Hadithi za Mapenzivichekeshokick za Townhadith za ukweli na uongo

Hadithi za Mapenzivichekeshokick za Townhadith za ukweli na uongo

Share

Utapata Habari zote za Town|story za mapenzi|Udaku|kick za town|Story za chemba|na kila kitu

20/10/2021

IMEANDIKWA NA : ATUGANILE MWAKALILE

*********************************************************************************

Simulizi : Nyumba Ya Maajabu
Sehemu Ya Kwanza (1)

Ilikuwa ni siku ya furaha sana walipohamia kwenye hii nyumba nzuri na ya kupendeza, tena iliyovutia katika macho ya watu wengi sana.
Mke alisikika akimuuliza mume wake,
“Ibra, uliwezaje kuwekeza pesa nyingi za kununua nyumba nzuri k**a hii?”
“Mke wangu Sophia, kwakweli mambo ya Mungu ni mengi sana, hata mimi sikutegemea kupata nyumba k**a hii kwa ile pesa ambayo nilikuwa nayo. Kwakweli tushukuru tu kwa kupata mwanga wa maisha”
“Nadhani sasa mipango yetu itatimia mpenzi”
“Ndio mke wangu kwa hapa lazima mipango itimie”
“Hivi tulipanga kuzaa watoto wangapi vile?”
“Watatu tu wanatosha mke wangu”
“Baby kwa jinsi nyumba ilivyokubwa kwanini tusifanye wanne!”
“Wewe ndio mzaaji mke wangu kwahiyo vyovyote tu inawezekana”
Sophia akakumbatiana na mume wake kwa furaha kwani hii ilikuwa ni moja ya ndoto zake kwenye maisha.

Baada ya wiki moja, Sophia aliamua kwenda kuwatembelea majirani zake wa sehemu aliyokuwa akiishi mwanzoni. Alifika na kuwakuta wakiendelea na shughuli za hapa na pale k**a kawaida, moja kwa moja aliamua kwenda kwa rafiki yake wa pekee Siwema ambapo alikaribishwa vizuri sana na rafiki yake huyo.
“Yani Sophia k**a usingekuja kunisalimia kwakweli ningekuona ni mtu wa ajabu sana.”
“Hivi Siwema naachaje kuja kukusalimia wewe! Nitakuwa nimerogwa basi, tena nitakuwa ni binadamu asiye na wema wala shukrani”
“Eeh hebu kwanza niambie shoga yangu mmehamia wapi maana si kwa mbwembwe zile za kuondoka hadi vigoda vyako umeacha”
“Shoga mwenzangu, yani wewe ni shoga yangu wa damu kwakweli na kukuficha siwezi. Kwakweli mwenzio nadhani kuna vitu Ibra alikuwa ananificha”
“Kivipi? Na vitu gani hivyo alivyokuwa anakuficha?”
“Hivi unaweza kuamini kwamba Ibra amenunua nyumba na gari!”
“Mmh kwa hela gani? Katoa wapi hiyo pesa ya kununua nyumba na gari?”
“Tena ninavyokwambia nyumba ni nyumba haswa shoga yangu wala sio nyumba uchwara, nitakupeleka na wewe ukajishangalie maajabu ya mume wangu Ibra”
“Mmmh kwahiyo shoga biashara ya mamantilie hufanyi tena?”
“Naanzaje kufanya biashara ya mama ntilie kwenye nyumba ile! Shoga hujaiona na wala sijisifii tu, kwakweli Ibra ana pesa, mpango wangu kwasasa ni kuzaa tu nicheze na wanangu pale maana nikichelewa nitakuta mwana si wangu”
“Shoga tusiandikie mate wakati wino upo, ujue umenitamanisha sana, naomba twende sasa hivi na mimi nikajishuhudie huo mjengo. Ngoja nijiandae fasta twende.”
Sophia akakubaliana na Siwema pale kwahiyo akamsubiri ajiandae ili aweze kwenda nae.

Siwema na Sophia walifika kwenye nyumba husika ambapo nje tu ya nyumba hiyo Siwema alibaki kushangaa na kuduwaa kwani hakutegemea k**a ile nyumba ipo vile k**a alivyoikuta.
“Khee jamani Sophia mbona umeokota dodo kwenye muharobaini shoga yangu, hebu jibebeshe mimba mapemaa maana hapa utashangaa ushaibiwa shoga yangu”
“Yani hapa ninachotaka ni kuzaa tu, yani toka nimeuona huu mjengo na dawa za uzazi wa mpango nikaziacha pale pale saivi nawaza watoto wa kucheza nae kwenye nyumba hii”
“Hongera sana shoga yangu ila kuwa makini na Ibra maana asije akakuletea mke mwenza bure”
“Thubutuu huyo mke mwenza atapitia mlango gani!! Labda sio Sophia niliyepo humu ndani”
“Nakuaminia Sophia, k**a uliweza kumchunga Ibra kule uswahilini ndio ushindwe kumchunga kwenye huu mjengo”
“Hapo sasa, yani hapa Ibra hazungushi amefika hapa Kigoma mwisho wa reli”
Sophia alikuwa akifurahi tu na shoga yake huyu, na leo walipika pamoja na kula pamoja hadi joini ambapo mume wa Sophia aliwasili kutoka kwenye mihangaiko yake ambapo alimkuta Siwema pale kasha Siwema akawapa hongera zao na kuwaaga.
“Hongera sana shemeji yangu Ibra, ila mimi ndio naomdoka shemeji”
“Mmh shemeji jamani ndio haraka haraka hivyo!”
“Shemeji nilikuwepo hapa tangu muda ila nitakuja tena maana ndio nishapapenda tayari ila saizi wacha niende”
Basi Ibra hakuwa na jinsi yoyote zaidi ya kumuaga tu huyu Siwema.
Kisha Sophia akatoka na kwenda kumsindikiza rafiki yake huyu,
“Kwakweli Sophia usizembee, pale ndio umshikirie vizuri Ibra yani umgande k**a ruba maana ule mjengo si mchezo shoga yangu. Yani wambea wa mtaa watanikoma nitakavyokuwa najidai kuhusu wewe Sophy.”
Sophia akacheka tu kwani alikuwa akifurahia kile alichokuwa akiambiwa na Siwema.
“Usicheke tu Sophy ila yafanyie kazi maneno yangu”
“Ondoa shaka dada, mambo yataiva tu maana hata mimi nimetamani kuwa na watoto kwasasa”
Wakabadilishana mawazo pale kasha Siwema akapanda daladala na kuagana vyema huku Sophia akisisitiza kuwa awasalimie majirani zao wengine.

