29/03/2020
*KILIMO CHA MCHICHA*
_UTANGULIZI_
Mchicha ni zao lililoka kwenye Jamii ya mboga za majani na linatambulika kwa kiingereza k**a Amaranth.Inaaminika aina nyingi za mchicha zilizosambaa dunian asili yake ni Amerika ya kati na kusini. Kuna aina nyingi za mchicha na zinatofautiana kwa vigezo mbali mbali kwa mfano Miiba ,rangi ya majani ,shina na kadhalika.Pamoja na mchicha kutumika k**a mboga ,pia ni mbegu za baadhi ya aina ya mchicha zimekuwa zikitumika k**a nafaka Kwa Tanzania yameanzia Mikoa ya Arusha ,Manyara ,Kilimanjaro na Dodoma
*UMUHIMU WA MCHICHA*
Nchini Tanzania mchicha umetumika k**a mboga ya majani inayojitosheleza bila kuchanganywa na mboga nyingine .Huliwa na vyakula vingine vya wanga k**a Ugali au Wali . Pia Mchicha katika kupikwa umekuwa ukichanganywa na mboga nyingine k**a vile dagaa,nyama,Samaki na mboga nyingine. Katika hali hiyo mchicha unatumika kuboresha na kukamilisha milo katika Familia mbalimbali ,migahawani ,mahotelin,shuleni na vyuo
Mchicha k**a mboga ya majani ina Vitamini na madini ya kutosha . Mchicha nafaka una virutubisho Lishe vingi zaid k**a vile Protini ,wanga ,chuma ,Chokaa,na mafuta ukilinganisha na mahindi.Pia zao hili la mchicha ni chanzo cha kipato kwa wakulima ,wafanyabiashara na wakala wa pembejeo za kilimo
```MAANDALIZI YA SHAMBA```
Shamba la mchicha linaandaliwa kwa kutifua ardhi kwa kina na kuondoa magugu yote.Kisha samadi ya mifugo ,mboji au makapi ya Tumbaku husambazwa na kuchanganywa na udongo kwa kutifua na husawazisha shamba vizuri.Maandalizi mazuri ya shamba ni muhimu kwa kuwa mchicha ukishapandwa hautarajiwi kupalilia hadi kuvunwa
*UPANDAJI WA MCHICHA MBOGA*
Mchicha huota na kukua vizur wakati wa joto .Mvua zikizidi mchicha hauoti vizuri na mwingi unakufa.Kipindi cha baridi baadhi ya aina za mchcha hazioti na kukua vizur .Mchicha kwa ajili ya kuvunwa k**a mboga hupandwa kwa kutawanya mbegu zikiwa zenyewe au zikiwa zimechanganywa na mchanga .
*```UKUAJI NA HUDUMA MUHIMU~*
Mchicha mboga huchukua kati ya siku 21 hadi 30 tangu kuota had kuvuna. Hata hivyo baadhi ya aina ya mchicha hasa wa kienyeji huchukua muda mrefu zaid kukua.Huduma muhimu kwa ukuaji wa mchicha ni umwagiliaji wa maji mara mbili kwa siku Hasubui na Jioni hasa kipindi cha Jua kali. Mbolea ya samadi ya kuku au mbolea za viwandani aina ya nitrojeni inaweza kutumika mchicha unapokuwa na wiki moja tangu Kuota ili kuongeza kasi ya ukuaji wa majani
馃憤Kilimo and na ufugaji kwanza馃尡
For more updates
31/08/2016
KUPANDA
Karoti hupandwa moja kwa moja shambani katika matuta au sesa .Kiasi cha gramu 80(sawa na vijiko vya chai 16)kinatosha kupanda eneo la mita Mraba 100.Hekta moja huitaji kilo 8 za mbegu.
