01/09/2023
OFA, OFA, OFA.
WIGO INSTITUTE chuo cha kisasa chenye usajili ( REG/NACTEVET/VTC/0837) kilichopo hapa Parokia ya MOYO MTAKATIFU WA YESU - Manzese- Jijini Dar es salaam.
Kinawatangazia watanzania wote , ofa kubwa ya punguzo la ADA kwa mwezi wa 6-9/2023.
1. KOZI NDEFU
a) INFORMATION TECHNOLOGY ( IT)- NVA Level 1-111- 550,000/Mwaka
b) BUSINESS OPERATIONS ASSISTANT (BOA)- NVA Level 1-111: 550,000/ Mwaka
2. KOZI FUPI
a)Komputa: 30,000tu Kwa program.
b)Kingereza - 30,000/Kwa mwezi
c)Graphics : 50,000/Kwa mwezi.
Tupigie: 0754051721
Karibuni Sana.
23/08/2022
Karibuni kozi nzuri za Komputa
WiGo Institute of Technology & Entrepreneurship, chuo bora kilichosajiliwa na mamlaka ya usajili wa vyuo vya kati na vya ufundi( NACTEVET), che usajili namba; Reg/Nactevet/VTC/0837. Kinawatangazia watanzania wote kuwa dirisha la udahili liko wazi Kwa kozi za mda mrefu( miaka 2) ngazi ya cheti; na kozi fupi kuanzia miezi 2 na kuendelea.
Sifa za mwombaji Kwa kozi ndefu awe na ufaulu wa angalau " D" mbili katika somo lolote isipokuwa somo la dini. Na Kwa kozi fupi ni Kwa mtu yeyote anayejua kusoma na kuandika na anayehitaji kujijengea uwezo Kwa kujipatia ujuzi kwenye fani husika.
Chuo kipo kwenye Majengo ya kanisa katoliki Parokia ya Moyo Mtakatifu Wa Yesu(Manzese), wilaya ya Ubungo -Urafiki karibu na kituo cha Big Brother. Kwa maelezo zaidi soma kipeperushi hapa chini pia unaweza kuwasiliana nasi Kwa; +255754051721. Wote mnakaribishwa
20/08/2018
It was a great Honor to carry out a training to MANZESE PARISH Yourth( VIWAWA) to share with them one of the important topic: VIJANA NA FURSA ( Kwa nini vijana kutoka nje ya Tanzania wanakuja na kufanikiwa hapa Chini wakati wengi wa Vijana wa kwetu bado wamekwama na nini kifanyike). It was very amazing giving our sharing as BRIFU AFRICA and having time to Listen from VIJANA MANZESE. We discovered that if our Taznanian yourth decide to wake up and take their success as their personal respeonsibility and work hard on it we can create incredible stories more than even those Yourth in SILICON VALLEY. Why Not!
02/07/2018
Je kwako mteja ni mfalme au "Beib"(Baby)?
Tutafakari kidogo tena kuhusu hali ilivyo katika suala zima la huduma kwa wateja. Je mteja tunamchukuliaje katika biashara zetu, je anapata nafasi ya kwanza.
Mara nyingi tuashuhudia wateja wakihudumiwa vibaya maofisini kwetu, wanapokuja saa nyingine tunaona k**a wanatuongezea kazi vile, mimi huwa najiuliza hivi tumefungua ofisi kufanya biashara na biashara zetu zinawategemea wateja kwa kiasi kikubwa sasa tunapoona kero kuwaelezea wateja juu ya bidhaa zetu, wanapouliza maswali mengi tunakasirika tunakuwa na maana gani. kwangu naiona kuwa changamoto na inaweza kuwa sababu ya wateja kuhama kutoka kwetu na kuhamia ofisi nyingine.
mtaalamu mmoja wa biashara alisema, kwa sasa mteja hatakiwi kuendelea kuwa mfalme, anatakiwa kuwa BABY.
yaani apewe huduma k**a " MTOTO", " K**a MPEZI.
kutokana na umuhimu aliyo nao katika biashara.
ebu fikiria kuhusu namna unavyoweza k*m care Baby
1. Akija nyumbani kwako ukimuona tokea Mbali utamkimbilia na k*mpokea kwa bashasha na Furaha.
hivi ndivyo mteja anavyotakiwa kupokelewa kwa furaha na bashasha anapokaribia sehemu zetu za biashara. Nyanyuka kwenye kiti chako ndugu yangu , mpokee mteja huyo ni mgeni muhimu kwako maana ni kwa sababu yake uko hapo.
inasikitisha kuona wengi wetu mteja anakuja k**a ni dukani anaingia anaagalia bidhaa anayoi hitaji na asipoipata anaondoka, bila hata kusalimiwa wala kuelezewa. huku muuzaji akicheza na simu. "JAMANI" JAMANI" . KWELI!
2. Baby huwa anapewa Zawadi.
hakuna mtu aliye na baby wake asiye mpa zawadi, usipofanya hivyo hakika utampoteza. je wateja wetu tunawapatia zawadi!.
au tunawaangalia tu, au tunaona k**a hawastahili! nakwambia wakipata sehemu ambamp wanawajali vizuri, wanawahudumia kwa heshima na kuwapa zawdi watahamia huko
....... itaendelea..............................
07/06/2018
DO YOU PAY YOURSELF FIRST OR YOUR WORKERS FIRST!
The principle of paying your self first is common to most people especially employers , but one can decide to pay the workers first then him self or her self later . what do you think , one should pay him self first or her workers First! what is your opinion.
23/05/2018
Katika urimwengu wa biashara saa nyingine hali ilivyo inashangaza, eneo hilo hilo watu, watu wale wale, bidha hiyo hiyo na bei ile ile ila utashangaa kwamba, Mtoa huduma huyu anafanikiwa kuuza na kupata wateja wengi hadi anashindwa kuwahudumia wakati mwingine anahangaika kupata wateja. sababu ziko nyingi ila binafsi hapa nafikiria suala zima la Huduma kwa wateja (Customer care).
hili ni suala linalotakiwa kupewa kipaumbele sana katika biashara na katika huduma yoyote mtu anayoitoa kwa wateja wake. Huduma kwa wateja ni huanza hata kabla mteja hajafika ofisini kwako au mahali pako pa kazi, huanza pale anapopiga simu , namna unavyopokea simu yake, namna unavyomwongelesha kwenye simu, atakapofika mlangoni pa ofisi yako namna unavyompokea, unavyomwelezea bidhaa ulizo nazo, unavyojibu maswali yake, unavyohudumia na baada ya huduma unavyomuaga pindi anapokuwa anatoka ofisini kwako.
haishii hapo, inaendelea hadi kwenye namna unavyohusiana na mteja wako baada ya kuwa umemhudumia, je unaendeleza mahusiano mazuri! au baada ya kutoa huduma na kulipwa basi huna haja n aye tena!
nwisho wa siku ni lazima mteja afurahi na ajisikie huru kabisa kufanya kazi na wewe na pia kuhusiana na wewe. hapo ndipo biashara itaenda vizuri. Mahusiano na mteja liwe jambo la msingi na la kwanza. hata asiponunua siku hiyo huenda akaja siku nyingine.
Changamoto ni pale ambapo mteja anaingia ofisini kwako kukuletea fedha yake ili apate huduma yako ila anatoka amefokewa na amekasirishwa kwa namna anavyojibiwa na wafanyakazi au kuonesha kutok*mjali.
Je huduma kwa wateja ikoje ofisini kwako