WANAWAKE,WANAWAKE,WANAWAKE!
Nimewaita mara tatu enyi mama zetu,bibi zetu,dada zetu wazazi na walezi wetu!
Uko wapi utu wenu?
Iko wapi thamani ya maungo yenu?
Nini hasa nafasi ya tupu zenu?
Huu ndio uhuru na usawa mnaoutaka?
Wako wapi tena wale wanawake waadilifu?
Wazazi na walezi na walimu wa mwanzo wa vizazi vyetu?
Wenye kutunza na kulea wana kwa mafunzo ya kujua stara na heshima?
Wale kina mama wa kuwatawaza na kuwavalisha mabinti na vijana wetu!
Wale wenye kujua kuwa utupu ni siri ya thamani kupita hazina ya wafalme wa dhahabu na almasi!
Wenye kujua kuwa sehemu za siri za mwanamke ni hekalu la uhai na chanzo cha maisha!
Wenye kutambua kuwa wao ni si wazazi na walezi pekee bali ni waumbaji na wetengenezaji wa jamii bora!
Wenye kujua kuwa uke ni lango la utukufu na chanzo cha amani na furaha hata penye dhiki ya njaa na vita!
Kwani nini hasa lengo lenu la kutuonesha matiti,mapaja,vitovu,makalio na hata mashavu ya uke au uke wenu kabisa?
Ya nini kujianika k**a mishikaki ya miamia ya pale stendi?
Huu ushamba wa kutaka likes,comments na sifa nyingi mitandaoni umetifikisha pabaya sana!
Kumbuka utasifiwa kwa kuwa na umbo zuri na matiti yaliyonona na hata kununuliwa na watu wakivutiwa na uzuri wako,utapa hizo sifa,fedha na kutumika kadri watakavyo waja,ila jua nafasi yako kwao ni sawa na ndala ya chooni ambayo haistahili kufika hata uani!
Kukubali kwenu kutumika kwenye picha na video mkitingisha na kuonesha utupu wenu kwa kigezo cha kutaka umaarufu na fedha vinaua UTU WENU! Utu wa mtu haununuliwi,nyinyi ni majabari,ninyi ni mak**anda na wapambanaji hodari wa kulinda hiki kizazi,k**a ninyi mnashindwa kusimama kwenye nafasi zenu ndio chanzo cha kuongezeka kwa uvunjifu wa maadili vikiwemo ufisadi,ushoga,usagaji na wizi!
Nadhani nguvu mnayoitumia kupigania haki sawa na uhuru wa kijinsia inapotea bure ikiwa tu mtaendelea kushindwa kujisimamia wenyewe kwenye maadili!
Niliwahi kuandika kuwa Dunia inatumia nguvu kumdhalilisha mwanamke bahati mbaya wanawake nao mnashiriki kwa nguvu zenu zote udhalilishaji wenu!
Nadhani ni vyema mkaanza kuyatazama mambo kwa mtazamo wa aina nyingine,k**a mnadhani nyie ni wadada na wamama warembo basi jua kesho mtakuwa mabibi wa hovyo kwa tabia zenu za leo!
Mnadhani zamani hakuku2a na makahaba?hakukuwa na warembo? Hakukuwa na mashababi? Acheni ushamba haya yana mwisho.
Nimeandika nikijua mpo mtakaopuuzia na wengine kunitukana ila poa tu! Mradi nshawaambia ukweli.
Mizambwa Midauli Midavudavu
26/11/2023
Tanzania - Afrika
Sauti Ya Moyo Wangu
The page is all about sharing different matters in all sphere of life as a way of getting more knowl
06/03/2020
Chakula cha moto hakizengewi na nzi
10/02/2019
Naomba jibu wadau
02/02/2019
Somo
Ubinafsi ukizidi sana unageuka kuwa roho mbaya
"Unachoweza kufanya ni kile unachoweza kufanya,lakini fanya kila unachoweza kufanya kwa uwezo wako wote!"
Wakutulinda wanatuua
Sema lolote la moyoni asubuhi ya leo
10/09/2017
Udikteta
19/06/2017
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Telephone
Website
Address
Dar Es Salaam