UKAWA news updates

UKAWA news updates

Share

We all need changes in our country and the only meaning of changes at the moment is by putting UKAWA in charge of the government #M4C #PEOPLE'S_POWER

11/10/2018

Mbunge wa jimbo la Ukerewe mkoani Mwanza kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ndugu Joseph Michael Mkundi jana 10/10/2018 amemwandikia Spika wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania barua ya kujiuzulu uwanachama wa Chama chake cha zamani (CHADEMA) na kujiuzulu nafasi yake ya Udiwani na Ubunge kwa kile alichodai Chama chake cha zamani (CHADEMA) kimepoteza heshima na utu baada ya kumtelekeza katika kipindi ambacho alihitaji msaada na mshik**ano pamoja na ushirikiano kutoka kwenye chama hicho na uongozi wake katika kipindi cha msiba wa ajali ya Kivuko cha MV Nyerere iliyotokea mwezi ukiona kupelekea kupoteza maisha ya watu zaidi ya mia mbili. Aidha mbunge huyo ameomba kujiunga na CCM ili aweze kufanya siasa safi na yenye kuleta maendeleo yenye tija katika taifa.

Unaielewaje hii hama hama kwasasa? Kwamba k**a ajali isingetokea basi mbunge huyu angeendelea kuwa CHADEMA, lakini kwa sababu ya ajali basi imekuwa sababu ya yeye kuhama.

Nini maoni yako.

Photos from UKAWA news updates's post 22/09/2018

Mamia ya Wakazi Wa Iringa Mjini Wakimsikiliza Mbunge wao Mh. Peter msigwa jana Uwanja wa Mwembetogwa.

14/09/2018

LEO NI KUMBUKUMBU YA KUZALIWA KWA MWKT. WA ( CHADEMA ) MH.FREEMAN MBOWE

MJUE FREEMAN AIKAEL MBOWE
FREEMAN AIKAEL MBOWE

Freeman Aikael Mbowe alizaliwa tarehe 14/09/1961 Wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro.
Mbowe ni miongoni mwa Watu waliofanya Kazi katika Bank kuu ya Tanzania k**a Afisa wa Bank Kuu (BoT) akiwa chini ya Edwin Mtei, Bob Makani.

Katika harakati za kisiasa, Freeman Aikael Mbowe aliingia rasmi katika siasa mwaka 1992.
Freeman Aikael Mbowe ni miongoni mwa WAASISI au waanzilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) chama ambacho kilisajiliwa usajili wa kudumu mwaka 1993 kwa namba 0000003 kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992 kifungu cha 7(1),(2),(3), kifungu cha 8(1),(2),(3)(4)& (5)pamoja na kifungu cha 9(1)(a)(b)(c) (2)(a),(b),(c),(d),(e) na 10(1)(a),(b),(c) na (d)
Mbowe akiwa ndio kijana mdogo kuliko Wote wakati wa uasisi wa CHADEMA aliingoza kurugenzi ya Vijana ya CHADEMA chini ya Uenyekiti wa Edwin Mtei. Waasisi wengine wa CHADEMA kutaja kwa uchache ni Pamoja na -
1/EDWINI MTEI - ARUSHA
2/BOB MAKANI - SHINYANGA
3/FREEMAN MBOWE - KILIMANJARO
4/BROWN NGWILUPIPI - MBEYA
5/EDWARD BARONGO - KAGERA
6/WASIRA-MARA
7/MENRAD MTUNGI - KAGERA
8/MARRY KABIGI-MBEYA
9/EVARIST MAEMBE - MOROGORO
10/COSTA SHIGANYA - KIGOMA

Wakati wa kusaka wanachama wa CHADEMA ili kupata usajili wa Muda(Provisional registration) kwa mujibu wa sheria ya vya siasa namba 5 ya mwaka 1992 kifungu cha 8 na usajili wa kudumu (Full registration) kwa mujibu wa kifungu cha 10(1)(b) kinachotaka chama cha siasa Ili kupata usajili wa kudumu ni lazima kiwe na wanachama miambili katika mikoa kumi(10) huku mikoa miwili ikiwa mmoja Pemba na mwingine Unguja, CHADEMA iliasisi hatua hiyo k**a SAFARI YA TREN KUTOKA DAR ES SALAAM KWENDA KIGOMA.