Hakikisha mbegu unazozipanda zinauwezo wa kuota kwa kuzifikicha.Mbegu zenye uwezo wa kuota hutoa harufu kali unapozifikicha .Ili mbegu ziote haraka ziloweke katika maji kwa muda wa saa 24 Baadae hapo changanya mbegu hizo na mchanga kwa kiasi kinacholingana ili kupata mtawanyiko mzuri wa mbegu wakati wa kupanda .k**a utapanda karoti katika matuta tengeneza matuta yaliyoinuliwa kidogo kiasi cha Sentimeta 10 mpaka 15.Matuta haya yawe na upana wa sentimeta 60 na urefu wowote. Sia mbegu katika matuta yenye nafasi ya sentimeta 30 mpaks 40 kat ya mstari na mstari na kina cha sentimeta moja mpaka moja na nusu.Iwapo utapanda katika sesa tumia nafasi ya sentimeta 40 mpaka 50 kati ya mstari na mstari.Nafasi ya kupandia itategemea aina inayokusudiwa kustawishwa Baada ya kupandwa .Weka matandazo k**a vile Majani makavu na kisha Mwagilia maji Hasubuhi na jioni Mapaka mbegu zitakapoot. Umwagiliaji hutegemea hali ya hewa .
Mbegu huota Baada ya Siku 10 mpaka 15 zikishaota ondoa Matandazo.
KUTUNZA SHAMBA
鈥umwagilia Maji
Hakikisha Udongo una unyevu nyevu wa kutosha hasa siku za mwanzo .Karoti Zilizokosa maji Kwa muda mrefu huzaa mizizi Midogo midogo. Pia udongo mkavu ukipata maji ghafla husababishia Karoti kupasuka .Hivyo Hakikisha Udongo unaunyevunyevu wa kutosha wakati wote .k**a hali ya hewa ni ya jua kali.
鈥upunguza Miche
Mimea ya karoti inahitaji kupunguzwa mara mbili Mara ya kwanza upunguzwa ikiwa na Majani matatu mpaka manne au wiki mbili tangu kupandwa na kuachwa katika nafasi ya sentimeta 5mpaka 7. mara ya pili Hupunguzwa ikiwa na urefu wa Sentimita 10 hadi 15.Karoti zilizopunguzwa zinaweza kutumika kwa chakula.
鈥alizi
Zao la karoti linahitaji kupaliliwa mara kwa mara Palilia kwa kupandishia Udongo na kuwa Mwangalifu usikate mzizi.
鈥bolea
Weka mbolea ya chumvichumvi aina ya S/A k**a mbolea za asili hazikutumika kwa kupanda.kiasi kinachotakiwa ni kilo 100 kwa hekta .Weka kilo 50 kwa hekta iwapo mbolea za Asili zimetumika.Mbolea iwekwe wakati wa kupunguza miche mara ya pili .Weka katikati ya mistari na kwenye mifereji na kisha fukia.
KUZUIA MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU
MaGonjwa
Niatakutajia baadhi ya magonjwa ambayo yanaweza kuikumba zao Hili
1)Madoa majani (Leaf spot)
Ugonjwa huu husababishwa na Ukungu na hutokea wakati na hutokea wakati karoti zinaurefu Wa sentimita 13 mpaka 15.hushambulia Majani na kufanya yawe madoa yenye rangi nyeusi iliyo changanyika na kijivu au kahawia. Sehemu zinaziunguka madoa hubadilika na kuwa njano.Ugonjwa ukizidi majani hukauka .Zuia ugonjwa huu kwa kunyunyuzia dawa za ukungu k**a vile Dithanem 45,Blitox,Copperhydroxide(Kocide),Copper oxychloride ,Cupric hydroxide (Champion).Antrocol
2)Kuoza Mizizi(Sclerotinia Rot)
Ugonjwa huu husababishwa na ukungu na hushambulia mizizi na majani.Dalili zake ni kuoza kwa mizizi na majani .Baadaye sehemu hizi hufunikwa na uyoga mweupre. Kwenye uyoga huu huota siklerotia kubwa zenye rangi nyeusi.
Kuzuia ugonjwa huu kwa kuzingatia yafuatayo-:
- Epuka kustawisha karoti kwenye Maeneo yaliyoshambuliwa na ugonjwa huu.
