Benson Chonya

Benson Chonya

Share

Karibu katika page hii, uweze kujifunza mbinu za kufanikiwa kimaisha na biashara

12/11/2024

Ili mtaji wako uwe salama zaidi kabla hujaamua kufanya uwekezaji wa aina yeyote ile amini ya kuwa kile unachokijua wewe hakitoshi bali unatakiwa kujifunza kwa watu wenye uzoefu na kitu hicho.

Na njia pekee itakayokusaidia kuweza kujifunzai kutoka kwa wazoefu hao, ni kuwatafuta wazoefu hao ili waweze kukuelekeza kile ambacho wao wana uzoefu nao.

K**a unataka kupata uzoefu kwenye uwekezaji wa biashara ya mkaa ni lazima umtafute mtu ambaye tayari ana uzoefu au ambaye anafanya biashara hiyo.

Ukiamua kujifunza biashara ya kuuza mkaa kwa muuza nyanya huenda ukapata majibu na hamasa za uongo zaidi kwa sababu mtu huyo hana uzoefu wa kutosha juu ya biashara ya kuuza mkaa.

Hivyo ili uweze kulinda mtaji wako kabla ya kufanya uwekezaji wowote ule uliza kuhusu kile unachotaka kuwekeza kwa mtu sahihi, kwani uwekezaji wowote ule bila taarifa sahihi ni hasara ya kiwango cha lami.

Benson Chonya Afisa Mipango

12/11/2024

Miongoni mwa sababu ambazo hupoteza fedha za watu wengi ni pamoja na watu hao kuwa na tamaa ya kuwa na utajiri kwa haraka, kitendo hiki ni kibaya na kimesababisha fedha za watu kupotea bila sababu ya msingi.

Wengi wamekuwa na tamaa za utajiri wa muda mfupi, kwa mfano mtu akishirikishwa kuhusu fursa au biashara fulani kwamba inalipa zaidi mtu huyo pasina kuhoji faida na changamoto zinazopatikana katika fursa hizo hujikuta aikiingia kichwa kichwa huku akiamini atapata faida.

Kitu ambacho huwa na kinyume chake, sasa ikiwa unataka kulinda fedha zako, acha kuwa na tamaa za utajiri wa haraka, kila kitu unachoshirikishwa kuhusu kitu fulani, kabla hujaamua kufanya uwekezaji wako ni lazima uelewe kitu hicho kwa undani zaidi.

Kwani k**a utaamua kufanya uwekezaji wako pasipo kulijua jambo hilo unalotaka kuwekeza basi jiandae kupoteza mtaji wako wote. Kabla hujafanya uwekezaji wowote ule hakikisha unajua hatari na mafungufu kwenye kile unachotaka kuwekeza.

©Benson Chonya Afisa Mipango

12/11/2024

Nukuu ya leo

11/11/2024

Watalamu mbalimbali wa masuala ya kifedha wanashauri ya kuwa njia pekee inakayomsaidia mtu binafsi kuweza kufanikiwa kwenye mambo ya kifedha ni pamoja na uwekaji wa akiba.

Lakini pia wanashauri ya kuwa kuwa akiba pekee haitoshi, bali muwekaji wa akiba huyo kile alichokiweka akiba baada ya muda fulani anatakiwa kufanya uwekezaji.

Uwekezaji ambao utazifanya fedha ziweze kujazalisha maradufu zaidi ya zilivyokuwa hapo awali wakati wa uwekaji akiba.

Na katika hili tunakumbushwa pia ya kuwa kwenye kila fedha tunayoipata baadala ya kufanya matumizi yasiyokuwa na tija basi tufanya fedha hizo zijizalishe zenyewe kupitia uwekezaji.

©Benson Chonya Afisa Mipango

11/11/2024

Changamoto kubwa waliyonayo watu wengi kwenye dunia hii ya leo ni kwamba wengi wao wanaishi mitindo ya maisha isiyo rafaki. Wengi hulalamika kuwa maisha ni magumu huku wakisahau kuwa ugumu huo husababishwa na wao wenyewe.

Wengi wanaishi maisha kutokana na kuiga, mtu akiona mtu mwingine ana simu nzuri, gari nzuri au kitu chochote kizuri naye anatamani awe na kitu hicho pasipo kuangalia uwezo wake.

Aina hii ya mtindo wa maisha ndipo niporejea kusema wengi wetu tunaishi mitindo ya maisha isiyokuwa rafiki kwa sababu mwisho wa siku huwa tunaambulia maumivu makali sana kwani huwa tumekuwa tumefanya maamuzi ya kununua vitu ambavyo hatukupanga kufanya hivyo.

Kitendo ambacho hufanya mwisho wa siku tusione thamani fedha zinazopita mikononi mwetu. Sasa ikiwa unataka kubadili aina ya maisha unayoishi na kuona kila thamani ya pesa unayoipata basi unatakiwa sana kuishi kulingana na uwezo wako, pia ishi kulingana na mtindo wa maisha unaokufaa.

Acha kuishi maisha ya kuiga kwani ukiendelea kufanya hivyo hutaona thamani ya fedha zako kwani utakuwa unafanya matumizi ambayo hukupanga kufanya hivyo.

©Benson Chonya Afisa Mipango.

10/11/2024

K**a ilivyo ule usemi maarufu usemao "hatma ya maisha yako ipo mikononi mwako" basi hata jukumu la kupanga bajeti yako ipo ndani ya uwezo wako.

Kumpa jukumu hilo la kupanga bajeti yako lifanywe na mtu mwingine ni sawa na kumwambia punda abebe mizigo anayotaka yeye.

