Lusajo Mwamakula

Lusajo Mwamakula

Share

Motivational speaker and teacher. Youths and kids consultant, books writer

15/01/2021

Jinsi ya kumsahau mtu aliyekuacha au mliyeachana na bado unamhitaji lakini haiwezekani Tena kurudiana๐Ÿ‘‰๐Ÿผ

1. Jua kuwa hakuna kisicho na mwisho, hata Hilo litaisha. Utamsahau. Kwanza unamfanya nani kwako hata moyo wako uendelee kuteseka?
Mwenzako usikute anakula kuku huko aliko hata hakufikrii. Halafu wewe kila siku unalia. Unajidharau Sana. Unakesha unalia halafu bank hamna salio. Hizo nguvu si ukatafutie pesa mwanangu!!๐Ÿ˜ƒ

2. Yanaumiza, sawa, ila kubali umeachwa. Usipokubali itakusumbua Sana. Kubali moyoni. Kubali hata K**a unajihisi bwege kwa Hilo. Ila kubali tu halafu amua kuanza upya Sasa. Huo ndio uanaume na u superwoman. Sasa superwoman kilio kila siku jamani!

3. Kaa chini fikiria vitu ambavyo ulikosea, na virekebishe, K**a huoni kosa Basi hakuwa wako. Je unataka asiye wako? Halafu ukihisi Yuko na mwingine, siyo kwamba hufai, ila haikuwa sahihi kwako

4. Kuna watu wazuri wengi jamanii. Kweli inauma lkn Kuna wadada na wakaka wazuri huko nje jamanii. Unang'ang'ania sahivi una miaka unateseka tu. Move on, start over. Muoneshe kuwa unaweza ukaishi bila yeye. Unambembeleza miaka inaenda kwani yeye Ni cake๐Ÿ˜ƒ

5. Angalia future yako. Focus on it. Tengeneza future yako, jiongeze, fanikiwa, ili aje ajilaumu. Unavyojiumiza unachakaa, piga kazi, Soma, baadaye ung'ae. Akirudi mwambie Am no longer the same person๐Ÿ˜ƒ

6. Uliyeachana naye usiwe adui yake. Usimfanye adui ila mind your own business. Usimfanye kitu kibaya maana hujui baadaye mtakuja kutana wapi.

6. Jiamini kuwa unaweza. Unaweza kuanza upya na unaweza kumpata aliyesahihi na ukatulia na kusahau kabisa maumivu. Move on.
7. Muombe Mungu akupe wepesi, apoze maumivu, na umsahau. Kwanza wewe siyo wa Kwanza.
Be strong, be strong, acha kuteseka.
God loves u

15/01/2021

Mambo machache ya kufanya kwa mtu aliyeumizwa kwenye mapenzi au mahusiano.

1. Baada ya kuachana, punguza mawasiliano na mtu huyo. Kuendelea kuwasilina ndivyo utaendelea kuumia. Najua haishi maramoja, lakini utagundua kuwa inapoa taratibu. Mwishowe utashangaa umeanza kuzoea kutokuwa naye. Unapoumia unaweza waza K**a huwezi kupona na kuwa ok Tena, lakini Mungu ametuumba vizuri, katupa kusahau. Kwahiyo usimtafute, na ikiwezekana fanya K**a hayupo maishani mwako, na hujawahi onana naye. K**a unaweza, delete namba kabisa. Kwasbabu ukiwa na namba kuna siku tu utatamani kumpa hi.

2. Mungu anasaidia Sana, ukimuomba kutoka moyoni. akupooze moyo anafanya, na mambo yatakuwa shwari. Maana anajibu watu wake anaowapenda.

3. Jichanganye na wengine au tafuta wa kuchat naye, au tafuta rafiki mpya, ambaye unajiskia Raha ukiwa naye au kuchat naye, lakini usiingie kwenye mahusiano Hadi upone maumivu. Kuwa na rafiki mpya unayevutiwa naye, inakufanya upone haraka.

