Ni vigumu sana kufanya dili na Mwarabu, hasa pale ambapo anatakiwa asimame upande wako (mtu mweusi) mbele ya Mwarabu mwenzake, atakumwaga tu.
Busara za Mpumbavu
Ukurasa huu ni maalumu kwaajili ya uchambuzi siasa, uchumi, mahusiano na michezo.
07/02/2026
Sijui ni hali ya hewa, au anacheza akiwa mgonjwa? Pacome tuliyemzowea si huyu wa leo.
Hata hivyo, hali k**a hizi humkuta mchezaji yeyote duniani.
Kocha Pedro anapaswa kumfanyia sub, pengine aingie Dube au hata Edmund ambaye anaweza kuinufaisha timu kutokana na speed.
Pacome hana game bora leo, ni sehemu ya kikwazo. Labda kipindi cha pili arudi mchezoni.
HT: Rabat 0-0 Yanga
07/02/2026
IRAN (WAAJEMI): URITHI WA ESTA NA MORDEKAI KATIKA HISTORIA YA KALE
Historia ya Esta (Esther) na Mordekai (Midekai) si hadithi ya mbali ya Biblia tu, ni simulizi iliyotokea ndani ya moyo wa Ufalme wa Waajemi (Persia), taifa linaloitwa leo Iran.
Wakati falme zikijiona zina nguvu, hadithi hii inaonyesha jinsi mamlaka ya kisiasa yalivyotumika bila kujua kutimiza kusudi la Mungu. Hii inadhihirishwa hadi hivi leo juu ya uthubutu, misimamo na nguvu ya Iran (Waajemi).
Matukio yalitokea Shushani (Susa), mji wa kifalme wa Waajemi uliopo Iran ya leo. Ndani ya jumba la kifalme, mwanamke Myahudi aliyekuwa hana sauti wala nguvu aligeuka kuwa Malkia, na sauti yake ikasimamisha hukumu ya maangamizi dhidi ya taifa zima.
Mordekai, Myahudi aliyeishi chini ya utawala wa kipagani, alikataa kuinama mbele ya mamlaka dhalimu. Ukaidi wake haukuwa wa kiburi, bali wa imani na msimamo wa haki. Ndani ya mfumo wa Waajemi, alisimama akijua hatima inaweza kuwa kifo, lakini historia ilimpa ushindi.
Sawa, nakiri kwamba Uajemi haikuwa falme ya Mungu, lakini ilitumika na Mungu.
Sheria zake, kasri zake na mihuri yake vilitumiwa kubadili hukumu ya mauti kuwa uhai. Hii ni hoja nzito kwamba, si kila falme inayotumiwa na Mungu inatoka katika falme za Mungu.
Hadithi ya Esta ni ukumbusho mkali kwamba nguvu za dunia zina mipaka, na kwamba wakati mwingine wokovu hutokea katikati ya mifumo ambayo haikuandaliwa kuwa rasmi mbele za Mungu, badala yake kwa mapenzi yake Mungu ameitumia mifumo hiyo.
Hadi leo, Purimu inaadhimisha ushindi huu, na Iran ya kale inabaki kuwa jukwaa la simulizi moja ya ujasiri mkubwa zaidi katika Biblia.
Kumbuka, historia haisimuliwi tu, bali inapangwa.
Na
Mwanahistoria
Dar, Tz
06/02/2026
https://youtu.be/5ea-PyoE6io?si=kl-B5Fh2JlGBdMoX
Msichana ALIYEHUSIKA kwenye VIDEO YA NGONO ya R KELLY ajitokeza **a
KAULI YA KHAMENEI KUHUSU MGOGORO WA IRAN NA MAREKANI
"Unaposikia wakizungumza kuhusu vita, wakisema tutakuja na mpango huu au ule na kufanya hili au lile, hilo si jambo jipya."
"Marekani wametutishia mara nyingi hapo nyuma, wakisema kila mara kuwa βchaguo zote zipo mezani,β ikiwemo chaguo la vita. Wamekuwa wakisema maneno hayo kwa miaka mingi. Vivyo hivyo, mtu huyu, (Donald Trump) huendelea kudai mara kwa mara kuwa wameleta manowari za kivita.
Lakini taifa la Iran halitatishwa na kauli za aina hii. Wananchi wa Iran hawatatetereka wala kuogopeshwa na vitisho hivi. Hawana hofu ya mapambano ya haki."
