MAISHA NI K**A KIKOMBE CHA KAHAWA.
Kikundi cha Wanafunzi waliomaliza chuo (alumns) miaka ya nyuma na ambao walikuwa wamezitendea haki taaluma (Careers) zao walienda kumtembelea Professor wao aliyewafundisha chuo kikuu miaka hiyo.
Maongezi na Professor wao wa zamani yalikuwa ni mengi ila baadae wale wanafunzi wa zamani wakaegemea katika kulalamika juu ya stress za kazi na maisha kiujumla.
Kwa kuwakalibisha wageni wake kahawa, professor alienda jikoni na kurudi na chupa iliyojaa kahawa na vikombe vya aina mbalimbali k**a vile vya udongo, vyenye rangi ya dhahabu, vya plastick, vya gharama na vya kawaida vya bei ya chini.
Kisha akawaambia wale wanafunzi wake wa zamani kila mmoja ajimiminie kahawa yake.
Baada ya kila mmoja kuwa na kikombe cha kahawa mkononi, professor akaanza kuwapa "lecture": akasema "k**a mmegundua, kila kikombe kizuri kinachovutia kimechukuliwa na kila mmoja wenu, na mmeacha vile vya bei ya chini ambavyo havina muonekano mzuri.
Hii inamaanisha nini?
Pale ambapo kila mmoja wenu atataka ajiridhishe na kile kilicho bora, hapo ndipo chanzo cha stress na matatizo katika maisha ya kila mmoja wenu mnayoyalalamikia huanza.
Hebu angalieni aina ya kikombe siku zote haiongezi ubora wowote katika kahawa utakayokunywa. Wote hapa mlichokua mkikihitaji ni kahawa na sio kikombe, ila wote mmekimbilia vikombe vizuri na kuanza kutizama huyu kachukua cha aina gani na huyu vipi.
Sasa nawapa hili, kuweni na fikra pana na wazeni nje ya box; maisha ni k**a "kahawa". Ila kazi, pesa na vyeo katika jamii ni "vikombe", vikombe hivi ni zana tu za kutubeba katika maisha.
Wanafunzi wangu, aina ya vikombe au zana hizi tulizonazo hazituelezei au kubadilisha aina ya maisha tunayoishi.
Hivyo basi, muda mwingine tunapokuwa busy sana kuchagua vikombe, mwisho wa siku tunashindwa kufurahia kahawa ambayo ndio maisha yenyewe.
Ni nini ninachokilenga?
Jitahidini sana kuthamini kahawa (maisha) na sio vikombe. Watu wenye furaha sio kwamba vitu vyao vyote vipo bora, ila wanajitahidi kadiri ya uwezo wao kufanya kila kitu kiwe bora, kwavyo ndimo furaha hutamalaki katika maisha yao na kufurahia kahawa.
Live simply. Love generously. Care deeply. Speak kindly.
Piga vita umaskini kwa kujiajiri
JINSI YA KUPIGA VITA UMASKINI KWA KUTUMIA FURSA MBALIMBALI ZA KIBIASHARA
NAZUNGUMZA NA WEWE KIJANA
Kuna vijana wanakuwa na ndoto za kufanikiwa. Namuomba Mungu awaangalie, awalinde na kufanikiwa katika kile ambacho kila siku mnakipigania.
Kuna vijana wameridhika, wanaona wamepata, kuwa na milioni ishirini kwenye akaunti zao wanajiona kumaliza kila kitu. Namuomba Mungu awakumbushe kwamba hakuna tajiri anayeridhika, hata Bill Gates ni tajiri wa dunia lakini bado anatafuta pesa.
Kuna vijana leo wanapanga kwenda kula maisha katika kumbi mbalimbali, watumie kwa staili wanayoiita kula bata. Namuomba Mungu japo awaambie kwamba kuna watu wanatafuta hata shilingi elfu ishirini tu wafungue biashara, wainue misingi ya biashara zao.
