tiaso_dsm

tiaso_dsm

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from tiaso_dsm, Education, Dar es Salaam.

27/05/2026

πŸ“’ GET PREPARED FOR IDRAS TRAINING – THIS SATURDAY!

TRA inaleta mafunzo ya mfumo mpya wa kodi (IDRAS) yatakayofanyika 30/05/2026 ndani ya TIA, yakihusisha vyuo mbalimbali vyenye jumuiya za kodi Dar es Salaam.

Ni nafasi muhimu ya kujifunza, kupata exposure na kuongeza uelewa wa mifumo ya kisasa ya kodi.

27/05/2026

πŸŒ™βœ¨ EID MUBARAK

TIASO DSM inawatakia Waislamu wote Eid yenye furaha, amani na baraka tele 🀍.

Mwenyezi Mungu akubali ibada zetu na atujaalie umoja, upendo na mafanikio mema.

Eid Mubarak to you and your family.

Photos from tiaso_dsm's post 21/05/2026

πŸ•ŠοΈ TAARIFA YA MSIBA

Kwa masikitiko makubwa, familia ya TIA DSM imempoteza mwanafunzi wetu Marion Evarist Minja (DBA), aliyefariki dunia tarehe 20/05/2026 katika Hospitali ya Kairuki, Dar es Salaam.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika Moshi, Uru.

Taarifa zaidi zitatolewa baadaye.

🀲 Apumzike kwa amani.

20/05/2026

KONTENA LA WANACHUO LIMEFUNGULIWA πŸ”₯πŸ”₯

Dirisha la usajili wa Msimu wa Nane wa Silent Ocean UNI AWARDS umefunguliwa rasmi.

https://uniawards.co.tz/participate.php

Bonyeza Link ya Usajili hapo juu Kujisajili , Tembelea Kurasa zetu za mitandao ya kijamii kwenye bio utakutana na link ukibonyeza itakupeleka sehemu ya kujisajili UTAHITAJI

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kwa namba : 0765533034 | 0738743417

SILENT OCEAN UNI AWARDS SEASON 8 πŸ”₯

15/05/2026

SPECIAL AND SUPPLEMENTARY RESULTS OUT NOW πŸ“Œ

13/05/2026

πŸ“ΆπŸ”₯ TTCL UNI WI-FI SASA TIA DSM

TTCL Corporation imefanya ufungaji na ufunguzi rasmi wa huduma za UNI WI-FI ndani ya TIA kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi, ikiwa na vifurushi vya unlimited internet kwa matumizi ya chuo na binafsi.

Rais wa Serikali ya Wanafunzi TIASO DSM amepongeza ujio wa huduma ya TTCL UNI WI-FI chuoni, akieleza kuwa huduma hiyo itakuwa na mchango mkubwa kwa wanafunzi katika kujifunza, kufanya tafiti na kuimarisha mawasiliano ya kidigitali.

πŸ’₯ Vifurushi Vinavyopatikana:
πŸ“Œ Tsh 1,000 – Unlimited kwa saa 24
πŸ“Œ Tsh 2,500 – Unlimited kwa siku 3
πŸ“Œ Tsh 5,000 – Unlimited kwa siku 7

πŸš€ Internet bila kikomo kwa experience bora ya kujifunza na ku-connect muda wote!

Photos from tiaso_dsm's post 09/05/2026

KIKAO CHA VIONGOZI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2026/2027

Viongozi mbalimbali wakiwemo Ma-CR, Wabunge, Viongozi wa Dini pamoja na Viongozi wa Associations wamekutana kwa ajili ya majadiliano muhimu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi 2026/2027.

Kikao hicho kiliongozwa na DEAN OF STUDENTS pamoja na jopo lake, wakisisitiza umuhimu wa uchaguzi wenye uwazi, mshikamano na uongozi bora kwa manufaa ya wanafunzi wote.

🀝 Uongozi bora huanza na maandalizi bora.

08/05/2026

πŸ“š FROM CLASSROOM TO CAREER

Karibu kwenye semina maalum ya INTERNAL AUDIT yenye lengo la kufungua fursa, kuongeza maarifa na kukuandaa kitaaluma kuelekea dunia ya kazi.

πŸŽ“ Learn. Grow. Succeed.
πŸ“ TIA University Main Hall
πŸ“… 09 May 2026 | ⏰ 09:00 AM – 02:00 PM

What to expect:

βœ… Career insights in Internal Audit
βœ… Networking opportunities
βœ… Free entertainment 🎢
βœ… Free meals πŸ›
βœ… Interactive sessions & inspiration
βœ… Fun and memorable experience πŸŽ‰

πŸ‘‰ Usikose nafasi hii muhimu ya kujifunza na kujijenga kwa ajili ya future yako.

07/05/2026

πŸ•ŠοΈ TAARIFA YA MSIBA

Kwa masikitiko makubwa, familia ya TIA DSM imepokea taarifa ya kifo cha mwanafunzi wetu KHAMIDA KHALID KIPONDAMALI, kilichotokea kufuatia ajali ya barabarani.

Tunatoa pole za dhati kwa familia, ndugu, jamaa pamoja na wanafunzi wote walioguswa na msiba huu mzito.

🀲 Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un.

πŸ•―οΈ Apumzike kwa amani.

Photos from tiaso_dsm's post 05/05/2026

πŸ›οΈ KIAPO CHA UONGOZI – TIASO DSM

Wabunge pamoja na Manaibu Mawaziri wa wizara mbalimbali wameapishwa rasmi, hatua inayoendelea kuimarisha uongozi na uwajibikaji ndani ya Serikali ya Wanafunzi TIASO DSM.

Uongozi ni dhamana, huduma na uwakilishi wa wanafunzi.

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Website

Address


Dar Es Salaam