Sophy alirudi nyumbani kwake, kwavile giza nalo lilianza kuingia ikabidi aandae chakula cha usiku, na kilipokuwa tayari alikaa na mumewe na kuanza kula huku wakitabasamu.
“Mmmh Sophy muda wote unatabasamu tu mke wangu”
“Hivi naachaje kutabasamu Ibra!! Bahati tuliyoipata ni kubwa sana mume wangu kwakweli sikutegemea k**a ipo siku tutaishi kwenye nyumba nzuri na kubwa k**a hii, si unajua tulizoea chumba kimoja tu yani jiko hapo hapo, viti, vyombo, kitanda hapo hapo yani shaghalabhagala lakini sasa hivi eti tunaishi maisha ya kitajiri namna hii lazima nitabasamu mume wangu.”
Wak**aliza kula kasha Sophy akatoa vile vyombo na kuvipeleka jikoni huku akitaka kuviosha kwanza ndimbo aende kulala na mumewe, ila Ibra alimfata kule jikoni na kumwambia,
“Sophy mke wangu, vyombo utaviosha kesho bhana hebu twende tukalale”
Sophy akatabasamu kisha akaacha vile vyombo na kuongozana na mumewe hadi chumbani ambako muda mwingi walionekana wakitabasamu.
Kisha wakaenda kuoga pamoja na kurudi kitandani, Ibra alimkumbatia Sophy na kumuuliza tena,
“Hivi ulisema tuzae watoto wangapi vile?”
“Wanne mume wangu au wewe hupendi”
“Mmmh hakuna kitu ambacho unakipenda wewe halafu mimi nisikipende, si unajua jinsi nikupendavyo Sophy! Yani mimi na wewe letu ni moja mke wangu”
“Tena napenda wawili wawe wa k**e halafu wawili wa kiume”
“Wow ni mpango mzuri sana hakuna tatizo, tutazaa kadri Mungu atakavyo tujaalia Sophy wangu.”
Wakatabasamu kisha wakalala k**a kawaida.

Kulipokucha, k**a ilivyoada Ibra aliamka mapema sana kisha akajiandaa kwaajili ya kwenda kwenye kazi zake, Sophy alitaka kujaribu kuinuka ili kumuandalia mambo mbalimbali mumewe ila ibra alimzuia na kumtaka mkewe aendelee kupumzika tu ambapo naye alifanya hivyo kwani alielewa ni jinsi gani Ibra alimpenda.
Kwenye mida ya saa mbili asubuhi, Sophy nae aliamka na kwenda kuoga ili kujiandaa kwa mambo ya hapa na pale.
Akaenda jikoni kwa lengo la kutaka kuosha vyombo vya jana na kujiandalia chakula cha asubuhi, ila alishangaa kuona vyombo vilishaoshwa na vilipangwa vizuri kabatini.
Hali hii ikamfanya Sophia ajiulize kuwa huenda Ibra alimzuia kuamka muda ule ili afanye kile kitu cha kumsahangaza. Kwakweli Sophia alitabasamu kwa jambo hili kwani aliweza kuona ni jinsi gani Ibra anampenda sana.
“Najua Ibra ananipenda sana ila safari hii kazidisha mapenzi jamani mmh yani amefikia hatua hata ya kunitaka mimi nilale halafu yeye akaosha vyombo, haya ni mahaba tena motomoto kwakweli nina kila sababu ya kumzalia watoto Ibra wangu. Kipindi kile nilikuwa najibana kuzaa sababu ya maisha duni ila kwasasa nina kila sababu ya kuzaa kwakweli.”
Kisha akajiandalia chakula pale na kuanza kukila halafu naye akatoka kwa lengo la kwenda kwenye mihangaiko yake mbalimbali.
Wakati yupo nje ya nyumba hiyo kuna mmama alipita na kumsalimia Sophia kisha Yule mama akamuuliza Sophia k**a ndiye anayeishi mule ndani,
“Unaishi humo ndani dada?”
“Ndio mama”
Sophia akahisi kuwa huyu mama labda anamuona kuwa haendani na hiyo nyumba, ikabidi amuulize
“Kwani vipi mama yangu! Kuna tatizo?”
“Hapana ila sisi ni majirani kwahiyo ni vyema tukafahamiana, mimi naitwa mama Jane na wewe je?”
“Mimi naitwa Sophia, na hapa naishi na mume wangu yeye anaitwa Ibra”
“Basi ni vizuri, karibu kwangu nyumba ya jirani tu hapo”
“Asante nitakaribia”
“Karibu sana, usiogope kitu sisi ni majirani tu na ni vyema kufahamiana ingawa kufahamu watu waishio humo huwa ni ngumu sana”
“Usijali utatufahamu tu”
Kisha Sophia akaagana na huyu mama halafu yeye kuendelea na safari zake.

Jioni ya siku hiyo Sophia akiwa ndani na mumewe akamsimulia kuhusu huyo mama aliyekutana nae wakati anatoka na vile alivyozungumza nae,
“Kwakweli ni vizuri kufahamiana na majirani ukizingatia tangia tumefika hapa hakuna jirani tuliyemsogelea kumsalimia”
“Basi tutafanya hivyo mume wangu. Ila kitu kingine sasa mmmhh”
Sophy akatabasamu kwanza kabla ya kuongea na kumfanya Ibra amuulize,
“Kitu gani hiki mpaka umeguna Sophy?”
“Mmh naona mapenzi yamenoga mume wangu hadi leo umeosha vyombo!”
Ibra akacheka kisha akasema,
“Mmh acha kunichekesha Sophy yani na uvivu huu mimi nikaoshe vyombo kweli!!”
“Sasa nani kaviosha vile vyombo asubuhi?”
“Nikuulize wewe uliyebaki nyumbani”
Sophia akakaa kimya kwa muda kwanza kwani hakuelewa hapo.