Dhana ya "SAFARI YA KUTOKA DAR ES SALAAM KWENDA KIGOMA ilimaanisha kwamba, katika dhamira ya kutafuta mabadiliko ya kweli na kuunda Serikali kwa kushinda uchaguzi , wapo watakaonunuliwa, wapo watakaoamua kuacha siasa, wapo watakaohama chama, wapo watakaoachana na CCM na kupanda Treni popote iwe Morogoro, Dodoma, Kibaha nk.

Kwa tafsiri nyepesi, Mbowe na Waasisi wenzake waliipa safari ya kutoka Dar Es Salaam kwenda Kigoma kwamba kufika Kigoma ni CHADEMA kushinda uchaguzi na kuunda serikali. Waliamini kwamba katika safari, wengine watashukia Kibaha, wengine watapanda, wengine watapanda Treni Morogoro, wengine watashuka, wengine watapanda Dodoma wengine watashuka.

Hivyo walimaanisha kwamba, katika safari ndefu ya kufika kigoma (Kipindi hicho safari ya Treni kutoka Dar Es Salaam kwenda Kigoma ilikua ni ya shida, mteso na maumivu. Ilichukua siku Tatu hadi Tano kutoka Dar Es Salaam kufika Kigoma.). Hivyo Mateso waliyoyapata Waasisi kuijenga CHADEMA walifananisha na safari ya kutoka Dar Es Salaam kwenda Kigoma. Mfano, Viongozi wa CHADEMA wakiongozwa na Edwin Mtei, Bob Makani, Freeman Mbowe, Mary Kabongo na Evarist Maembe walipigwa mawe na kufukuzwa na wananchi Morogoro. Waliambiwa kwamba CHADEMA ndio nini?? Kwa nini mnampinga chama chetu kilichotukomboa Kutoka kwa utumwa wa wakoloni. Kwa nini mnapinga chama cha Mwalimu Nyerere baba wa taifa ??.Kwa nini mnapinga chama cha wanyonge CCM chama chenye matumaini kwa wakulima na wafanyakazi????. Waasisi hawa walipigwa mawe, kufukuzwa maeneo mbalimbali, kutukanwa, kudhalilishwa na kudhihakiwa. Kuzungumza siasa za upinzani ilionekana ni usaliti, uhaini nk. Yote hayo, walivumilia. Wengine walikata tamaa,wengine waliamua kurudi Ccm, wengine waliamua kulinda Vyeo vyao na maslahi yao na kurudi Ccm.

Mwaka 1995 Edwin Mtei na Bob Makani wote wawili walichukua Fomu ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wote walionekana kuwa na nguvu. Mapambano huo ulileta sitofahamu kubwa ndani ya CHADEMA. Freeman Mbowe k**a kijana alitoa ushauri kwa chama kwamba CHADEMA isisisimamishe mgombea urais ili kuepusha mpasuko ndani ya chama na badala yake CHADEMA imuunge mkono mgombea wa urais kupitia NCCR MAGEUZI Agustine Lyatonga Mrema. Ushauri huu wa Mbowe uliungwa Mkono na wanachama na Viongozi. Mtei na Makani waliacha mchakato huo na CHADEMA ilimuunga mkono mgombea urais Lyatonga Mrema.

Freeman Aikael Mbowe alichukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Hai mwaka 1995. Mbowe wakati wa Kampeni jimbo la Hai , aliombwa kugharamia Mkutano wa mgombea urais Lyatonga Mrema na aliahidiwa kwamba Mrema atamnadi jukwaani. Mbowe kwa kuwa alikua na Fedha na uchumi mzuri, aligharamia Mkutano na malazi ya timu ya kampeni ya Mrema nk. Lakini Mrema alipofika Jukwaani alimpuuza Freeman Mbowe wa CHADEMA na kumnadi mgombea wa NCCR MAGEUZI aliyeitwa Mwinyihamisi Mushi. Katika uchaguzi huo Mgombea wa NCCR MAGEUZI Mwanahamisi Mushi alishinda uchafu kwa kupata kura 29,046 (52.0%) huku Freeman Mbowe akiambulia kura 15,995(28.6%)

Mbowe hakukata tamaa, Mwaka 2000,Freeman Aikael Mbowe aligombea tena ubunge jimbo la Hai na kupata ushindi mnono wa kura 64.5% dhidi ya mpinzani wake wa NCCR MAGEUZI ambaye alipata mweleka kutokana na chama chake kuwa na mvurugiko mkubwa ndani ya Chama kutokana na mgogoro mkubwa wa kisiasa kati ya Mabere Nyaucho Marando na Agustine Lyatonga Mrema. Mbowe aliongoza jimbo la Hai mpaka mwaka 2005.

