24/09/2023
Kazi kazi kazi
Ukurasa huu una lengo la kushirikikisha habari za matukio na shughuli mbalimbali katika Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam
24/09/2023
Kazi kazi kazi
22/08/2023
USAJILI WA MTIHANI WA HSK 1-4 TAASISI YA CONFUCIUS CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
Mwisho wa usajili: 13/9/2023
Tarehe ya mtihani: 15/10/2023
WAHI UJISAJILI SASA
15/03/2023
Walimu na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Baobab watembelea Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Tarehe 15 mwezi wa tatu majira ya asubuhi, walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Baobab walitembelea Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mwalimu Li Xiaoping wa Taasisi ya Confucius aliwapeleka wanafunzi hao wa shule ya sekondari Baobab kutembelea maktaba ya Taasisi ya Confucius, kisha akatambulisha utamaduni wa chakula wa Kichina, utamaduni wa Cheongsam (gauni la Kichina) na Ukuta Mkuu kwa wanafunzi katika chumba cha darasa namba 205 katika jengo la Taasisi ya Confucius chuo kikuu cha Dar es salaam.
02/03/2023
Mafunzo kwa njia ya mtandao kutoka chuo kikuu cha “Zhejiang Normal University”. Tarehe 21 hadi 31 mwezi wa tatu. Usajili wa mafunzo utafungwa tarehe 10/3/2023. Jisajili kupitia “QR code hiyo kabla ya tarehe 10/3/2023.
Mafunzo ya HSK na HSKK kwa ajili ya mtihani wa tarehe 18/3/2023, taasisi ya Confucius-UDSM.
Muda na mahali
1. Saa 2:30-4:00 asubuhi
-CI201
-CI205
2. Saa 4:30asubuhi-6:00 mchana
1&2-CI201
22/01/2023
Taasisi ya Confucius Chuo Kikuu cha Dar es salaam inapenda kuwatakia Heri ya Mwaka Mpya wa Kichina 22/01/2023.
Heri ya mwaka wa sungura.
HSK TEST ANNOUNCEMENT/
Subject :HSK level 2/4/6
Test Date 2023-01-07
Test Time:9:00
Subject :HSK level 1/3/5
Test Date 2023-01-07
Test Time:13:30
Subject :HSKK
Test Date 2023-01-07
Test Time:16:30
HSK Test instruction
1. Test takers must check personal information after getting the admission ticket. Any
incorrect information please contact the test center for help as soon as possible.
2. Test takers must present their admission ticket and original ID document with a photo to enter the test room. (The ID document is subjected to the one used for registration.)
3. For the paper-based test, please bring a 2B pencil and an eraser.
4. Test takers must enter the test room 30 minutes before the test time. Before the beginning of the listening test, test takers are allowed to enter the test room. When listening part has begun,test takers who arrived late are not allowed to enter the test room until listening part finished. After reading part has begun, Test takers who arrived late are not allowed to enter the test room.
5. Test takers can check test result through the official website of www.chinesetest.cn with their admission ticket number and name. Internet based test is available online two weeks after the testand paper based test result is available online one month after the test.
6. Score reports will be delivered to the test center within 1-2 months after the test date, and test takers can go for collecting by presenting test admission ticket and valid ID documents.
16/12/2022
Hafla ya Tuzo ya Balozi wa Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Mchana wa tarehe 14 Desemba 2022, Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ilifanya Sherehe ya Tuzo ya Balozi wa China 2022 katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Confucius. Prof. Bonaventure Rutinwa, Makamu mkuu wa chuo taaluma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na Dk. Rose Upor, Mkuu wa ndaki ya Insia, walihudhuria na kutoa hotuba. Prof. Mutembei, mkurugenzi wa Mtanzania wa Taasisi ya Confucius, alitoa hotuba ya ufunguzi. Liu Yu, mwanafunzi wa mwaka wa tatu anayesomea ualimu wa Kichina-Kiingereza katika Taasisi ya Confucius, alitoa hotuba k**a mwakilishi wa wanafunzi walioshinda tuzo hiyo. Prof. Zhang Xiaozhen, mkurugenzi Mchina wa Taasisi ya Confucius, pamoja na walimu wote na wanafunzi zaidi ya 100 walishiriki katika shughuli hii.
Jumla ya wanafunzi 37 na walimu 2 (Zhang Feng na Ding Xiang) kutoka Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam walishinda Tuzo ya Balozi.
03/12/2022
Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yafanikiwa kufanya mafunzo ya awali kwa walimu mwaka 2022.
Siku ya tarehe 25 Novemba 2022 saa 3:00 asubuhi, Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ilifanya sherehe za ufunguzi wa mafunzo ya awali ya mwaka 2022 katika ukumbi wa mikutano ulioko katika jengo la Taasisi ya Confucius. Hafla ya ufunguzi iliongozwa na Prof. Mutembei, mkurugenzi Mtanzania wa taasisi ya Confucius, Mheshimiwa Wang Siping, mshauri wa balozi kitengo cha utamaduni cha ubalozi wa China Tanzania na Prof. Mfinanga, makamu mkuu wa chuo utawala, chuo kikuu cha Dar es salaam walihudhuria na kutoa hotuba zao. Prof. Zhang Xiaozhen, Mkurugenzi Mchina wa taasisi ya Confucius chuo kikuu cha Dar es salaam, na Viongozi saba wa chuo kikuu cha Dar es salaam kutoka idara mbalimbali walihudhuria mkutano huo, na Mwalimu Liu Fang alizungumza kwa niaba ya walimu wapya wa kujitolea. Walimu wote wa Taasisi ya Confucius chuo kikuu cha Dar es salaam walihudhuria sherehe ya ufunguzi wa mafunzo haya ya kabla ya kazi.
Viongozi na wawakilishi kutoka Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Idara ya Mafunzo ya Shahada ya Kwanza, Ofisi ya Utumishi, Ofisi ya Mambo ya Nje, ndaki ya Insia, Shule ya Elimu na Ofisi ya Udhibiti Ubora walitambulisha kwa ufupi kazi zao na muundo wa idara zao, pamoja na uhusiano uliopo kati ya Taasisi ya Confucius na idara hizo. Inatarajiwa kuwa walimu na wanafunzi zaidi wa Taasisi ya Confucius watashirikiana kikamilifu na idara hizi katika siku zijazo.
17/11/2022
达累斯萨拉姆大学孔子学院39名师生荣获大使奖
当地时间2022年11月10日下午,中国驻坦桑尼亚大使馆举办第五届中国大使奖颁奖仪式。中国驻坦桑尼亚大使陈明健阁下;坦教育和科技部部长代表、教育总干事利亚布温博士及中国驻坦大使馆文化参赞王思平等出席活动。
来自达大孔院的学生王帅作为获奖学生代表发表感言。达大孔院的金佳伟表演了单口相声《报菜名》,赢得了到场中外嘉宾的阵阵掌声。
2022年“中国大使奖”获奖者共133名,34名卓越奖,91名鼓励奖。达大孔院12名学生获得卓越奖,25名学生获得鼓励奖,孔院本土教师张丰和丁香还获得了特别贡献奖。