Sophia akakaa kimya kwa muda kwanza kwani hakuelewa hapo, akamuangalia mumewe kanakwamba amwambie kuwa alichokuwa anakisema kilikuwa ni utani tu kisha akamwambia tena,
“Acha masikhara Ibra”
“Wewe ndio uache masikhara, unajua fika kuwa mimi ni mvivu wa kimataifa haya sasa huko kuosha vyombo ningeanzia wapi? Hebu kaandae chakula tule kwanza”
“Lakini Ibra….”
“Lakini nini Sophy? Wewe kaandae chakula tule bhana, mada zingine achana nazo usifikirie ni rahisi hivyo mimi kuosha vyombo”
Sophia akaenda jikoni huku akiwa na mawazo sana ila kuna wakati alihisi kuwa Ibra anatania tu kwani kule ndani walikuwa wao wawili tu kwahiyo akahisi kuwa ni lazima Ibra ndio aliosha hivyo vyombo ila anajigelesha tu, alijiaminisha hivyo huku upande mwingine akiwa na mashaka kiasi.
“Kesho nitampigia simu Da’ Siwema nimsimulie, Yule ni mtu mzima anaelewa vizuri sana”
Kisha akaendelea na uandaaji wake wa chakula cha usiku.
Akapeleka mezani na kuanza kula na mumewe Ibra,
“Yani leo nimechoka Sophy maana nimejikuta nikiwa na kazi nyingi sana”
“Pole mume wangu ila ndio ukubwa huo”
“Kweli kabisa ukubwa jalala maana sio kwa kuchoka huku”
Walipomaliza kula, leo Sophia hakutaka kuacha vyombo vichafu kwahiyo alienda kuviosha na kuvipanga kisha kwenda chumbani kulala na mume wake ambapo alimkuta ameshalala tayari.
“Mmmh kweli leo Ibra kachoka jamani maana yupo hoi kabisa”
Kisha na yeye akatafuta usingizi pale na kulala, alipopitiwa na usingizi tu akajiwa na ndoto.
Kwenye ndoto hii alijiona yeye akiwa mjamzito ila mumewe alionekana kutokuifurahia kabisa ile mimba na alionekana kuongea maneno machafu sana ya kumkaripia,
“Aliyekwambia ubebe mimba nani? Na utaenda kuzalia kwake huyo mtu, sitaki ujinga mimi”
Sophia akashtuka sana kutoka kwenye ule usingizi huku akiilaani ile ndoto na kuona kuwa ni kitu cha ajabu sana kwake kwani haikuwa rahisi kwa Ibra kuikana mimba yake kiasi hicho ila ndoto hiyo ilimfanya asipatwe na usingizi tena hadi panakucha.

Ibra alipoamka tu, Sophy nae alikuwa macho na swali la kwanza ambalo Sophy alimuuliza Ibra ilikuwa ni kuhusu mimba.
“Hivi kwa mfano mimi nikiwa na mimba yako je utafurahi mume wangu?”
“Sophy, ninavyokupenda hivi naachaje kufurahi? Pia nahitaji mtoto Sophy wangu, na mimi napenda niitwe baba. Nakupenda sana mke wangu, najua watoto ndio watakamilisha furaha yetu mpenzi.”
“Asante Ibra”
Kisha Ibra akaanza kujiandaa pale halafu akamuaga Sophy kwa kumbusu kwernye paji la uso.
Ibra alipoondoka tu, Sophy nae akaamka na kwenda kukaa sebleni ili kujipotezea mawazo mbalimbali huku akiona wazi kuwa ile ndoto ni uchizi tu na ni kitu cha kusadikika.
“Ndoto zingine k**a zimetumwa loh! Ndoto gani sasa ile? Yani Ibra kabisa akane mimba thubutuu, yani ile ndoto ishindwe na ilegee ujinga ujinga sitaki.”
Muda ulipoenda kidogo akampigia simu Siwema na kuanza kuzungumza naye kuhusu kilichotokea jana na vile ambavyo Ibra alimjibu kuwa hakuosha hivyo vyombo.
“Hayo ndio mahaba mdogo wangu, mwenzako Ibra anakupima tu lakini vyombo kaosha mwenyewe, we unadhani ataosha nani wakati ndani mpo wawili tu?”
“Ndio hapo dada nimeshindwa kuelewa kwakweli maana mimi nimekuta vimeoshwa halafu ni yeye aliyesema nisivioshe halafu anakataa kuwa hajaviosha loh!”
“Anakuchanganya akili tu huyo mdogo wangu, kwani wanaume hujawajua tu, wanapenda kutupima Sophy mdogo wangu. Hata usiwe na shaka mwaya mwenzio saivi anakuonyesha mahaba kimya kimya”
“Kweli dada haya ni mahaba maana ila hapendi kuosha vyombo, hata niumwe ataviacha hadi nipone ila kuona ameosha safari hii tena nikiwa mzima kabisa kweli ni mahaba”
“Ndio mapenzi hayo mdogo wangu hata usistaajabu sana, hapo ndio kupendwa yani wewe jiongeze tu.”
Sophia akafurahia sana ushauri aliopewa na Siwema kwani aliona ushauri huo ukimfaa sana, kisha akaagana nae kwenye simu na kuendelea na mambo mengine.
Wakati akifanya shughuli zake za hapa na pale mule ndani, akasikia hodi na kwenda kufungua mlango ambapo alimkuta Yule mama ambaye walikutana siku ya nyuma huku akiwa ameambatana na binti aliyeonekana kufanana nae sana, Sophia akawakaribisha vizuri sana watu hao ndani kwako huku akitabasamu,
“Karibuni sana jamani”
“Asante tumekaribia Sophy”
Wakaingia ndani huku Yule mama akianza utambulisho kwa binti aliyeongozana nae,
“Huyu ni binti yangu anaitwa Jane”
“Wow ndiomana umefanana nae sana mama, hongera kwa kuwa na binti mzuri”
Huyu mama akatabasamu kidogo kisha akaendelea,
“Nimeona ni vyema akufahamu jirani yetu ili hata siku akiwa mbweke nyumbani basi aje akutembelee, unajua huyu mtoto ametoka kumaliza kidato cha nne kwahiyo tunangoja matokeo tu kwasasa. Mara nyingi anashinda nyumbani kwahiyo akija kuongea ongea hapa si vibaya.”
“Umefanya jambo jema mama maana hata mimi huwa na upweke sana maana huwa nashinda mwenyewe mahali hapa, pia hongera sana Jane kwa kuhitimu kidato cha nne.”
“Unampa hongera ya bure tu huyu, akili yake yenyewe sijui k**a atafaulu huo mtihani, na akifeli ndio atakaa nyumbani atafute mume aolewe tu”
“Jamani mama usiseme hivyo inakuwa k**a unamuombea mabaya mtoto”
“Mabaya kajiombea mwenyewe hata sio mimi, mtu gani alikuwa anajijua kabisa kuwa ana mitihani ila ndio tamthilia sijui michezo kila kitu anakijua yeye na hatma yake inakuja kwakweli naona kabisa zero ikimuangalia.”
Jane alionekana kuwa kimya kabisa kwani ilionyesha wazi hakupendezewa na maneno ya mama yake, ili kuondoa ule mzozo ilibidi Sophia abadilishe mada kisha akaenda jikoni na kuwaletea wageni juisi huku wakizungumza mawili matatu.
Muda kidogo Ibra alirudi hata kumshangaza Sophia kwani alionekana kuwahi sana siku hiyo na alionekana kuwa na uchovu.
Sophia akamkaribisha mumewe na kumtambulisha kwa wale wageni ambao walifahamiana na kusalimiana, ingawa Ibra alikuwa amechoka ila alivunga kidogo kwenda chumbani ili wale wageni wasijihisi vibaya, ila huyu mama nae aliaga muda ule ule kwahiyo Sophia akatoa zile glass na kupeleka jikoni kisha akamuaga mumewe na kwenda kuwasindikiza wale wageni, ambapo Sophia alienda nao hadi nyumbani kwao ili kuweza kupafahamu wanapoishi watu hao.
Sophia aliweza kuona mazingira ya uswahili anayoishi huyu mama ila hakushangaa sana kwavile ndio mazingira ambayo hata yeye amekulia na ameyaishi kwa kipindi kirefu sana.
“Sophia, ukiwa na tatizo usisiste kuja, hapa ni k**a nyumabani kwenu tu kwahiyo usiogope chochote”
“Usijali mama tupo pamoja”
Sophia hakukawia sana kwani aliaga na kuondoka.

