Jifunze Kilimo na Ufugaji

Jifunze Kilimo na Ufugaji

Share

Tunafundisha kilimo na ufugaji, tunauza pembejeo za kilimo na bidhaa za kilimo. Ukitaka kujifunza Wasiliana Nasi

16/07/2020

Ndugu yangu ameipokea Challenge Yetu Ya Kupanda Mbogamboga na Ame Share Video.

Na Ww Pia unaweza uka share Picha Au Video ukilima Mbogamboga na sisi Tutakupost.

Tuma kwa Whatsap Namba 0714 606706

hasttag

cc;

Photos 10/05/2020

Imekua Siku Njema Sana Baada Ya Mimi na Kumtembelea na Kumtia Moyo Ndugu Jumanne, ( )Mdogo Wake na Rojas ambae Tulikua Tunashirikiana Nae Kwenye Kilimo.

Kwa Mahitaji Ya Mbegu Za Mbogamboga,Miche Ya Matunda,Elimu Ya Kilimo,Usisite Kumcheki Kupitia Page Yake Ya




Cc;

Photos 09/05/2020

AINA ZA MASOKO YA BIDHAA ZA KILIMO
(Part 4)

4.Export Market (Soko La Nje Ya Nchi)

Hili ni Soko La Nje Ya Mipaka Ya Nchi,Katika Soko Hili Unaweza Ukawauzia Wateja Wa Jumla (Wholesalers),Mawakala (Agency) au Wasambazaji (Distributors)

Soko hili linahitaji Bidhaa Zenye Ubora Wa Hali Ya Juu,Pia Kabla Ya Kusafirisha Bidhaa Zako Unahitajika kua na Vibali na Vyeti Kutoka Kwny Mamlaka Za Afya.

Ni Soko Lenye Faida Nzuri.Kwa Sasa Mazao Ya Mbogamboga na Matunda k**a Parachichi Yanafanya Vizuri katika Soko Hili.

By Rich Farmer

Cc;

Photos 09/05/2020

AINA ZA MASOKO YA BIDHAA ZA KILIMO
(Part 3)

3.Agro-Processing Industries (Soko La Viwandani)

Hivi ni Vile Viwanda Vinavyohusika Kuongeza thamani bidhaa za Kilimo.Mfano Viwanda Vya Kutengeneza Tomato Sauce,Viwanda Vya Juisi,Viwanda Vya Nguo,Viwanda Vya Maziwa n.k

Sifa Kubwa ya Soko Hili Huwa Wanahitaji Mazao Mengi Kutoka Kwa Mkulima.

By Rich Farmer



Cc;

Photos 09/05/2020

AINA ZA MASOKO YA BIDHAA ZA KILIMO (Part 2)

2. Corporate Market
Hili ni Soko La Kishua Mfano Ni Super Markets,Hoteli za Kitalii,Camp Sites etc.

Sifa Kubwa Ya Hili Soko; Bidhaa Lazima Ziwe Kwny Vifungashio (Packaging),
Ubora Wa Bidhaa Lazima Uwe Wa Hali Ya Juu,Wanahitaji Consistency ya Bidhaa zako,Sio Leo Unapeleka Bidhaa baada ya Siku Kadhaa Unawaambia Huna Mzigo.

Kikubwa Zaidi Wanahitaji Taaluma (Proffesionalism) katika kufanya nao Biashara Hawahitaji uswahili wala Janja Janja Ambazo Zipo kule Kwny Local Market.

By Rich Farmer



Cc;

Photos 09/05/2020

AINA ZA MASOKO YA BIDHAA ZA KILIMO.(Part 1)

Pale Unapoamua Kuanza Kilimo Lazima Ujue Unataka Mazao Yako Uuze Kwenye Soko Lipi.

Nimejaribu Kutenga Masoko Ya Bidhaa za Kilimo Katika Makundi 4.

1.Local Market (Soko La Mtaa)
Hapa Tunazungumzia Masoko K**a K'koo,Mabibo (DSM), Soko La Buzuruga,Mirongo (Mwanza),Samunge (Arusha),Majengo (Dodoma)

Sifa Mojawapo Kubwa ya Soko Hili Huwa Hawazingatii Sana Ubora Wa Bidhaa ndo Maana Unaweza Ukaenda Sokoni Ukauziwa Nyanya Masalo au Ukauziwa Matunda Yaliyoharibika.

Changamoto Yake;Asilimia Kubwa Ya Wakulima Wanategemea Aina Hii Ya soko na Wakulima Huwa Wanalima Kwa Misimu Inayofanana Hii Upelekea Wakati Wa Mavuno Mazao Kua Mengi Sokoni na Mazao Kushuka Dhamani Na Kuuzwa Kwa Bei Ya Hasara.

By Rich Farmer



Cc;

08/05/2020

Mtu Wa Kwanza Anaelinda Usalama Wa Nchi ni MKULIMA

06/05/2020

Kabla Hujaamua Kulima Zao Lolote Hakikisha Unaanza Kufanya Utafiti Wa Soko Lako.