Kuna vijana wanashinda katika mitandao ya kijamii, wakibadilisha picha, kuchati na kufanya mambo mengine. Namuomba Mungu awape nguvu ya kutambua kwamba kuna maisha nje ya mitandao ya kijamii, awape utashi wa kugundua kwamba unapokaa sana kwenye mitandao ya kijamii, kuna baadhi ya vitu havitosonga maishani mwako, na k**a vikisonga, havitosonga kwa kasi inayotakiwa kusonga.
Napenda kuzungumza na vijana kwa sababu...
i) Wewe ni mtu muhimu.
ii) Ukifanikiwa wewe, taifa limefanikiwa.
iii) Sitaki nikikuona ukianguka, ukianguka wewe, taifa limeanguka.
iv) Taifa linatakiwa kujengwa, halitojengwa na wazee, sisi tumeshajichokea, tunakupa kijiti wewe kuendelea kuliendeleza taifa hili.
v) Maisha mazuri ya uzeeni, hayatengenezwi uzeeni, hutengenezwa ujanani.
Kijana, chukua kalamu na karatasi, andika vitu unavyotaka kufanya mwaka huu, hata k**a akaunti ina shilingi elfu moja halafu unatamani kununua gari, andika kwamba mwaka huu lazima ununue gari. Mwaka ukiisha hujanunua gari, jiulize tatizo lilikuwa nini, pale utakapoliona tatizo, usiliache, litatue, mwaka huo, weka tena lengo la kununua gari, nakuhakikishia, utalipata tu.
Naomba SHARE kuwasaidia vijana wengine.
MUNGU AKUBARIKI.
22/02/2016
Yafuatayo ni mambo ambayo unayotakiwa kusema HAPANA katika maisha yako yote:
1. Sema hapana kwa uvivu.
2. Sema hapana kwa tabia ya kuahirisha mambo.
3. Sema hapana kwa tabia ya kufuata mkumbo.
4. Sema hapana kwa tabia ya kulalamika.
5. Sema hapana kwa tabia ya kutoa au kupokea rushwa.
6. Sema hapana kwa tabia ya kutokujiwekea akiba.
7. Sema hapana kwa mahusiano ambayo hayakujengi.
8. Sema hapana kwa vipindi vya TV vinavyokupotezea muda.
9. Sema hapana kwa tabia ya kutegemea wengine ndio wabadili maisha yako.
10. Sema hapana kwa tabia ya kukwepa majukumu yako.
11. Sema hapana kwa tabia ya kutafuta njia ya mkato ya kupata mafanikio.
12. Sema hapana kwa tabia ya kutegemea kupata vitu vya bure.
13. Sema hapana kwa tabia ya kusengenya wengine, kupika majungu.
14. Sema hapana kwa tabia ya kufikiri hakuna fursa.
15. Sema hapana kwa imani kwamba wewe huna bahati.
16. Sema hapana kwa imani kwamba wenye fedha wana roho mbaya.
17. Sema hapana kwa kazi ambayo unaifanya lakini huipendi.
18. Sema hapana kwa biashara ambayo unaifanya lakini inakusumbua.
B
19. Sema hapana kwa ulevi.
20. Sema hapana kwa tabia ya kufuatilia maisha ya wengine.
21. Sema hapana kwa tabia ya kufanya mambo kwa mazoea.
23. Sema hapana kwa kwa hofu zinazokuzuia kufanya mambo makubwa
24. Sema hapana kwa tabia ya kutokujiamini.
25. Sema hapana kwa kuendelea kuwa wa kawaida.
26. Sema hapana kwa tabia ya kupoteza muda mwingi kwenye mitandao.
27. Sema hapana kwa tabia ya kukosa uaminifu.
28. Sema hapana kwa tabia ya kunyanyasa au kukandamiza wengine.
29. Sema hapana kwa tabia ya kufikiri kwamba kuna uhaba wa fedha.
30. Sema hapana kwa tabia ya kuanza mambo na kuishia katikati.
09/02/2016
MASWALI 10 KWA KILA MTU ANAYETAKA UMILIONEA
Ukita uwe milionea miaka michache ijayo, ni vyema na lazima kujihoji maswali. Haya hapa ni mojawapo:
1. Je siku ya leo nimefanya jambo gani ambalo litanifanya kesho niishi maisha niyatakayo ya umilionea?
2. Je haya ninayoyafanya sasa hivi au hii kazi niko nafanya sasa au ninayotaka nifanye ndiyo itanipeleka kwenye umilionea niutakao?