Katika nafasi ya Urais, Mbowe na CHADEMA Kwa ujumla walikubaliana kwamba CHADEMA isisimamishe mgombea yeyote bali chama kimuunge mkono mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof Ibrahim Haruna Lipumba.

Mwaka 2004,Freeman Mbowe aligombea uenyekiti wa CHADEMA TAIFA na kushinda akimpokea Bob Makani ambaye aliongoza kuanzia mwaka 1999. Mbowe baada ya kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA alifanya mabadiliko makubwa Sana ndani ya chama.

Baada ya kuchaguliwa, Mbowe alifanya mabadiliko makubwa Sana Ni kipindi hiki Mbowe alianza kutembelea vyuo vikuu mbalimbali vya Tanzania, kufuatilia wanasiasa mbalimbali kutoka CCM, NCCR MAGEUZI, CUF, TLP na vyama vinginevyo. Mifano iko Mingi.

John Mnyika ambaye alikua mwanaharakati wa kutetea haki za wanafunzi na watu mbalimbali na pia akiwa mtangazaji wa Redio One Stereo, Freeman Mbowe alimshawishi kujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili kuungana na wanamabadiliko wengine. Hata hivyo, UWEZO mkubwa wa John Mnyika ambao aliuonesha katika ukumbi wa Nkrumah Chuo kikuu cha Dar Es Salaam (ingawa yeye alikua akisoma masomo ya jioni) alisimama na kupinga sera ya uchangiaji wa masomo elimu ya Juu (cost sharing) na kusababisha wanafunzi kuanza Mgomo chuoni hapo. Mnyika akiwa Morogoro, aliombwa kutuliza hali hiyo na alipofika chuoni, aliita wanafunzi na kuwaambia mambo kadhaa ili kupima ujasiri wao. Alimuomba Rafiki yake kurusha jiwe katikati ya kusanyiko Mabibo Hostel, baada ya kurushwa jiwe Hilo, wanafunzi walitawanyika kukimbia ndipo Mnyika akasema ninyi ni waoga. Hamuwezi kupambana. Nawataka muache Mgomo endeleeni na masomo.

Mnyika alikua mfuasi wa CHADEMA tu mpaka 2005 alipoamua kujiunga rasimi CHADEMA na kuchukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Ubungo. Alipochukua fomu ya Ubunge, Chuo kikuu cha Dar Es Salaam kilimfukuza k**a njia ya kumdhoofisha. Mbowe alipoona uwezo wa Mnyika wa hoja, umakini, weledi na akili Alimuomba kujiunga na CHADEMA. Hotuba ya John Mnyika Bungeni mwaka 2001 akielezea kuhusu UONEVU na uharibifu wa Serikali baada ya kumuua mwanafunz mmoja Kule shule ya Sekondari Iyunga Mbeya ni rekodi pia kubwa kwa Mnyika.

Mbowe pia alifanikiwa kumvua samaki nguli wa siasa Zitto Zuberi Kabwe (ZZK) akiwa ni kiongozi chuo kikuu cha Dar Es Salaam. Zitto Kabwe akiwa Waziri mkuu wa chuo kikuu cha Dar Es Salaam na mwanaharakati wa utetezi wa wanafunzi (moja ya WAASISI wa TSNP) alifanikiwa kuvuliwa na Mbowe. Mbowe alimshuhudia Zitto Kabwe katika majukwaa ya chuo kikuu cha Dar Es Salaam hasa mahali maarufu k**a REVOLUTION SQUARE. Zitto alionekana kutoa matamko mbalimbali yaliyoitetemesha Serikali akihoji Ufisadi, kuibua uchafu mbalimbali wa Serikali ya Mkapa, na pia utetezi wa wanafunzi. Mbowe alimuona Zitto na kushawishi ajiunge CHADEMA.