"Sisi si waanzilishi wa vita, wala hatutaki kuishambulia nchi yoyote. Hata hivyo, taifa la Iran litatoa pigo kali dhidi ya yeyote atakayelishambulia au kulihangaisha. Wamarekani wanapaswa kujua kwamba iwapo wataanzisha vita, safari hii vita hivyo vitakuwa vya kikanda."
Huyu Mzee ana msimamo mkali sana.
Mashabiki wa Simba wamvamia Mangungu.
01/02/2026
SIMBA OUT π¦β
Baada ya suluhu dhidi ya Esperance de Tunis, sasa ni rasmi: Simba SC ameaga michuano ya Klabu Bingwa Afrika.
Kwa wasiofahamu, msimamo wa Kundi D kwa sasa uko hivi:
1οΈβ£ Stade Malien β pointi 8
2οΈβ£ Esperance Tunis β pointi 6
3οΈβ£ Petro de Luanda β pointi 5
4οΈβ£ Simba SC β pointi 1
Hebu tuangalie mahesabu π
πΉ Mchezo unaofuata:
Simba π Petro de Luanda
β‘οΈ Tuseme Simba anashinda β atafikisha pointi 4
πΉ Mchezo mwingine:
Stade Malien π Esperance
β‘οΈ Tuseme Stade Malien anashinda β atafikisha pointi 11, Esperance anabaki na pointi 6
πΉ Mchezo wa mwisho:
Simba π Stade Malien
β‘οΈ Simba akishinda β atafikisha jumla ya pointi 7
Wakati huo huo:
Esperance π Petro de Luanda
β‘οΈ Wakitoa sare, Esperance atafikisha pointi 7 sawa na Simba
β οΈ Lakini kikanuni, Esperance atasonga mbele kwa sababu alimfunga Simba kwenye mchezo wa kwanza (head to head).
β‘οΈ Na hata k**a Petro de Luanda akishinda mechi yake ya mwisho, atafikisha pointi 8, hivyo Stade Malien na Petro ndio watakaokwenda robo fainali.
π Kwa hiyo, hata Simba akishinda mechi zote mbili zilizobaki, hana nafasi ya kusonga mbele. Mwendo umeishia hapa.
β½ Tunapowaambia kuwa michuano ya Klabu Bingwa hatua ya makundi inachezwa kwa mahesabu muwe mnaelewa.
Baba Jeni bye bye!!
Na
Mchambuzi Huru
Dar, Tz
01/02/2026
YANGA WAHITAJI POINTI 4 TU KUSONGA ROBO FAINALI π°β½
Yanga SC bado wapo nafasi ya pili kwenye Kundi B, wakitanguliwa na Al Ahly.
Kikanuni, Yanga wanahitaji pointi nne (4) tu kwenye mechi mbili zilizobaki ili kufuzu hatua ya robo fainali.
πΉ Mechi ijayo: FAR Rabat vs Yanga (Morocco) β Sare inatosha
πΉ Mechi ya mwisho: Yanga vs JS Kabylie (Amaan Complex) β Ushindi lazima
β
Sare + Ushindi = Pointi 4
β‘οΈ Kwa matokeo hayo Yanga watakuwa wamefuzu bila kuangalia matokeo ya timu nyingine.
π NB: Kwa mujibu wa kanuni za CAF, timu zikifanana pointi, huangalia kwanza head-to-head, sio goal difference. Kumbuka Yanga waliwafunga FAR Rabat kwenye mchezo wa kwanza. π₯
31/01/2026
Saa ngapi tutaanza kuzungumza ubora wa huyu jamaa kwenye game dhidi ya Al Ahly?
Anaitwa
Ni mashine kweli kweli.
31/01/2026
Vikosi vya Yanga vs Al Ahly
27/01/2026
π¨ Laurindo Dilson Maria Aurelio-Depu amefunga goli 2 dhidi ya Dodoma Jiji akifikisha goli 3 na assist 1 kwenye mechi 2 za Ligi Kuu alizocheza.
Jamaa hahitaji kupewa muda, huu uliopo unamtosha.
Hili ni balaa lingine kwenye NBC Premier League 2025/26 πͺπΎπͺπΎ
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Contact the school
Telephone
Website
Address
Dar Es Salaam