Dar es Salaam Institute of Technology - DIT

Dar es Salaam Institute of Technology - DIT

Share

We believe that success comes out of the skilled hand and the innovative mind. And Innovation is no It provides information of academic programmes. KARIBU!!

The Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) is located in the Dar es Salaam city centre, at the junction of Morogoro Road and Bibi Titi Mohamed Street. Historically, DIT was established in 1997 by the Act of Parliament, “the DIT Act No.6 of 1997” to replace the Dar es Salaam Technical College, which had a long history of technical training in Tanzania. This history dates back to 1957 when its

24/12/2025
06/11/2025

PONGEZI

Photos from Dar es Salaam Institute of Technology - DIT's post 20/03/2025

BENKI YA DUNIA YARIDHISHWA UTEKELEZAJI MRADI WA EASTRIP DIT

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini Victoria Kwakwa ameipongeza Serikali ya Tanzania kupitia Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kwa utekelezaji unaoridhisha wa mradi wa Kujenga Ujuzi na Ushirikiano Afrika Mashariki (EASTRIP) unaotekelezwa na nchi tatu za Afrika Mashariki—Tanzania, Kenya, na Ethiopia kupitia ufadhili wa Benki ya Dunia.

Ametoa pongezi hizo alipozuru DIT akiongozana na mwenyeji wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda kukagua miradi ya EASTRIP inayotekelezwa chuoni hapo ikiwa ni pamoja na Jengo la Umahiri wa Tehama lenye uwezo wa kuchukua zaidi ya wanafunzi 2000 kwa wakati mmoja.

Aidha Makamu wa Raisi huyo wa Benki ya Dunia amepongeza jitihada zinazozidi kuchukuliwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe, Rais Daktari Samia Suluhu Hassan kuwarejesha shuleni wasichana waliokatishwa masomo kwa sababu ya changamoto mbalimbali pamoja na jitihada za kuongeza wigo wa wanafunzi wa k**e kudahiliwa katika masomo ya STEM (Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, na Hisabati).

Kwa Upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf F. Mkenda ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kufadhili miradi ya Elimu kuanzia Elimu Msingi (BOOST), Elimu ya Sekondari (SEQUIP) Mradi wa Kuongeza Umahiri wa TEHAMA (EASTRIP) hadi Elimu ya Juu (HEET).

"Kwa sasa tunafurahi kwasababu Benki ya dunia inatusikiliza nchi inataka nini, na Serikali yetu inataka nini halafu wanaungana na sisi kuhakikisha wanafanikisha kile ambacho tunakitaka"

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Mhandisi Dkt. Richard Masika amesema mradi wa EASTRIP unaleta mageuzi makubwa kwa wanafunzi kwa kuwajengea uwezo wa kuunganisha nadharia na vitendo ili kupunguza pengo lililopo kati ya yanayofanyika katika Taasisi za Teknolojia na kilichopo kwenye ulimwengu wa Viwanda.

Aidha Dkt. Masika amebainisha DIT inaendelea kuendeleza na kulea ujuzi wa wanafunzi kupitia kituo chake,

"kuna kituo ambacho kinawasaidia wanafunzi bunifu zao. Wanapata fursa ya kubaki hapa chuoni (DIT) na kuendeleza zile bunifu zao ambazo zinauwezekano wa kuingia sokoni kwa maana ya kwamba kuziwezesha kufikia ngazi hiyo ya kwenda sokoni kiasi cha kupelekea kwamba wao wanaweza wakaanzisha kampuni zao wenyewe na wakajitegemea"

Kupitia utekelezaji wa mradi wa EASTRIP Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) imeweza kuongeza udahili wa wanafunzi, hususani kwa kuongeza asilimia 25 ya udahili wa wanafunzi wa k**e katika masomo ya sayansi na teknolojia.

Kwa ujumla, EASTRIP inalenga kuboresha ujuzi na kuongeza ushindani wa kikanda katika sekta za kipaumbele, hivyo kuchangia katika ukuaji wa uchumi na maendeleo endelevu ya nchi zinazoshiriki.

Photos from Dar es Salaam Institute of Technology - DIT's post 07/02/2025

DIT YASAINI HATI YA MAKUBALIANO NA SHIRIKA LA VIWANGO ZANZIBAR (ZBS)

Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Prof.Preksedis Marco Ndomba (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Zanzibar (ZBS) Yussuph Majid Nassor (wa pili kulia) wakisaini hati ya makubaliano (MoU) baina ya Taasisi hizo tukio lililofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa DIT leo Ijumaa tarehe 7 Februari, 2025.