Aliporudi nyumbani kwake hakumkuta Ibra pale sebleni na moja kwa moja akahisi kuwa Ibra atakuwa ameenda chumbani kupumzika tu, kisha nae akaenda chumbani alipo Ibra kwani alipenda kujua ni kwanini mumewe amechoka kiasi kile.
Alimkuta Ibra amejilaza kitandani, akamfata na kumsogelea karibu mumewe kisha akakaa pembeni yake na kumuuliza kuwa tatizo ni nini,
“Vipi tena Ibra mume wangu, nini kimekukumba baba?”
“Kwakweli hata sielewi ila nimechoka mwili na viungo vyote”
“Pole sana mume wangu, ngoja nikuandalie chakula ule kwanza ndipo ulale”
“Usijali kuhusu hilo, nilishaenda jikoni nimepakua chakula na nimekula tayari”
“Dah nisamehe mume wangu jamani”
“Usijali kitu mke wangu, wale ni wageni wetu sote kwahiyo hata usijali na ndiomana hata mimi sikuona tataizo kwenda jikoni na kujipakulia chakula”
“Pole sana mume wangu, basi ngoja nikakuandalie maji uoge”
“Kwakweli sijisikii kuoga kwasasa subiri nipumzike kwanza ndio nitaoga”
Sophia alitulia kwa muda akiitafakari hali ya mume wake kwani haikuwa kawaida kabisa kwa Ibra kuwa vile alivyokuwa.
Alienda sebleni huku akihisi kuwa huenda Ibra akawa na malaria ila ndio hivyo anajikaza kwavile ni mwanaume, kisha akaelekea jikoni na kufunua sofuria alilopikia chakula na kukuta kweli kilipakuliwa kwamaana hiyo ni kweli Ibra amekula kile chakula kisha akaangalia Ibra alipoweka sahani aliyotoka kula nayo ila hakuona sahani wala nini hapo ndipo aliposhangaa na kwenda tena sebleni kuwa huenda ameiacha huko ila hakuona sahani yoyote chafu, wazo likamjia kuwa aangalie na zile glasi ambazo wageni wamenywea juisi ila hakuziona pale zaidi aliziona zimeshawekwa kabatini tena zikiwa safi kabisa,
“Mmh huyu Ibra si anaumwa huyu sasa iweje ameosha vyombo vyake alivyolia na zile sahani jamani wakati mtu ni mgonjwa? Haya ni maajabu mapya kwangu, sasa nitamuulizaje na anaumwa? Ila lazima nimuulize?”
Sophia akatoka jikoni na kuelekea chumbani tena alipo Ibra kwa lengo la kumuuliza kulikoni maana hakuelewa kabisa.
Alimkuta Ibra akiwa bado anagalagala tu kitandani kwani hata usingizi haukumjia, kisha akamuuliza,
“Mume wangu leo umechoka sana ila kwanini umeosha vyombo ulivyolia chakula?”
“Sophy, toka lini hunijui mimi jamani! Mimi naoshaje vyombo mke wangu, kwanza naumwa halafu wewe unaniletea habari zingine kwanini unakuwa hivyo Sophy?”
“Samahani mume wangu ila ningependa twende hospitali”

“Sijisikii kwenda hospitali kwakweli, tafadhali niache nipumzike”
Sophia hakumuelewa Ibra kabisa na akahisi huenda Ibra ana malaria ambayo imempanda kichwani na ndiomana amekuwa vile alivyokuwa.
Sophia aliamua kuinuka tena ili atoke mule chumbani ila kabla hajafika malngoni alijihisi kichefuchefu na kumfanya aanze kukimbilia chooni ili atapike ila kabla hajafika chooni alijikuta kashatapika tayari kwahiyo chooni alienda k**a kumalizia tu na alitoka akiwa amechoka sana ila hakuweza kuvumilia kuangalia yale matapishi yake yaliyotapakaa chumbani kwao karibia na mlanngo wa chooni, hivyobasi Sophia akaenda jikoni kuchukua tambala na maji kwa lengo la kufuta matapishi yale.
Ila aliporudi chumbani ili afute alikuta yale matapishi yalishafutwa na pale palishakaushwa kabisa, kwakweli Sophia alichoka gafla, akamuangalia Ibra pale kitandani ila Ibra alionyesha kutokuwa na habari yoyote kwani alikuwa amejilaza vile vile.