4. Fanya vitu uvipendavyo au vinavyokufanya ujisikie vizuri. Mfano unaweza kwenda saloon ukanyoa nywele style nzuri, K**a Ni mdada unaweza fanya mambo ya nywele zako zikawa poa, ukipendeza inakusaidia uwe chanya na kujiona Bora, inasaidia usijidharau kupata munkari wa kusonga mbele.

5. Jua kuwa kuumizwa si Jambo lililotokea kwako tu, wapo waliyotangulia. Kwahiyo Ni Jambo la dunia nzima. Wewe siyo wa Kwanza. Move on usije ukafa Bado kijana, future yako huijui usikute unatakiwa kuwa Rais baadaye. Ajuaye maisha yako Ni Mungu.

6. K**a unapata tabu Sana. Usiogope kuomba ushauri. Tafuta mtu unaedhani atakusaidia. Kuongea tatizo, ile tu kumwambia mtu, Ni sawa na kutatua tayizo kwa asilimia 50. Usitunze maumivu, yanaua, yansababisha ugonjwa wa moyo Kisha stroke. Sisi tunakupenda, kwhiyo jipende pia.

7. Tafuta sehemu kaa peke yako, halafu Lia Tena Lia kwa sauti, inasadia kuondoa uchungu moyoni, Lia Hadi uchungu uishe. Kisha amua Jambo la kufanya maishani lilio jema, then move on.

NB: Mvua inaweza kunyesha Sana, lakini baadaye, angani kunakuwa kweupe. Hivyo amini kuwa hata Hilo linapita na Ni changamoto tu.
Be strong girl, strong boy, Strong man, strong woman.
God loves you.
0752247575

29/12/2020

Mambo matano ambayo mwanamke akikupenda lazima ayafanye. Tujicheki wanaume.

1. Anajitahidi Sana kukupendeza. yaani hataki uwe na huzuni na yupo tayari kufanya chochote uone tu kuwa anakupenda. She shows her feelings.

2. K**a yupo nyumbani ukirudi toka job au kokote anakukaribisha na kukukiss sometimes. Mwnamke asiyekupenda hawezi fanya hivyo. Labda awe amevurugwa na Mambo yako ya ajabu

3. Ukimsifia ana smile kana kwamba ndiyo siku ya kwanza
Unaanza kumsifia K**a kwenye uchumba vile, huhuu

4. Ukiwa na stress, atajitahidi akausaidie ukae sawa. Atajaribu hata njia ya kukusaidia uwe ok. Mwanamke asiyekupenda hawezi fanya hivyo.

5. Mwanamke anayekupenda ukirudi home, haanzi na Mambo yake ya kelele za nyumbani, anatamani ajue ulikotoka K**a Ni salaama kwanza ndipo ukitulia atakusimulia ya nyumbani.

NB:. Anaweza akawa anakupenda , ila wewe unamvuruga Sana Hadi anashindwa kufanya hayo, moyo unasiita maana una maumivu. Kwahiyo mwanaume jiongeze ukiona tofauti na hapo.
Upendo Ni amri kuu
To God be the Glory

29/12/2020

Jinsi ya kunfundisha mtoto amjue Mungu๐Ÿ‘‰๐Ÿผ
1. Omba Mungu akiwepo mtoto akuone. Hiyo ni bonge la shule kwake
2. Soma biblia au kitabu kitakatifu huku anaona.

3. Unapotoa sadaka aone, na fanya kumshukuru Mungu huku anasikia

3. Omba toba kwa Mungu pamoja na mtoto hataK**a aombi lakini anajifunza kwako.

4. Ukiwa unafanya hayo, thibitisha kwa kuwa na tabia njema Kila siku.
Hiyo ni shule tosha kwa mtoto. Kisha mfundishe pia

Mwalimu wa Kwanza wa mtoto ni mzazi au mlezi. Ulivyo mzazi ndivyo mtoto anaweza kuwa karibu 99%

29/12/2020

Mke wako ni mzuri, sema anakosa matunzo na pamba unazopenda kiujumla.
Goodnight

29/12/2020

Jinsi ya kumfanya your girl au mke awe happy.

