04/03/2020
Kilakona Schools tunatambua urithi mkubwa mzazi anaweza akampa mwanae ni Elimu tena elimu bora.
Ndo maana kila mzazi hufurahi mwanae anapokua na maendeleo mazuri shuleni maana hiyo humpa uhakika wa kesho njema kwa mwanae.
tunataka mzazi utabasamu na mwanao kutokana na taarifa njema za maendeleo yake ya shule.
Tunayo system nzuri ya kiteknolojia ambayo tunahakika itaweka tabasamu kwa mtoto na mzazi pia.
Tupigie kwa #0623952938 tuzungumze au tu .
04/03/2020
Upo msemo unaosema “ukimuelimisha mwanamke umeelimisha dunia nzima “
Msemo huu ni kweli na haupingiki...maana mwanamke ambae ndie mama baadae,huwa ndio mwalimu wa kwanza kwa mwanae ama mwanafunzi maana mwanafunzi atakulia kwanza mikononi mwa mama k**a mtoto kabla ya kwenda kua mwanafunzi shuleni.
Mtoto wa k**e anahitaji elimu ya darasani ndio ila pia anahitaji sana elimu dunia ambayo hiyo itampatia nidhamu katika elimu yake ya darasani na akaweza kufikia malengo yake.
Clouds media group tunawapongeza sana sana maana wamelitambua hili na wakaanzisha program ya wakishirikiana na mh. na inayomlenga sana mtoto wa k**e wakimpa elimu dunia juu ya kupotezea ngono na tamaa mbalimbali wakati wakiwa bado wako shuleni.
Wameweza kuwafikia wasichana wengi kwa ziara zao za kwenda mashuleni,
Tunawapongeza kwa hilo. @ Dar es Salaam, Tanzania
28/02/2020
Kila mwenye kujua umuhimu wa elimu haachi kuzifurahia na kuziunga mkono kila shughuli za kuboresha elimu ya Tanzania.
Mbali na serikali yetu hasa wizara ya elimu,wako watu mbalimbali wenye kujitoa katika shughuli za kielimu wakiungana na serikali na kuifikisha elimu kwa walengwa na katika ile sura wanayoitazamia kufika.
Mmoja wapo ni na taasisi yake ya na hapo katika ni wakati kahudhuria Shughuli ya usambazaji wa vitabu kwa lugha ya kiingereza na nukta nundu kwajili ya wanafunzi vipofu.
Tunampongeza sana kwa moyo huo.
#0623952938
26/02/2020
🔵HABARI NJEMA KWA MZAZI🔵
Sasa bado mzazi unayo nafasi ya kuendelea kujua na kuona maendeleo ya mtoto anapokua shuleni bila ata ya kumngoja mpaka atakaporudi kutoka shule kupitia simu ya mkononi.
inakuletea teknolojia hii nzuri yenye lengo la kumuweka mzazi Karibu na mwanae wakati wote.
Bila Kua na kikwazo katikati labda cha kazi ama shughuli zingine mbalimbali.
utaweza kuona mahudhurio ya kila siku ya mwanao kila anapokua shuleni ukiwa popote ulipo kwa simu yako ya mkononi tu.
utaweza kuona majaribio na mazoezi yote ya mwanafunzi na kujua maendeleo yake.
zote za shule utaziona bila kusubiri kupewa na mwanafunzi.
System hii kikubwa inampa mzazi nafasi ya kuendelea kumlea mwanae ki elimu pia pamoja na walimu.
Tupigie kwa namba #0623952938 au tu nasi tukuhudumie. 🔹 tunaunganisha na kufanikisha
26/02/2020
K**a ilivyo kwa jua na mwezi kutupatia mwangaza unaosaidia macho kuweza kuona vyema wakati wa kutembea ili tujue tunakoelekea kuepusha kupoteza mwelekeo na kutofika tuendako...Ndivyo mwenyezi Mungu pia alitupa na mwanga mwingine wa ndani ya mtu kumulika ndani na mtu akaweza kuiona na kuitambua njia yake mwenyewe... Na mwanga huo ni 📚
Elimu humpa mwanafunzi ama mfunzwaji ufahamu ambao hutia mwanga akili yake nae akapata kujitambua mahali alipo,anakotakiwa kua na ata alikotoka...ndiomaana watu husema "Elimu ni msingi wa maisha"
Nchi yetu ya Tanzania, uongozi wake pamoja na mashirika na watu wengine binafsi imejitahidi sana hadi leo kuhakikisha kila mtoto anapata elimu tena elimu iliyo bora.Wazazi nao wanajituma kwa kila hali ili tu watoto wao wapate kwenda shule maana huo ni urithi mkuu watakaoweza kuwaaachia wanao.