Zitto Kabwe alikubali kujiunga CHADEMA na Mwaka 2005 Zitto Kabwe aligombea ubunge jimbo la Kigoma Kaskazini na alinadiwa na Freeman Mbowe k**a mgombea urais wa CHADEMA. Zitto Kabwe alishinda jimbo hilo na kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini.

Halma James Mdee naye ni miongoni vijana ambao Mbowe aliweza kuwashawishi kuingia katika siasa. Zitto na Halma Mdee wakiwa marafiki Sana chuoni, Halma Mdee akisomea Sheria na Zitto akisomea Uchumi, k**a iliyokua kwa Zitto, Halma Mdee k**a mwanaharakati wa Kutetea wanafunzi (Muasisi wa TSNP) alikubali kujiunga na CHADEMA.

Tundu Antipas Lissu ambaye alikua mwanachama wa NCCR MAGEUZI pia alifuatwa na Freeman Mbowe kuomba msaada wake katika mambo ya Sheria kutetea wanachama wa CHADEMA, wananchi katika migodi mbalimbali nk. Tundu Lissu alikua ni tishio kubwa katika mambo ya Sheria na mtetezi mambo ya mazingira. Alipinga na kupambana vikali Sana na serikali ya Benjamin Mkapa iliyowapa wawekezaji migodi na kufukuza wananchi maeneo mbalimbali ya nchi hasa Geita, Shinyanga, Mara nk. Harakati hizi za Lissu ziliifanya Serikali ya Mkapa kumtafuta na baadaye Lissu alielekea Uingereza na baadaye Afrika Kusini. Kutokana na rekodi hiyo ya harakati za mapambano, Freeman Mbowe alimuona Lissu ni silaha nzuri dhidi ya Ccm na silaha njema katika ukombozi wa Mtanzania. Alimuomba kujiunga CHADEMA.

Wengine waliojiunga na CHADEMA kipindi cha uongozi wa Mbowe kuanzia mwaka 2004 ni Pamoja na Prof Mwesigwa Baregu, Livingstone Lusinde (alirudi Ccm na sasa ni Mbunge wa Mtera), Peter Msigwa kutoka TLP, David Ernest Silinde na wengine wengi. Ni kipindi hiki CHADEMA ilifungua milango kwa wanachama kujiunga, Wasomi na vijana walijiunga CHADEMA. Baadhi ya watu walianza kuita CHADEMA ni Chama cha vijana Wasomi ingawa hata wazee Wasomi walijiunga.

Mabadiliko mengine aliyotaka Mbowe ni Pamoja na kutumia ngumi k**a ishara ya salamu ya chama
Mwaka 2005 Freeman Mbowe aligombea uraurais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa na mgombea mwenza kutoka Zanzibar bwana Jumbe Rajab Jumbe ambaye alifariki siku chache kabla ya uchaguzi mkuu uliokua ufanyike tarehe 30/10/2005 na hivyo uchaguzi kuahirishwa mpaka tarehe 14 /12/2005.

CHADEMA ilimteua mgombea mwenza Anna Maulid Komu kuwa mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika uchaguzi ule, Mbowe alitumia chopper au Helkopta kupiga kampeni maeneo mbalimbali nchini na kubatizwa jina "Kamanda wa Anga".Katika kampeni za urais Mbowe aliasisi Vazi la Magwanda ya Khaki na neno Kamanda kwa mwanachama yeyote wa CHADEMA .

Wakati wa kampeni, Mbowe alipendelea kuvaa Nguo za khaki zenye sura ya gwanda kwa kuwa zilikuwa hazichafuki Sana na Muda wa kufua mara kwa mara haukuwepo. Alipofika eneo fulani kwa ajili ya kampeni za urais, wananchi walimshangilia na kumwambia kwamba amependeza Sana kuvaa zile nguo za kik**anda(Magwanda ya khaki). Aliwauliza wananchi, niendelee kuvaa mavazi ya kik**anda?? Maelfu ya wananchi wakajibu ndio oooooooo oooooooo. Mbowe akawaahidi wananchi kwamba atapeleka pendekezo k**ati kuu, Baraza kuu na Mkutano mkuu ili gwanda la khaki kuwa Vazi rasimi la Kamanda wa CHADEMA (mwanachama wa CHADEMA).Mbowe alifikisha pendekezo hilo k**ati kuu ya CHADEMA baadaye Baraza kuu na kupitishwa na Mkutano mkuu 2006 kuwa Vazi rasimi la chama.