1. Msuprise na maua sometimes. Kweli kwa Tz maua yanaonekana hayana thamani Ila pesa. Lakini K**a mnapendana kweli, UA linathamani sana kwa mpenzi wako na kumuweka awe happy

2. Ukiwa mbali naye mfano kazini. Jifunze kumtumia meseji nzuri nzuri au tamu. Atajisikia unamkumbuka na kufurahia kuwa wako. Pia atajua yupo peke yake na kuwa secured.

3. Muite kwa jina lake muda mwingine. Kuna Siri kubwa katika kumuita mtu jina lake. Ukiita jina lake, muito anauhisi Hadi moyoni. Anafurahia Ila kuambii tu

4. Msifie. Kuna watu tangu wameoa hawajawahi wasifia wapenzi wao. Hakuna anayechoka kusifiwa. Hata Mungu hachoki. Mwanadamu anapenda kusifwa na moyo unakuwa mweupe na furaha. Mwambie you are beautiful hata siku moja moja basi. Anafurahia na kukupenda.

5. Mwambie nakupenda. Hili neno Ni adimu. Ukimwambia nakupenda unamfanya afikirie mengi na kuwa happy. Hakuna asiyetaka kupendwa. Neno kupenda anaposikia, linaenda kugonga moyo na kubadilisha mzigo wa moyo na kuwa mwepesi, na kusikia raha. Kupendwa raha jamaniiiiii hata kuambiwa tu.

6. Uwe kiongozi kwake. Hakuna mwanamke mwenye hekima anapenda mume mlegevu au ambaye hawi kichwa. Mwanamke anafurahia kuwa chini ya mume. Anajisikia yupo salaama na happy. Hata awe na pesa kiasi gani lakini mume kwake anamhitaji hataK**a hasemi naturally tu yaani. Kwasbabau wametokans na wanaume.

7. Mwambie wewe Ni watofauti, na Ni kweli hafanani na wengine. She is unque
8. Usiruhusu mkeo ateseke. Muondolee mizigo aliyonayo, wewe ndiye mume kwake

NB: wanawake acheni jeuri, mturuhusu tuwatendee mema. Ukiwa jeuri,sahau yote hayo juu kutendewa. Kaa katika nafasi yako Kwanza.

Ushauri 0752247575.

29/12/2020

Makosa 10 wanayofanya wanawaake kwa ndoa.

1. Mkipata watoto mnahamishia Upendo wote kwa watoto. Mahaba kwa baba hamna Tena. Anaweza kuenda kazini, siku nzima hakuna hata meseji ya I miss u. So boring

2. Mnachukia sana kutembelewa na ndugu hasa upande wake mwanaume. Roho mbaya. Japo siyo wote but wanawake mnafeli wengi hapo. Unamfanya mume apunguze penzi kwako

3. Uchafu. Ulivyodondokewa na tone la ziwa mtoto akinyonya hubadilishi nguo Hadi jioni. Halafu unavyovaa vaa ukiwa home hata huvutiii. Mwanaume huvutiwa na panapo vutia

4. Hamna romantic. Ulifanyaga kipindi Cha uchumba, sahivi K**a unakaa na kaka

5. Kutoa Siri za ndani. Mnafeli sana aise. Mwanaume akipita mitaani anakuwa uchi coz watu wnaajua Siri zake zote. Mdomo unawasha sijui haha.

6. Kiburi, jeuri, dharau, kebei, maneno K**a yote hamna breki.

7. Kumsingizia mume kuwa anatoka na fulani hata huna hakika kisa umesikia tu. Usikute baba wawatu hata Hana. Fanya uchunguzi Kwanza kabla ya kufokaa na kulaumu.

8. Tabia yako mbayaa hata watoto hawawezi kujifunza kwako. Na wanakushangaa.

9. Kujisahahu. Kwa kuwa umeolewa basi ndiyo umemaliza kumbe Upendo hujengwa na watu wawili. Umejiachia kumbe Kuna watu wnamtaka mumeo. Jiongeze.

10. Kuchagua marafiki feki. Ndoa nyingine huvunjika kwa sababu ya marafiki wasiofaa. Wanapoteza wenzao.

Yote haya yanapunguza Upendo kutoka kwa mume. Akibadilika usishangae.
Mwanamke ukikaa katoma nafasi yako vizuri mume atatulia. Japo wapo wenye tabia zao tu. Wameshindikana, wanaahitaji maombi may be.

