri au kuajiriwa? Usifanye haraka kujibu swali hili. Fikiri kwa kina kwanza.

Kila upande utakao chagua una faida na hasara. Itategemea wewe unatafuta nini katika maisha yako.

Natambua unalo jibu lako.Hebu tuangalie faida za kila kimoja. Baada ya hapo utakuwa katika nafasi nzuri ya kuweza kuchagua upande unaoutaka.

FAIDA ZA KUAJIRIWA

1️⃣Uhakika wa kipato kila baada ya muda fulani. Kipato chako kinatabirika hivyo ni uhakika.

2️⃣Unakuwa katika nafasi nzuri kuweza kukopesheka na taasisi za fedha. Taasisi za fedha ziko tayari kumkopesha mtu mwenye kipato cha kuaminika (reliable source of income)

3️⃣Kujihakikishia kiinua mgongo au pensheni ya uzeeni.

4️⃣Fursa ya bima ya afya kwa wafanyakazi huwa ni rahisi zaidi.

5️⃣Ni shughuli ambayo haina risk kubwa. Hakuna uwezekano wa kupoteza pesa zako. Upande wa kujiajiri kuna wakati unapoteza mtaji wako kutokana na kupata hasara.

6️⃣Mbali na mshahara unaweza kupata marupumarupu ya hapa na pale pamoja na safari za kulipiwa.

FAIDA ZA KUJIAJIRI

1️⃣Mtu aliyejiajiri anapata faida za kodi (Tax advantages).Mwajiriwa hawezi kuepuka makato ya kodi kirahisi.

2️⃣Uhuru wa muda wako. Una maamuzi na muda wako. Unaamua kuutumia upendavyo wewe.

3️⃣Uhuru mkubwa zaidi wa maamuzi. Unakuwa na uhuru wa kufanya maamuzi yako bila kuingiliwa au kupangiwa na mtu mwingine.

4️⃣Uwezekano wa urithishaji. Mradi au shughuli binafsi unaweza kurithisha kwa watoto au ndugu zako. Lakini ajira hakuna kurithisha.

5️⃣ Uwezekano wa kuingiza mapato makubwa zaidi. Kwa aliyejiajiri hakuna ukomo wa kipato chake k**a ilivyo kwa mwajiriwa. Kadiri biashara inavyokwenda vizuri na kipato hupanda zaidi na zaidi.

6️⃣Kuna uwezekano wa kutajirika kwa haraka sababu biashara haitabiriki k**a ilivyo kwa ajiri. Mazingira yakiwa mazuri unatoka haraka.

Vp, bado una msimamo wako ule ule juu ya masuala haya? Nimeeleza upande wa faida pekee. Sijaeleza hasara au madhaifu ya kila upande.

Wewe unayo nafasi ya kuchagua unataka kuwa nani. Si jambo zuri kufuata mkumbo. Angalia malengo yako ni nini hasa. Kisha chagua upande unao utaka. Mimi si wale wanaoshinda wanadanganya watu mitandaoni.

Shea na marafiki
_____________
The best way to learn is to learn from the best

24/12/2022

Kuna pahala ifike tuache kujidanganya
wenyewe. Kuna pahala ifike Visingizio uamue kuviweka pembeni na kupambania kweli kile umedhamilia.
K**a unasema unakosa usingizi
sababu ya Maono uko nayo, Basi kweli
uwe unakosa usingizi sababu ya watu wengine wengi tu ambao wanawezakuwa tegemeo Lao 📌

23/07/2022

Ukiambiwa kwa mtaji wa 125,400/= inaweza kukusaidia kutimiza malengo ilikuwa nayo,unafikiriaje?

Najua majibu uliyonayo ni HAIWEZEKANI,MATAPELI au HAWA NI WALE WALE.

Sasa achana na mawazo haya kwasababu ninachoenda kukukwambia sio cha KUWA WALE WALE unaokutana nao.

Bila kupoteza muda.

Bonyeza neno WHATSAPP uje INBOX ili nikuelekeza mfumo salama wa biashara ambao kwa uwekezaji wa 125,400/= utautumia kukuingizia kipato kitachokusaidia KULIPA KODI,KUNUNUA GARI,KIWANJA ,KUJENGA NYUMBA NA KUKIDHI MAHITAJI YAKO MENGINE YA KILA SIKU tofauti na unavyodhani.

Kumbuka kuna nafasi 20 Tuu hivyo wahi nafasi yako ikiwa bado mapema.