3. Nani tusaidiane kufanya hii kazi ninayoifanya ili tunufaike wote? Hakuna milionea duniani anayefanya kazi zake zote peke yake. Ukitaka uwe milionea tafuta watu wakusaidie kufanya kazi.
4. Nifanye nini leo ambacho kitaniwezesha kuishi kimilionea ifikapo kesho?
5. Ni madhaifu gani makubwa niliyonayo sasa yasizidi 3 hivi ambayo yatanikwamisha Kuwa milionea? Ninawezaje kuyarekebisha ili yasinikwamishe?
6. Ninawezaje kutoa msaada kwa watu wengi zaidi duniani ili kuwaondolea shida walizonazo? Usipokuwa tayari Kusaidia watu wengi ambao wamekwama kimaisha tarajia na wewe kukwama. Unavyosaidia wengi kujikwamua ndivyo utapata kufanikiwa.
7. Nikiambiwa nijirekebishe tabia zangu zinazonizuia kufikia mafanikio ni tabia zipi hizo? Je niko tayari kuziacha? K**a unayo tabia fulani inayokuzuia kufanikiwa; ngono, sigara, ulevi, wizi, uvivu, wapenzi wengi, nk usikubali kurudishwa nyuma. Jitoe sasa hivi. Anza upya.
8. Je, nina mpango wa kufanya kazi gani au kazi zipi kwa Januari hadi Machi au Aprili hadi Juni? Miezi 3 ijayo nataka kazi ipi iwe imekwisha?
9. Nifanyeje kuwasaidia watu wengi zaidi wajikwamue? Hapo ulipo kuna watu wengi sana wanasubiri hekima zako ili watoke kimaisha. Jiulize kila siku mbinu za kufanya ili kuwawezesha wengine kutoka shimo la umaskini.
10. Nifanyeje ili kuboresha kazi yangu iweze kupendwa zaidi na ipanuke kuwafikia watu wengi zaidi ya hawa? Kila siku fikiria kufikiri kuboresha kazi zako.
Nakutakia siku njema.
Mbinu 5 Za Kukuwezesha Kuishi Maisha Ya Malengo
Siri kubwa ya kufikia mafanikio unayoyahitaji katika maisha yako ni kuhakikisha unaishi maisha yanayoendana na malengo yako. Kinyume na hapo utakuwa ni mtu wa kupoteza muda wako kutokana kuishi maisha yasiyo na mwelekeo kitu ambacho ni hatari kwako.
Ili uweze kufanikiwa hiki ni kitu ambacho hutakiwi kukwepa hata kidogo. Jukumu kubwa unalotakiwa kulitambua ni kuelewa misingi na malengo yako unayotakiwa kuyafuata kila siku bila kupotea. Je, ni mbinu zipi unazoweza kuzitumia ili zikusaidie kuishi maisha yenye malengo?
1. Jifunze kusema HAPANA.
Watu wengi kutokana na kuwaogopa au kuwahofia watu waliokaribu nao, hujikuta wao ni watu wa kukubali karibu kila kitu wanachoambiwa hata k**a kitu hicho kinawabana. Hiki ni kitu ambacho kinaonekana kuwa kigumu kwa wengi hasa linapokuja suala la kusema HAPANA.
Kwa bahati mbaya sana kutokana na hilo wengi hujikuta wakiishi maisha ya kuyumbishwa yasiyo na msimamo wala malengo. Ili uweze kuishi maisha ya malengo na kuishi maisha yako ni lazima kujifunza kusema HAPANA kwa mambo mengi usiyaelewa kwako. Hilo litakusaidia sana kuishi kwa malengo siku zote.