Na maisha ya kielimu ya mwanafunzi inahusisha watu watatu ambao ni mwenyewe na .Wote hawa wanahitajika kua katika umoja ili kumshika mwanafunzi mkono katika elimu yake.walimu kwa sehemu kubwa sana wanasimama kwa nafasi yao ila kwa wazazi kumekua na changamoto kidogo,mtoto anakosa kupata sapoti ya kutosha kutoka kwa mzazi ama mlezi hata ya kutiwa moyo ama kuhimizwa juu ya masomo yake akiwa nyumbani na inakua hivyo sababu wazazi wanakua busy na shughuli za kiuchumi zenye kumfaidia mtoto pia hivyo hatuwezi kuwalaumu kwa vyovyote vile ila tupo kuwapa suluhisho katika hilo.
Sisi schools tumeliona tatizo hili na mengine mengi tutayaongelea na tumeona tutoe msaada kwa wazazi pia walimu katika kumsukuma mtoto apate elimu bora..post inayofuata tunaelezea zaidi kuhusu 📚
25/02/2020
Mheshimiwa amepost katika ukurasa wake wa Instagram maneno yenye kuonyesha furaha na kujivunia juu ya Kijiji cha kilichopo akisema mwaka jana alienda kijijini kwao na kukuta shule iliyokua na uhitaji mkubwa wa vyumba vya madarasa na vyoo na akanuwia kuchangia ujenzi wa madarasa mawili na matundu Sita ya vyoo.
Ila kilichomfurahisha sana ni kukuta zaidi ya kile alichokitegemea...kwa Juhudi kuu ya wananchi wa kijiji cha Visiga pamoja na mchango kutoka kwa mbunge wao mpendwa mh Jafo alikuta madarasa yamejengwa vizuri mpaka Ofisi za walimu,madawati ya wanafunzi,viti na Meza za walimu.
Sio hapo tu,wananchi wa kijiji cha Visiga kwa kujua umuhimu wa usalama wa afya zao wamemjengea Mganga wa zahanati yao nyumba.
Mheshimiwa kwa kujua umuhimu wa mazingira mazuri kwajili ya wanafunzi,ana haki kuwafurahia wananchi wa Visiga Kisarawe kwa juhudi yao kubwa.Nasi pia tunawapongeza sana sana sana wananchi wa Visiga kwa juhudi yao,tunampongeza na mbunge wao Seleman Jafo of course na mh. kwa mafanikio hayo.
na kufanikisha
25/02/2020
*from the previous post*
KILAKONA SCHOOLS inakuletea teknolojia nzuri na rahisi yenye lengo kuu la kutoa mkono wa usaidizi kwa wazazi,walimu, wanafunzi na taifa kwa ujumla katika kuhakikisha ile elimu bora iliyokusudiwa kutolewa kwa wanafunzi inawafikia bila kuwepo na kikwazo chochote.
Teknolojia hii ina system inayoweza kuwaweka wahusika wakuu wote watatu yani walimu,wazazi na wanafunzi kwa pamoja Katika ukaribu mzuri kupitia tu simu zao ama kifaa chochote cha umeme k**a laptop au kompyuta na hivyo kuiondoa gepu kubwa iliyokua kati ya walimu,mwanafunzi na mzazi ambayo ilisababishwa na mambo kadhaa ama changamoto ikiwemo wazazi kua busy sana na shughuli za kiuchumi mpaka kushindwa kufwatilia kwa ukaribu mzuri maendeleo ya shule ya mwanae.
Na hiki ndicho sisi tupo kwajili ya kukitatua na kuwezesha watoto wetu kufaulu kwa vyovyote vile.
technology yetu mzazi ataweza kuona mahudhurio yote ya mwanae darasani.
ataweza kuona majaribio mbalimbali na mazoezi ya darasani ya kila Siku ya mwanae
ataona ratiba nzima ya shule ya mwanae ya mwaka mzima.
ataweza kujua kila mahala atapokua mtoto wake kwa kipindi chote atakachokua shuleno hivyo kua na uhakika wa usalama wake.
Hayo na mengine mengiiii yanatolewa na kampuni yetu ya kiteknolojia ya .. tunatamani sana tukuhudumie wewe mzazi na shule aliyopo mwanao tukiwa na kiu kubwa ya kuona wanetu,wadogo zetu,ndugu zetu wanafaulu vizuri katika masomo yao na taifa likiongezeka wasomi.
tupo kuunganisha na kufanikisha🌻
Kwa maswali ama maelekezo zaidi usisite kututafuta Ama tupigie/tuma sms alafu tutapiga kwa #0623952938 or #0766250000