Jakaya Mrisho Kikwete alishinda kwa kishindo uchaguzi mkuu ule kwa kupata ushindi wa 80.28% akifuatiwa na Prof Haruna Ibrahim Lipumba aliyepata 11.68% na Freeman Mbowe akishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 5.88%.

Miaka ya 2008,2009 CHADEMA chini ya Mbowe ilishiriki chaguzi ndogo ambazo ni Pamoja na Uchaguzi wa Jimbo la Busanda, Jimbo la Tarime na Mbeya vijijini. CHADEMA ilishinda Tarime na kushindwa Busanda huku jimbo la Mbeya vijijini Shambwee Sh*tambala alijiapisha kupitia ofisi yake ya Mawakili hali iliyopelekea CCM kupitia mgombea wao Luckson Mwanjali kuweka pingamizi dhidi ya Sh*tambala na hivyo CCM kupata ushindi dhidi ya wagombea dhaifu wa TADEA, TLP nk.
Mwaka 2009, Freeman Mbowe aligombea tena uenyekiti wa CHADEMA. Alipata mpinzani Zitto Zuberi Kabwe.

Zitto alitangaza kugombea uenyekiti wa CHADEMA taifa na kutoa sababu zake za kutaka nafasi hiyo katika gazeti la The Citizen la tarehe 26/08/2009. Zitto alieleza kwamba anaweza kuisaidia CHADEMA kushinda serikali za mitaa 2009 na uchaguzi mkuu 2010.Wazee wa CHADEMA walimuomba Zitto Kabwe kujitoa kugombea ili Freeman Mbowe kupita bila Kupingwa. Jambo hili liliwaumiza Sana wafuasi wa Zitto Kabwe akiwepo Habib Mchange, David Kafulila, Mtemelwa, Nyakarungu, Mtela Mwampamba nk.

Katika uongozi wa Freeman Mbowe mwaka 2004-2010 ilifanyika Operation maarufu Sana "OPERATION SANGARA KANDA YA ZIWA " ambayo ilihusisha Katibu Mkuu Dk Slaa, John Mnyika k**a mkurugenzi wa vijana, Zitto Kabwe na Viongozi mbalimbali.

Operation Sangara ilisababisha CHADEMA kuungwa mkono na kupata wabunge wengi Kanda ya ziwa katika majimbo ya Maswa Magharibi, Maswa Mashariki, Bukombe,Ukerewe Musoma mjini, Nyamagana, Ilemela,na majimbo mengine mengi mikoa ya Kagera, Shinyanga, Mwanza
Baada ya Mbowe Kushinda tena k**a Mwenyekiti wa CHADEMA (Kupita bila Kupingwa) mwaka 2009 aliongoza chama katika uchaguzi mkuu mwaka 2010 ambapo yeye aligombea tena ubunge jimbo la Hai na kupata kura 28,545(51.63%) huku mgombea wa CCM Godwin Kimbita akipata kura 23,349(42.17%)

Baada ya kushinda ubunge, Mbowe alipewa nafasi ya kuunda serikali Mbadala yaani Kambi Rasimi ya Upinzani Bungeni (KUB/KRUB) huku akisaidiwa na Naibu kiongozi wa kambi rasimi ya Upinzani Bungeni Zitto Zuberi Kabwe ambaye alivuliwa nyadhifa zake mwishoni mwa mwaka 2013, Mnadhimu wa kambi Rasimi ya Upinzani Bungeni Tundu Antipas Lissu nk. Mwaka 2010 mpaka mwanzoni mwa mwaka 2014 Mbowe aliunda serikali Kivuli ya Baraza la mawaziri vivuli (Shadow government) yenye mawaziri vivuli (Shadow ministers) kutoka CHADEMA pekee yake na Mwaka 2014 Mawaziri vivuli waliongezwa kutoka vyama vya NCCR MAGEUZI na CUF.