2. Kuwa makini na muda wako.
Vipo vitu vingi unavyoweza kuvipoteza katika maisha yako ukavipata lakini siyo muda. Muda ulionao ni wa thamani sana na kwa bahati mbaya ukishaupoteza umepotea kabisa hauwezi kurudi tena. Hiyo yote ni dalili tosha inayoonyesha kuwa kuna uthamani mkubwa ulio ndani ya muda wako ambao hutakiwi kuupoteza.
Sasa k**a wewe unaishi maisha ya kupoteza muda sana, inabidi uelewe kuwa hivyo ndivyo unavyopoteza maisha yako na mwisho wa siku unajikuta ukiishi maisha yasiyo na malengo kabisa ikiwa na pamoja utakosa mafanikio. Unaweza usilione hili mapema sana lakini kwa kadri unavyozidi kupoteza muda wako nafasi ya kufanikiwa inakuwa ndogo.
3. Sahau yaliyopita.
Itakuwa haina maana sana kwako k**a utaendelea kungang’ania mambo mengi ambayo yameshapita. Hiyo itakuwa ni sawa na kupoteza muda. Maisha siku zote ni kusonga mbele na wala siyo kurudi nyuma. Sasa basi, inapotokea sehemu umekosea, jifunze kutokana na makosa hayo kisha endelea mbele.
Utakuwa ni mtu ambaye huishi kwa malengo ikiwa utazidi kushikilia, kujilaumu na kung’ang’ania mambo yaliyopita. Tafuta mwelekeo na dira mpya itakayokufanya uzidi kufanya mambo yako kwa upya hadi kufanikiwa zaidi na tena kwa viwango vya juu.
4. Tambua mambo yapi ni ya muhimu kwako.
Siyo kila kitu ni cha muhimu kwako. kwa maana hiyo ni muhimu kuyachagua mambo ambayo ni muhimu na ya lazima katika maisha yako na k**a ni kuyatekeleza ndipo uanzie hapo. K**a ni malengo chagua yale kwanza ya muhimu kwako, kisha utekelezaji ufuate.
Acha kujidanganya kuwa kila kitu ni cha muhimu kwako. Na k**a utazingatia kila kitu na kukiona ni cha muhimu kwenye maisha yako basi, utakuwa umepotea. Hii ni kwa sababu utajikuta mambo yako mengi unashindwa kuyakamilisha kutokana na kukosa uzingativu kwa kile unachokifanya..
5. Jiwekee malengo kila wakati.
Hiki ni kitu ambacho hupaswi kukisahau hasa linapokuja suala la kuweka malengo. Mara nyingi malengo unapokuwa nayo yanakuwa yanakupa mwelekeo wa kuweza kusonga mabele na kukupa hamasa zaidi. Unaweza ukajiwekea malengo ya muda mrefu au ya muda mfupi hata kwa siku ili yakupe mwelekeo sahihi na kuishi maisha ya malengo.
Kwa vyovyote vile unahitaji kuishi maisha ya malengo ili uweze kufikia mipango na malengo makubwa uliyojiwekea katika maisha yako.
ANZA MWAKA NA MALENGO MAPYA ACHANA NA YALIYO PITA SONGA MBELE.
Napenda kumshukuru mwenyezi mungu kwa kadri anavyozidi kutupigania katika maisha yetu ya kila siku,napenda kukushukuru ewe msomaji wa jumbe zangu mbalimbali za kupiga vita umaskini kwani huyu ndiye adui mkubwa wa maendeleo.
Leo ningependa tujifunze vitu ambavyo wengi wetu tunaona ni vidogo ila ndio vizingiti kufanikiwa katika biashara zetu za kila siku.
1.NIDHAMU
Biashara yeyote ina hitaji nidhamu nasema hivi nikiiamanisha ya kwamba jifunze mambo mapya kila siku iitwayo leo katika biashara yako,ungependa kuwa mjasiriamali jitahidi kuhudhuria semina,warsha mbalimbali za wajasiriamali wenzako ili uongeze ujuzi zaidi na elimu.penda kusoma majalida mbalimbali kwa watu waliofanikiwa,Kila utakacho fundishwa au kusoma kiweke katika matendo.