Photos from Dar es Salaam Institute of Technology - DIT's post 01/02/2025

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT,SAMIA SULUHU HASAN ATEMBELEA BANDA LA DIT.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT), Prof.Preksedis Marco Ndomba leo tarehe 1, Februari 2025 wakati wa maonesho ya siku ya uzinduzi wa sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023, yaliofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre Dodoma.

Aidha, Mh.Rais amesema"Nimepita katika mabanda mbalimbali, nimepita katika banda la DIT na nimejionea mambo makubwa kwa namna walivyojipanga wanaendelea kuzalisha vijana makini na kusaidia nchi."
Ameeleza kuwa kuwepo kwa Sera na mitaala pekee hakutaleta ufanisi bali utekelezaji wa sera na mitaala ndio utakaoleta mafanikio.

Photos from Dar es Salaam Institute of Technology - DIT's post 14/12/2024

DIT YAPONGEZWA KWA KUTOA WAHITIMU MAHIRI KATIKA SEKTA YA TEKNOLOJIA YA UTENGENEZAJI WA BIDHAA ZA NGOZI NA SAYANSI YA MAABARA KATIKA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI.

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia QS Omary Kipanga ameipongeza Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kwa kuendelea kutoa Elimu Bora na wahitimu mahiri wenye uwezo wa kutatua changamoto mbalimbali za kijamii kupitia Ujuzi wanaoupata wakiwa mafunzoni.

Naibu Waziri amesema hayo, leo tarehe 13/12/2024, akimwakilisha Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Faustine Mkenda katika Mahafali ya kumi na nane Duru ya pili katika kampasi ya DIT Mwanza.

Mhe, Kipanga amesema serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, inajivunia maboresho yanaofanyika katika sekta ya elimu ili kuzalisha wataalam wanaoajirika, kujiajiri na kutengeneza ajira kwa wengine.

Naibu waziri Kipanga, ameipongeza DIT kwa kupunguza baadhi ya changamoto zilioainishwa katika mahafali iliyopita. "Nirudie tena kuwapongeza menejimenti ya DIT kwa kuendelea kuratibu suala la mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi, ili kuwapatia ujuzi unaotaokiwa katika soko la ajira".amesema Kipanga.

Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi la DIT, Mhandisi,Dkt. Richard Masika, ameunga mkono hoja ya uboreshaji sekta ya elimu, huku akiishukuru serikali kwa kuanzisha kituo cha ujasiriamali, ubunifu, uhaulishaji wa teknolojia pamoja na malezi ya kampuni kwa Taasisi yake ya DIT.

Ni baada ya serikali kupata mkopo wa masharti nafuu wa Yuro 19.6 kutoka serikali ya Italia, ambapo asilimia 60 za fedha hiyo zitaelekezwa Kwa Taasisi ya DIT kwa ajili ya kituo hicho ambacho pamoja na mambo mengine, kitatumika kupeleka sokoni bunifu za wanafunzi.

Naye Mkuu wa Taasisi ya DIT, Prof. Preksedis M. Ndomba, amesema kwa Kampasi ya Mwanza, maboresho yanafanyika kupitia mradi wa Kujenga Ujuzi kwa Maendeleo na Uingiliano wa Kikanda katika Afrika Mashariki (EASTRIP), unaofadhiliwa na Benki ya dunia kwa gharama ya Sh 37 billioni.

Mradi huo unahusisha ujenzi wa miundombinu, baadhi yake ikiwa ni madarasa, mabweni, maktaba na kituo cha umahiri cha uchakataji ngozi ghafi.

Hatahivyo, DIT inafanya Mahafali ya kumi na nane (18) Duru ya Pili katika Kampasi yake ya Mwanza ikiwa na jumla ya Wahitimu 106 wa kozi za muda mrefu na muda mfupi ambapo asilimia ya wanafunzi wa k**e wanaohitimu katika Mwaka wa masomo 2023/2024 imeongezeka kwa 29.6%.

Photos from Dar es Salaam Institute of Technology - DIT's post 06/12/2024

PROF MUSHI: DIT NI KIWANDA CHA KUZALISHA WATAALAMU WENYE WELEDI KUTUMIKA SEKTA YA VIWANDA.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia masuala ya Sayansi Profesa Daniel Mushi ameipongeza Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kuzalisha vijana Mahiri wenye ujuzi unaohitajika katika kujenga uchumi unaoakisi maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.

Ametoa pongezi hizo alipomuwakilisha Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda katika mahafari ya 18 Duru ya kwanza ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Kampasi ya Dar es Salaam.