Kati ya mwaka 2010 mpaka 2014 , Chini ya uongozi wa uenyekiti wa Mbowe, Chaguzi ndogo zimefanyika za udiwani na ubunge. Majimbo ya uchaguzi mdogo wa ubunge ulifanyika katika majimbo ya Igunga, Chalinze, Arumeru Mashariki, Kalenga huku CHADEMA ikishinda jimbo moja la Arumeru Mashariki na mengine kuangukia mikononi mwa CCM

Katika kipindi hicho hicho cha uongozi wa Mbowe 2010 - 2014, CHADEMA imefanya Operation za kichama ikiwepo Vuvuvugu la Mabadiliko (Movement For Change-M4C),CHADEMA ni Msingi, Pamoja DAIMA. Operation hizo zilileta changamoto kubwa kwa siasa za CHADEMA mfano kejeli ya "COPPER TATU KATA TATU" operation ambayo kwa kiasi kikubwa ilikua ni kudhibiti madhara zaidi ya kufukuzwa Zitto Kabwe ambaye vijana wake walifanya Kazi kubwa kuhujumu CHADEMA Kwa njia halali na za nuruni, gizani na mafichoni ikiwa ni Pamoja na kuchoma bendera za CHADEMA, kadi, kushusha bendera za CHADEMA na kupandisha za ACT Wazalendo na CCM, kutoa matamko ya kupinga CHADEMA na Viongozi, matusi na kejeli nyingi.Hata hivyo Operation hizo zimesaidia CHADEMA kushinda serikali za mitaa nchi nzima ikiwepo kusini pamoja na uchaguzi mkuu mwaka 2015 ambapo CHADEMA na UKAWA kwa ujumla imevuna majimbo Mtwara, Lindi, Tabora, Tanga, Dar Es Salaam nk ambazo zilikuwa ngome za CCM.

Pia ni kipindi hiki, CHADEMA iliungana na vyama vingine vya CUF, NCCR, ND NA DR ingawa kilijitoa baadaye kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) mwezi Septemba 2013 na kuuimarisha zaidi mwaka 2014 na 2015

Septemba 14, 2014,Freeman Mbowe aligombea tena Uenyekiti wa CHADEMA akipambana na Gambaranyere Mwagateka. Katika uchaguzi huo, Freeman Mbowe aliibuka mshindi kwa kupata kura 789 huku mpinzani wake Gambaranyere Mwagateka akijipatia kura 20.

Disemba 14,2014 ulifanyika uchaguzi wa Serikali za mitaa nchi nzima kasoro Sumbawanga mjini na maeneo machache. CHADEMA na UKAWA kwa ujumla ilipata ushindi katika maeneo mbalimbali nchini hata ngome za Ccm. Mfano, Wilaya ya ILEJE ambayo mwaka 2009 CHADEMA ilikua na kijiji kimoja tu Cha Ikumbilo lakini katika uchaguzi wa Serikali za mitaa 2014 ilivuna vijiji 22 na CUF kijiji 1 na kuifanya Ileje kuwa wilaya ya tatu kuchagua CHADEMA Mkoa wa Mbeya. Hali ilikua hivyo Dar Es Salaam, Tanga, Mwanza, Kigoma, Mtwara, Lindi nk

Katika uchaguzi Mkuu mwaka 2015,Freeman Mbowe aligombea ubunge jimbo la Hai na kushinda kata zote 16 kasoro moja ya 17 ambayo uchaguzi uliahirishwa baada ya mgombea kufariki. Mbowe alishinda uchaguzi kwa kupata kura 51,124 huku mgombea wa CCM Dastan Mally akipata kura 26,996,Nuru Muhammed wa ACT Wazalendo akijizolea kura 315 na Ndashuka Issa wa APPT - Maendeleo akijinyakulia kura 279.

Katika nafasi ya Urais, Mbowe na k**ati kuu walishirikiana kumuingiza Edward Lowassa ndani ya CHADEMA na kupeleka Jina Lake Baraza kuu na hatimaye kupitishwa na Mkutano mkuu wa CHADEMA tarahe 04/08/2015 k**a mgombea urais wa CHADEMA anayeungwa mkono na UKAWA. Lowassa alijipatia kura zaidi ya milioni 6 kwa mujibu wa Tume ya uchaguzi chini ya Jaji Damian Lubuva huku CHADEMA ikisema imeshinda uchaguzi kwa 62% dhidi ya CCM na vyama vinginevyo.