2.KUTOKUJITOA
Ili upate mafanikio inabidi ujitoe kwa ajili ya watu wengine,Angalia wafanyabiashara wengi waliofanikiwa au k**a umewahi kusoma makala zao wengi walijitoa kwa ajili ya watu wengine,usiwe mchoyo wa fikra jitoe kwa ajili ya mafanikio ya watu wengine.
3.KUKOSA SHAUKU.
Kukosa shauku na unacho kifanya au na biashara unayofanya hutofanikiwa,hutoendelea utaishia kulalamika tu! Ukiwa na shauku utapambana,utapenda uwe k**a MO,Ukiwa na shauku hutokata tamaa kabisaa utapenda kufikiwa malengo yako na inakuwa hivyo-
4.KUSUBIRI SIKU IFIKE
Usisubiri kufanya kesho itumie leo yako kufanya kitu k**a vile kesho haipo,Kuhairisha vitu vitakufanya ufe na ndoto zako,kila unachoweza kufanya leo kifanye punguza visingizio visivyo kuwa na sababu za msingi hizo ni hila za shetani kutaka kuchelewesha maendeleo yako.
5.KUOGOPA KUKATALIWA
Nakumbuka nilipoanza biashara ya mtandao jamii iliniangalia kwa jicho la tofauti ila kwa sababu dhamira yangu ilikuwa ni mafanikio sikuwasikiliza walichokuwa wanakisema bali nilipuuza na kusonga mbele kwa lugha ya nyumbani wanasema REJECTION IS EQUAL TO SUCCESS
Mwisho kabisa ningependa kusema katika biashara kuwa jasiri na ujiamini usiangalie au kufiria kwamba walimwengu watasema nini juu yangu,napenda nikutakie kheri ya mwaka usherekee kwa amani na utulivu.
AMUA SASA,FIKIRI SASA,TENDA
Mambo Muhimu Ambayo Ni Lazima Uyafanye Katika Maisha Yako:
Kwa kawaida kila mtu ana kanuni, taratibu au ambazo amejiwekea na kuishi nazo. Kanuni hizi zinaweza zikawa ni za kupanga au bahati mbaya lakini zipo. Ndio maana utakuta mtu yule maisha anayoishi yanatofautiana kwa kiasi kikubwa sana na mtu mwingine.
Lakini hata hivyo pamoja na kanuni au sheria hizo kuweza kutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine, huwa yapo mambo ya lazima ambayo kila mtu analazimika kuyafanya katika maisha yake. Haya ni mambo ya lazima ambayo unatakiwa uyafanye siku zote na mara kwa mara katika maisha yako:-
1. Jifunze kuwa mtoaji kuliko mpokeaji.
2. Onyesha heshima kwa kila mtu.
3. Linda maneno yako sana. Acha kuongea ongea hovyo.
4. Fanya mambo yako kwa ubora kila siku.
5. Kuwa na muda wa kuwasikiliza wengine.
6. Wape wengine moyo pale wanapokata tamaa.
7. Unapokosea, sema samahani kwa yule unayemkosea.
8. Kuwa mkarimu.
9. Jifunze kujisamehe wewe na kuwasamehe wengine.
10. Mara nyingi jifunze kuwa mtu wa shukrani katika maisha yako.
11. Jenga, tabia ya kujifunza kila siku.
12. Kuwa king’ang’anizi wa maisha yako mpaka ufanikiwe.
Hizo ndizo kanuni rahisi tu, ambazo unaweza ukaishi nazo katika maisha yako na kuishi maisha ya ushindi na amani.
CALL /WHATSUP 0759670912 UPATE ELIMU YA BIASHARA YA MTANDAO NI BUREEEE KABISA
MAMBO 10 UNAYOTAKIWA KUYAACHA KATIKA MAISHA YAKO ILI UFANIKIWE..!!👐🏼
Siku zote maisha ya mwanadamu yanaongozwa na miiko au kanuni,
Ni miiko hiyohiyo ambayo ilianza toka zamani,lengo lake kubwa lilikuwa ni kutuelekeza mambo yapi tufanye,na mambo yapi tusiyafanye katika maisha ili tufanikiwe...!
