Al Ameen foundation - AIF

Al Ameen foundation - AIF

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Al Ameen foundation - AIF, Education, kijitonyama Alimaua, Dar es Salaam.

Ukurasa wako ambao utakukumbusha na kukueleza yaliyo Mazuri na Mabaya tuyaepuke kwa Uwezo wake Allah Tusaidiane kuutangaza Ukurasa huu ili upate waafikia Waislam wote

🔴 #LIVE MASHINDANO YA DUNIA YA QUR'AN TUKUFU BENJAMIN MKAPA STADIUM 05/04/2026 05/04/2026

تابعوا مسابقة القرآن الكريم العالمية 2026، المقامة في ملعب بنيامين ويليام مكابا، دار السلام – تنزانيا، بتاريخ 05/04/2026

ضيف الشرف الرسمي:
رئيس زنجبار الدكتور حسين علي مويني.

الضيف الخاص:
إمام المسجد الحرام – مكة المكرمة، المملكة العربية السعودية.

شاهدوا البث المباشر عبر الرابط:

اضغط هنا للمشاهدة المباشرة

https://www.youtube.com/live/OWLY2gBnKO0?si=BhoEWUrerHDnq9dl

لا تنسوا:

المشاركة، والاشتراك، والتعليق.

AL AMEEN TV 📺

🔴 #LIVE MASHINDANO YA DUNIA YA QUR'AN TUKUFU BENJAMIN MKAPA STADIUM 05/04/2026 Enjoy the videos and music you love, upload original content, and share it all with friends, family, and the world on YouTube.

14/03/2026

Zakatul-Fitr ni zaka inayotolewa mwishoni mwa mwezi wa Ramadhan kabla ya Swala ya Eid al-Fitr.

1. Lengo la Zakatul-Fitri

Hikma yake

Mtume ﷺ amesema:
عن ابن عباس رضي الله عنهما قال:
فرض رسول الله ﷺ زكاة الفطر طُهرةً للصائم من اللغو والرفث وطُعمةً للمساكين.
رواه أبو داود.

Maana yake:

Mtume ﷺ ameifaradhisha Zakatul-Fitri ili:
Kumsafisha aliyefunga kutokana na makosa madogo aliyoyafanya wakati wa kufunga.

Kuwasaidia maskini ili nao wapate chakula siku ya Idi.

2. Kiwango cha kutoa

Mtume ﷺ amesema:
فرض رسول الله ﷺ زكاة الفطر صاعًا من تمر أو صاعًا من شعير...
رواه البخاري ومسلم

Maana:
Mtume ﷺ amefaradhisha Zakatul-Fitri Saa moja (صاع) ya chakula.

Kiwango chake

1 Saa = takribani kilo 2.5 – 3 za chakula.

Chakula kinachotolewa hutegemea chakula kikuu cha watu wa eneo husika.

Mfano:

Mchele
Ngano
Mahindi
Tende

3. Ni nani anatakiwa kutoa
Zakatul-Fitri

Ni wajibu kwa
Kila Muislamu
Mwenye chakula cha ziada siku ya Idi

Hutolewa kwa ajili ya:

Nafsi yake
Watoto wake
Watu anaowalea

4. Muda wa kutoa
Wakati wa kutoa una ngazi tatu:

1. Wakati bora
Baada ya kuzama jua mwisho wa Mwezi Mtukufu Ramadhan mpaka kabla ya Swala ya Idi

2. Inaruhusiwa mapema

Siku 1 au 2 kabla ya Idi

K**a ilivyofanywa na Maswahaba.

3. Ikiwa atatoa baada ya Swala ya Idi

Mtume ﷺ amesema:
من أداها قبل الصلاة فهي زكاة مقبولة ومن أداها بعد الصلاة فهي صدقة من الصدقات
رواه أبو داود

Maana: Mwenye kutoa
Kabla ya Swala ya Idi itakuwa Zaka sahihi na Mwenye kutoa
Baada ya Swala inakuwa sadaka tu

5. Je inafaa kutoa pesa badala ya chakula?

Wanazuoni wamekhitalifiana:
Rai ya wengi

(Jamhuri ya wanazuoni)

K**a:
Imam Malik
Imam al-Shafi'i
Imam Ahmad ibn Hanbal

Wanasema:

➡️ Inatolewa chakula si pesa kwa sababu hiyo ndiyo aliyofanya Mtume ﷺ.

Rai ya baadhi ya wanazuoni
K**a:

Imam Abu Hanifa
Wanasema:

➡️ Inaruhusiwa kutoa pesa ikiwa ni manufaa zaidi kwa maskini.

Taasisi ya AL AMEEN FOUNDATION - AIF inakusanya na KUGAWA na ZAKKATUL FITRI kwa makundi Maalum.

WASILISHA Zakatul Fitri Yako Kupitia Namba za Simu

+255 715 800 772
+255 657 277 747

Matarajio siku ya KUGAWA ni Siku Moja Kabla ya EID

08/02/2026

Asalaam alaikum

Kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani TAASISI YA AL AMEEN FOUNDATION AIF .