Ila aliporudi chumbani ili afute alikuta yale matapishi yalishafutwa na pale palishakaushwa kabisa, kwakweli Sophia alichoka gafla, akamuangalia Ibra pale kitandani ila Ibra alionyesha kutokuwa na habari yoyote kwani alikuwa amejilaza vile vile.

Sophia hakuelewa kwakweli yani hakuelewa kabisa, akaenda tena pale kitandani alipokuwa amejilaza Ibra na kumshtua, ambapo Ibra aliongea kwa kulalamika,

“Sophia jamani mbona hivyo mke wangu? Kwanini unanifanyia hivi lakini si nimekwambia kuwa najisikia vibaya! Sasa kwanini hutaki mwenzio nipumzike jamani unanifanyia mambo ya ajabu, kwanini kunishtua shtua kila muda?”

“Samahani Ibra lakini nani kazoa matapishi yangu?”

“Matapishi?”

“Ndio, kwani hukunisikia wakati natapika?”

“Sijakusikia bhana, unanisumbua tu Sophy hebu acha nipumzike”

Ibra akageuka tena na kulala, kwakweli Sophia hakuelewa chochote alijikuta akijishika tama tu kwa mawazo kwani aliona k**a vile Ibra anamchanganyia mada huku nayeye akizidi kujiuliza kuwa k**a sio Ibra anayefanya hayo je yatakuwa yanafanywa na nani? Hapo ndio ilikuwa ngumu kabisa kwa yeye kuelewa.

Akajikuta akikaa pale kitandani huku akitafakari kwa muda mrefu sana bila ya kupata majibu hadi akapata wazo la kumpigia simu tena Siwema ili amuulize ila aliona k**avile ni kumsumbua tu huyo Siwema, kwahiyo akatulia kimya kwa muda mrefu kidogo kisha akainuka pale na kuelekea jikoni kwa lengo la kuandaa vizuri mlo wa usiku.

Akiwa jikoni alijiuliza sana kitu kilichopelekea yeye kutapika ni nini,

“Hivi ni kwanini nimetapika ikiwa siumwi wala nini? Ni kitu gani kimepelekea mimi kutapika?”

Alijiuliza bila ya kupata jibu la aina yoyote ile kwahiyo akaamua kuandaa chakula tu.

Alipomaliza kuandaa chakula alitoka jikoni na kuelekea sebleni ambapo alimkuta mumewe amekaa na kwakweli alionekana kuwa sawa kabisa kwasasa tofauti na mwanzo,

“Khee Ibra kumbe umeamka tayari!”

“Ndio nimeshaamka”

“Eeh unajisikiaje na hali!”

“Nipo salama kabisa mke wangu”

“Basi ngoja nikakuandalie maji ya kuoga”

“Hata usijali mke wangu nimeshaoga labda ulete chakula tule”

Basi Sophia hakutaka kuhoji zaidi kwahiyo akaenda kuleta chakula kisha yeye na mumewe wakaanza kula chakula hicho huku wakizungumza mambo mawili matatu,

“Kwahiyo Ibra saivi unajiona umepona kabisa!”

“Ndio nimepona kwani nilikuwa naumwa sana eehh!”

“Yani hadi mimi ulinitia mashaka mume wangu mpaka hofu ilinitawala kabisa”

“Hata usiwe na mashaka mke wangu maana mimi ni mzima kabisa kabisa”

“Basi vizuri mume wangu k**a ndio hivyo”

“Ila nakushukuru sana Sophy kwa mapenzi yako unayonionyesha na jinsi unavyonijali”

Sophia akatabasamu huku wakiendelea kula kile chakula, walipomaliza k**a kawaida Sophia alitoa vyombo na kutaka kwenda kuviosha ila Ibra alimuita na kumfanya Sophia asioshe vyombo vile.

“Sophy mke wangu napenda nikae na wewe tupumzike pamoja”

“Naelewa mume wangu ila huwa sipendi kulala na vyombo vichafu ndani ndiomana huwa napenda kuviosha pindi tunapomaliza kula”

“Ngoja nikuulize swali, kwani kesho unaenda wapi?”

“Nipo tu siendi popote”

“Sasa tatizo liko wapi hapo? Utaosha hata kesho, mi napenda tukae tuzungumze na tupumzike pamoja”

Ikabidi Sophia atumie nafasi hii kumuuliza Ibra kuhusu matapishi yake,

“Hivi Ibra hukunisikia wakati natapika?”

“Kwani unaumwa?”

“Hapana ila nilitapika”

“Mmmh sijakusikia kwakweli”

“Mmmh kwahiyo nani alizoa matapishi yangu?”

“Mmmmmh Sophy acha habari hizo bhana tumetoka kula, hebu tubadilishe mada”

Sophia hakuwa na jinsi zaidi tu ya kufata matakwa ya Ibra na kisha wakaamua kwenda kulala, Ibra alipopitiwa na usingizi Sophia akakumbuka vile vyombo akaona ni vyema akavioshe ili asipate tena maswali ya kujiuliza kuwa vyombo vimeoshwa na nani, kwahiyo akatoka mule chumbani na kwenda jikoni kwa lengo la kuosha vyombo.

Alivikuta vyombo vipo pale pale jikoni na kisha akaanza kuviosha, muda kidogo alikuja Ibra kutoka chumbani huku akitikisa kichwa baada ya kumkuta Sophia akiosha vyombo,

“Ona sasa mke wangu halafu unakazana kuuliza nani kaosha vyombo wakati unaamkaga mwenyewe usiku wa manane kuviosha jamani unakuwa k**a mwanga, majukumu gani hayo ya usiku wa manane?”

“Unajua nini Ibra sikupenda nipate tena shida ya kudadisi juu ya mtu aliyeosha vyombo ndiomana nimeamua kuviosha mwenyewe”

“Kwakweli umenishangaza Sophy yani nashtuka kitandani sikuoni kumbe upo jikoni unaosha vyombo, jamani mke wangu kwanini unakuwa hivyo jamani? Nadhani mtu yeyote atakayesikia hili lazima ashangae, kwani kuna umuhimu gani wa kuosha vyombo usiku k**avile hapatakucha?”

