30/12/2023
Mkinipenda, mtazishika amri zangu. [16] Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; [17] ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. Yohana 14:15-17
Roho mtakatifu ni nguzo kubwa katika maisha yenye uhusiano na Mungu.
Kifupi ni kwamba hakuna mtu ambaye amemkataa Roho mtakatifu ambaye anaweza kuwa karibu na Mungu.
Katika video ambayo nimekuwekea link hapo chini utajifunza jambo kuhusu utendaji kazi wa Roho mtakatifu katika maisha ya mwanadamu.
Bonyeza 👇
ROHO MTAKATIFU KATIKA MAISHA YA MWANADAMU |Mwl Helman John
Roho mtakatifu ni Mungu katika utendaji, suala la yeye kutenda kazi katika maisha ya mwanadamu ni muhimu Kwa kiwango kwamba mwanadamu huyo anakuwa milki ya M...
21/09/2021
Kuna wakati hii ilisikika ndani yangu kwamba nahitaji kufanya kazi ya kuwajengea mtazamo sahihi wanafunzi.
Hapo ndipo kazi yangu ya academic coaching ilipoanzia.
Katika kazi hii nafanya vitu vifuatavyo.
1. Kumjengea mwanafunzi tabia ya kujisomea.
2. Kumsimamia kuhakikisha amefuta ratiba yake.
3. Kumpatia ushauri wa kitaalamu (career guidance)
Natiwa nguvu sana kila ninapoitwa kuongea na wanafunzi.
Lakini kinachonifurahisha zaidi ni zile shuhuda ninazo zipata kutoka kwa walionufaika.
kufanya
kwa ajiri ya watu
kufanya hayo
To God be the glory.
09/09/2021
Niliwahi kupitia changamoto ambayo mtoto wako anaipitia Sasa hivi.
Mwanafunzi anapohitimu darasa la saba anakuwa na uwezo mdogo wa kuzungumza na kuandika kiingereza hasa k**a hakusoma shule ya english medium.
Changamoto hii mimi nilipoipitia niliyaona madhara ya kuanza kidato cha kwanza Bila kujua kiingereza, niyomaa niliamua kuwekeza kwenye kuwasaidia vijana.
Katika kuwasaidia vijana waliohitimu darasa la saba mwaka huu, kabla hawajaanza kidato cha kwanza, nimeandaa program nzuri ya pre form one iliyoanza tar 13/09/2021.
Program hii itamsaidia kila mwanafunzi kujifunza kiingereza cha kuongea na kuandika na ataongea ndani ya mwezi mmoja, pamoja na kujengewa misingi imara ya kufaulu hisabati (Mathematics) ya sekondari.
Kupitia somo la Stadi za Maisha (Life skills) nitatumia uzoefu wangu wa kufanya academic coach kuwafundisha wanafunzi wangu mbinu za kufanikiwa kitaaluma na kuwajengea tabia mpya hili waweze kujisomea hata wakiwa nyumbani.
Tupo kigamboni CCM, jirani na mahak**a ya wilaya ya kigamboni au jirani na kituo cha police kigamboni.
Ada ni Tsh 45,000/= kwa kipindi chote cha miezi 3.
Ofa zetu ni T-shirt na ziara itakayofanyika mwishoni Mwa program yetu.
Mzazi mlete mtoto wako ajengewe uwezo na afundishwe mbinu za kusoma na kufaulu darasani.
Mwl Helman John
Academic coach & author.
0657 572 523
08/09/2021
Linapokuja suala la mimi na wanafunzi mimi nasimama k**a coach wao.
Tangu nimeanza kufanya kazi hii ya academic coaching nimejifunza mambo mengi sana.
Nimejifunza na kugundua kwamba hakuna mwanafunzi asiye na akili. Kila mmoja anaweza kufanya vizuri akiapata mtu wa kumsimamia.
07/09/2021
Wakati E.M.C inaanza.
Kipindi hiki siyo watu wengi waliokuwa wakiamini katika kile nilichokuwa nikifanya.
Hili likuwa tukio letu la kwanza, mwaka 2018.