19/04/2024
jamani pamoja nakuwa tunahitaji kuwa na pesa nautajiri lkn usiokoke kwakuwa unataka hela okoka kwasababu umechoshwa na maisha ya dhambi na unataka kuishi maisha yanayompendeza Mungu...maana baada ya kuwa na maisha haya kuna maisha mengine bora kuliko haya na usidanganyike kwamba ukipata pesa ndio umemaliza bado huwezi kutoshezwa k**a huna Yesu dhiki haita isha
07/01/2024
Mungu akufanye ustawi mbele ya adui zako nakukutosheleza kwa wingi wa NEEMA y'ake ,acha sema wake ukufunike ukapande KTK killer cha uzuri wa MUNGU ktk jina la Yesu..mwaka 2024 wewe ni mtu mkuu k**a unaamini sema Ameeen!!!
18/12/2023
💯 Neno la leo; Jipende.
Leo ikiwa ni tunaona jinsi ambavyo kujipenda wewe mwenyewe kwanza kulivyo ufunguo wa mengine makubwa kwenye maisha.
Mapenzi ndiyo yanaendesha dunia.
Watu huwa wanafanya kitu chochote kile kwa sababu kuu mbili;
Moja ni wanapenda kufanya kitu hicho.
Na mbili ni kufanya kitu hicho kunawapa kile wanachopenda.
Ni vigumu sana kwetu binadamu kuchukua hatua k**a hakuna mapenzi yanayohusika.
Pamoja na kuendeshwa na mapenzi kwenye yale tunayofanya, bado huwa tunakutana na magumu na changamoto ambazo mapenzi tunayokuwa nayo kwenye kile tunachofanya au matokeo tunayopata hayawezi kuvuka.
Hapo ndipo unapokuwa unahitaji mapenzi ya juu zaidi ambayo ni kujipenda wewe mwenyewe kwanza.
Unapoanza kwa kujipenda wewe mwenyewe, mengine yote yanakaa mahali pake.
Hakuna magumu au changamoto zozote zinazokuwa na nguvu ya kukukwamisha kwenye chochote unachofanya.
K**a unataka kufanya makubwa kwenye maisha yako, ni lazima uanze kwa kujipenda sana wewe mwenyewe.
Lazima ujipende wewe kuliko kitu kingine chochote.
Ni kupitia kujipenda sana ndiyo unaweza kujiamini na kujikubali.
Na kupitia kujiamini na kujikubali unaweza kukabiliana na chochote kwenye maisha yako.
Imani kuu inayopaswa kuyaendesha maisha yako inapaswa kuwa ya upendo. Hapo unaanza kwa kujipenda wewe mwenyewe kwanza, kisha unawapenda wale wanaokuzunguka na mwisho unapenda kile unachofanya.
Hivyo ndivyo unavyopaswa kuyapangilia mapenzi yako vizuri ili uweze kupata chochote unachotaka.
Ukianza kwa kujipenda wewe mwenyewe, hakuna kinachoweza kukuangusha au kukukatisha tamaa.
Ukiwapenda wengine, inakuwa rahisi wao kukupa kile unachotaka.
Ukipenda kile unachofanya, utakifanya kwa muda mrefu zaidi hata k**a matokeo hayaji k**a ulivyotarajia.
Kujipenda na kujikubali ni moja ya njia za kuachilia breki ambazo zimekuwa kikwazo kwa wengi kufanikiwa.
Zingatia haya mara zote ili kuweza kufanya makubwa kwenye maisha yako.
14/12/2023
Mungu akupe kicheko na furaha izidiyo unapomalizia siku za huu mwaka naakupe kibali cha kuingia mwaka 2024 kwa ushindi na mafanikio ktk familia yako
Nakuombea
22/04/2023
Huu mkesha wa marafiki wa Yesu utafanyika kigamboni vijibwen mtaa wa soweto,kanisa la maisha ya ushindi hivi unapangaje kukosa mim nitakuwepo na nitaimba pia wale mnaompenda Yesu mnakosaje aiseee yaan sikuhiyo ni ni kumfanyia Yesu burudani kucheza kuimba kujifunza neno la Mungu maombi na maombezi k**a kawaida umeona hapo Bishop Michael Peter Imani atakuwepo na mchungaji mwenyeji watafundisha aiseee usijaribu kukosa!!!!! Tukutane pale tumfanyie shangwe Yesu
19/04/2023
Usikose huu mkutano utakuja kunishukuru nakwambia
07/04/2023
Maisha yenye utawi na Furaha ni yale yenye upendo ndani yake
13/11/2022
Yohana 8
31 Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli;
32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
33 Wakamjibu, Sisi tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wasemaje, Mtawekwa huru?
34 Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.
35 Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote.
36 Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.
22/09/2022
Mungu ayakumbuke machozi yako ambayo umekuwa ukimlilia muda mrefu
🤍🤍🤍❤️❤️❤️🤍🤍🤍
Aimurike njia yako kwa nuru yako