Baada ya uchaguzi Mkuu 2015 , Freeman Aikael Mbowe aliunda Serikali mbadala (Shadow Government) au Kambi rasimi ya Upinzani Bungeni (KUB/KRUB) mapema mwaka 2016 ambayo inahusisha vyama vyote ndani ya UKAWA..... Happy Birthday Kamanda✌✌

******MWISHO******

Photos from UKAWA news updates's post 13/09/2018

Mwenyekiti wa chadema Taifa mh,Freman Mbowe Leo ameungana na waziri mkuu mstaafu Mh,Edward Lowasaa katika mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea ubunge wa jimbo la Monduli, Jonas Masiaya Laizer

Wanamonduli twendeni na Yonas Masiaya Laiser

13/09/2018

Anaandika Mbunge Tundu Lissu

Waheshimiwa habari za jioni na poleni kwa mapambano.

Nimeona clip ya Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Pala Kabudi akitoa 'lecture' bungeni juu ya masuala mbali mbali ya kisheria na kikatiba.

Clip hiyo imeanzia katikati, kwa hiyo ni vigumu kwangu kufahamu hoja ya msingi iliyomfanya azungumze alichozungumza. Hata hivyo, nimevutiwa na alichokisema juu ya mamlaka ya Rais ya kutunga sheria. Ndicho ninachotaka kukizungumzia kwa ufupi hapa.

Kabla sijafanya hivyo niseme tu kwamba Prof. Kabudi ni bingwa wa kuchapia, hasa kwa watu wasiomuelewa au walio wavivu wa kusoma au wenye uelewa wa juu juu, hasa wa masuala ya kikatiba na kisheria. Naomba hoja yake juu ya mamlaka ya Rais ya kutunga sheria k**a mfano.

Prof. Kabudi amedai Rais ana mamlaka ya kutunga sheria kwa kutumia decrees, instruments na proclamations. Hajafafanua matumizi ya hizo decrees, instruments na proclamations. Kwa kumsikiliza tu, mtu asiyejua mambo haya anaweza kufikiria, kimakosa, kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano ana mamlaka ya kutunga sheria juu ya jambo lolote, wakati wowote kwa kutumia hizo njia tatu. Ukweli ni kwamba mamlaka ya Rais ya kutumia instruments na proclamations yanahusu mambo mahsusi ambayo yametajwa kwenye Katiba. Instrument (waraka) au proclamation (tangazo) ni njia au namna tu anayotumia kutekeleza mamlaka yake. Katiba yenyewe ndio inayofafanua mamlaka gani yatekelezwe kwa kutumia instrument na yapi yatekelezwe kwa kutumia proclamation.

Kwa mfano, Rais ana mamlaka ya kutangaza hali ya hatari kwa mujibu wa Katiba. Sasa Rais anatekeleza mamlaka hayo kwa kupitia tangazo (proclamation) ya hali ya hatari.

Tangazo hilo sio source ya mamlaka yenyewe, source ni Katiba na Sheria ya Ukasimishaji wa Mamlaka ya Uwaziri. Proclamation ni ushahidi tu kwamba Rais ametumia mamlaka yake ya kikatiba.

Mfano mwingine. Rais ana mamlaka kikatiba ya kuunda au kuvunja ofisi za umma, i.e. Wizara, n.k. Katiba yenyewe imeelekeza kwamba Rais atatumia instrument (waraka) pale anapounda Wizara, kufafanua majukumu yake, etc.

Maana ya kusema hivi ni kwamba k**a Katiba haijasema kwamba Rais atatumia utaratibu fulani katika kutekeleza jukumu lake fulani kikatiba, yeye hawezi kujiamulia kutumia utaratibu wa instrument au proclamation katika kulitekeleza jukumu hilo.

Kwa mfano, Rais hateui Majaji au Mawaziri au Wakuu wa Wilaya au Mkoa au Makatibu Wakuu wa Wizara au watendaji wa taasisi mbali mbali za umma kwa kutumia instruments au proclamations.

