DoktaTz

DoktaTz

Share

Looking for an online doctor advice? Look no further than Online DoktaTz. We are your one-stop, online destination for fast, safe medical advice.

02/02/2023
Photos from DoktaTz's post 03/10/2022

01/10/2022

.

01/10/2022

Photos from DoktaTz's post 01/10/2022

EBOLA ni nini???

20/06/2022

TEZI DUME NI NINI?
⚫️Tezi dume ni moja ya tezi la uzazi la kiume ambalo kila mwanaume analo, tezi hili lipo chini ya kibofu cha mkojo na linazunguka njia ya mkojo toka kwenye kibofu kwenda kwenye uume.
⚫️Jinsi umri unavyoongezeka tezi dume nalo huongezeka ukubwa ambao unaweza kuwa wa kawaida au saratani.

▪️Kuna aina tatu za magonjwa ya tezi dume.
• Maambukizi ya Bakteria (Prostatitis).
• Kukua kwa tezi dume ambalo sio saratani (Benign Prostatic Hypertrophy-BPH).
• Saratani ya tezi dume.

KAZI YA TEZI DUME
Kutoa majimaji anayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) kutengeneza manii (semen).

⚫️SARATANI YA TEZI DUME
Saratani ya tezi dume inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vitokanavyo na saratani kwa wanaume duniani.
Pia ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wenye umri wa miaka 70 na kuendelea.

VITU VINAVYOSABABISHA SARATANI YA TEZI DUME
▪️Chanzo hasa cha saratani ya tezi dume hakijulikani, saratani hii ina uhusiano mkubwa na;
• Umri, Wanaume wenye umri kuanzia miaka 60 na kuendelea wanapata zaidi saratani ya tezi dume.
• Vyakula vyenye kiasi kikubwa cha mafuta, hasa ya wanyama.
• Historia ya tatizo hili kwenye familia (Genetic).
• Kuwa na uzito uliokithiri.

DALILI ZA SARATANI YA TEZI DUME
Katika hatua za awali, dalili hazitofautiani sana na zile za kuvimba kwa tezi dume lisilokuwa saratani (BPH). Dalili hizo ni pamoja na;
• Kusikia kupata haja ndogo mara kwa mara hasa nyakati za usiku
• Haja ndogo kuchelewa kutoka
unapoanza kukojoa.
• Kutoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
na kuchuruzika kidogo kidogo
baada ya kumaliza kukojoa.
• Kujikakamua wakati wa kukojoa na
kushindwa kumaliza mkojo wote.
• Kutoa mkojo au manii
yaliyochanganyika na damu
• Maumivu makali sehemu mbalimbali za mwili k**a saratani
imesambaa.
• Kupunguauzito,kuhisikichefuchefu,
uchovu na kizunguzungu.

⚫️UCHUNGUZI / UPIMAJI
◼️Kipimo cha damu kuangalia kiwango cha aina ya ‘protein’ iitwayo ‘Prostate Specific Antigen (PSA), proten’ hii huwa juu kuliko kawaida k**a mtu ana saratani ya tezi dume na wakati mwingine k**a ana maambukizi (prostatitis).
◼️Kuchukua kipande cha nyama kwenye tezi (Prostate Biopsy) kwa uchunguzi wa kimaabara.
v Kipimo cha mawimbi sauti (Ultrasound) ambacho husaidia kuonyesha ukubwa na sura ya tezi dume.
◼️Vipimo vya CT scan, MRI kutambua k**a saratani imesambaa sehemu nyingine za mwili.

TIBA YA SARATANI YA TEZI DUME
◼️Matibabu ya saratani ya tezi dume
yanategemea hatua ya ugonjwa na
umri wa mgonjwa.
◼️Aina za tiba hizo ni pamoja na;
• Upasuaji ( Surgey)
• Mionzi (Radiotherapy)
• Vichochezi (Homonal therapy) • Kemikali (Chemotherapy)-
• Ubaridi (Cryotherapy)

KINGA
Fanya mazoezi ya mwili na uwe na uzito unaostahili ukilinganisha na urefu wako.
Kula vyakula vyenye mafuta kiasi na hasa ya mimea, vyakula vyenye asili/ vyenye soya, vyakula vyenye “Lycopene” – inapatikana kwenye nyanya, tikiti maji, na matunda mengine, mboga za majani kwa wingi na samaki.

Crdt:

www.udsm.ac.tz

13/04/2022

SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

SHINGO YA KIZAZI NI NINI?

Shingo ya kizazi (cervix) ni kiungo cha mwili kinachopatikana kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke. Ni sehemu ya mji wa mimba (Uterus) inayotokezea kwenye uke (tupu) wa mwanamke. Tazama picha

SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI NI NINI?
Ni mabadiliko hasi (yasiyo ya kawaida) ya chembechembe hai zilizopo kwenye shingo ya kizazi. Mara nyingi saratani hii ikiwa inaanza haionyeshi dalili yoyote hivyo mgonjwa hawezi kuchukua hatua yoyote kukabiliana na tatizo hili kwa wakati huu.

Kwa kiasi kikubwa saratani hii husababishwa na maambukizi ya mda mrefu (persistence infection) ya virusi viitwavyo Human papilloma, ambavyo huenezwa kwa njia ya kujamiiana. Kawaida mwili una uwezo wa hudhibiti maambukizi haya yaingiapo mwilini, lakini yasipodhibitiwa kikamilifu na kuwepo mwilini kwa mda mrefu husababisha ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.

MAMBO MENGINE YANAYOCHANGIA KUPATA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Kufanya ngono zembe
Kuwa na wapenzi wengi
Kukoma siku katika umri mkubwa
Utumiaji mafuta mengi katika chakula.
Kutokufanya mazoezi ya mara kwa mara.
Unene kupita kiasi
Uvutaji sigara.
Utumiaji wa pombe kupita kiasi.
Historia ya saratani ya matiti katika familia.
DALILI ZA UGONJWA WA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Dalili za ugonjwa huu huanza kujitokeza baada ya tatizo kuanza kukomaa, zifuatazo ni baadhi ya dalili

Kutokwa na maji maji yenye harufu ukeni
Kutokwa damu baada ya kujamiiana
Kutokwa damu kusiko kwa kawaida (siyo damu ya hedhi)
Kuumwa mgongo na kiuno
Kuumwa miguu
Kizunguzungu na kuishiwa nguvu
NINI KIFANYIKE?

Saratani ya shingo ya kizazi inazuilika au kutibika kabisa endapo itagundulika ikiwa kwenye hatua za awali.

Hivyo ni muhimu kufanya uchunguzi wa afya yako kwa kadiri utakavyoshauriwa na wataalam wa afya

Wanawake wote walio na umri kuanzia miaka 30 na kuendelea wanatakiwa kufanya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi.

Kumbuka: Wakati wa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi ni sasa usisubiri hadi uone dalili, fika kituo cha huduma za afya kwa ushauri/mwongozo Zaidi,

https://www.orci.or.tz/shingo-ya-kizazi/

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address


Dar Es Salaam