Ushauri 0752247575

29/12/2020

Mambo ambayo mkaka unatakiwa kuyafanya siku ya kwanza ya kumtoa out mchuchu ili usiharibu show๐Ÿ˜„๐Ÿ‘‰๐Ÿผ

1. In your first date. Usimwambie yote kuhusu wewe, atajua unajiproud then ataona hufai aendelee na wewe. Mara nafanya kazi TRA,Nina gari mbili, juzi nilikuwa marekani, yaani kwanza ndiyo siku ya kwanza jamaniii. Mwache akujue taratibu

3. Actually, K**a mnaenjoy out yenu, you can kiss her a soft kiss๐Ÿ˜„ kwa shavu tu Basi. Akimind Omba msamaha but hataisahau na atakukumbuka. ๐Ÿ™Œ๐Ÿฝ

4. Unapotaka kumfahamu siyo mpaka umuulize What you do? Aah boring. in the first day not necessary. Kuna vitu Ni vya baadaye. Lakini unaweza.muuliza anavyopenda na asivyopenda. Likes and dislikes

5. Uwe mjasiri(confident). Sijakuambia umtiishe au too serious. But ujue kuwa hakuna mdada anayependa mkaka muoga, hata kuongea tu k**a umeshikwa degedege. Hawezi kubali hata out ya pili, hatajosikia secured into your hands. K**a hujiamini it means siyo man bado.

6. Uwe mbunifu. Siyo baada ya out hatamani Tena umtoe, kwasababu umembore Hana hamu Tena na haoni maana ya out. ๐Ÿ˜„

7. Usifanye Mambo yoyote yanayoashisiria s*x. Mfano touching sensitive parts of her. Utakuwa umechemuka mno.

8. Be yourself. Usionekane Sasa yeye Ni Mungu kwako. Kana kwamba unajipoteza wewe kwasababu umempenda. Don't loose yourself. Baada ya out, continue be busy na Mambo yako ila usimsahau.
Bye bye

0752247575

26/04/2020

Mume Hakikisha mkeo anafika Mbinguni, na we we mke hakikisha mumeo anafika kwa BABA pia.
Jukumu hili letu sote

26/04/2020

Mkaka anayetaka s*x kabla ya kuku oa, maana yake anaweza akawa ni prayer lakini hujui. Na atakusumbua sana hata ukiolewa naye. Mwanaume anayetaka ndoa anafocus kwenye ndoa, anayetaka s*x before hakutakii mema mdada, kweli unaweza kuwa unapenda sana, lakini dalili k**a za kutaka s*x kabla ni dalili mbaya sana na ni za laana vizazi na vizazi. Zinapelekea madhara k**a vile kuzalia nyumbani na ni aibu kwa wazazi, aibu mbele za Mungu, aibu kwako mwenyewe, na pia unamwaibisha Mungu. Pia unawapa mzigo wasiotegemea wazazi kuanza kulea mtoto wako, wanachukiaga Sema tu hawakuambii. Boys siyo uungwana kumzalisha mpenzi akiwa home, na unamkataa, ni laana inaweza kufuatilia hata watoto wako baadaye.

Ukiwaka tamaa mwanaume oaaa. Usichezee wadada wa watu na huku huna mpango nao, Hiyo ni laana. Na apandacho MTU ndicho atakachovuna.

Hizi T-shirt ni 13000/= tu kila moja, 0752247575

05/04/2020

Alimua kukuacha kwasababu hakuona thamani yake kwako, kwasababu upendo wake kwako ulitumia k**a udhaifu wake, na akiamua kuondoka maana yake kaamua kweli kwasababu hukuona umuhimu wake kwako.
Girls need care, love and protection (safety). Men need respect.

Na uaminifu ukishuka ni ngumu sana kupanda tena.
Team love

05/04/2020

Mke unalalamika mume wangu siyo Romantic, je wewe ni romantic? Umewahi fanya hivi hata siku moja tuone k**a mume wako hajarudi na zawadi yako jioni hahaah

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address


Dar Es Salaam