-Nyunyuzia Dawa za ukungu k**a vile Dithane M-45,Blitox ,Topsin M70% wakati wa kupalilia kuvuna na Kusafirisha.
KUVUNA
Karoti huwa tayari kwa kuvunwa Baada ya wiki 10 hadi 12 tangu kupandwa kutegemea hali ya hewa .Wastani wa mavuno kwa hekta Moja ni Tani 25 au zaidi
Nawatakia Siku njema 馃悡馃崒
07/08/2016
KAROTI
Karoti ni zao la mizizi ambalo hulimwa zaidi katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Iringa, Mbeya na Kagera.
Zao hili hutumika k**a kiungo katika mapishi ya vyakula mbalimbali. Huweza kutafunwa mbichi au kuchanganywa kwenye kachumbari. Karoti zina vitamin A, C na madini aina ya chuma.
MAZINGIRA:
Karoti hustawi vizuri kwenye sehemu zenyejoto la wastani (nyuzi joto 15 hadi 27 za Sentigredi).
Kiasi cha mavuno yanayoweza kupatikana na ubora wa karoti, hutegemea sana aina ya udongo. Hivyo karoti hustawi vizuri katika udongo mwepesi, wenye rutuba ya kutosha, kina kirefu na usiotuamisha maji.
AINA:
Kuna aina nyingi za karoti. Zifuatazo ni aina zinazolimwa hapa Tanzania.
路 Nantes:
Karoti za Nantes ni ndefu, huvunjika kwa urahisi, zina umbo la kuchongoka na ncha kali. Aina hii hupendwa sana kutafunwa na walaji, kutokana na ladha yake tamu. Karoti za Nantes hazifai kwa kusindikwa.
路 Chantenay Red Core
Hizi ni nene kwa umbo, na zenye ncha butu. Unene wa nyama ya nje na ndani hulingana hivyo zinafaa sana kwa kusindikwa.
Huwa na rangi ya machungwa iliyofifia na ladha yake siyo tamu.Aina hii hustawi vizuri kwenye udongo mzito.
路 Oxheart:
Karoti za Oxheart ni fupi na nene. Huvunwa baada ya muda mfupi kulinganisha na aina zingine.
路 Cape Market:
Aina hii hupendwa sana kutafunwa zikiwa mbichi pia zinafaa kusindikwa.
路 Flacoro:
Aina hii huzaa sana na mizizi yake ni mirefu. Hufaa kwa kuhifadhiwa na kusafirishwa, kwa sababu haziharibiki haraka.
路 Top Weight:
Aina hii ina sifa k**a za Flacoro.
Karoti
KUTAYARISHA SHAMBA
Ili kupata mavuno mengi na bora, eneo la kupanda halina budi kutayarishwa vizuri. Iwapo shamba ni jipya, miti na visiki vyote vikatwe. Visiki na takataka zote ziondolewe shambani. Baada ya hapo shamba lilimwe vizuri na katika kina cha kutosha. Lainisha udongo ili kurahisisha uotaji wa mbegu za karoti ambazo ni ndogo sana.
K**a eneo lina udongo wa mfinyanzi au wa kichanga ni muhimu kuweka mbolea za asili zilizooza vizuri. Mbolea hizi hufanya udongo wa mfinyazi uwe mwepesi wa kuweza kuruhusu maji na hewa kupenya kwa urahisi.
Endapo karoti zitastawishwa wakati wa mvua nyingi zipandwe kwenye matuta yaliyoinuliwa.
12/12/2015
KILIMO CHA KABICHI
sehemu ya pili (2)
KITALU
kitalu ni muhimu katika uzalishaji wa zao hili. Ni vema kutengeneza matuta yenye upana wa Mita moja na urefu wowote kulingana na Matakwa ya Mkulima.Mbolea za samadi na zenye asili ya chokaa zichanganywe vizuri kwenye Udongo kiasi cha gramu 500 za mbegu huhitajika kwa hekta Moja.