Note; Hii sio kwaajili ya kila mtu lakini kwa wale wenye malengo na mawazo chanya ya kimaendeleo.
WhatsApp 0716712618

23/04/2022

K**a wewe ni kijana, mjasiriamali ama muajiriwa na ungependa kuongeza mkondo wa kipato kupitia mda wako wa ziada bila kuathiri shughuli zako za sasa wasiliana na si kwa namba +255716712618 au bonyeza link
👇👇
https://wa.me/255716712618 kuja moja kwa moja WhatsApp kwa muongozo zaidi.

03/03/2022

MASWALI 7 YA KUJIULIZA KABLA HUJALALA, KUHUSU HALI YAKO YA KIFEDHA

1.Je leo umeandika kila pesa uliyopata kwa uaminifu bila kupuuzia wala kudharau kiwango chake?

2.Je leo umeandika kila pesa iliyotoka mkononi mwako (uliyotumia) kwa uaminifu bila kujidanganya wala kupuuzia udogo au ukubwa wa pesa husika?

3.Je, unajua jumla ya mapato yako na Jumla ya matumizi yako kwa leo tu?

Uwiano wake upoje?

Balance yako ipoje? Ni hasi au chanya?

5.Je leo umejitahidi kupunguza gharama za matumizi kadiri ilivyowezekana?

6.Kuna kitu chochote umenunua ambacho ulikuwa hujapanga kukinunua?

7.Je leo katika pesa uliyoipata umeweka akiba?

K**a ndiyo! Hongera.

K**a hujaweka akiba, kwanini?

Tafakari malengo yako ya mwaka, jipime mwenendo wako, halafu jijibu k**a ukiendelea hivyo, UTAFIKA?

k**a jibu ni hapana. jiulize itakuwaje...

03/03/2022

Adui Wa Malengo Yako Ni Tabia Ya Kughairisha Malengo...

Unashindwa kutimiza malengo yako kwa sababu ya kusema utafanya baadae au kesho na sio kuchukua hatua ya kuanza...

..sasa ili uweze kutimiza malengo yako

Una malengo makubwa sana ya;

1. Biashara, unapenda kuwa mfanyabiashara kubwa na mwenye kufanikiwa kwenye eneo la biashara

2. Ujasiriamali, kuna fursa umeiona na umeweka malengo kuwa fursa hiyo itabadili kabisa Maisha yako

3. Huduma, malengo kuwa Huduma yako itakuwa kubwa sana na mwenye mwenye ushawishi kupitia Huduma yako

4. Mahusiano, una malengo mahusiano yako kudumu kwa muda mrefu kwa kuwajibika ipasavyo kwenye mahusiano yako

5. Kipaji, Una malengo kuwa kipaji chako ukiendeleze kitakuingizia kipato na kuwa ajira yako

Nakadhalika

Una malengo makubwa sana lakini unashindwa kupiga hatua kwenye maisha yako sababu

Unasema utafanya kesho na kesho ikifika unasema utafanya kesho nyengine kiasi kesho nyingi pasipo kufanya

Unasema utafanya mwakani na mwakani ikifika unasema utafanya mwaka unaokuja pasipo kufanya

Unasema utafanya baadae na baadae ikifika unasema utafanya baade tena pasipo kufanya

Kwa maana hiyo!

Ili utimize malengo yako ni lazima ushinde tabia ya kughairisha malengo yako

Kushinda tabia ya kughairisha ni pamoja na kuanza kufanya muda huo huo yani sasa

Usisubiri uwe na kila kitu ndio uanze Hakuna “Parfect Time” ya kuanza zaidi ya wewe kuanza na kile ambacho unacho

Kushinda tabia ya kughairisha Tumia Kanuni ya dakika mbili (Two Minutes Rule)

Kazi yeyote ambayo unaweza kufanya chini ya dakika mbili ifanye mara moja bila kusubiri

Ukifanya kazi kwa dakika mbili utaweza kufanya zaidi ya dakika mbili na hii mbinu inaitwa kutrick ubongo wako kutoka kwenye eneo la kuridhika “Comforting Zone” na kuendelea kufanya kazi husika

Acha kughairisha malengo yako sasa kwa kutumia Kanuni ya dakika mbili

Je wewe unafanya nini ili kushinda tabia ya kughairisha malengo yako?

Kauli Mbiu: “Maisha Ni Kuthubutu”

______
ZINGATIA: “Muda sahihi wa kutimiza malengo yako ni sasa na sio kesho”
_______

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Address


Dar Es Salaam