Amesema DIT ni kiwanda cha kuzalisha wataalamu wenye weledi wanaotarajiwa kutumika katika sekta ya viwanda. Ametumia fursa hiyo kuyasihi Mashirika ya Umma na ya binafsi kuwatumia wahitimu hao wa ufundi sanifu, Teknolojia na Uhandisi aliowatambua k**a hazina kubwa kwa Taifa kuendesha miradi mikubwa ya kimkakati inayolenga kutoa matokeo chanya kwenye uchumi wa Taifa.

"njooni sasa mchukue/mshirikiane na vijana hawa (Wahitimu 1463) katika kutatua changamoto zinazotusibu katika shughuli mbalimbali za kijamii na za kiuchumi"

Aidha, amewasihi wahitimu hao wa fani za ufundi stadi na Uhandisi kutumia ujuzi walioupata kwa manufaa ya Jamii na Taifa kwa Ujumla na kujiepusha na matumizi mabaya ya ujuzi wao kufanya maangamizi katika Jamii.

"Najua kwamba Elimu mliyoipata ni kubwa ninaomba tu kuwaasa mkaitumie kwa manufaa ya Jamii, kwa sababu najua mkiamua kutumia maarifa na ujuzi mlionao vibaya mnaweza mkaiumiza Jamii pia"

Pia amepongeza juhudi zinazochukuliwa na Menejimenti ya DIT kutoa nafasi kwa Walimu na watumishi wote kwenda kujiendeleza kielimu ili kuongeza ujuzi mpya unaoboresha maarifa wanayotoa kwa wanafunzi.

Vilevile ameipongeza DIT kwa kuwa na mashirikiano na Taasisi za Elimu za nje ya Nchi (China, Ethiopia, Urusi, Ufaransa, Uganda, Uturuki, Kenya, Korea, Hungary na Afrika kusini) kwa lengo la kuhakikisha wataalamu wanapata ujuzi na uzoefu unaoendana na mahitaji ya kikanda na Kimataifa.

Akizungumzia Jitihada zinazochukuliwa na Serikali kuboresha Elimu na ufundi stadi na Uhandisi, Prof Mushi amesema Serikali imefanya imezijengea uwezo vyuo vya ufundi stadi kuongeza udahili wa wanafunzi kutoka Wanachuo 171,851 hadi kufikia wanafunzi 235,804 sambamba na ongezeko la vyuo kutoka 465 hadi 474 kwa mwaka wa 2022/2023.

Sambamba na hayo Serikali imetoa mafunzo kwa wakufunzi 45 kutoka Taasisi za Elimu na mafunzo ya Elimu ya Ufundi stadi kwa lengo la kuongeza uwezo wa ufundishaji wa mitaala inayoendana na mabadiliko ya kiteknolojia na mahitaji ya soko.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Mhandisi Dkt. Richard Joseph Masika amesema lengo la kufanya mahafali hayo ni kuitangazia Umma bidhaa Bora ya wahitimu Mahiri katika kada ya uhandishi wanaozalishwa na DIT.

Photos from Dar es Salaam Institute of Technology - DIT's post 05/12/2024

WABUNIFU DIT WAPONGEZWA KWA KUWA NA BUNIFU ZINAZOSAIDIA KUTATUA CHANGAMOTO KATIKA JAMII

Wabunifu wa Taasisi ya Teknolojia Dar-es-salaam (DIT) wapongezwa kwa juhudi kubwa katika kuvumbua bunifu kubwa zitakazosaidia kutatua changamoto za jamii.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Daniel Elias Mushi kwenye sherehe ya kutoa tuzo kwa wanafunzi bora waliohitimu na wanaoendelea wa Taasisi hiyo.

Prof. Mushi ambae alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu kwenye sherehe hiyo ya utoaji tuzo ambapo ameeleza kufurahishwa kuona kuna jinsia ya k**e na kusema kuwa hii ni dalili njema kwa Taifa.
.."nimefurahishwa sana kuona kuwa kwenye tuzo hizi kuna wanafunzi wa jinsia ya k**e ambao nao wamefanya vizuri kwenye fani za sayansi na teknolojia hii ni dalili nzuri kwa Taifa letu kuwa limefanikiwa kuongeza idadi ya wanawake katika masomo ya sayansi, hesabu na teknolojia."amesema Prof.Mushi.

