14/11/2025
DODOMA \ Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza msamaha maalum kwa vijana waliohusishwa na vurugu wakati wa kipindi cha uchaguzi, ambao walijikuta wakifuata mkumbo bila kufahamu uzito wa matendo yao.
Akitangaza uamuzi huo wakati akilihutubia Bunge la 13 leo Novemba 14, 2025, Rais Samia alisema lengo la msamaha huo ni kuwapa nafasi vijana hao kurejea katika familia zao na kuanza upya maisha yao wakiwa na maadili na uelewa zaidi.
Uamuzi huu umepokelewa k**a hatua muhimu ya kuhimiza maridhiano, umoja na ustawi wa taifa.
13/11/2025
Dodoma | Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.
12/11/2025
NUMERIC SPORTS I Nyota wa soka duniani, Cristiano Ronaldo, ametangaza kuwa yuko kwenye hatua za mwisho za safari yake ya soka, akionyesha kuwa Kombe la Dunia 2026 huenda likawa fainali yake ya mwisho uwanjani, akiwa na umri wa miaka 40.
Ronaldo amesema amekuwa akijiandaa kwa maisha baada ya soka kwa muda mrefu, tangu akiwa na miaka 35, jambo linaloonesha utayari wake wa kuhamia kwenye sura mpya ya maisha.
Aidha, Ronaldo anakaribia kufikisha magoli 1,000 katika maisha yake ya soka,lengo ambalo amekuwa akiliwekea binafsi.
Safari yake inashangaza wengi, si tu kwa mafanikio yake uwanjani, bali pia k**a mfano wa maandalizi ya maisha baada ya soka.