Kwa upande mwingine, Rais hana mamlaka kabisa, kwa Katiba ya sasa, ya kutunga sheria kwa kutumia decrees. Decrees (amri) ni Sheria zinazotungwa pale ambapo hakuna Bunge la kawaida kwa sababu yoyote ile. Mfano mzuri ni tawala za kijeshi au za kimapinduzi k**a ilivyokuwa Zanzibar kati ya miaka ya '64 na '79.

Sasa ilikuwaje Mwalimu Nyerere akatunga Sheria mbili kwa kutumia decree mwaka '64??? Jibu ni Mapinduzi ya Zanzibar ya Jan. '64, na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa Aprili ya mwaka huo huo.

Kwa sababu ya Mapinduzi, Bunge la kawaida la Zanzibar lilivunjwa na badala yake Baraza la Mapinduzi likajipa madaraka ya kutunga sheria kwa kutumia decrees.

Na mara baada ya Muungano kuzaliwa, hakukuwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya kutunga sheria zinazohusu masuala ya Muungano.

Hivyo Mwalimu Nyerere alipewa mamlaka hayo kwenye Hati ya Makubaliano ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ili kumwezesha kutunga sheria zinazohusu masuala ya Muungano wakati wa kipindi cha mpito mara tu baada ya Muungano.

Mamlaka hayo yalifikia mwisho wake mwaka '65 ilipotungwa Katiba ya Mpito ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tangu wakati huo Rais hana tena mamlaka ya kutunga sheria kwa amri (decrees).

Mwisho, ni muhimu kuelewa kwamba mamlaka ya Rais ya kutumia instruments na proclamations yanahusu tu mambo yaliyotajwa kwenye Katiba. Nje ya mambo hayo, Rais hana mamlaka anayoyazungumzia Profesa Kabudi.

13/09/2018

Maneno ya muasisi wa nchi yetu baba wa taifa Mwl. Julius K. Nyerere!
Mwenyezi mungu aendelee kumpumzisha kwa amani🙏

13/09/2018

JIHADHARI NA HII; KUTOKA BUNGENI!

13/09/2018

👇👇👇

12/09/2018

HELLO! UKONGA
NAITWA ASIA DAUDI MSANGI
Mgombea ubunge Jimbo la Ukonga, nakutakia siku njema huku nikikukumbusha kuwa tarehe 16|9|2018 ni siku ya kupiga kura, hivyo naomba mjitokeze kwa wingi ili mnipigie kura niwe Mbunge wa Jimbo letu la Ukonga, yote niliyoahidi na ninayoendelea kuahidi katika mikutano yangu ya kampeni hakika nitatekeleza kwa uadilifu na uaminifu Mkubwa
Naomba kura yako.

Note: Tupige Kura kwa wingi, Tulinde Kura na Tulinde matokeo yasichakachuliwe!

11/09/2018

Mgombea wa Ubunge jimbo la Ukonga kupitia CHADEMA Asia Msangi akiwaeleza Wana Ukonga kwanini yeye "Nimesoma Kitunda toka mdogo, najua kero zinazotukabili Wana Ukonga, kuanzia miundombinu ya barabara kuunganisha kata na kata huwa mbaya zaidi wakati wa mvua" Asia Msangi.

11/09/2018

HELLO! UKONGA
NAITWA ASIA DAUDI MSANGI
Mgombea ubunge Jimbo la Ukonga, nakutakia siku njema huku nikikukumbusha kuwa tarehe 16|9|2018 ni siku ya kupiga kura, hivyo naomba mjitokeze kwa wingi ili mnipigie kura niwe Mbunge wa Jimbo letu la Ukonga, yote niliyoahidi na ninayoendelea kuahidi katika mikutano yangu ya kampeni hakika nitatekeleza kwa uadilifu na uaminifu Mkubwa
Naomba kura yako.

Note: Tupige Kura kwa wingi, Tulinde Kura na Tulinde matokeo yasichakachuliwe na mkoloni mweusi.

07/09/2018

Mbunge Anaeongoza Binadamu na Wanyama Pale mikumu Mh. Joseph Haule () katika picha ya pamoja na Baba yake Mzazi Aliefikwa na Umauti Mchana wa Leo😢

Pole sana Mh. Tupo nawe katika kipindi hiki kigumu. Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake libarikiwe🙏
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un🙏

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Address


Mbezi Beach, Dar Es Salaam
Dar Es Salaam
22771