Katika upandaji kwenye kitalu ni vizurikutengeneza Mistari katika Tuta Umbali toka mstari hadi Mstari uwe na sentimita Ishirini (20). Udongo kiasi kidogo utumike katika kufunika Mbegu.
Baada ya mbegu kuota ni vizuri kupunguza baadhi ya Miche na uwe katika kipimo cha sentimeta 2-3 toka Mche hadi Miche.Hii itasaidia kuwa na Miche mifupi yenye nguvu. Inafaa kunyeshea au kumwagilia kitalu Mara moja au Mbili kwa siku na katika Sehemu za joto ni Vizuri kuweka kivuli katika matuta.Katika wiki Tatu hadi nne ni vyema kuondoa kivuli kidogo huku ukipunguza unyeshaji au umwagiliaji.Hii itasaidia Miche isipate mshtuko wa uhamishaji shambani.
MBOLEA
Ni vizur kuweka kiasi cha viganja 2-3 vya mbolea ya Samadi iliyooza vizuri katika kila Shimo.
PALIZI
Wakati wa kupalizi mkulima ni vizuri akawa Mwangalifu ili asihalibu Miziz.Wakati kabichi inapoanza kufunga hufunika ardhi hivyo inasaidia kuzuia Magugu yasiote wakati huu hakuna haja ya kupalilia.
KUVUNA
kabichi hukomaa katika kipaindi cha Siku 60-100 tangu kupandwa . Kwa ajili ya kuuza ni vizuri kuvuna wakati vichwa vinapofunga Vizuri na huwa na Uzito wa kutosha kabichi iangaliwe na kutunzwa baada ya kuvunwa ili isikwaruzane na kuoza kabla ya kutumiwa . kwa kawaida hekta moja hutoa Mavuno kiasi cha Tani 50-80
FAIDA
Kabichi soko lake la Uhakika katika kipindi chote na Muhimu kwa afya.Pia linaweza kutumika k**a Malisho ya Mifugo.
19/09/2015
KILIMO CHA KABICHI
Kabichi ni moja ya mazao yaliyomo katika jamii ya mimea inayojumuisha mimea ya kaulifulawa(cauliflower),kibichi kichina na kale.
MIZIZI
mizizi ya kabichi hutawanyika ardhin vizuri kwa kawaida huenda chini kiasi cha sentimita ishirini (20 CM) na hujitawanya kwa kiasi cha sentimita sabini na tano(75CM)
SHINA
Shina La mmea wa kabichi huwa na rangi ya kijani au Zambarau.Hii hutegemeana na aina ya kabichi na kwa kawaida ni fupi.
HALI YA HEWA
Kabichi hustawi vyema katika sehemu yenye hali ya baridi.Joto Jingi pia husababisha kulegea kwa kichwa vilivyofunga.Zao hili hustawi vema katika maeneo yenye mwinuko wa zaidi ya mita 100 toka usawa wa bahari
UDONGO
Zao hili linaweza kustawishwa kwenye udongo wa aina yoyote mradi tu udongo huwo usiwe na chumvi chumvi nying na usiotuamisha maji.Udongo wa kichanga na ule usio na rutuba ya kutosha husababisha kabichi kukomaa upesi na kuzaa kabichi hafifu zenye vichwa vidogo
07/06/2015
UHURU WA KIFEDHA
uhuru wa kifedha ni nin? Kwa mujibu wa Buckminster Fuller uhuru wa kifedha ni uwezo wa kuendelea kuishi siku nyingi mbele au kwa maana nyingine hata k**a ukiacha kufanya kazi kuanzia leo Muda gan ungeliishi?
Uhuru wa kifedha ni kiasi cha mtiririko wa fedha kutoka kwenye vitega uchumi vyako ukilinganisha na matumizi yako.Inamanisha idadi ya siku unazoweza kuishi wewe pamoja na wote katika familia yako bila kulazimika kufanya kazi na bado ukaendelea kudumisha viwango vya kuishi.