Wale waliofuata miiko hiyo ni kweli walifanikiwa,na wale waliokiuka walishindwa katika maisha yao kwa namna Fulani.
Kwa bahati mbaya au nzuri kanuni au miiko hii inafanya kazi katika maisha yetu mpaka sasa,wengi huwa hawajui katika hili,lakini upo ymuhimu sana wa kulijua na kuifuata hiyo miiko au kanuni,na kuachana na mambo ambayo yanaweza kuwa ni kizuizi kwetu cha mafanikio.
YAFUATAYO NI MAMBO UNATAKIWA KUYAACHA KATIKA MAISHA YAKO ILI UFANIKIWE..!
√1:Acha kuruhusu makosa madogo madogo hatimaye yakawa makosa makubwa na yakazuia kufanikiwa.
√2:Acha kukimbia changamoto zinazokukabili,pambana nazo mpaka ufanikiwe kuyafikia mafanikio makubwa maishani mwako.
√3:Acha kusahau ulikotoka yapo mambo ya kujifunza kutokana na kule tulikotoka.
√4:Acha Siku zote kujijengea Tabia ya kulalamika,K**a utaendelea kufanya hivyo utashindwa katika mambo yako mengi sana.
√5:Acha kuamini kuwa utashindwa kwa kile unachokifanya,KILA MARA NA KILA WAKATI AMINI KUWA WEWE NI MSHINDI WA MAISHA YAKO
√6:Acha kuruhusu Pesa ikutawale,badala yake itawale Pesa,na hiyo itakufanya kufikia Uhuru wa kipesa.
√7:Acha kuruhusu hofu ikakutawala maisha yako,maana kwa kadri utakavyozidi kuwa na hofu ndivyo ambavyo maisha yako yatazidi kuwa magumu,hiyo yote ni kwa sababu utashindwa kufanya mambo yako vizuri kwa sababu ya hofu ulizo nazo.
√8:Acha kuanzisha Biashara huku ukitegemea bahati ndiyo ufanikiwe..!,Ondoa mawazo ya Bahati fanya Biashara yako kwa kujiamini UTAFANIKIWA.
√9:Acha kujijengea tabia ya KUFURAHIA, hasa pale mambo ya wengine yanapokuwa MABAYA, badala yake watie moyo na kuwafariji,hakika UTABARIKIWA..!
√10:Acha kuogopa kusonga mbele,hata k**a kuna wakati unahisi k**a vile unakwama,wewe endelea kukazana kusonga mbele na mwisho wa siku UTAFANIKIWA.
MAFUNZO YA UJASIRIAMALI YANATOLEWA KUTOLEWA BURE KWA NJIA YA WHATSAAPP NICHEKI 0784670912 UPATE ELIMU BILA MALIPO
UBUNIFU
Ubunifu ni uwezo wa kuvumbua bidhaa au huduma mpya ama mbinu mpya za namna ya kukamilisha jambo, k**a inavyotakiwa.
Uwezo huu, upo kwa kila mmoja. Namna ya kuujua na kuutumia ndiyo hutofautiana, kati ya mtu na mtu.
Pamoja na kuwa sifa ya mjasiriamali halisi, ubunifu ni ujuzi unaoweza kujifunza, kujaribishwa na kutumiwa hata k**a hukuzaliwa nao.
Maisha ya karne hii, ni tofauti na karne iliyopita. Katika karne hii, ubunifu wa kila mtu unahitajika sana, hata k**a mtu huyu si mjasiriamali au mfanyabiashara. Ubunifu unatakiwa kwa wafanyakazi wa kawaida pia.
Mfanyakazi hodari ni yule anayetumia ubunifu katika kukamilisha majukumu ya kazi zake; kwa haraka na kwa ufanisi.
Ubunifu kwa meneja au mkurugenzi, unahitajika sana katika kubuni na kusimamia utekelezaji wa mipango ya biashara yake.
Mjasiriamali naye, hawezi kusonga mbele; k**a hatokuza ujuzi wa ubunifu wake. Ujuzi katika ubunifu ni uwezo wa kutumia maarifa na mbinu zinazo mhamasisha mtu atambue kile anachoacha kufanya au kinachomshinda; akifanye au akishinde. Na kwa kukifanya au kukishinda; ubunifu wake utaoonekana.
