25/10/2025
SLEEP PARALYSIS
Ni hali ya muda mfupi ambapo mtu akiwa amelala anashindwa kusogeza mwili wake, kuzungumza, au hata kupumua vizuri, licha ya kuwa anajitambua (yuko macho kiakili). Hii hutokea katika kipindi cha mpito kati ya usingizi na kuamka.
Kinachotokea:
- Wakati wa usingizi, mwili hupitia hatua ya REM (Rapid Eye Movement) ambapo misuli ya mwili hulemazwa ili kuzuia mwili kuiga harakati zisizo za lazima.
- Katika sleep paralysis, ubongo huamka kabla ya mwili kuondoka kwenye hali hiyo ya kupooza.
- Mtu hushindwa kusogeza miguu, mikono, au mwili mzima kwa sekunde chache hadi dakika chache.
Dalili:
- Kushindwa kabisa kusogea licha ya kuwa macho
- Kupoza kwa kifua au kushindwa kupumua vizuri
- Hali ya hofu au mfadhaiko
- Hisia ya uzito juu ya mwili (k**a kubanwa)
Sababu zinazoweza kusababisha:
- Uchovu au usingizi duni
- Kulala muda usiotosha
- Mabadiliko ya ratiba ya usingizi
- Kulala chali
- Msongo wa mawazo
Sasa mwili wa binadamu hufanya marudio ya vitu ambavyo mtu huvifikiria sana kupitia ndoto, ndio unakuta mtu akikutwa na hali hii halafu akaota ndoto fulani ya kutisha ambayo ni ya kimazingira tu halafu akakupa habari kuhusu WACHAWI unaweza ukajenga hofu ambayo hujawahi itarajia lkn ukweli hakuna mtu mjinga kiasi cha kuacha usingizi wake halafu aje kukusumbua ukiwa umelala 😄 HII SI KWELI
16/10/2025
10/10/2025
15/09/2025
08/08/2025
08/08/2025
14/07/2025
13/07/2025
04/03/2025
04/03/2025
30/10/2024