Tuchukulie mfano:Una mtiririko wa fedha kutoka kwenye aseti zako wa shilingi 1 000 000 kwa mwezi.Na unamatumizi ya mwezi ya shilingi 2000,000.Je nini uhuru wako wa kifedha?Tukirudi kwenye dhana ya uhuru wa kifedha kwa kutumia maana ya Buckminster Fuller's:Siku ngap mbele unaweza kuendelea kuishi?
Uhuru wa kifedha unapimwa katika muda siyo katika kiasi cha shilingi ulizonazo.unapimwa siku ngap?miaka mingap?vizaz vingap vitaish bila kulazimika kufanya kazi.
Je wewe una Uhuru wa kifedha?
Siku njema
27/04/2015
KILIMO BORA CHA MDALASIN
Endelea
KUVUNA
*uanzwa kuvunwa miaka mitatu baada ya kupanda
*Mazao ya mdalasini ni maganda ya mashina ya mti
*Kata shina la mti na tenganisha maganda na mti kwa njia ya kumenya
*Seli la nje ya ganda la mdalasini ni chungu hivyo ni vizuri ziondolewe kwa kukwaruza kwa kisu
*kausha vizuri siyo kwenye jua kali
*Mavuno 0.25kg-10kg maganda yaliyokaushwa kwa mti mmoja kiasi cha mazao hutegemea na ukubwa na umri wa mti
*Ubora wa mdalasini hushuka kulingana na mti.Mti wa umri ukubwa hutoa maganda yenye Ubora wa chini
MATUMIZI
Mdalasini baada ya kukaushwa ikiwa imesagwa au bila kusagwa hutumika k**a-:
1)Kiungo kwenye vyakula na vitafunwa k**a keki na maandazi na vitumbua
2)Vikolezo kwenye vinywaji k**a chai,kahawa
3)Dawa ya tumbo hasa wakati wa kuvimbiwa, kutoa hewa tumboni pia kuongeza hamu ya kula
4)Dawa ya ngoz
MANUFAA
*Miti hii hudumu shambani zaid ya miaka 20,miti huchipua na kutoa machipukiz mengine kila baada ya kuvuna
*Gharama ni ndogo ya uzalishaji
*magonjwa na wadudu kidogo
02/12/2014
KILIMO CHA MDALASINI
Mti wa mita 10 au zaidi.Hutoa machipukizi na kuota miti zaidi ya mmoja kwenye shina moja na kuongeza mavuno mengi.Haya mashina mapya yasing'olewe bali yaachwe yakuwe na kuwa mti mkubwa.
AINA YA MDALASIN
Za kienyej(ndogo)
za kigeni(kubwa)
KUSIA MBEGU KWENYE VITALU
*Mbegu hupatikana kwenye miti iliyokomaa
*Sia mbegu kitaluni zi kiwa nusu sentimeta chini ya Udongo.
*Baada ya kuchipua mbegu huchukua miezi 6 hadi mwaka mmoja kufikia umri wa kupandikiza shambani.
*Panda mishe wakati wa Masika.
*Panda kwa nafasi ya 2m x 2m
Nafasi hizi huwezesha miti kutoa machipukizi mengi.Nafasi kubwa hufanya matawi mengi pia na mashina hayanenepi wala kurefuka.
UTUNZAJI
*Acha machipukizi kwenye shina-
*Toa matawi kwenye mashina ili kunenepa mashina.
*weka shamba katika hali saf
*Zuia magonjwa k**a vinundu(galls)wanaosababishwa na utitiri na wadudu scale na meal bugs kwa kutumia dawa za sumu k**a selecron, karate nk.
itaendelea
23/11/2014
KILIMO CHA TANGAWIZI
5 UPANDAJI
ENDELEA
Tandaza nyasi shambani kuhifadhi unyevu nyevu hasa pale kivuli kinapokosekana.Paliz hufanywa mara magugu yanapoota,dawa ya kuua magugu,k**a simazine au Round up hutumika.