Ubunifu unawawezesha watu kung'amua fursa zilizojificha na kujiandaa kuzichangamkia haraka.
Hatua za kujiandaa, ni pamoja na kujitayarisha kushinda vikwazo vinavyoweza kuzuia utekelezaji wa ubunifu mzuri.
UBUNIFU UNAANZIA KWAKO KUWA MBUNIFU KWA KILA FURSA INAYOPITA MBELE YAKO.
MAFANIKIO SIYO AJALI
Watu wengi wanafikiri mafanikio ni kitu ambacho kinatokea tuu k**a ajali lakini mafanikio sio ajali wala sio bahati mafanikio ni mipango dhahiri ambayo inapangwa na mtu anayeyataka na ayenuia kutoka katika vilindi vya moyoni mwake kwamba anataka kutoka katika sehemu moja kwenye maisha ambayo inakuwa ni duni na kwenda sehemu nyingine ambayo ni ya hadhi nzuri.
Wengi wamekuwa wakijidanganya kwamba ipo siku moja watafanikiwa (watatoboa)lakini hawana mpango wowote wa kuwawezesha kufanikiwa katika iyo siku moja na nataka niwaambie kwamba iyo siku moja haitakaa itokee k**a hauna mpango dhahiri wa kupata unachokitaka katika maisha yako.
Unatakiwa kuwa na picha halisi ya kitu unachokitaka kwanza ndipo uende ukakitafute, kumbuka kumiliki kunaanzia kwenye akili kwanza acha kusema nahitaji nyumba nzuri,gari zuri,biashara nzuri, wakati hujapata picha halisi katika akili yako kile unachokihitaji unataka kiweje. Vijana wengi wamekuwa wakimaliza chuo Kikuu na kusema nipo tayari kufanya chochote huu ni ujinga na kutokuwa na maono hivi kweli k**a upo tayari kufanya chochote nkikuambia ukachimbe vyoo utachimba? Be definate (unataka nini kwanza) na hicho unachokitaka hakikisha una picha yake kwenye akili yako jinsi kitakavyokuwa ndipo unaanza jitihada zote zitakazokupelekea kupata kile unachohitaji.
Jambo hili limekuwa likisumbua watu wengi sana la kukosa picha halisi ya kile wanaachokihitaji na hivyo wamejikuta wakifanya vitu ambavyo hawavihitaji zikiwemo kazi wanazozifanya na kadhalika. Na hii pia ni mpaka kwenye kuoa/kuolewa kuwa na picha halisi ya mtu unaemtaka na sifa zake unataka aweje ndipo unapomuomba Mwenyezi Mungu sasa wewe unatafuta bila kujua unachokitafuta unataka kiweje? Weka hili katika akili yako litakusaidia sana.
Pindi utakapopata picha halisi ya kile unachokihitaji jicho lako lisiangalie nyuma, achana na hao marafiki wanaokuambia haiwezekani, maadamu akili yako imeweza kuwa na picha ya hiko kitu inamaanisha unao uwezo wa kukimiliki, watu wengi wameacha kufuata ndoto zao kwa kusikiliza maoni ya watu wengine ambao wamewakatisha tamaa na wakaacha kufanya kile walichokuwa wanataka kufanya.Hili naomba lisitokee kwako kabisa hakuna anaejua kile ambacho una uwezo wa kukifanya hata mzazi wako hajui unao uwezo mkubwa sana wa kufanya mambo makubwa na ya ajabu ni kiasi cha wewe kujiamini na kutenda tuu.
Anza kupambana fanya juhudi zote zitakazokupelekea kupata kile ulichonacho katika akili yako k**a ni kuna masomo ya ziada inakubidi ukasome hakikisha unasoma hayo masomo, k**a kuna watu fulani unatakiwa uwaone hakikisha unawaona hao watu kwa sababu siri ni hii huwezi kufanikiwa katika maisha haya pasipo msaada wa watu/mtu fulani, niliwahi kusema hivi na ninasema tena leo kwa mara nyingine achana na huu msemo nitafanikiwa mwenyewe (natoboa )itakuchukua muda mrefu na pia utatumia nguvu nyingi sana.