Ibra alionekana kutokupendezwa kabisa nah ii tabia aliyoiona leo kwa Sophy kwani yeye alipenda anapogeuka kitandani basi amkute mkewe akiwa pembeni,

“Basi nisamehe mume wangu, nakuahidi hii hali haitajirudia tena k**a nikishindwa kuosha muda ambao tumemaliza kula basi nitakuwa nasubiria hadi kesho yake. Nisamehe tafadhari”

Basi akavimalizia na kuviacha pale juu huku akipanga kuviweka kabatini kesho yake kwani hakutaka kumkwaza mume wake zaidi.

Wakaongozana pamoja kuelekea chumbani ambapo Ibra alionekana kutokuwa na usingizi sana kwani yote ilitokana na vile alivyolala jioni ya siku hiyo, kwahiyo walivyofika tu kitandani Ibra akaanzisha maongezi tena.

20/10/2021

Chuma Cha Reli 🏅

20/10/2021

Genius 🏅

20/10/2021

AMINA; MWANANGU SITAKI UWE K**A MIMI MAMA YAKO—SEHEMU YA TATU

Mume wangu hakua amejua kitu alichokifanya, bado alikua kalewa lewa, alimunamia mtoto na kutaka kumnyanyua akidhani kuwa alikua anaigiza, lakini haikua hivyo, ila kumgusa alikutana na damu.
“Juma! Juma! Juma mwanangu!” Aliita hukua kimnyanyua nyanyua mtoto lakini hakunyanyuka.
“NImefanya nini jamani? Juma! Juma!” Niliona kabisa kuwa pombe zopte ilikua zimemuishia ghafla, mtoto alikua hapumui kabisa. Alianza kupiga kelele kuomba msaada, mara kaite watu, mara usiite, maneno yalikua mengi sana, mume wangu alianza kuwa k**a kachanganyikiwa.

Aliniambia mimi kubaki nyumbani na yeye alimchukua mtoto kumpeleka hospitalini, nilitamani sana kwenda lakini alinikataza katakata. Sikujua kampeleka wapi na wala hakuwasiliana na mimi mpaka asubuhi, usiku ulikua mrefu, nilijihisi k**a nachanganyikiwa kwani kwa hali aliyokua nayo mwanangu nilijua kabisa kuwa hawezi kupona. Nilimpifia Mama na kumuambia kila kitu, aliishia tu kulia na kuniambia nisali sana kumuombea mwanangu. Sijui nini kilitokea lakini mwanangu alipona, asubuhi yake tu mume wangu alirudi na mtoto.

Alikua na bandeji kichwani lakini alikua anatembea mwenyewe.
“Hakikua kitu kikubwa, wamemshona nyuzi sita tu!” Mume wangu aliongea kamna kwamba hakikua kitu cha ajabu sana. Nilimuangalia mwanangu alikua na kidonda kichwani.
“Muache apumzike, nasitaki kabisa kusikia umemuambia kitu mtu yeyeyote, haya ni mambo ya kifamilia, mambo ya kutangaza tangaza changamoto zetu nitakuja kukuua siku!” nilimuitikia kukubaliana naye, akili yangu haikua inawaza k**a anajisikiaje, mimi mwanangu kupona ilikua ni k**a miujiza, nilipiga tena magoti kumshukuru Mungu kwa hilo.

Jioni Mama alinipigia simu, alitaka kujua hali ya mtoto, mume wangu alikua katoka, sikujua k**a alirudi saa ngapi, lakini wakati namuambia Mama kuwa mtoto anaendelea vizuri mume wangu aliingia.
“Unaongea na Nani?” mume wangu aliuliza. Nilishtuka na kuweka simu pemebni, nilikua naogopa na kuwa k**a mtu aliyefumaniwa.
“Naongea na... naongea na...” nilijiongelesha, lakini kabla ya kumalizia kumuambia naongea na nani nilish*tukia teke la uso, mume wangu alikua k**a kanikangaga hivbi usoni.
“Nilikuambia usimuambie mtu, lakini naona ushaanza kunitangaza! Yaani naona unamuambia kila mtu kuwa nimempiga mwanangu, sasa nimekuchoka, nataka uondoke!” Mume wangu alipiga kelele huku akiendelea kunipiga sehemu mbalimbali.

Bado nilikua sijakata simu hivyo Mama alikua akisikia kila kitu, namna nilivyokua nikipigwa. Alinipiga mpaka hasira zake zikaisha, aliondoka nayumbani na hakurudi mpaka baada ya siku tano, wakati wote huo michepuko yake ilikua ikinitumia picha zao wakila bata, wakifurahia maisha. Mimi nilinyamaza, Mama aliniuliza kilichotokea lakini nilikana, aliniambia.
“Mwanangu nimesikia kila kitu, huyo mwanaume ipo siku atakuua!” Nilinyamaza bila kumjibu kwani nilijua kuwa haitasiadia chochote, nilishachoka na maneno vumilia, nilitamani kuondoka lakini sikujua niende wapi.

Maisha yaliendelea, mume wangu hakubadilika, suala la kunipiga lilikua k**a la kawaida. Baaada ya kunipiga mbele ya watoto mara moja na watoto kuanza kumuogopa nadhani hasita zilimzidia. Alikua hajali tena k**a watoto wanaona, alianza kunipiga mbele za watoto na kuwapgiga watoto. Mwanzoni alikua angalau anatoa ada za watoto, lakini baada ya muda aliacha kabisa kutoa ada. Alikua hahudumii familia kwa chochote na k**a nikilalamika basi nikipigo, akija nyumbani na kukuta hakuna chakula basi ni kipigo. Nilishazoea hiyo hali na nilikua sijui nini cha kufanya.

Siku moja mume wangu alikuja na mtoto mkubwa, alikua na k**a miaka sita hivi, aliniambia ni mtoto wake na anataka nikae naye, nilikubali tu kwani sikutaka kumjibu, kwa hasira zake nilijua k**a nikimjibu anaweza kuniua. Nilianza kuishi na yule mtoto k**a mwanangu. Sikua nikimnyanyasa kwani pamoja na kujua kuwa ni mtoto wa nnje ya ndoa nilikua nafahamu fika si kos alake, hakuapanga kuzaliwa na mume wangu nnje ya ndoa. Alikua ni mtoto wak**e na alionekana huko alikokua alikua hahudumiwi vizuri.