6)MAGONJWA YA WADUDU
*Madoa ya majani
yanasababishwa na viini vya magonjwa viitwayo Colletotrichum Zingiberis na phyllosticta zingiberi
*Kuoza kwa tunguu(rhizome)
Inasababishwa na Viini vitwavyo Pithium spp
*Mizizi fundo
inasababishwa na Meloidegyne Spp
7)UVUNAJI
Tangawizi huweza kuwa tayari kwa kuvunwa kati ya miezi 9-10 baada ya kupanda.Wakati majani yake yanapogeuka rangi kuwa njano na Mashina kusinyaa
Tangawiz inayohitajika kwa kuhifadhi kwenye kemikali (Preserved ginger in brine )huvunwa kabla haijakomaa kabisa wakati ile iliyokomaa kabisa huwa kali Zaidi na huwa na nyuzi hivyo hufaa kwa kuzikausha na kuzisaga.
Mavuno hutofautiana kulingana na huduma ya Zao.
*THE END *
(share kwa wengine iwafikie weng zaid
26/10/2014
KILIMO CHA TANGAWIZI
4.HALI YA HEWA NA UDONGO
Zao hili hustawi katika maeneo yenye hali ya kitropiki kutoka usawa wa bahari hadi mwinuko wa Mita 1,500 au zaidi.Huitaji mvua kiasi cha mm 1,200-1,800 na joto la wastani nyuzi za sentigredi 20-25.Hustawi vema katika udongo tifutifu wenye rutuba na usiotuamisha Maji
5)UPANDAJI
Zao hili la tangawizi hupandwa kwa kutumia vipande vya vitunguu vyenye kichipukizi kizuri angalau kimoja na huweza kukatwa katika urefu wa sm 2.5-5.Wakati mwingine vichipukizi vinavyopatikana katika kumenya tangawizi huweza kuhifadhiwa na kutumika kwa kupanda.Kiasi cha kilo 840-1700 cha vipande vya tunguu huweza kutumika kwa kupanda katika hekta moja.
Nafasi inayotumika kupanda ni kati ya sentimenta 5-10 na mara nyingi hupandwa katika matuta.Baadhi ya mazao huweza kupandwa katika shamba la tangawizi ili kuweka kivuli chepesi ingawa si lazima.
Wiki 1-2 kabla ya kupanda weka mbolea ya samadi au mboji kiasi cha tani 25-30 kwa hekta na kwakukuzia wek MPK kwa uwiano 36:36:80
ita
12/10/2014
KILIMO CHA TANGAWIZI
Jina la kitaalamu ni ZINGIBER OFFICINALE
Tangawizi ni aina la kiungo ambalo sehemu inayotumika ni tunguu(rhizome]ambalo huonekana k**a mizizi ya mmea.
Asili ya zao hili ni maeneo ya kitropiki ya bara la Asia na hasa katika nchi za India na china.Zao hili linazalishwa kwa wingi katika nchi ya Jamaica na Tanzania hulimwa katika Mikoa ya kigoma,Morogoro,Pwani,Mbeya na Kilimanjaro
AINA YA TANGAWIZI
Hakuna uthibitisho wa aina za tangawizi ambazo hulimwa hapa nchini. Ila kuna dalili ya kuwa na aina za white Africa(Jamaica) na Cochin(flint:hili huwa na tunguu zenye nyuzi.
TABIA YA MMEA
Tangawizi ni mmea unaotambaa chini ya ardhi wakati wa Masika hutoa majani juu ya ardhi.Jamaica ina rangi hafifu ya kahawia na tunguu fupi wakati Cochin ina tunguu fupi zaidi lenye ngozi ya rangi iliyo kati ya kijivu na nyekundu.Mmea una urefu wa futi mbili na majani yake ni membamba marefu ambayo hufa kila mwaka yakiacha tunguu ardhini likiwa hai Maua ya mmea huwa rangi nyeupe au njano.
05/10/2014
unaweza kutuambia huu ni mmea ambao unazalisha zao gan?