Ili kufanikiwa inakubidi SAA zingine utafute waliofanikiwa wakushike mkono. Mfano hebu jenga taswira kwenye akili yako kuna watu wawili wote wamekaa chini kwenye sakafu ninachotaka hapa ni kwamba mmoja amuinue mwingine aliekaa nae kwa kumvuta mkono,Je hilo zoezi litawezekana wakati wote wamekaa chini?
Bila shaka haliwezekani kadhalika na kwenye mafanikio huwezi ukainuliwa na mtu ambaye yupo sawa kiuwezo wa kufikiri,kiutendaji,na kiuchumi k**a wewe tafuta aliekuzidi katika nyanja hizo au ambaye anaweza kukushauri,au ambaye tayari kashasimama ndipo atakapokunyooshea mkono na kukuvuta kisha utainuka.
10/09/2015
BADILISHA FIKRA ILI UFANIKIWE.
JE?UNGEPENDA KUMILIKI BIASHARA YAKO BINAFSI
JE? UNGEPENDA KUPATA KIPATO CHA ZIADA UNGALI UPO KWENYE AJIRA YAKO.
JE?UNGEPENDA KUWA NA UHURU WA KIFEDHA
JE?UNGEPENDA KULETA MABADIRIKO KATIKA MAISHA YAKO.
JE? UNGEPENDA KUFANYA BIASHARA POPOTE
JE? UNGEPENDA KUPATA KIPATO ENDELEVU
JE? UNGEPENDA KUISAIDIA JAMII KIAFYA NA KIUCHUMI.
Hayo yote yanapatikana katika biashara ya karne ya 21 kwa kuzingatia mda,watu na jitahada zako binafsi,Mafunzo yanatolewa kwa njia ya whatsaap kuanzia jumatatu hadi jumamosi,ungependa kushiriki nitumie majina yako kamili na namba yako ya simu kwenda 0784670912, napenda watu wapenda mabadiriko yaani wenye uchu na maendeleo au ambao wamechoshwa na mkate wa kila siku,MAFUNZO NI BUREEEEE.WAHI SASA.
08/09/2015
KATIKA KILA JAMBO LA MAFANIKIO LAZIMA UPATE WAPINZANI
Ili kuuthibitishia ulimwengu kuwa unaweza hupaswi kuishia kuwaambia kwa maneno tu bali fanya kwa vitendo! Usikubali hata siku moja kuishi k**a watu wanaokuzunguka wanavyotaka! Ili uwe ICON/ SUPERSTAR LAZMA USEMWE, USONYWE, UTUKANWE, UTENGWE, UWEKEWE VIKAO KILA SEHEMU NA UONEKANE ADUI AMA MSALITI. Unapokutana na mambo hayo ujue mafanikio yako yamekaribia mpendwa!
Usishangae kuvunjika hadi kwa mahusiano yako kwà ndugu zako marafiki hata mpnz/Mme au mke wako hasa kila siku atakavoona unamuaga mara leo uko na Fulani kesho na Fulani kwenye semina kubwa kubwa tena kwenye hotel kalikali!
Tambua kuwa haya ni mapigano/ vita ambayo lazma ushinde hvyo maadaui ni wengi. Huna budi kufunga mkanda tayari kuingia vitani,
Fanya maamuzi sahihi kwa wakati unapopata fursa ya kufanya biashara, Embu leo kaa chini kwa mara nyingine tena utafakari wewe unakosa nini cha kukufanya uwe shuhuda wa mafanikio kwa watu wengine! Changamoto unazopitia ni njia mojawapo ya dalili za mafanikio au ni mbinu za kukuwezesha akili ifanye kazi!
Mungu ni mwema anazijua nia zetu na tutafika endapo tu tuna nia. PENYE NIA PANA NJIA"
PAMOJA TUNAWEZA
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Telephone
Website
Address
Magomeni
Dar Es Salaam