Jifunze Kiingereza na Teacher Othman

Jifunze Kiingereza na Teacher Othman

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Jifunze Kiingereza na Teacher Othman, Education Website, Chanika nyeburu, Dar es Salaam.

๐Ÿ‡ฌ๐Ÿ‡ง Learn English Easily โ€“ For Students, Adults & Professionals
๐Ÿ“š Grammar โ€ข Speaking โ€ข Common Expressions
๐Ÿ“ฒ Join My Class on WhatsApp: https://wa.me/255744707166๏ฟฝ
โœจ Karibu ujifunze Kiingereza kwa urahisi, kujiamini, na kwa vitendo!

21/02/2026

Learn English

21/02/2026

๐Ÿ“˜ SOMO: Matumizi ya โ€œSINCEโ€ Kuonyesha Sababu

๐Ÿ”น Maana

Tunatumia since kuonyesha sababu (reason).

Ina maana sawa na โ€œbecauseโ€ au โ€œasโ€, lakini mara nyingi hutumika zaidi kwenye maandishi rasmi au sentensi za kawaida za maelezo.

๐Ÿ”น Muundo (Structure)

Since + subject + verb, main clause

au

Main clause + since + subject + verb

๐Ÿ”น Mifano

I took a taxi since it was raining.
โž Nilichukua teksi kwa sababu ilikuwa inanyesha.

Since she was tired, she went to bed early.
โž Kwa sababu alikuwa amechoka, alilala mapema.

Since you are here, letโ€™s start the lesson.
โž Kwa kuwa uko hapa, tuanze somo.

We stayed at home since it was very late.
โž Tulikaa nyumbani kwa sababu ilikuwa usiku sana.

๐Ÿ”น Tofauti kidogo na โ€œbecauseโ€

Because hutumika sana kwenye mazungumzo ya kawaida.

Since hutumika zaidi kwenye maelezo au maandishi rasmi kidogo.
Mara nyingi since huonyesha sababu ambayo tayari inajulikana au iko wazi.

Mfano:

I didnโ€™t go out because I was sick. โœ…

I didnโ€™t go out since I was sick. โœ…

Zote ni sahihi.

๐Ÿ”น Zoezi kwa Wanafunzi

Jaza nafasi kwa kutumia since:

1.______ it was raining, we stayed inside.

2.I am happy ______ you came.

3.She didnโ€™t answer the phone ______ she was busy.

21/02/2026

Katika somo hili utajifunza:
โœ… Jinsi ya kuuliza leo ni siku gani
โœ… Jinsi ya kuuliza kesho au jana ilikuwa siku gani
โœ… Jinsi ya kujibu kwa usahihi
โœ… Mifano ya mazungumzo ya kila siku
๐Ÿ”น Maswali Muhimu:
What day is it today?
What day was it yesterday?
What day will it be tomorrow?
What day is your English class?
๐Ÿ”น Majibu:
Today is Monday.
Yesterday was Sunday.
Tomorrow will be Tuesday.
My English class is on Saturday.
Somo hili ni muhimu sana kwa wanaoanza kujifunza Kiingereza na wanaotaka kuzungumza kwa ufasaha.
Jiunge na darasa letu la English kupitia WhatsApp kwa mafunzo ya kina zaidi.
Ada ni Tsh 25,000 kwa mwezi.









21/02/2026
21/02/2026

JINSI YA KUULIZA SIKU KWA LUGHA YA KIINGEREZA

19/02/2026
19/02/2026

Katika somo hili utajifunza jinsi ya kujitambulisha kwa Kiingereza kwa usahihi na kujiamini. Utajifunza sentensi rahisi za kusema jina lako, umri, kazi, mahali unapoishi na mambo unayopenda. Somo hili linafaa kwa wanafunzi wa ngazi ya mwanzo na kati.
Jiunge na darasa letu la WhatsApp kwa mafunzo zaidi ya Kiingereza kwa bei nafuu.









19/02/2026

๐Ÿ“˜ SOMO: Matumizi ya โ€œASโ€ Kutoa Sababu

๐Ÿ”น Maana
Tunatumia โ€œASโ€ kutoa sababu ya jambo fulani.
Ni sawa na โ€œbecauseโ€, lakini mara nyingi hutumika zaidi kwenye Kiingereza rasmi (formal English) au maandishi.

๐Ÿ”น Muundo (Structure)

โœ… Main clause + as + subject + verb
Mfano:
I stayed home as it was raining.

Au

โœ… As + subject + verb, main clause
Mfano:
As it was raining, I stayed home.

๐Ÿ”น Mifano Zaidi
She was happy as she passed the exam.
We canceled the match as it was too late.
As he was tired, he went to bed early.
As I had no money, I stayed at home.

๐Ÿ”น Kumbuka
โœ”๏ธ โ€œAsโ€ mara nyingi huwekwa mwanzo au katikati ya sentensi.
โœ”๏ธ Usichanganye na โ€œasโ€ ya kulinganisha (k**a โ€œas tall asโ€).

๐Ÿ“Œ Exercise kwa wanafunzi
Badilisha sentensi hizi kwa kutumia AS:
I didnโ€™t come because I was busy.
She cried because she was sad.
We stayed inside because it was cold.

19/02/2026

How to Introduce Yourself in English | Beginner Friendly Lesson

Katika somo hili utajifunza jinsi ya kujitambulisha kwa Kiingereza kwa usahihi na kujiamini. Utajifunza sentensi rahisi za kusema jina lako, umri, kazi, mahali unapoishi na mambo unayopenda. Somo hili linafaa kwa wanafunzi wa ngazi ya mwanzo na kati.
Jiunge na darasa letu la WhatsApp kwa mafunzo zaidi ya Kiingereza kwa bei nafuu.
๐Ÿ”– HASHTAGS:









18/02/2026

๐Ÿ“˜ SOMO: Matumizi ya โ€œBecause ofโ€
๐Ÿ”น Maana ya Because of
Because of humaanisha โ€œkwa sababu yaโ€.
Tunaitumia tunapotoa sababu kwa kutumia noun (jina) au pronoun (kiwakilishi) โ€” si sentensi kamili.
๐Ÿ”น Kanuni Muhimu
๐Ÿ‘‰ Because of + Noun / Pronoun
โŒ Hatutumii sentensi kamili baada ya because of
โœ… Tunatumia jina au kiwakilishi tu
๐Ÿ”น Mfano kutoka kwenye picha:
The flight was delayed because of fog.
(Ndege ilichelewa kwa sababu ya ukungu.)
โœ”๏ธ fog ni noun
๐Ÿ”น Mifano Zaidi:
She was absent because of illness.
(Alikosa kwa sababu ya ugonjwa.)
The match was cancelled because of rain.
(Mechi iliahirishwa kwa sababu ya mvua.)
He failed because of laziness.
(Alifeli kwa sababu ya uvivu.)
We stayed home because of it.
(it = pronoun).

๐Ÿ”ฅ Makosa ya Kuepuka
โŒ Because of it was raining
โœ… Because it was raining
โœ… Because of rain

Andika sentensi 3 ukitumia because of ๐Ÿ‘‡

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address


Chanika Nyeburu
Dar Es Salaam