Kwa akili yako unafikiri ukifanya hivyo je punda huyo atafanya k**a wewe unavyotaka? Jibu ni hapana bali punda huyo atabeba mizigo kulingana na yeye anavyotaka.

Kwa muktadha huo utaona ni kwa namna gani jukumu la kupanga bajeti yako linatakiwa lianzishwe na wewe ili mambo mengine yaende k**a vile utakavyo wewe.

Kupanga bajeti yako ni muhimu sana, kuishi bila kuwa bajeti ni sawa kuanzisha safari ghafla huku ukiwa huna uelekeo ya kule uendako ni lazima utapotea tu.

Ili usipotee ni muhimu kila mmoja wetu kuwa na bajeti yake ambayo anakuwa anaipanga yeye mwenyewe.

Kuwa na bajeti ni muhimu sana kwa sababu hii itatumika k**a ramani ambapo itakusaidia sana kwenye kufanya matumizi na kujua hela zako zinatumika wapi zaidi.

Je ni kwenye matumizi ya lazima au kwenye matumizi yasiyokuwa na ulazima? Panga bajeti ili kujua matumizi ya lazima na yale siyo kuwa na lazima.

©Benson Chonya Afisa Mipango

10/11/2024

Ili uweze kuishi maisha yenye furaha na amani tele ndani yako hususani suala la kufanya matumizi sahihi ya pesa, unatakiwa kuchunguza namna unavyoishi na unavyofanya matumizi yako ya kila siku.

Wengi wetu hatuna tabia ya kuandika matumizi tunayotaka kuyafanya kwa siku husika, kitendo ambacho kinatupelekea kufanya matumizi ambayo wakati mwingine hayana ulazima wowote wa sisi kuweza kufanya hivyo.

Jukumu pekee ambalo unatakiwa kulifanya ni kuhakikisha unaandika mahitaji yako kisha angalia ni yapi ya muhimu na yapi si ya muhimu kuweza kuyanunua.

Yale ambayo si ya lazima ni muhimu sana uweze kuachana nayo na yale ambayo ni ya muhimu basi unaweza kuyatekeleza.

Anza mara moja utaratibu huu wa kuandika yale unayoyahitaji kununua kupitia pesa yako ili kuepusha kufanya matumizi kwenye yale yasiyokuwa na ulazima.

©Benson Chonya Afisa Mipango

09/11/2024

Kanuni pekee ambayo unaweza kuitumia ili uweze kuona kila thamani ya fedha inayokatisha kwenye mikono yako ni kuwa na ukomo katika matumizi.

Unapokuwa na pesa kuwa makini sana matumizi yako. Usitumie fedha nyingi kwa sababu eti unazo fedha hizo au una uhakika wa kupata tena nyingine.

K**a umezoea kutumia shilingi mia tano kwa siku kwenye kipato chako cha shilingi elfu mbili, basi jitahidi sana hata kipacho chako kikiongezeka matumizi yako yabaki yale ya shilingi mia tano labda vinginevyo kuwe na ulazima wa wewe kuongeza matumizi yako.

Nimesema hivyo kwa sababu pesa mara nyingi huwa sina makelele za kumkumbusha mmliki wa fedha hizo kwamba afanye matumizi, na kelele hizo hutokea hasa pale mtu huyo kipato chake kinapoongezeka.

Njia pekee ya kuthibiti matumizi yako hasa pale kipato chako kinapoongezeka, ni kuwa na ukomo wa kufanya matumizi yako. Si kila kitu lazima ukinunue, si kila safari lazima usafiri, si kila mtindo wa maisha lazima uishi, si kila gari la thamani lazima uwe nalo.

Kuwa na ukomo wa matumizi yako itakusadia sana.

© Benson Chonya Afisa Mipango

09/11/2024

Ili uweze kufanikiwa kifedha unapaswa kujifunza kutofautisha kati ya matumizi ya lazima na matamanio.

Wengi wetu tunapoteza fedha zetu nyingi kwenye vitu vya matamanio zaidi.

Tunafanya matumizi kwenye vitu ambavyo wakati mwingine hatuna hata uhitaji navyo ila tunafanya hivyo kwa sababu tunaendeshwa na hisia za matamanio tu.

Unakuta mtu hakupanga kununua kitu fulani ila kwa sababu mtu huyo anaendeshwa na hisia tu za matamanio unakuta kanunua kitu hicho pasipo kupanga.

Kuendelea kufanya kitu hiki si sawa hata kidogo kwa sababu k**a utaendelea kufanya hivyo hutaona thamani ya pesa ambazo hukatisha mbele yako, hii kwa sababu kila fedha itakuwa inapitiliza tu kwenye matumizi yasiyokuwa na maana.

K**a nilivyosema hapo awali kuwa wengi wetu huendeshwa zaidi na hisia za matamanio na kila kipato chetu kinavyoongezeka pesa hizo huishia kwenye kununua vitu hivyo visivyokuwa na ulazima.

Pia ukweli pekee usioufahamu kuhusu vitu vya matamanio ni kwamba huwezi kuvitimiza vyote kwa mara moja. Kila unapotimiza hiki kinakuja kitu kingine ambacho kinakuwa ni kizuri zaidi ya kile ulichonunua mwanzo mwanzo.

Ikumbukwe kuwa hata uwe na fedha nyingi kiasi gani ila ukiwa unaongezwa na akili ya matamanio hakuna kitu cha maana utakachofanya, kwa sababu pesa yako yote itakuwa inaishia kwenye mambo hayo ya kimatamanio.

Sasa ili tuweze kufanikiwa kifedha ni muhimu sana kupunguza matamanio mengi yasiyokuwa na ulazima ili tuweze kufanikiwa.

©Benson Chonya Afisa Mipango

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address


Dar Es Salaam
52112