Inapenda kukushirikisha wewe Mpenda kheiri katika kuchangia PROGRAM HII MAALUM ya Iftar Kwa Makundi Maalum katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Matarajio kugawa iftar Awamu ya kwanza kabla Mwezi wa Ramadhani.

Vifaa ambavyo Tunavyo hitaji kukusanya

1.Mchele
2.Tambi
3.Unga Ngano
4.Maharage
5.Sukari
6.Mafuta
7.Tende n.k

Tuikimbilie kheiri hii.

Mawasiliano zaidi : 0715800772

02/02/2026

KARIBUNI SAANA

13/01/2026
Photos from Al Ameen foundation - AIF's post 11/01/2026

Watoto wetu wanufaika wa PROGRAM YA ORPHANS BACK TO SCHOOL 2026 inayo simamiwa na Taasisi ya AL Ameen foundation - AIF wakiongoza Dua ya Shukran kwa wadau walio changia Program hii kabla ya Zoezi la Ugawaji .
Tukio zima unaweza lishuhudia kupitia Youtube chanel yetu : AL AMEEN TV
au Bonyenza Link hii : https://www.youtube.com/live/xgnXmAukK8A?si=5O-_fLs1JqcHXOb6

Photos from Al Ameen foundation - AIF's post 10/01/2026

Alhamdulillāh 🤲

Kwa fadhila na rehema za Mwenyezi Mungu ﷻ, jambo limepita salama katika program ya Orphans Back to School 2026 iliyoandaliwa na Taasisi ya Al Ameen Foundation – AIF.

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuwafikia watoto yatima 150 na kuwapatia msaada unaowasaidia kurejea shule wakiwa na matumaini mapya.

Taasisi ya Al Ameen Foundation – AIF inatoa shukrani za dhati kwa wafadhili wote, wadau, viongozi, wanachama na kila aliyeshiriki kwa hali na mali katika kufanikisha mradi huu wa kheri.

Mwenyezi Mungu awabariki, awaongezee riziki, na ayakubali matendo yenu mema.

Program hii ni ushahidi kwamba ushirikiano katika kheri huleta matokeo makubwa, na kwa pamoja tunaendelea kujenga kesho bora kwa watoto yatima kupitia elimu na malezi mema.

📚🤝 Orphans Back to School 2026
Chini ya uratibu wa Taasisi ya Al Ameen Foundation – AIF

🟢 Kauli mbiu:
“Kusema na Kutenda Ndiyo Msingi wa Maendeleo kwa Jamii.”

Mwenyezi Mungu atujalie tuendelee kuwa sababu ya kheri kwa wengine. Aamiin.

Photos from Al Ameen foundation - AIF's post 10/01/2026

Alhamdulillāh 🤲

Kwa uwezo na neema za Mwenyezi Mungu , leo tarehe 10/01/2026, Taasisi ya AL AMEEN FOUNDATION – AIF imefanikiwa kugawa vifaa vya shule kwa watoto yatima wapatao 150, ikiwa ni sehemu ya juhudi zetu za kuinua elimu, utu na matumaini ya watoto wetu.

Hafla hii tukufu ilipambwa na uwepo wa viongozi na wanazuoni mbalimbali wa dini, wakiongozwa na:

Sheikh Mohammed Nassor Amran – Kiongozi Mkuu wa Taasisi

Sheikh Omar Mgaza – Kutoka Ofisi ya M***i

Sheikh Dau Silima – Kutoka Waqf na Mali Amana Zanzibar (Kitengo cha Zakaah na Sadaka)

Sheikh Ahmad Rajab Msomi – Kutoka Chuo Kikuu cha Al Azhar Shareef, Misri.

Viongozi hawa walitoa nasaha, dua na hamasa, wakisisitiza umuhimu wa kuwalea yatima kwa misingi ya dini, elimu na maadili mema, sambamba na kushirikiana katika kazi za kheri kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu.

Tunatoa shukrani za dhati kwa wafadhili wote, wadau, wanachama na kila aliyeshiriki kwa njia moja au nyingine kufanikisha tukio hili.

Mwenyezi Mungu awalipe kheri nyingi, abariki mali zenu na aweke matendo haya katika mizani ya mema.

📌 AL AMEEN FOUNDATION – AIF itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhudumia jamii, kusaidia yatima na kuwekeza katika elimu kwa ajili ya kizazi cha leo na kesho.

“Na wanakuuliza watumie nini. Sema: Kheri mnayotoa ni kwa wazazi, jamaa, yatima, masikini na wasafiri.” (Al-Baqarah: 215)

🤝 Karibu tushirikiane katika kheri.
Goreeb & Yateem Trust Fund
Kijana Wa Kiislam Dsm
Kijana wa Kiislam Tanzania
Najivunia kuwa Bint wa Kiislam
Najivunia kuwa Muislam

07/01/2026

ASalaam alaikum

Karibuni saana

Kwa wale wanao taka kuchangia

0797 800 772
0657 277 747

AL AMEEN FOUNDATION AIF

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Address


Kijitonyama Alimaua
Dar Es Salaam