“Kwani wewe ndiyo Mama yangu wa kweli?” Siku moja Angel (si jina lake halisi) aliniuliza.
“Hapana kwanini?”
“Nimeuliza tu, sasa k**a wewe ni Mama yangu wa kambo, mbona unanipenda kuliko Mama yangu mzazi, mimi nilikua mtu wa kupigwa kila siku. Baba alikua akija nyumbani naambiwa niende jikoni, nafungiwa jikoni Baba na Mama wanabaki sebuleni, wanakumbatiana na kufanya mapenzi, nilikua nasikia kelele nachungulia kwenye tundu la funguo naona kila kitu!”

Alianza kuongea, kwa namna alllivyokua anaongea alionekana kuathirtika tayari, alikua anajua kila kitu na walikua wanamnyanyasa.
“Kuna siku Mama alijua nawachungulia akawa ananipiga sana, baadaye wakawa hawanifungii tena jikoni bali wanafanya mambo yao wakati mimi nimelala!”
“Kwanini walikua wanafanyia sebuleni, inamaana hawakua na chumba?” Kipo lakini wanafanyia kila sheemu, hata kwenye gari wanafanyia na kila siku Mama alikua ananitukana kuwa mimi ndiyo nimemharibia maisha yake sina furaha. Nilipelekwa kwa Bibi alipokufa ndipo nilikuja kuishi na Mama yangu.

Sikutaka kumdodosa sana kwani alikua mdogo, lakini nilijua kuwa sababu za yeye kuletwa kwangu ilikua ni kwaajili ya kuwapa uhuru wa kufanya mapenzi. Nilikaa naye kwa mwaka mmoja bila Mama yake kuja kumuona wala kupiga simu. Lakini siku moja nakumbuka ilikua jumamosi, nilienda kazini na niliwahi kutoka kwani tunafanya nusu siku. Nilirudi nyumbani na kumkuta Agel analia, alikua chumbani kwake akikusanga nguo, nilimuuliza tatizo ni nini akaniambia kuwa Mama yake alikua kaja na anataka kumchukua.

“Naomba unisaidie Mama, mimi sitaki kuondoka! Wala hata hanitaki, ameona nina furaha hapa anataka kunichukua.” Aliniambia kwa namna alivyokua anaongea nilimuonea huruma, lakini nilijua k**a mume wangu kashaamua basi nisingeweza kufanya chochote. Nilimdanganya tu kuwa nitaongea na Mama yake.
“Kwani mama yako yuko wapi?” nilimuuliza, aliniambia katoka na Baba na kamuambie akusanye kila kitu ili aondoke. Nilirudi chumbani nikiwa na mawazao, kweli hakua mwanangu lakini kwa mambo aliyokua amenielezea nilijua kabisa kuwa mtoto anaenda kutelekezwa. Ni mara nyingi walikua wanatoka usiku na kurudi asubuhi wakimuacha nyumbani bila hata binti wa kazi.

Kuna kipindi Mama yake alishawahi kusafiri akakaa siku tatu bila kujulikana yuko wapi majirani ndiyo walijitolea kumpa chakula. Mume wangu alirudi usiku, alikua na Mama Angel, mimi nilimsalimia vizuri tu lakini yeye alikua kanuna.
“Unataka kunichukulia mwanangu! Mwanamke mshenzi sana wewe na kwa taarifa yako huyu ni mtoto wangu, k**a ulikua unaamini kuwa atakupenda kuliko anavyonipenda mimi basi umenoa!” Alianza kunitukana, mimi nilishangaa lakini nilikuja kugundua kuwa alikua analalamika kwakua alikuta mtoto wake kanawiri na alipotaka kuondoka naye basi alikataa na kusema anabaki.

Kitendo hicho kilimkera sana Mama Angel na kuamua kuondoka na mtoto wake. Mimi nilijitetea lakini haikusaidia, kalizuka kaugomvi flani, tukashikana, lakini k**a kawaida mume wangu alikua upande wa mchepuko, alianza kunipiga, alinipiga sana mpaka nikapoteza fahamu, baada ya kuona sina fahamu, alinichukua na kwenda kunifungia stoo. Aliondoka akimchukua Angle, wanangu ndiyo walienda kuita majirani, wakaja wakavunja mlango nika[pelekwa hospitalini.

Nilikaa kw aisku tatu, mume wangu hakuja hospitalini, mtu pekee aliyekuja kunihudumia alikua ni mama yangu.
“Ukitoka hapa hurudi kwa mume wako!” Maama aliniambia kwa hasira, alikua anaonekana kuuumia sana.
“Nitaenda wapi Mama yangu, Baba hataki nirudi nyumbani...” Nilikua nimechoka, natamani kuondoka na kumuacha mume wangu lakini nilijua sijui ni kwa namna gani naweza kuondoka.
“Mwanangu unakumbuka nilivyokusomesha kwa shida, Baba yako alikua hataki usome kwakua ni mtoto wa k**e, lakini kila siku nilikua napigwa, kila siku nilikua nalia, nilikopa mpaka ukasoma.”
“Nakumbuka Mama.”
“Basi mwanangu, sikukusomesha ili uje kuwa k**a Mimi, mimi nilikua sina pekwenda, sikua na kazi, sikua na chochote, nilikua na watoto wadogo ambao nisingeweza kuwahudumia mwenyewe. Lakini wewe mwanangu una kila kitu, una kazi nzuri, una elimu, unaweza kuhudumia watoto kwanini uteseke k**a mimi?”

Mama aliniuliza maswali ambayo sikua na majibu yake, alinisihi sana, sikua tayari kuondoka, mmbali na mateso yote lakini bado nilikua naamini kuwa siku moja mume wangu atakuja kubadilika. Nilikua najua kuwa labda ipo siku mume wanvgu shetani la chuki litamtoka na kurudi kwangu. Lakini Mama yangu hakukubali, aling’ang’ania akisema kuwa kuondoka ni lazima nipende nisi[pende.
“Lakini Mama siwezi kuwaacha wanangu, mimi nikiondoka mume wangu atawataka, hatakubali kuniachia watoto wangu!”
“Atakuachia mwanangu, ninapokuambia kuwa unaondoka basi jua ni unaondoka, huyo mwanaume atakuacha wewe! Niamini mimi ni mama yako, niliteseka kwaajili yako sitaruhusu uteseke tena.”

