Shariff Hassan Jamalullayl

Shariff Hassan Jamalullayl

Share

Ni Shariff anayetokana na nasabu ya Mtume Muhammad (S.A.W)

06/09/2022

Hatua ni njia yetu , maombi ni jitihada zetu ila mtengenezaji ni Allah s.w

Allah atujaalie tuwe miongoni mwa wenye kumtaja kwa wingi.

Amiin

22/08/2022

Usimshawishi mkeo akusamehe deni la mahali yake haifai pambana ulipe.

28/07/2022

Karibu sana tujumuike pamoja kumtukuza muumba wetu.

26/05/2022

MwenyeziMungu pekee ndiye anaetoa riziki kwa waja wake bila ya kutaka malipo kwa yeyote yule.

24/05/2022

Allah S.W ni muweza wa yote.

22/05/2022

Hakika kwenye kumdhikiri Allah S.W nyoyo hupata utulivu. QURAN

17/05/2022

Mimi na wewe hatujui mwisho wetu.

Kuna watu wanakufa katika hali mbaya sana.

Kuna watu wanakufa kwa kupondwa na magari barabarani.

Kuna watu wanakufa wakiwa katika sehemu za kumuasi Allah (S.W).

Kuna watu wanakufa wakiwa wamegombana na ndugu zao.

Je mimi na wewe tunaujua mwisho wetu ?

Ni wazi kwamba hatuujui.

Hatuna budi kumuomba MwenyeziMungu atupatie mwisho mwema.

Tuseme kwa pamoja

"Yaa Allaaahu bihaaa Yaa allaaahu bihaa Yaa Allaahu Bihusnil Khaatimah"

16/05/2022

Alhamdulillah !

Group letu la WhatsApp limekamilika.

Ndani ya hili group nitashare elimu inayohusu masuala ya ndoto , tiba & ushauri.

Group hili ni bure kabisa.

Halina malipo yoyote.

Tuma namba zako za WhatsApp pamoja na jina lako kamili kwenda WhatsApp 0674676470 uweze kusajiliwa ndani ya group.

والله ورسوله أعلم
شريف حسن جملليل

14/05/2022

BISMILLAH RRAHMAAN RRAHIIM

PART TWO

Kwa upande wa ISTILAHI Sharifu ni mtu anayetokana na kizazi au ukoo wa Mtume S.A.W.

Hivyo Sharifu ni sifa ya jina inayotumiwa na jamii nyingi za waislamu kumaanisha kizazi cha Mtume S.A.W

Ila kuna tofauti ndogo ya matumizi hayo kwa baadhi ya jamii moja kwenda jamii nyengine kulingana na tumbo gani au ukoo gani mtu huyo wa kizazi cha Mtume S.A.W inamalizika nasaba yake hadi kufika kwa Mtume S.A.W

Kwa upande wa waislamu wa mataifa ya Ghuba , Indonesia , Malaysia na nchi nyengine za mashariki ya mbali kutoka Hadhramout au Yemen kwa ujumla walihamia kwa shughuli mbalimbali ikiwa pamoja na mataifa ya Afrika ya Mashariki kusini mwa Afrika na kwengineko.

Watu wa kizazi cha Mtume kinachopitia kwa Sayyiduna Al- Husayn huitwa Saadah (kumaanisha wengi) au Sayyid (Kumaanisha mmoja).

Vile watu wa kizazi cha Mtume S.A.W kinachopitia kwa Sayyiduna Al- Hassan kaka wa Sayyiduna Al- Husayn huitwa Sharifu au Ashraf.

Wakati mwingine huchukuliwa jina la mmoja wapo wa mababu wa ukoo husika na kuitwa kizazi cha tumbo hilo kwa jina la mmoja wa mababu zao maarufu. Kwa mfano Kizazi cha Mtume nchini Hadhramout na Yemen huitwa BAALAWIYY yaani ukoo wa Baa- Alawy huyu ndie Babu mkuu wa karibu matumbo yote ya masharifu wa Hadhramout na kusini mwa Bara Arabu.

Jina jengine ni Al-Alawiyyin yaani kizazi cha Sayyidina Aliyy bin Abi Twalib.

Huu ndio muhtasari wa neno Sharif au Shareef tokea upande wa matumizi ya lugha tu hadi matumizi ya ISTILAHI.

11/05/2022

BISMILLAH

Sharifu kwa upande wa lugha ni mtu mwenye kuheshimika au ni kitu chenye kutukuzwa na kuheshimika.

Aghalabu mtu huitwa Sharifu na wala hajiiti Sharifu.

Maana kujiita Sharifu kwa maana ya kuheshimika ni kiburi na kiburi ni haramu katika uislamu.

Vyovyote iwavyo kidini haijuzu kujitukuza kwa kujiita Sharifu maana hicho ni kiburi , kujinata na kujitutumua Jambo ambalo halifai katika uislamu (haramu).

Ila watu wanaweza kumuita mtu Sharifu kutokana na matendo mazuri anayoyafanya.

Pia mtu anaweza kupewa jina halisi "Sharifu bin Fulani" hapo haimanishi kutukuzwa bali ni jina halisi k**a jina lolote jengine , K**a Karim ,Azizi ,Rahim na kadhalika.

Nakala ijayo nitazungumzia maana ya Sharifu kwa upande wa ISTILAHI.

Allah is the most merciful

09/05/2022

Usikufuru.

Usikufuru kwa sababu ya mapenzi.

Usikufuru kwa sababu ya ugumu wa maisha.

Usikufuru ukawa mwizi.

Usikifuru ukaangamiza watu.

Tambua ndugu yangu ....

.... huwezi kufanikiwa kwa njia za udanganyifu.

Mtegemee yule ambaye anazimiliki roho zetu.

Anaejua lini tutarejea kwake.

Anaejua rizki yako ipo wapi.

Mungu ndiye muweza wa kila kitu.

Mtegemee yeye pekee.

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Address


Dar Es Salaam