Hata hivyo, Prof. Mushi amewaeleza wanafunzi kuwa kila mwanafunzi aliyedahiliwa katika Taasisi hiyo ana nafasi ya kujifunza kwa bidii na kufanya vizuri katika masomo yake nakustahili kupata zawadi na tuzo, hivyo amewataka wanafunzi wengine kuongeza bidii ili na wao waweze kupata zawadi k**a ambavyo wenzao wamepata.

Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Prof. Preksedis Marco Ndomba amewataka vijana kuchangamkia fursa ya nafasi ya mafunzo kwa njia ya vitendo ambazo zimeelezwa na wadau kutoka viwandani kuwa zinapatikana kwa ajili yao na kuwataka kuongeza bidii ili pindi wanapofika kwenye maeneo hayo waweze kuonesha ujuzi wao.
"Nipende kuwashukuru wadau mbali mbali waolijumuika nasi leo katika shughuli hii lakini niwaeleze wanafunzi wote kuwa fursa za mafunzo kwa njia ya vitendo zimetangazwa hapa na mmezisikia sasa kazi kubwa imebaki kwenu kuzitumia na kuweka juhudi pindi wanapowachukua na kuwafundisha kwa njia ya vitendo kwa kuwa hii ndio nyezo kubwa ya kuwaongezea ujuzi unaotakiwa na utakaowasaidieni katika kuongeza ubunifu zaidi"amesemba Prof. Ndomba.

Aidha, tukio la utoaji tuzo kwa wanafunzi wanaomaliza na wale wanaoendelea katika Taasisi ya DIT limekuwa likifanyika kila mwaka ikiwa ni maandalizi kuelekea kilele cha maadhimisho ya Mahafali. Mwaka huu DIT itaadhimiaha Mahafali ya kumi na nane siku ya Ijumaa, Desemba,2024.

Photos from Dar es Salaam Institute of Technology - DIT's post 22/11/2024

WAZIRI HIRAYAMA WA USWISS ATEMBELEA DIT KUONA ILIVYOJIPAMBANUA KATIKA MASUALA YA TEKNOLOJIA UFUNDI NA BUNIFU

Waziri wa Elimu, Utafiti na Ubunifu Mheshimiwa Martina Hirayama toka Uswiss ametembelea Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na kuona jinsi Taasisi hiyo imejizatiti kwenye masuala ya Teknolojia, ufundi na bunifu.

Hirayama ameeleza kuwa ziara hiyo inalenga kujifunza zaidi kutoka DIT na DIT kujifunza kwao ili kuona k**a kuna uwezekano wa kuanzisha programu za kubadilishana wanafunzi na wahadhiri katika maeneo mbalimbali ya ufundi.

Waziri Hirayama amepata fursa ya kutembelea maabara za Taasisi hiyo ikiwemo atamizi na maabara ya uzalishaji na amefurahi kuona namna wabunifu wa DIT wanavyofanya bunifu mbalimbali ambazo zinalenga kutatua changamoto za jamii.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Sayansi, Teknolojia na ubunifu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Ladislaus Mnyone amesema kuwa matamanio yao ni kuifanya DIT kuwa eneo la kukusanya wabunfiu kutoka kwenye maeneo mbalimbali ili waweze kuzalisha vitu vinavyoonekana na ambavyo vitawasaidia hata wale ambao hawawezi kuzalisha bunifu zao wapate mahali pa kujiunza.

Aidha,ameushukuru ujumbe kutoka Uswis kuja DIT kwa kuwa kwa kushirikiana na DIT kutawezesha kuifanya DIT kuwa sehemu ya kuzalisha bunifu mbalimbali.
“Tunataka DIT iende zaidi ya ilipo sasa kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali ikusanye wabunifu na kuwaendeleza ili kuhakikisha ubiasharishaji wa bunifu unachukua nafasi yake na kuzalisha bidhaa nyingi zenye ubora mkubwa".ameeleza.

Nae Mkuu wa Taasisi ya DIT, Prof. Preksedis Ndomba amesema kuwa DIT imejipanga kuhakikisha inatatua changamoto katika jamii katika kila nyanja badala ya kutegemea bidhaa na teknolojia kutoka nje pekee.

Aidha,Prof.Ndomba amesema..."Taasisi inakuwa kwa kasi kubwa kwa sasa ina Kampasi nne na kila moja inajikita kwenye utaalama tofauti ya masuala ya teknolojia ili tu kuhakikisha tunaweza kutatua changamoto zozote zilizopo katika jamii kwa kufanya tafiti na kuzalisha mashine na bunifu husika zitakazoweza kushindana katika soko la kitaifa na kimataifa.

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address


P. O. Box 2856
Dar Es Salaam
P.OBOX2952