Mama aliongea, nilimkubalia kishongo upande nikijua kuwa mume wangu hawezi kuniacha na kunipa talaka. Nilipotoka hospityalini Mama alinisindikiza mpaka nyumbani, mume wangu hakuepo lakini alimsubiri mpaka kurudi.
“Mwanangu nimekusubiri kwakua nataka umuache mke wako! Najkua yeye anakupenda na hawezi kukuacha, na kwa sheria ya dini mwanamke hatoi talaka, ila nataka umuandikie mwanangu talaka tatu.” Mama aliongea kwa kujiamini, mume wangu alimuangalia kwa dharau.
“Umechanganyikiwa wewe, mimi najua kuoa tu sijui kuacha!”

Mume wangu alionge kwa dharau, mama alinyanyuka alimuangalia mume wangu usoni kwa muda wa k**a dakika mbili bila kupepesa jicho kisha akanigeukia.
“Mwanangu kesho kutwa nitakuja kukusaidia kuchukua vitu vyako, mume wako atakua ashakupa talaka.” Mama alimaliza kwa tabasmau, aliondoka na kutuacha wote tunashangaa.
“Huyu Mama yako kichaa nini? Anafikiri k**a nitakuacha, sikuachi na k**a ukitaka kuondoka ondoka lakini watoto wangu niachie na utaondoka na nguo zako tu!”

Mume wangu alifoka, lakini mama hakua amefika mbali, alisikia na kugeuka akarudi, akamuangalia mume wangu kisha akamuambia.
“Mwanangu ataondoka na watoto wake, talaka utampa na ataondoka na kila kitu alichochuma kwa jasho lake.” Alinigeukia.
“Mwanangu anza kuorodhesha vitu vyako vyote katika hii nyumba, usiache chochote hata k**a ni nyanya ulinunua zimeoza utaondoka nazo.” Aliongea na kuondoka, mume wangu alianza kufoka, alinifuata na kutaka kunipiga, lakini kabla ya kufanya chochote alianza kupiga kelel.

“Mamaaa nakufaaa!” alipiga kelele huku akivua nguo. Alikua anapiga kelel hukua kishika sehemu zake za siri, alivua nguo na kubaki k**a alivyozaliwa, uume wake ulikua umesimama. Nilijua ni mambo ya mapenzi nikamuambia hawezi kunigusa kwani naumwa lakini alikua anapiga kelele analia k**a mtoto. Kwa namna ulivyokua umesimama nilikua sijawahi kumuona, aulikua umesimama, umekua mkubwa kuliko kawaida yaake, mishipa ya damu mirefu tena vmyekundu ilikua inaonekana.

Alionekana kuwa katika maumivu makali,a lipiga kelele akilalamika kuwa uume wake ulikua unawake moto. Aliniambia nimletee maji tabaridi, nilileta akamwagia lakini wapi, alikimbia mpaka kwenye friji na kuchukua mabarafu lakini wapi, alikua k**a mtu aliyechanganyikiwa. Hata watoto walipokuja ilibidi kuwatoa nnje kwani Baba yao alikua uchi. Alianza kulia akiniomba nimpeleke hospitali, nilimfunika na kumuingiza kwenye gari, huko alipelekwa walimhangaikia lakini hakulala. Alikaa hivyo hivyo mpaka asubuhi, uume umesimama, unauma mpaka umekua mweusi.

“Mama yako ndiyo kanifanyia haya, mpigie nimuombe msmaaha.” Nilimpigia Mama lakini hakupokea, nilimpigia Baba ambaye alipokea huku akiongea kwa shida, alionekana k**a anaumwa, aliniambia kuwa Mama ametoka na hajui kaenda wapi. Kabla sijampigia tena Mama meseji yake iliingia, muambie akupe talaka zako tatu. Nilimuonyesha ile mseji mume wangu, alianza kulia kuniomba msamaha aking’ang’ania kuwa hawezi kuniacha. Hospitalini walisema hawana cha kumsaidia, tulirudi nyumbani akiwa katika maumivu makali.

Mpaka usiku mume wangu aliniandikia talaka zangu tatu bila kuambiwa na mtu yeyote. Cha ajabu aliponikabidhi ile talaka uume wake ulilala na kuwa k**a kawaida na hapohapo Mama yangu alipiga simu.
“Hiyo nyumba najua ni ya mwanangu, kesho nitakuja na mwanasheria, mtaandikishana kugawa vitu na wewe utaondoka.” Mume wangu alikubali k**a zoba, sijui Mama alifanya nini lakini alitafuta mwanasharia, tukaandikishiana na mume wangu, tukaenda mpaka mahak**ani na kila kitu kikawa sawa.

Mume wangu hata hakuomba msamaha, alinikinahi na hakurudi tena kwangu, Mama yangu aliniangalia na kuniambia mwanangu k**a ni kutubu nitatubu baadaye ila jua nilikusomesha ili usiteseke k**a mimi. Tangu kuachana na mume wangu nimekua mtu wa furaha sana, Mama yangu alishafariki (Mungu muweke mahali pema) Baba anaishi mwenyewe, tunamhudumia lakini watoto wote hatumpendi, kwa namna alivyokua akimnyanyasa Mama hakuna mtoto hata mmoja ambaye anataka kuishi ney.

Tumemuwekea mfanyakazi wa kuishi naye, mume wangu alioa tena lakini mwanamke akashindwa kuvumilia wakaachana, kazini alishafukuzwa muda mtrefu kwani alikua na kesi ya kumpa mimba mtoto wa sekondari. Kidogo imfunge lakinia lihonga sana, sasa hivi nasikia yupo mwanza na sijui hata anafanya nini. Mimi nina maisha yangu, mambo ya wanaume kwa sasa sitaki nalea wanangu kwanza. Nimeteseka sana kiasi kwamba kila mwanaume ninayekutana naye nahisi k**a anataka kuniumiza k**a mume wangu.

***MWISHO

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Address


Kino
Dar Es Salaam
255