Kuna Mwingine Hataki Tena Kusikia Kuhusu Kilimo Cha Matikiti Maana Alishawahi Pata Hasara Baada ya Kukosa Soko, ila Kuna Mwingine Anakwanbia Ana Soko Kubwa La Matikiti Zanzibar Hadi Anashindwa Kulihudumia.

Kuna Mwingine Alilima Nyanya Mwaka Juzi Zikaozea Shambani Kwa Kukosa Soko Wakati HuoHuo Kuna Mtu Mwingine Anauza Nyanya Hadi Anachanganyikiwa Kwny Viwanda Vya Tomato Sauce.

Kuna Mwingine Analima Mbomboga Hajui Akauzie Wapi Maana Masokoni Zimejaa ila Kuna Mwingine Anasumbuliwa na Shule za Boarding Mboga Anazowapelekea Hazitoshi.

Wakati Mwingine Ni Ngumu Sana K**a Mkulima Kua Na Ujuzi Wa Kutafuta Masoko Maana Ni Taaluma Ya Watu Na wanasomea Darasani.Ila Yakupasa Mkulima Kujifunza Pia Hii Taaluma Either Uingie Darasani Usome hata k**a Course Fupi za Mitandaoni au Utafute Mtu Mwenye Ujuzi na Uzoefu Wa Masoko Akusaidie.


Photos 03/05/2020

Viazi lishe aina ya Kabode kutoka Kiegeya -Morogoro vinapatikana kwa bei elekezi ya kizalendo.

Kilo 1@ 2,000/= tu

Faida za Viazi Lishe

-Vina utajiri mwingi wa Vitamin A ambayo ni muhimu kwa afya ya macho,ngozi.

-Ni kinga ya mwili dhidi ya maradhi.

-Vinaupa mwili nguvu

-Nyuzinyuzi zake zinasaidia mmeng'enyo wa chakula tumboni hivyo vinapunguza uwezekano wa kansa ya utumbo mkubwa.

-Vinafaa kwa watoto,wamama wajawazito,wazee,wagonjwa na watu wazima wa rika lolote.

Kwa mahitaji ya viazi lishe jumla na rejareja,Piga Kwa Mahitaji Ya Mbegu piga ni 0685700700.

Photos 03/05/2020

AHSANTE Wateja Mnaoendelea Kutoa order , Kwa mahitaji ya KUKU WA KIENYEJI karibu MALEMBO FARM (MF)Bei inaanzia Tzs 16,000/= mpaka Tzs 20,000/= Pia ukihitaji nusu 7500/= Robo 3500/=

Karibu Sana,Huduma ya Delivery Ipo.

Follow

+255747981275

[email protected]

Photos 03/05/2020

CHANGAMOTO YA MADALALI SOKONI

Moja ya Changamoto tunazokumbana nazo wakulima hasa wadogo ni MADALALI masokoni.

Nature ya Masoko yetu yote yameshikwa na madalali,Madalali wapo kwenye Nafaka,Kwenye Mbogamboga, kwenye Matunda n.k.

Mfano;Mkulima ukipeleka matikiti 6000 sokoni ,Wewe k**a mkulima huwezi kuyauza ni lazima umkabidhi Dalali ayauze hizo ndo taratibu za masoko yetu.Na kwa kila tikiti litakalouzwa dalali yake ni Tsh 200.Haijalishi tikiti limeuzwa kwa Tsh ngapi either elfu 2,elfu 1 au hata Mia 5.

Kwa matikiti 6000 Dalali anatengeneza hela yake Tsh 1.2M.Matikiti elfu 6 yanaweza yakauzwa ndani ya siku 1 au mbili Tu.

Hii hupelekea wakati mwingine mkulima kupata hasara au faida ndogo na kuchukia kilimo kabisa,maana gharama za uzalishaji huwa kubwa ukizingatia mkulima kahangaika na matikiti zaidi ya miezi 2,kakodi shamba,kaajiri vijana,kanunua mbegu,madawa,mbolea,usafirishaji kutoka shamba hadi sokoni n.k.

Nini Kifanyike?
1.Serikali (Wizara ya Kilimo,Wizara Ya Viwanda Na Biashara),Taasisi zinahusika na Kilimo & Masoko i.e zitusaidie katika ku control madalali masokoni.

2.Mkulima kabla ya Kulima hakikisha unajipanga na suala zima la soko.Usitegemee aina moja ya soko.

3.Wakulima tupate platform ambayo inaweza ikatuunganisha moja kwa moja na mnunuzi au mlaji wa mwisho wa mazao yetu bila kupitia mikononi mwa madalali.

Hii itasaidia kuinua wakulima na kuhamasisha watu wengi zaidi kuingia kwenye kilimo na kupunguza tatizo la ajira Nchini.


02/05/2020

Kwa Mahitaji Ya Mbogamboga Za Jumla, Pembejeo,Elimu Ya Kilimo Cha Mbogamboga Usisite Kutucheki Kwa Namba 0710100824

Pia Tuna Miche Ya Matunda Yote.

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address


Dar Es Salaam
255

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00